Naombeni msaada wapendwa!!!!!

Kazini na mwanamke asiye mke wake "Amri ya ngapi tena vile "USIZINI" then "USITAMANI MWANAMKE ASIYE MKE WAKO"

Kwanini hawajasema Mwanaume??? Hilo ndo kosa umenisoma.

Mie mzima nammiss BE wangu tu sijui yuko wapi

Hapo unazungumzia dhambi DA (kama BE hajui wajibu wake mi nitamsaidia)......hapa tunazungumzia kosa.....usiende kwenye maandiko (na mimi nikitumia maandiko ya nabii tito tutapoteza mwelekeo wa mada)
 
Kyabushaija aka.....
Shikamoooo!!!
Eti wasema, Mpe ushauri mother house basi!!!

Ushauri kwa motherhouse ni mmoja tu:-

Apige magoti na kumuombea Mumewe apate mipango mingine ya nje japo miwili zaidi ili yeye na watoto wakae kwa amani...

Basi...
 
MJ1, alipoachia shule ni mbali sana. umri wa zaidi ya miaka 50, atakaa darasa gani ukiziangatia aliachia la saba, takribani akiwa na miaka 14? Ila mimi huwa nasikitishwa sana na wamama wanaokaa tu nyumbani bila kujishughulisha, kisa waume zao wana hela. kuna mifano mingi tu, tena wengine waume wenyewe wanamwambia mama "wewe bora ulee tu watoto hapa nyumbani, kama mshahara wako nitakulipa"
Darl FP penye nia pana njia mpenzi, si lazima aende darasani ajifunze zis,zat..kuna shule za vitendo aingie moja kwa moja kwa busness............kutie and dye n.k. inategemea na kuamua kwake....................Si they say uzee uko kwenye akili ya mtu?? Ukikubali kuwa umezeeka hata ukiwa 35 utajiita mzee......mie tu hapa na hii 40 yangu bado najiona sweet 16 mamii.......Its all about attitude
 
okay aksante Teamo kajiswali ka uzushi...................is it possible kwa karne ya sasa kuwa na ndoa kama zile za babu zetu??.......yaani ambazo hazibase kwenye love?

hamna kitu kama hicho.....!

i expected this question from you...

''IS IT POSSIBLE FOR OUR GENERATION TO BUILD UP THE NEW WORLD WITH FAITHFULLY LOVE MARRIAGES?.....the love marriages with FAITHFULLY PARTINERS...'''

maanake nini...utandawazi unatulazimu ku-move foward sasa
 
Hapo unazungumzia dhambi DA (kama BE hajui wajibu wake mi nitamsaidia)......hapa tunazungumzia kosa.....(na mimi nikitumia maandiko ya nabii tito tutapoteza mwelekeo wa mada)

Nimekusoma Mkuu sawa kakosea kutoka nje ya ndoa yake hapo ni sawa
 
Huyu mme alimwacha mke nyuma katika maisha yake....sisemi ni lazima mke awe msomi, ila ile kuamini katika umiliki wa ndoa na mazao ya ndoa ndio jambo la muhimu...!
Hapa mwenye nafasi kubwa kufata nguvu za giza ni mke......so ndo asiyejiamini?

Nimekupata kaka!!
 
hamna kitu kama hicho.....!

i expected this question from you...

''IS IT POSSIBLE FOR OUR GENERATION TO BUILD UP THE NEW WORLD WITH FAITHFULLY LOVE MARRIAGES?.....the love marriages with FAITHFULLY PARTINERS...'''

maanake nini...utandawazi unatulazimu ku-move foward sasa

Aksante swali langu lilikuwa na maana yake.........aksante sana Babu so are you under the same trail and Mama G ategemee heat one of her life time eh?
 
Darl FP penye nia pana njia mpenzi, si lazima aende darasani ajifunze zis,zat..kuna shule za vitendo aingie moja kwa moja kwa busness............kutie and dye n.k. inategemea na kuamua kwake....................Si they say uzee uko kwenye akili ya mtu?? Ukikubali kuwa umezeeka hata ukiwa 35 utajiita mzee......mie tu hapa na hii 40 yangu bado najiona sweet 16 mamii.......Its all about attitude

Ni kweli unayosema my dear, lakini huyo mama sidhani kama anaweza lolote, yaani alishazoea kuamka, kudeki, kubandika mboga, kusonga ugali, kupika ubwabwa wa jioni................................. sidhani kama ataweza hata kuingia darasa la vitendo, maana alishaanzishiwa biashara akaiua
 
Jamani jamani, akiona wife hapa umekwisha! lazima mdhungu wa 4 leo

FP, salama lakini?

Kwa bahati mbaya sana ndoa nyingi hujengwa na mifarakano ya mara kwa mara. Unapoona ndoa tulivu fahamu kuwa haitadumu! Kugombana ndani ya ndoa kuna tengeneza "bond"...

The good thing, motherhouse nikiwahi nyumbani kila siku lazima ijumaa jioni anilazimishe nichelewe kurudi! Huwa ananiambia kuwa anahitaji uhuru at least for Friday evening! Akae na watoto waangalie "tamthilia" e.t.c! see!
 
hamna kitu kama hicho.....!

i expected this question from you...

''IS IT POSSIBLE FOR OUR GENERATION TO BUILD UP THE NEW WORLD WITH FAITHFULLY LOVE MARRIAGES?.....the love marriages with FAITHFULLY PARTINERS...'''

maanake nini...utandawazi unatulazimu ku-move foward sasa

Aksante swali langu lilikuwa na maana yake.........aksante sana Babu so are you under the same trail and Mama G ategemee heat one of her life time eh?

Sijui nyie mko na sredi yenu nje ya hii ya LD au macho yangu yanaona vibaya......
 
Ushauri kwa motherhouse ni mmoja tu:-

Apige magoti na kumuombea Mumewe apate mipango mingine ya nje japo miwili zaidi ili yeye na watoto wakae kwa amani...

Basi...

Duuuuu, natamani kukuona kwa macho,
Ngoja nimuombe Babu afanye mpango wakunileta huko uliko!!
 
Aksante swali langu lilikuwa na maana yake.........aksante sana Babu so are you under the same trail and Mama G ategemee heat one of her life time eh?

si rahisi kwa sasa kuizungumzia future kwa hali ilivyo sasa.......!

lakini inapobidi naweza kuizungumzia....!ni hivi:
WE ARE STILL IN LOVE......!a very serious one!kitu kama hicho kwa sasa naweza kusema ASIKITEGEMEE!...(as long as tutakuwa hivi)

concern yangu sasa mwanajamii,
Mimi sina uzoefu mkubwa sana kwenye ndoa.....!ninachokifanya huwa naziangalia kwa makini sana ndoa kadhaa za watu ninaowafahamu (marafiki na ndugu pia),huwa naona kuna ''tatizo'' kubwa sana.halafu mbaya kabisa ni ''a common problem''
 
Sijui nyie mko na sredi yenu nje ya hii ya LD au macho yangu yanaona vibaya......
Hapana St RR tupo pamoja ni katika kujustify point ya Teamo alosema kuwa huyu Baba alikosea kuchagua mother house kwa kuwa alichagua mtu ambaye si right partner wake. Na argument yake kubwa ni kuwa yote haya yanasababishwa na the so called love marriages................
 
Kwa kweli inasikitisha kwa hiyo hali iliyopo kwa huyo madha haus, lakini hata hivyo asione kuwa mmewe ni mbaya kuliko wengine wote, kwani kwa scenario iliyopo hapo, kwa wanaume wengi ungekuta hali ni mbaya zaidi, pengine baba alishahamia kwa huyo wa nje, au alishamtimua mama kabisa.

Kabla sijajibu moja kwa moja maswali yako, napenda niseme kwa mtazamo wangu kwenye ndoa kuna mihimili mikuu mitatu..

  1. Love affairs (between husband and wife)
  2. Social Affairs (Children, relatives, housing, etc care taking)
  3. Developmental/Economic affairs

Ingawa maelezo yako yamebase sana kwenye mhimili wa tatu na wa pili, lakini ni rahisi mtu ku-predict kuhusu mhimili wa kwanza.

Inavyoonyesha ni kuwa hawa wamama wawili wanazidiana namna tofauti. Huyu mama mkubwa inaonyesha pamoja na kuwa hana kipaji katika kubuni na kusimamia developmental/economic affairs, lakini bila shaka ana kipaji katika love and social affairs, ndo maana akaonwa, akapendwa, akaolewa, na amedumu katika ndoa yake. Ndo maana pamoja na kuwapo kwa huyo wa pembeni, lakini mume wake anaona umuhimu wa kuendelea kuwa naye, tena anakaa (analala), kwake. Hata hivyo inaonyesha lakini kuwa mama mdogo ana viwango fulani katika love and social affairs nda maana pamoja na mchango wake kwenye uchumi, bado 'ameleta mtoto'

Huyu mama asijisikie vibaya wala mnyonge, kwa ni alichokifanya huyu baba ni udhaifu kama ulivyo kwa wababa wengi, bahati mbaya nyumba ndogo imekuja kuonyesha strengths za kipekee, na baba akatekwa na hiyo opportunity. Huyu mama afikirie kuwa ingekuwa huyu mama mdogo ni average woman, angeweza kutumia strength yake kushawishi huyu baba amfukuze, au angemfanyia chochote.

Huyu mama akubali tu matokeo akijua kuwa strings zilizomuunganisha mumewe kwa huyo wa pembeni ni strong kuzikata. Hata hivyo hiyo isimkatishe tamaa, wanadamu wanazidiana. Kikubwa zaidi, isidhaniwe kuwa uwezo wa kimawazo ya biashara au vinginevyo alio nao huyu bi mdogo ni kutokana na elimu yake pekee, hapana, ni kipaji. Wapo watu waliosoma sana tena wana madegree ya uchumi, lakini mpe hata biashara ya nyanya, inamshinda.

Kwa hiyo, kwa kujibu maswali yako:

Huyu baba hakukosea kumuoa mke wanayetofautiana kielimu. Kuoana ni kupendana, na bila shaka alimpenda. Wapo wengi waliooana wakiwa na viwango sawa au vinavyoendana vya elimu, na bado ndoa zao zimevunjika, au ni za mateso

Kumuendeleza kielimu kwa sasa na umri wao, na majukumu ya kifamilia inaweza isiwe rahisi sana. Lakini pia kama nia itakuwa kumuendeleza ili 'waendane' kimawazo inaweza isiwe suluhisho la matatizo yao kwenye ndoa. After all, inaweza kuongeza matatizo.

Ni vizuri mtu kuoana na mtu ambaye akili zenu zinaendana, ndiyo. Hata hivyo kuendana kwa akili hakutathminiwi tu na elimu ya darasani, bali pia na hobby, vipaji n.k. Hata hivyo, kuendana kwa akili ni jambo moja, lakini kupendana, na kuwa na uwezo wa kuvumiliana ndilo la muhimu zaidi. Narejea tena, wapo wengi waliooana na viwango sawa vya elimu, wasiendane, na wapo waliooana na viwango tofauti sana vya elimi, na wanaishi raha mustarehe.

Huyu baba hafanyi makosa kumfanya mpango mdogo kuwa mshauri wa masuala ya maendeleo. Hatujui kipi kilianza; kuwa huyu baba alikutana na huyu bi Mdogo kwenye biashara, baadae 'shetani akampitia' au 'shetani alimpitia' kwanza baadae akaja kugundua mna kipaji cha biashara. All in all, imeshatokea, wana mahusiano, na huyu baba ana hobby ya biashara, then mshauri mzuri, sio mtu baki, bali ni huyu dada, as long as ni bi Mdogo wake. Hatuna hakika kama akiacha kuwa mshauri wake, then ataacha na kuwa mpenzi wake.

Kama unaweza kumfikia huyu mama, mshauri kuwa hajajaaliwa kipaji cha biashara, lakini kajaaliwa mengi ambayo wengi hawajajaliwa, ndo maana kaolewa, na kadumisha ndoa mda wote. Asijisikie mnyonge, bali amshukuru Mungu kwa hilo alilomjaalia. Asidhani huyo bi. Mdogo kamzidi kila kitu, kwani angemzidi kila kitu, angekuwa ameolewa, na ana mume wake wa ndoa.

Ubarikiwe sana Tuko!!!
ASANTE KWA USHAURI MZURI.
 
Teamo....aka mfalme wa amani....usiwe unatuchunganya akili eeehhh?yaani nimetoka hapa kwenda nyonyesha nawaza Teamo atakuwa kasema nini kule kwa thread kuhusu ku-cheat ....kurudi nimepata kazi ya kuanza huko nyuma only kuwa confused zaidi.......nakuomba sana.....:hand::hand:
 
si rahisi kwa sasa kuizungumzia future kwa hali ilivyo sasa.......!

lakini inapobidi naweza kuizungumzia....!ni hivi:
WE ARE STILL IN LOVE......!a very serious one!kitu kama hicho kwa sasa naweza kusema ASIKITEGEMEE!...(as long as tutakuwa hivi)

concern yangu sasa mwanajamii,
Mimi sina uzoefu mkubwa sana kwenye ndoa.....!ninachokifanya huwa naziangalia kwa makini sana ndoa kadhaa za watu ninaowafahamu (marafiki na ndugu pia),huwa naona kuna ''tatizo'' kubwa sana.halafu mbaya kabisa ni ''a common problem''

Okay so kuna uwezekano au room ya kuwa na exceptions eh..(If all other factors remain constant...............)
 
Hao wanaozihubiri Amri za Mungu, hao mnaokwenda kwao kutubu dhambi zenu na kurudishwa sijui kundini......nawazungumzia hao hao.....ni waasherati na wazinzi wakubwa tena wazoefu!

LD kubali usikubali lakini ukweli ndio huu: Sisi waname haturidhishwi na wala hatukuumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.... Na hilo si kwa binadamu tu; Angalia majogoo, mabeberu, simba, fisi, na wanyama kribia wote.

Kufuata Sheria Za Mungu huwa tunazifuata kinafiki!

Hapa rafiki nakuunga mkono, ingawa huu ukweli unauma sana. lakini mjue hata sisi hatukuumbwa kwa ajili ya mwanaume mmoja (wote si ni binadamu!!!!) lakini tunaamua tu kujiheshimu tukijua kuwa MIILI YETU NI HEKALU LA BWANA!!
 
FP, salama lakini?

Kwa bahati mbaya sana ndoa nyingi hujengwa na mifarakano ya mara kwa mara. Unapoona ndoa tulivu fahamu kuwa haitadumu! Kugombana ndani ya ndoa kuna tengeneza "bond"...

The good thing, motherhouse nikiwahi nyumbani kila siku lazima ijumaa jioni anilazimishe nichelewe kurudi! Huwa ananiambia kuwa anahitaji uhuru at least for Friday evening! Akae na watoto waangalie "tamthilia" e.t.c! see!

Rafiki salama, hofu kwako.
sasa hapa rafiki unaonekana ni mkorofi sana ukiwa nyumbani, mpaka mother house anakutimua! lol! punguza kutumahasa trip za chumbani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom