Naombeeni msaada

Bizzly

Member
May 3, 2010
79
21
wakuu/wasomi naombeni ushauri wa kitaalam, nina kiwanja changu, nimekuta jamaa wameanzisha njia/ anapitisha gari bila hata ya kunitaarifu, nami nataka nichukue uamuzi wa kuiziba/ kuweka fence, je niko sahihi?
 
Kama kiwaja chako kimepimwa naamini ramani inaonyesha fika kuwa hilo ni eneo la kiwanja sio barabara. Kama kimepimwa/hakijapimwa na bila ruhusa yako watu wamepitisha barabara hapo nafikiri inabidi uende kwenya baraza la ardhi la kata wanaweza kabisa kukusaidia au kutoa mwanga wa jambo hilo. Hujaeleza ni muda gani barabara hiyo imeanza kutumika, hata hivyo kama ni huu upitishaji barabara wa kiholela kutokana na kuuziwa viwanja kienyejienyeji bila kuzingatia umuhimu wa barabara nafikiri unaweza kuifunga ila ni vizuri ukawatumia viongozi wa serikali ya kijiji ili hata kama itafungwa hiyo barabara kuwe na barabara mbadala hii itasaidia kujenga maelewano na watu waliokuwa wanatumia hiyo barabara.
 
Back
Top Bottom