Mchumba wangu ana karama ya unabii, ananitisha!

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,816
6,396
Wakuu habarini za wakati huu...

Niliwahi kuleta Uzi humu kuhusu mchumba wangu ambaye ni Mcha Mungu, bikira, mpole, mkarimu, mzuri n.k.

Nimegundua kwamba huyu mwanamke ana karama ya unabii pia (muonaji). Zamani manabii waliitwa waonaji.

Kwanini nimefikia hii conclusion? Mjomba wangu alikuwa anaumwa, yaani kaka yake mama yangu. Siku Moja kabla ya kifo cha mjomba wangu, mchumba wangu akanipigia simu kunimbia anaona huzuni KUBWA Kwa mama yangu, kesho yake mjomba akafariki, kweli mama aliumia sana!

Mimi ni Wakili, nilikuwa na kesi Tanga Jana, kabla sijaondoka akanipigia simu kuniambia anaona vita KUBWA kwenye hiyo kesi, na ananiona Niko hospitalini! Baada ya kesi, ule upande wa pili wakaniomba tuonane nje ya Mahakama nikiwa na mteja wangu ili tufute kesi tuyazungumze, kweli tukaenda kuonana nao, nikawekewa sumu kwenye kinywaji changu, nikapelekwa hospitalini kweli na nikalazwa, Sasa hivi ndio wameni-discharge.

Hayo ni machache tu kati ya mengi. Ama kweli, ukimtanguliza MUNGU mbele HUWEZI kuikataa taasisi ya NDOA. NDOA ni baraka.

Huyu nikimuoa inabidi niwe makini sana

Muwe na jioni njema.
 
Wakuu habarini za wakati huu...

Niliwahi kuleta Uzi humu kuhusu mchumba wangu ambaye ni Mcha Mungu, bikira, mpole, mkarimu, mzuri n.k.

Nimegundua kwamba huyu mwanamke ana karama ya unabii pia (muonaji). Zamani manabii waliotwa waonaji.

Kwanini nimefikia hii conclusion? Mjomba wangu alikuwa anaumwa, yaani kaka yake mama yangu. Siku Moja kabla ya kifo cha mjomba wangu, mchumba wangu akanipigia simu kunimbia anaona huzuni KUBWA Kwa mama yangu, kesho yake mjomba akafariki, kweli mama aliumia sana!

Mimi ni Wakili, nilikuwa na kesi Tanga Jana, kabla sijaondoka akanipigia simu kuniambia anaona vita KUBWA kwenye hiyo kesi, na ananiona Niko hospitalini! Baada ya kesi, ule upande wa pili wakaniomba tuonane nje ya Mahakama nikiwa na mteja wangu ili tufute kesi tuyazungumze, kweli tukaenda kuonana nao, nikawekewa sumu kwenye kinywaji changu, nikapelekwa hospitalini kweli na nikalazwa, Sasa hivi ndio wameni-discharge.

Hayo ni machache tu kati ya mengi. Ama kweli, ukimtanguliza MUNGU mbele HUWEZI kuikataa taasisi ya NDOA. NDOA ni baraka.

Huyu nikimuoa inabidi niwe makini sana

Muwe na jioni njema.
Wewe ni mwehu tuu😂😂😂😂😂😂
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom