Naomba msaada namna ya kuwafukuza wapangaji wasumbufu na wachafu kwenye nyumba yangu

Haupo siriazi
Siku zote hakuna mpangaji jeuri mbele ya mwenye nyumba

Hao ni wapangaji sio nduhuzo
Kitendo cha mpangaji kutolipa kodi tayari keshajifukuzisha sijui unasubiri nii zaidi ya kuwaandikia notisi ya kuhama

Inaonekana mzembe sana
Mkuu nisaidie Sheria inasemaje maana huu ni mwaka wapili notice ya mdomo wamegoma kutoka.
 
Siku mvua ikiwa inanyesha katoe bati waambie linavuja halafu unakauka hakuna kurudishia. Kama nyuma ina geti ondoa geti lote wakae wazi. Ongea na Tanesco wake waharibu luku na baadae unawaambia mwenye kufuatilia suala la umeme ni wewe mzee kaa wiki mbili lazima wakufuate tu kuja kuomba msamaha.mwisho waambie unafanya marekebisho ya milango unaondoka nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukua yai la bata, liandike kama kiarabu kutumia damu ya kuku. Chukua nazi tatu, moja indoe manyoya halafu nayo iandike kiarabu. Pasua nazi moja, chukua gunzi halafu livishe kitambaa cheuzi chini na chekundu juu. Hivyo vyote kaviweke chooni kwenye ungo Mpya usiku wa manane ili wakutane navyo asbh wakiingia chooni.
Nishukuru baadae
 
Mkuu pole sana kwa hiyo changamoto sijajua masharti yaliyopo mkataba wa kupangishana kama yameainisha namna ya malipo ikiwemo na suala la usafi zikiwemo na hatua zitakazochukuliwa kwa aliyekiuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani naomba msaada niwwfukuzeje wapangaji wa aina hii kwenye nyumba yangu.

1.Mmoja hajalipa kodi miezi mitano
2.Wapili hajalipa miezi miwili
3.Amemaliza juzi baada ya kukaa miezi minne bila kulipa Kodi.

Juu ya yote ni wachafu sana mpaka nyumba yangu mimingreatthinker mwenzenu naionea aibu.

Mbaya zaidi mimi sikai nao na Niko mbali kwahiyo wanatake hiyo advantage kunilipa miezi watakayo.

Nyumba iko dar namimi niko mbali sana hivyo ufwatiliaji wa karibu unakuwa mgumu.sana.
Siwataki kabisa Yani ningeweza wangeondoka hata usiku huu.

Ndugu yangu aliepo hapo dar ana mitkas yake mingi hivyo hana muda wakuwafwatikia.

Naomba msaada niwafukuzeje?
Wape Notisi ya mwezi mmoja ya kuondoka notisi hiyo ipitie kwa mjumbe

Baada ya mwezi mmoja nenda na Mjumbe kwa ajili ya kutoa vitu mjumbe yupo kama shahidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
superbug,
Acha wakae mkuu nyumba nyingi zipo wazi shukuru wewe jibane na Kodi siku wakihama utakarabati, ila huyo asiyelipa mhhh timua kuanza moja sio ujinga-mwache akapambane na Hali yake
 
superbug,
Ukishaanza kuona Wapangaji hawakulipi Kodi na wanakusumbua jua hata wao pia wameshaanza Kukudharau na wameona Udhaifu ndani yako. Na vile vile ukiona Wapangaji ni Wachafu jua ya kwamba kuna uwezekano mkubwa tu wakawa wameuakisi huo Uchafu walionao kutoka kwa ama mwenye Nyumba wao au wana Familia wake.
 
Kuna njia kadhaa za kufanya.
1/Leta fundi ili akate huduma za umeme na maji kama yapo. Ng'oa kabisa miundombinu.
2/Leta fundi wa mbao, jifanye unarekebisha paa, ng'oa sehemu ya paa, paache wazi halafu sepa zako.
Makonda amewaambia wasilipe kodi kipindi hiki cha COVID-19.
Waambie una CORONA chief...watakimbia wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh kuna wapikasumu humu duh sijawahi kuona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukua yai la bata, liandike kama kiarabu kutumia damu ya kuku. Chukua nazi tatu, moja indoe manyoya halafu nayo iandike kiarabu. Pasua nazi moja, chukua gunzi halafu livishe kitambaa cheuzi chini na chekundu juu. Hivyo vyote kaviweke chooni kwenye ungo Mpya usiku wa manane ili wakutane navyo asbh wakiingia chooni.
Nishukuru baadae


🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom