Naomba msaada namna ya kuwafukuza wapangaji wasumbufu na wachafu kwenye nyumba yangu

Jamani naomba msaada niwwfukuzeje wapangaji wa aina hii kwenye nyumba yangu.

1.Mmoja hajalipa kodi miezi mitano
2.Wapili hajalipa miezi miwili
3.Amemaliza juzi baada ya kukaa miezi minne bila kulipa Kodi.

Juu ya yote ni wachafu sana mpaka nyumba yangu mimingreatthinker mwenzenu naionea aibu.

Mbaya zaidi mimi sikai nao na Niko mbali kwahiyo wanatake hiyo advantage kunilipa miezi watakayo.

Nyumba iko dar namimi niko mbali sana hivyo ufwatiliaji wa karibu unakuwa mgumu.sana.
Siwataki kabisa Yani ningeweza wangeondoka hata usiku huu.

Ndugu yangu aliepo hapo dar ana mitkas yake mingi hivyo hana muda wakuwafwatikia.

Naomba msaada niwafukuzeje?
Toa location ya mjengo tukakutolee wapangaji, utatulipa baada ya kazi
 
Mikataba niliwapa inayosoma hayo yote uliyoainisha mkuu mi Niko mbali na Dar na tz nadhani ndio maana wananipanda kichwani subirini hi korona iishe mtasoma magazeti ya Tanzania siku moja mwenye nyuma afanya ubaya kwa wapangaji wake.
Ndio hapo umuhimu wa madalali unapoonekana. Dalali ana-act kati ya mwenye nyumba na mpangaji na hiyo kazi ungempa dalali angemaliza dk 0 tu. Analeta watu kuangalia nyumba kila siku
 
Ndio hapo umuhimu wa madalali unapoonekana. Dalali ana-act kati ya mwenye nyumba na mpangaji na hiyo kazi ungempa dalali angemaliza dk 0 tu. Analeta watu kuangalia nyumba kila siku
Sijakuelewa mkuu
 
Wape Notisi ya mwezi mmoja ya kuondoka,
notisi hiyo ipitie kwa mjumbe
Baada ya mwezi mmoja nenda na Mjumbe kwa ajili ya kutoa vitu mjumbe yupo kama shahidi
Hapo ni sahihi pitia hizo hatua km uliwapangisha bila ya Mikataba
lkn km Mikataba ipo usiendelee tena waambie nataka kukarabati/ kuvunja /au kujenga vitu muhimu km vyoo vya ndani
kuna njia ya kupitia Baraza la nyumba la Kata, hapo ni kiboko wataitwa na watapewa muda km miezi mi3 lkn kodi walipe ikiisha unarudi kwenye Baraza unapewa kibali cha kumchukua Dalali ambaye naye atawapa Muda wa Kisheria km mwezi wawe wamelipa la sivyo wakamatiwe mali zao kufidia deni.
Baada ya hapo nuda ukifika Dalali atakukabidhi nyumba ikiwa haina wapangaji. Njia hii ni salama lkn ia gharama sana na huwa wapangaji wanakimbia na madeni hivyo deni linabaki wewe superbug na Dalali
 
Jamani naomba msaada niwafukuzeje wapangaji wa aina hii kwenye nyumba yangu.

1. Mmoja hajalipa kodi miezi mitano
2. Wapili hajalipa miezi miwili
3. Amemaliza juzi baada ya kukaa miezi minne bila kulipa Kodi.

Juu ya yote ni wachafu sana mpaka nyumba yangu mimi great thinker mwenzenu naionea aibu.

Mbaya zaidi mimi sikai nao na Niko mbali kwa hiyo wanatake hiyo advantage kunilipa miezi watakayo.

Nyumba iko Dar namimi niko mbali sana hivyo ufwatiliaji wa karibu unakuwa mgumu.sana.
Siwataki kabisa Yaani ningeweza wangeondoka hata usiku huu.

Ndugu yangu aliepo hapo Dar ana mitikasi yake mingi hivyo hana muda wakuwafwatilia.

Naomba msaada niwafukuzeje?

Mbona rahisi sana hiyo tangaza umeuza nyumba wape notice ya mwezi mmoja kila mtu alale mbele

Sent using IPhone X
 
Zipi wakati Kodi hawalipi washamaliza muda.
usitumie kabisa Madalali wa mitaani kupangisha nyumba yako pangisha mwenyewe
Baraza la nyumba la Kata au la Wilaya wana madalali wa mahakama km vile Majembe auc mart, Ikivella, Yono nk ndio naowazungumzia
Kwa Dsm kuna Kipindi waziri wa Ardhi Wailliam Lukuvi aliyafuta Mabaraza ya Ardhi ya kata, km kweli fika Ofisi ya Kata watakupa msaada usiache kukata mpunga watakupa na mgambo
 
Kwa kuwa hawajalipa we nenda na mtu ajifanye ananunua nyumba wambie wahame ndani ya weekly, ila usiwadai ela wape offa habaki mtu apo
 
Jamani naomba msaada niwafukuzeje wapangaji wa aina hii kwenye nyumba yangu.

1. Mmoja hajalipa kodi miezi mitano
2. Wapili hajalipa miezi miwili
3. Amemaliza juzi baada ya kukaa miezi minne bila kulipa Kodi.

Juu ya yote ni wachafu sana mpaka nyumba yangu mimi great thinker mwenzenu naionea aibu.

Mbaya zaidi mimi sikai nao na Niko mbali kwa hiyo wanatake hiyo advantage kunilipa miezi watakayo.

Nyumba iko Dar namimi niko mbali sana hivyo ufwatiliaji wa karibu unakuwa mgumu.sana.
Siwataki kabisa Yaani ningeweza wangeondoka hata usiku huu.

Ndugu yangu aliepo hapo Dar ana mitikasi yake mingi hivyo hana muda wakuwafwatilia.

Naomba msaada niwafukuzeje?
nenda kwa mganga mkuu atakusaidia
 
Haupo siriazi
Siku zote hakuna mpangaji jeuri mbele ya mwenye nyumba

Hao ni wapangaji sio nduguzo
Kitendo cha mpangaji kutolipa kodi tayari keshajifukuzisha sijui unasubiri nii zaidi ya kuwaandikia notisi ya kuhama

Inaonekana mzembe sana
....Yah, hayupo Serious. Yaani Suala la kumfukuza mpangaji wako msumbufu anayechelewesha Kodi ni Sula la Kuomba Ushauri JF???
Hauko serious.
Unless ulitaka tu kutujulisha kwamba una Nyumba Dar na ina Wapangaji.
Noted.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom