Naomba kujua historia ya Urusi

Hizi nondo vipi wakuu, Kabaunyeri na The Emperor mmetuacha na Kiu, tunaomba mzilete wenyewe kwa hiyari ama sivyo tutatumia nguvu.
 
Asante mkuu mimi nilitaka kujua ilikuwaje Urusi pamoja na uwezo wake mkubwa wa Kijeshi akashindwa huko Afghanistan,na pia Marekani kushindwa huko Vietnam

Hivi vita ulivyovitaja hapo juu naweza sema vinafanana hasa ukiangalia sababu za kuanza kwake na matokeo yake baada ya kuisha yani kushindwa kwa mataifa hayo makubwa.

Kwanza tuanze na kusema kuwa baada ya vita vya pili vya dunia, U.S na U.S.S.R waliibuka washindi na hivyo kupelekea kuwa superpowers pekee duniani (kijeshi na kiuchumi). Lakini hawa jamaa walikuwa na itikadi tofauti sana hasa katika muonekano mpya wa kisiasa na kiuchumi duniani. Wamerekani walihubiri ubepari na wasoviet walihubiri ukomunisti. Kila mmoja aliamini kuwa mfumo wake ndio zitawezesha kuinua upya uchumi wa kidunia (mana vita viligharimu nchi nyingi sana kifedha, watu na mali). Hii tayari iliweka uhasama mana wote wababe na hakuna aliyekubali kushindwa. Kilichofuata hapo ni nani ataweza kushawishi nyingi zaidi zimuunge mkono katika hizo sera zake. Pia baada ya kulipuliwa kwa mabomu ya kiatomiki huko Japan, warusi walitia jitihada kubwa na hatimaye waliweza kutengeza ya kwao. Hii ndio mwanzo wa COLD WAR. Hii ilipelekea nchi ndogo hasa Africa, Asia na Amerika ya kusini kuwa katika hali flani ya tutoke vipi maana wasoviet wanakuja na sera zao na ahadi kibao, na hapo hapo warekani nao wanakuja na sera zao na ahadi kibao. Hii ilileta kuibuka vikundi na vuguvugu la kisiasa na kutetea sera tofauti na mara nyingine demokrasia iliposhindikana basi watu waliingia mwituni. Sababu kubwa ya kuchagua ipi ni ipi ilitofautiana nchi na nchi, historia ya taifa husika, jiografia na tamaduni za watu wake. Kumbuka pia mataifa mengine makubwa nayo tayari yalishachagua pande zao mapema kama China, Japan, Western Europe karibu nchi zote n.k. Pia hawa wababe walitumia mbinu kadhaa kutekeleza hiyo mipango yao kwa wale wabishi hata kupindua serikali na kuweka watu wao (puppet governments).
 
Hivi vita ulivyovitaja hapo juu naweza sema vinafanana hasa ukiangalia sababu za kuanza kwake na matokeo yake baada ya kuisha yani kushindwa kwa mataifa hayo makubwa.

Kwanza tuanze na kusema kuwa baada ya vita vya pili vya dunia, U.S na U.S.S.R waliibuka washindi na hivyo kupelekea kuwa superpowers pekee duniani (kijeshi na kiuchumi). Lakini hawa jamaa walikuwa na itikadi tofauti sana hasa katika muonekano mpya wa kisiasa na kiuchumi duniani. Wamerekani walihubiri ubepari na wasoviet walihubiri ukomunisti. Kila mmoja aliamini kuwa mfumo wake ndio zitawezesha kuinua upya uchumi wa kidunia (mana vita viligharimu nchi nyingi sana kifedha, watu na mali). Hii tayari iliweka uhasama mana wote wababe na hakuna aliyekubali kushindwa. Kilichofuata hapo ni nani ataweza kushawishi nyingi zaidi zimuunge mkono katika hizo sera zake. Pia baada ya kulipuliwa kwa mabomu ya kiatomiki huko Japan, warusi walitia jitihada kubwa na hatimaye waliweza kutengeza ya kwao. Hii ndio mwanzo wa COLD WAR. Hii ilipelekea nchi ndogo hasa Africa, Asia na Amerika ya kusini kuwa katika hali flani ya tutoke vipi maana wasoviet wanakuja na sera zao na ahadi kibao, na hapo hapo warekani nao wanakuja na sera zao na ahadi kibao. Hii ilileta kuibuka vikundi na vuguvugu la kisiasa na kutetea sera tofauti na mara nyingine demokrasia iliposhindikana basi watu waliingia mwituni. Sababu kubwa ya kuchagua ipi ni ipi ilitofautiana nchi na nchi, historia ya taifa husika, jiografia na tamaduni za watu wake. Kumbuka pia mataifa mengine makubwa nayo tayari yalishachagua pande zao mapema kama China, Japan, Western Europe karibu nchi zote n.k. Pia hawa wababe walitumia mbinu kadhaa kutekeleza hiyo mipango yao kwa wale wabishi hata kupindua serikali na kuweka watu wao (puppet governments).
Tuendelee tuendelee mkuu
 
COLD WAR: Phase 5- THE INTERWAR PERIOD


"Not through speeches and majority decisions will the great questions of the day be decided - that was the great mistake of 1848 and 1849 - but by iron and blood" - Otto Von Bismarck

Kauli hii ilitajwa mwaka 1862 katika bunge la nchi ya Prussia ambapo mataifa yanayotengeneza nchi ya Ujerumani yalitaka kutengeneza muungano kwa njia ya kidemokrasia. Ikumbukwe hadi kufika mwaka 1871 Ujerumani ilikuwa ni muunganiko wa mataifa madogo zaidi ya 300 ambayo yaliunganishwa kwa mtutu wa bunduki. Katika kauli ya hapo juu ilitolewa na mwanasiasa wa Prussia ambaye alikuja kuwa Waziri mkuu wa Ujerumani pindi ilipomaliza kuungana. Alisema "Ujerumani kama taifa haliwezi kuunganishwa kwa kutumia njia za kidiplomasia bali kwa damu na chuma.


Maneno hayo yalionekana ni ya kishujaa kwa wakati ule na hata kwa vizazi vijavyo. Ujerumani ndiyo taifa pekee duniani ambalo hadi sasa limeweza kupigana vita na mataifa mengi wakati wa muunganiko wake bila kushindwa vita hata moja. Kuanzia miaka ya 1814 baada ya taifa la Ufaransa kupoteza nguvu na ushawishi wa kijeshi baada ya Mfalme Napoleon Bournaparte kushindwa vita ya Waterloo, nchi kama Austria, Denmark na Prussia ndizo zilikuwa na nguvu barani Ulaya. Ila Prussia iliweza kupigana na mataifa hayo yote mawili yalikuwa na nguvu Ulaya na kufanikiwa kuliunganisha taifa la Ujerumani.

Toka kipindi cha mwaka 1871 hadi mwaka 1914 wakati wa vita ya kwa kwanza ya dunia. Wajerumani waliamini taifa lao lina damu ya kipekee hasa ukikumbuka katika historia makabila ya kijerumani yalichangia sana kuangusha dola ya Mrumi. Kauli ya Otto Von Bismarck ilisemwa kwa nia njema sana lakini ilikuja kuleta laana kwa vizazi vingi vya baadae nchini Ujerumani.

Adolf Hitler aliitumia ile kauli kuwaahidi Wajerumani kwamba nchi yao itarudi katika Utukufu wa mwanzo na zaidi kwasababu hawatatawala tu Ulaya bali dunia nzima. Aliwaaminisha Wajerumani kuwa wao ni taifa teule na wahenga wao ndiyo biandamu halisi na mataifa mengine si kitu. Hitler alitamani mambo makubwa mengi, alitaka kutawala kuunganisha madola yote ya Ulaya lakini ikashindikana.

Ikumbukwe hata Rumi ilikuwa kubwa lakini haikutawala dunia nzima. Mfalme Alexander Mkuu wa Ugirki na Mfalme Napoleon wa Ufaransa walijaribu lakini hili halikuwezekana. Hitler aliamini kwamba yeye angeweza kufanya mambo ambayo wafalme wa dunia hii walishindwa huko nyuma. Kitu kimoja cha kukumbukwa na ambacho hata kwenye madarasa ya historia huwezi kukisoma ni kwamba Hitler pamoja na ukorofi wake wote aliwachukulia Wafaransa na Waingereza kama ndugu zake wenye damu moja . Wote hawa walikuwa ni Saxons au Makabila ya Kijerumani.

THE AGE OF APPEASEMENT AND FUTILE PEACE.

"With two lunatics like Mussolini and Hitler you can never be sure of anything. But I am determined to keep the country out of war." April 1936

“Huwezi kutegema chochote kutoka kwa wendawazimu kama Mussolini na Hitler. Lakini ninawiwa kuiepusha nchi yangu na vita” April 1936.

Hii ilikuwa ni kauli ya Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa wakati huo, bwana Stanley Baldwin.
Baada ya Hitler kuchukua madaraka Ujerumani alijenga mazingira ambayo yatamfanya awe na ushawishi mkubwa Ulaya kuliko taifa lingine lolote. Ulaya ilikuwa imeharibika kiuchumi na hawakutamani vita kwasababu waliona madhara ya vita ya kwanza ya dunia. Hitler alitumia hofu hii pamoja na huruma kwamba Ujerumani ilionewa kwenye Mkataba wa Versailles huko Ufaransa mwaka 1919 ili kufanikisha mambo yake.

Ukweli unaoshangaza ni kwamba baada ya mkataba kuisha mwaka 1919 huko Ufaransa Mkuu wa majeshi ya Ufaransa Marshal Ferdinand Foch alinukuliwa akisema “ Huu siyo mkataba wa Amani, bali ni mkataba wa kusitisha tuu mapigano kwa miaka 20” Alitabiri hivi akijua kwa mwenendo wa nchi za Ulaya vita nyingine lazima ingetokea tu, na kweli hakukosea. Aliamini Ujerumani itakuja kuinuka tena na kuleta madhara hivyo aliwaonya sana mataifa ya Ulaya kwamba huu mkataba ni adhabu ndogo sana kwa taifa jehuri kama Ujerumani.

Ferdinand Foch aliichukia Ujerumani kwasababu ilikuwepo kwenye Vita ya mwaka 1871 ambapo Mfaransa alipigwa na kunyang’anywa majimbo mawili muhimu. Tena kwenye vita ya kwanza alishuhudia jinsi Ufaransa inapata kipondo kutoka kwa Mjerumani.

Ukiangalia kwa undani haya mambo, utagundua tatizo lilikuwa si Ujerumani wala Hitler tatizo lilikuwa ni mfumo wa kibepari ambao mataifa ya Ulaya yalijijengea. Wazungu walijisikia utukufu sana pindi wakiona taifa lao ni tajiri kuliko jingine. Frantz Fanon mwanazuoni mweusi wa Ufaransa anasema chanzo cha vita siyo Mjerumani bali ni mfumo wa kibepari.

Ukiangalia katika masuala ya kiuchumi hasa katika ngazi za kimataifa utakuja kugundua kwamba mbali na sababu za kisiasa, kiutamaduni na kijamii vita za dunia zilisababishwa na mvutano wa kiuchumi huko Ulaya. Mfano mzuri hadi mwaka 1870 kulikuwa hakuna taifa la Ujerumani, uchumi ulikuwa chini ya Muingereza, Mfaransa na Austria. Ujerumani ilivyoinuka basi hii ikapelekea kuongezeka kwa changamoto za kimasoko huko Ulaya.

Mwaka 1933 Hitler aliitoa Ujerumani kwenye Umoja wa mataifa. Ambao ulikuwa na mkataba kwamba kila jambo litafutiwe suluhu bila vita. Aliamini kwenye kauli ya Bismarck “Through Iron and Blood”. Hakuishia hapo mwaka 1934 Hitler alipeleka vikosi vyake vya kijeshi kwenye mpaka wa kaskazini mwa Ufaransa maeneo ambayo Mkataba wa Versailles uliinyang’anya Ujerumani.

Sasa ili kumtuliza Hitler kwa kuogopa vita mataifa ya Ulaya yakiongozwa na Uingereza yalianzisha sera maarufu inayoitwa APPEASEMENT POLICY. Kwamba Hitler na mataifa mengine yaliyo makorofi yapewe tu maeneo watakayovamia ili tu kuzuia vita na kumridhisha Hitler. Hili lilikuwa kosa kwasababu lilimfanya Hitler ajiamini sana kwamba anaweza kufanya chochote kwasababu mataifa mengine yanamuogopa.

Appeasement policy ilikuwa sera ya hovyo kabisa kwasababu Waingereza na Wafaransa walikuwa radhi kuyagawa mataifa mengine ili mradi tu kujilinda wao na maslahi yao. Mfano mzuri ni katika sehemu zifuatazo:

  • Mwaka 1936 Hitler alivamia maeneo ya RHINE ambayo yaliwekwa yawe huru. Lakini waziri Mkuu wa Uingereza Stanley Baldwin mwaka 1935 akasema Ujerumani apewe tu ili kuzuia vita. Ikumbukwe maeneo ya RHINE ni mpaka wa Kaskazini mashariki wa nchi ya Ufaransa. Hitler alituma vikosi ili kuwapima Wafaransa na akasema ukiona majeshi ya Ufaransa yamejibu mapigo basi rudini. Lakini kwa bahati mbaya ufaransa hakujibu mapigo basi wajeumani wakaka pale na kuzidi kujijenga huku wakijua wanaogopwa.

  • Mwaka 1936 tena ililipuka vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Hispania na Ufaransa walitaka kwenda kuisaidia serikali ya Hispania lakini waziri mkuu wa Uingereza aliwashawishi sana wasihusike ili kuzuia matatizo na Ujerumani. Mwaka huo huo mataifa yakaitwa Uingereza ili kusaini mkataba ambao utayafanya yasihusike na vita. NON- INTERVENTION PACT. Matifa 27 yalisaini huo mkataba yakiwemo yale makubwa ya Ulaya.

  • Lakini chini kwa chini Hitler na Mussolini walipeleka msaada mkubwa wa kijeshi nchini Hispania ili kuwasaidia waasi wanaopinga serikali. Hivyo serikali ya Hispania ilivyopinduliwa basi Hitler na Mussolini walikubaliana na Serikali ya Jenerali Francis Franco kwamba ikitokea vita na Ufaransa basi waruhusiwe kujenga kambi za kijeshi nchini humo. Italy ilipeleka silaha nyingi sana huko Hispania. Ndege 130, Mabomu tani 2500, Mizinga 500 ya kuvuta(Canon), Bunduki Mizinga(Mortars) 700, Bunduki 12000, vifaru vidogo 50 na Magari 3800 ya kivita. Ili kuhadaa dunia silaha zote walizipitishia nchini Ureno.

  • Kambi ya Hitler ilizidi kuwa kubwa na kwa Upande wa pili Japan ilivamia Uchina mwaka 1931. Na serikali ya China ilienda kupeleka madai umoja wa mataifa wa wakati huo The LEAGUE OF NATIONS lakini hawkusikilizwa. Hitler na Mussolini wakawa Marafiki wa watawala wa Japan.

  • Mwaka 1936 Mussolini alivamia Ethiopia na kuitawala kwa muda lakini dunia nzima ikanyamaza huku Mafashisti wakiendelea kujitanua kwa nguvu.

  • Mwaka 1938 Hitler alivamia Czechslovakia akisema anaenda kutuliza ghasia na kulinda haki za binadamu zisivunjwe. Hapa napo Waziri mkuu mpya wa Uingereza Neville Chamberlain alienda hadi Ujerumani kumsikiliza Hitler akisema wamuachie Czechslovakia yote bila ubishi. Hitler baada ya kupewa Czechslovakia.

BY: MALCOM LUMUMBA a.k.a COBBLEPOTS

CC: Globu , Ziroseventytwo , mtoto wa bata , saidi yande , Bayyo , Mchumba , Tanzanite klm , Vlad , t blj , Walas Ba , majeshi 1981 , born again pagan , kireri jr , kilamuruzi , Victor wa happy , semper saratoga , MeinKempf , Erijo , mtembea kwa miguu , Nando , Gide MK , Amanito , Necha Lauwo , jay-millions , Ramark , kilwakivinje , WhySoSerious , Mwamba028 , eden kimario , Kabaunyeri , mkamangi2 , k_dizle , OME123 , Paw , kagombe , Mkereketwa_Huyu , mmmkme , cognition , Lazaroj , white-frank mhiro , mr letter , BATISTUTA , The hammer , Chakochangu , vErSatiLe , pyramid , Kyalow , Washawasha , Yusomwasha , maalimu shewedy , wambura marwa
 
COLD WAR: Phase 6- THE INTERWAR PHASE AND THE SOVIET REACTION TO APPEASEMENT POLICY

STALIN'S MOTTO : BRING YOUR FRIENDS CLOSE BUT YOUR ENEMIES MUCH CLOSER.

Upande wa pili wa sarafu Urusi chini ya Joseph Stalin walijua kabisa hata kama Appeasement Policy imepangwa kumtuliza Adolf Hitler lakini Warusi walijua sera hiyo ina malengo mawali makuu. Lengo la kwanza ni Kuepusha vita lakini lengo kuu lilikuwa na kumfanya Hitler azuie Ukomunisti usifike Ulaya Magharibi. Kwasbabu baada ya Vita ya kwanza ya Dunia mataifa mengi yalikubaliana na sera ya Ukomunisti. Hili mabepari hawakulipenda sana kwasababu walilichukulia kuwa na hatari kuliko hata Ufashisti.

Wakati wote wa Appeasement Policy Stalin ilibidi asijitenge na Ulaya kwasababu aliwachukulia watu wote wa Ulaya kama maadui wa Ukomunisti. Na hili lilikuwa kwasababu hata Hitler mwenyewe aliwahi kukiri akiwa anahutubia bunge lao kabla ya kuvamia Ufaransa mwaka 1939. Alisema :

“Germany has no further claims against France. I have always expressed to France my desire to bury forever our ancient enmity and bring together these two nations, both of which have such glorious pasts”. Akimaanisha kwamba haoni sababu yoyote kubwa ya Ujerumani na Ufaransa kuwa maadui na angependa mataifa haya yenye historia nzuri yaungane.

Na kwa Upande wa Uingereza Hitler ananukuliwa akisema “I have devoted no less effort to the achievement of Anglo-German understanding, no, more than that, of an Anglo-German friendship. At no time and in no place have I ever acted contrary to British interests. Why should this war in the West be fought? For the restoration of Poland? The Poland of the Versailles Treaty will never rise again”. Akimaanisha haoni sababu kwanini mataifa ya Ulaya Magharibi yapigane.

Stalin baada ya Kuona hivyo ilibidi aende Ulaya kwa Mkakati mkubwa kwamba “Bring your friends close, but your enemies much closer” Alijua ukweli kwamba Hitler hata kama ni Fashisti lakini ni bepari kama walivyo wengine. Hivyo alifanya yafuatayo ili kuwagawa wasiwe wamoja:

Mwaka 1934 Urusi ilijiunga na Umoja wa Mataifa wa wakati huo. (The League of Nations) Dhumuni lake kubwa ni kuwafanya wamzoee, asambaze ushwishi wake Ulaya na kubwa kabisa kuzuia vita isifike kwenye mlango wa Urusi.

Mwaka 1935 Urusi walienda kusaini mkataba wa Ulinzi ili kama na Ujerumani basi wasaidiane kama ilivyofanyika kwenye vita ya kwanza ya dunia. Lakini ikumbukwe kwamba Wafaransa walikuwa hawapendi Ukomunisti na pindi Wakomunisti wamepindua Urusi, Ufaransa, Marekani na Uingereza walikuwa upande wa Mabepari wa Urusi.

Mwaka 1936 Urusi alisaini NON-AGRESSION PACT ya kutoingilia vita ya Hispania lakini Stalin akijua kabisa dhumuni la Ulaya lilikuwa ni kuondoa Ukomunisti nchini Hispania. Kipindi hiki Hispania ilikuwa na Uongozi wa kikomunisti na kila kitu kilikuwa chini yao hivyo Moscow kichini chini alipeleka Majasusi wa NKVD baadae KGB ili kuwasaidia Wakomunisti wenzao. Ambapo Jasusi Alexander Orlov ndiye aliyetumwa kuratibu mambo yote huko Uhispania.

Urusi walipeleka ndege 1000, vifaru 900, vifaa 1500 vya bunduki mzinga, magari ya kijeshi 300, bunduki 15000, bunduki za kiautomatiki 30000, mizinga 30000, magobore 500000 na tani 30000 za risasi. Mbali na yote haya serikali ya kikomunisti ya kihispania ilishindwa vita mwaka 1939.

Mwaka 1939 Stalin Alipendekeza Uingereza, Ufaransa na Urusi watengeneze muungano wa kumpinga Hitler maana walijua lazima angevamia Poland kwasababu kuna Wayahudi wengi sana. Sasa kwa bahati mbaya mwezi April Waziri mkuu wa Uingereza Chamberlain alikataa kwasababu hakuwapenda sana Warusi kama nilivyosema kwenye aya za juu. Stalin alijua kabisa kwamba Urusi akitengeneza muungano na Uingereza na Ulaya Hitler asingevamia lakini baada ya kujua hawewezi kumuunga mkono basi inabidi afanye mkatba wa siri Hitler kwamba wao wasipigane ila waivamie Poland na kuigawa kati yao.

Mkataba kati ya Mrusi na Mjerumani haukudumu hata mwaka na matamanio ya Stalin yaliyeyuka na hofu zake kwamba Hitler angemvamia zilitimia. Hitler alisaini mkataba lakini chini kwa chini alikuwa anajiandaa kuwavamia Warusi chini ya Operesheni waliyoiita "THE MARCH TO THE EAST"
Mwaka 1939 Hitler alivamia Poland na hapo ndipo ukawa mwisho wa Appeasement Policy Muingereza na Mfaransa hawakukubaliana na Hitler japo hawakumwamini kabisa Stalin ilibidi tu waungane naye ili kumpinga Mjerumani ambaye kwa wakati huo ilishindikana kumtuliza kwa kutumia APPEASEMENT POLICY.

Mwaka 1939 vita inapoanza Marekani iliona kuwa hiyo ni nafasi ya kisiasa na ikaitangazia dunia kutofungamana na upande wowote ule. Ikumbukwe Marekani alikuwa anatumia ISOLATION POLICY au sera ya kujitenga, ambapo aliamini kwamba Marekani litakuwa taifa salama endapo tu halitajihusisha na mizozo na migogoro ya kisiasa ya Ulaya. Lakini alitumia Ujanja mkubwa wa kutoa mikopo na kuuza silaha nyingi kwa mataifa yote yaliyopigana vita.


BY: MALCOM LUMUMBA a.k.a COBBLEPOTS
 
HITIMISHO: INTRODUCTION TO COLD WAR AND RUSSIAN HISTORY.

Mpaka sasa nimefikia hitimisho ya sehemu ya kwanza kabisa ya historia ya Urusi.
Nimeeleza kwa upana kabisa ili kujenga msingi kwa ajili ya kupanua uelewa mkubwa juu ya vita baridi.
Kwenye bandiko langu la kwanza kuhusiana na historia ya Urusi ambalo ni bandiko #2, katika ukurasa wa kwanza, nimejaribu kuelezea kwa kikifupi mambo muhimu yaliyojiri kwenye vita vya pili vya dunia.
Tukijikumbusha ni kwamba Mataifa yaliyoibuka washindi ni Jamhuri ya Kisovyeti ya Urusi, Jamhuri ya Muungano wa nchi za Kimarekani na Ufalme Mkuu wa Uingereza.

Tokea kipindi hiki hadi mwaka 1956 wataalamu wanasema SUPER POWER alikuwa bado ni Muingereza lakini nchi yenye uchumi mkubwa kwa upande wa nchi za kibepari ilikuwa ni Marekani. Na katika hili Kwenye sehemu za mbele za nitaelezea kiundani zaidi. Mwaka 1945 ndipo Vita Baridi ilianza rasmi na chanzo ni sababu nilizojaribu kuzijenga na kuzielezea kwenye kurasa zilizopita. Kama ambavyo vita ya kwanza ya dunia ilisababishwa na mambo lukuki yaliyotokea kwenye karne ya kumi na tisa, basi vivyo hivyo VITA BARIDI alisababishwa na mambo yaliyotokea kwenye vita vya kwanza na vya pili vya dunia.

Mungu akitujalia tutanza na COLD WAR AND THE NEW WORLD ORDER. Hapa nitaelezea Vita Baridi ilivyoanza na nini hasa maana ya SUPER POWER; BALANCE OF POWER na NEW WORLD ORDER katika lugha za kisayansi ya siasa ili tupate kujua ukweli na tuweze kuwa huru. Pia, nitazungumzia mapinduzi katika uchumi wa dunia, sheria za haki za binadamu, mpangilio wa kijamii na sheria za kimataifa.
Lakini pia nitazungumzia mambo ya kijeshi mathalani mapinduzi ya kiteknolojia za kijeshi, mapinduzi katika nyanja nzima za ujasusi.

Ila kwa kudra za mwenyezi Mungu nitaweza kuzungumzia VITA BARIDI AFRICA hasa jinsi gani vilikuwa na ushawishi mkubwa kwenye siasa za Tanzania na Uchumi wa kijamaa hapa nchini. Tuatapitia baadhi ya vitabu vya kihistoria vya watu mbali mbali ili tuweze kuakisi mambo yalijificha kwa muda mrefu.
Niwashukuru sana ndugu zangu wote mliokuwa mkinisoma kwa utulivu mzuri, uvumilivu na subira nyingi japo majukumu yanakuwa yanabana na naweza kupotea kwa kitambo kidogo.
Kama mlivyonivumilia hapo juu basi naomba mnivumilie na sasa ninapoenda kuandika kuhusu vita baridi: Na kwa kipindi hiki nitajitahidi siku isipite bila kuleta hata bango la vimaneno hata 500 tu.

Popote mtakapoona nimekosea naomba msisite kunirekebisha kwasababu wote tupo hapa kwa ajili ya kujifunza, na hata mimi mtoa mada hii najifunza na nategemea sana uwepo wenu ninyi wasomaji hapa.
Natanguliza shukrani zangu zote.
Mbarikiwe sana na Alamsik.

BY: MALCOM LUMUMBA a.k.a COBBLEPOTS

CC: Gide MK , pyramid , Kabaunyeri , mtembea kwa miguu , born again pagan , MALCOM LUMUMBA , Washawasha , WhySoSerious , semper saratoga , MeinKempf , kilamuruzi , jay-millions , Bayyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom