Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,268
HISTORIA YA UONGOZI YA ALI HASSAN MWINYI KAMA RAIS HAIKO WAZI
UTANGULIZI
Makala hii nimeiandika baada ya kuulizwa maswali baada ya kufanya kipindi cha Maisha ya Rais Ali Hassan Mwinyi na Afrika TV2.
Najaribu hapo chini kujieleza.
Katika kipindi hiki cha televisheni yapo mengi katika maisha ya Rais Ali Hassan Mwinyi ambayo hayakuzungumzwa.
Pengine hayakuzungumzwa kwa kuwa mtayarishaji wa kipindi alipenda kumjua Sheikh Ali Hassan Mwinyi kwa upande wake mmoja tu kama Rais Muislam.
Hakutaka kuniingiza katika siasa.
Kwa uhakika hapa ndipo alipokazia katika maswali yake.
Huu ni upande mmoja wa historia ya Rais Mwinyi.
Upo upande mwengine wa Rais Mwinyi katika utawala wake.
Upande huu wa utawala wake unazunguka ndani ya serikali, unazunguka ndani ya CCM na mwisho unazunguka ndani ya taasisi zote nchini zenye uhusiano wa kuendesha nchi ukianzia vyama vya siasa hadi "argencies."
Hizi ni "ecological factors," mfano wa viumbe wanavyo uhusiana mazingira wanayoishi.
Mathalan ndani ya mbuga kuna majani ambacho ni chakula cha swala na kuna simba ambae chakula chake ni swala.
Simba kama hakula swala na swala wakawa wengi zaidi na majani ni yale yale mbuga si muda mrefu itakuwa jangwa.
Mbuga ikiwa jangwa simba na swala wote wataathirika.
Humu ndimo ilipo historia nyingine ya Rais Ali Hassan Mwinyi.
Historia hii inasisimua.
Historia hii Rais Mwinyi hakuieleza katika kitabu chake, "Mzee Rukhsa Safari ya Maisha Yangu."
Historia si kama haipo kabisa lakini alipoigusia alipita pembeni kama vile hataki kukanyaga ukoka wake alioupanda na kuutunza vizuri.
Kwani ikiwa atapita katikati ya ukoka wake kuna hatari ya kutengeneza njia na wengine watapita.
Hawa wengine wakipita patakuwa njia na uzuri wa ukoka utapotea, utanywea na kuwa mfano wa majani ya kawaida yaliyokauka.
Bustani itapoteza haiba yake yaani itapoteza uzuri wake.
Mengi Rais Mwinyi kayanyamazia ndani ya kitabu chake.
Haya hayakuwa mambo ya kawaida.
Naamini waliokuwa karibu na yeye katika serikali na CCM walishangaa kuona yale mazito na muhimu kwake karashiarashia na mengine hakuyasema kamwe.
Mlango bado uko wazi kwa watafiti na wanafunzi wa historia kulijaza ombwe hili.