Historia fupi ya mji wa ROMA

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,896
155,920
KWANINI MJI ULE ULIITWA ROMA?

Roma ni mji mkuu wa nchi ya Italy, ni mji wenye historia ndefu duniani... Kwa maana historia yoyote ya dunia haitokamilika kama hujaizungumzia au kutaja Neno Roma.

Roma imeanza kukaliwa na watu kwa zaidi ya miaka elfu 2 iliyopita. Ni mji wa 3 kwa umaarufu katika nchi za umoja wa ulaya na ndani ya mipaka ya Roma ndio unapata Vatican City ambayo ni makazi ya kiongozi mkuu wa kanisa katoliki (ukumbuke Vatican ni nchi inayojitegemea)

Wengine wanapenda kuiita Roma kama Mji mkuu wa nchi Mbili

Roma iliendea miaka mingi iliyopita tokea karne ya 3 walishakuwa na mtandao wa babrabara, chuo kikuu kilianzishwa mwaka 1303 na duka kubwa la kuuza bidhaa mbalimbali (shopping mall) zilianzishwa tokea mwaka 110

KWANINI MJI HUU ULIITWA ROMA?

Kwa mujibu wa hadithi za kale ambazo zimeaminiwa na baadhi ya watu asili na historia ya jina la mji huu unaturudisha mbali kabisa

Tunakutana na hadithi ya vijana mapacha Romulu na Remo waliozaliwa katika mji wa Alba Longa...Mama yao aliitwa Rhea Silvia ambaye alikuwa binti wa mfalme Numitor.

Mama wa Romulus na Remo aliyetakiwa kuwa kiongozi wa himaya hiyo aliondolewa na kaka yake aliyeitwa Amulius.

Kutokana na mashaka na wasiwasi wa kuona huenda hawa watoto mapacha watakuja kumpindua na kuchukua madaraka yake alituma miongoni mwa wasaidizi wake awaue Romulu na Remo ....lakini msaidizi huyo hakuwaua na badala yake aliwatia kwenye kikapu na kuwaacha kwenye mto Tevere

Watoto wale wakaokotwa na Mbweha wa kike na kuwalea kwa kuwanyonyesha maziwa yake na ndio maana kwenye nembo ya klabu ya Roma utaona kijimnyama kikiwa kinanyonyesha watoto maana yake wanaenzi historia hii

Romulu na Remo walikuwa na wakafanikiwa kurudi kwenye mji waliozaliwa wa Alba longa babu yao mfalme Numitor aliwatambua kisha akashirikiana nao kumuondoa madarakani mjomba wao Amulius na madaraka yakarudi tena kwa babu yao mfalme Numitor

Baada ya kazi hiyo kubwa waliamua kwenda kuanzisha mji wao

Katika kuanzisha huko mji wakatofautiana kwenye jina la mji watauitaje?? Kila mtu alikuwa na wazo Lake baadae wakapigana wenyewe kwa wenyewe na Romulu alifanikiwa kumuua Remo

Na hapo ndipo aliamua kuupa jina lake mji huo mpya

Tokea wakati huo mji ukawaitwa Roma

Na hii ndio asili ya jina la mji wa Roma
 
original name is from the Sanskrit word डोम, doma and means a member of the Dom caste of travelling musicians and dancers
 
Bwana gilLeSi hii chai ni ya kitumbua au chapati?
 
1713374926424.png
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom