Nani atashinda vita ya rangi ya bluu kati ya Yanga na Simba?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,132
7,903
Kuna mengi yanaongelewa mpaka sasa kuhusiana na jezi mpya za Yanga chini ya udhamini wa Haier. Sitagusia kuhusu migogoro hiyo ya mikataba ila nitaongelea kuhusu uchaguzi wa rangi ya blue katika moja ya jezi hizo.

Msimu uliopita Simba kwa mara ya kwanza walitambulisha jezi zenye mchanganyiko wa rangi mbalimbali ambazo hapo kabla hawakuwa wanazitumia huku katika jezi mojawapo blue ikiwa ndiyo rangi inayochukua sehemu kubwa. Jezi hizo Simba wamekuwa wanazitumia katika mazoezi.

Simba Queens sijajua walianza lini ila wameanza rasmi kuzitumia jezi hizo za blue katika mechi zao. Inawezekana kabisa kuwa Simba kwa kuwa walionyesha blue kuwa ni rangi wanayoikubali walikuwa kwenye mipango ya kuintroduce jezi za blue kwa timu ya wanaume pia na Yanga wamefanya tu kuwapiku na inawezekana ilichangia wao kuwa na munkari ya kuzileta jezi hizi wakati bado hawajakubaliana na SportPesa. Inawezekana waliona wakichelewa tu itakula kwao.

20230202_133429.jpg

Nadhani pia Yanga wanaenda kuachana rasmi na rangi za kijani na njano. Hizi siyo rangi nzuri kwenye soka ndyo maana timu chache sana kubwa duniani zimewahi kuzitumia. Uwanjani, wachezaji hawaonekani vizuri maana rangi za jezi zinashindana na majani ya uwanjani.

Na hata kwenye mavazi ya kawaida au yale rasmi kama masuti au magauni na hata masuruwali rangi hizo hazivaliwi sana. Ndiyo maana si ajabu tulivyoona mashabiki wa Yanga kuzikubali zaidi jezi mpya za blue kuliko zingine.

Siyo jambo geni kwa timu kubwa za ligi moja kuvaa jezi zinazofanana rangi. Huko EPL tumeona Man U, Liverpool na Arsenal wote wamekuwa watumiaji wa rangi nyekundu na nyeupe. Je tutegemee hivi karibuni kwa Simba na Yanga wote kuwa na nyuzi za blue? Mabadiliko haya yatamaanisha nini katika soka letu?
 
View attachment 2503614

kasome katiba ya uto
Ibara ya 3
 
Attachments

  • 62D9814A-B634-47BE-8607-42EEC83E42CF.png
    62D9814A-B634-47BE-8607-42EEC83E42CF.png
    14.5 KB · Views: 11
wabongo kila kitu kinachambuliwa sasa hivi mmeanza kuchambua rangi! Yanga kutengeneza rangi ya blue imekua ngongwa, inataka kuonekakana amewaiga Simba wakati Azam FC, Dodoma FC, Singida,JKT Tanzania wamekua wakitumia hizo rangi mda mrefu
 
Kuna mengi yanaongelewa mpaka sasa kuhusiana na jezi mpya za Yanga chini ya udhamini wa Haier. Sitagusia kuhusu migogoro hiyo ya mikataba ila nitaongelea kuhusu uchaguzi wa rangi ya blue katika moja ya jezi hizo.

Msimu uliopita Simba kwa mara ya kwanza walitambulisha jezi zenye mchanganyiko wa rangi mbalimbali ambazo hapo kabla hawakuwa wanazitumia huku katika jezi mojawapo blue ikiwa ndiyo rangi inayochukua sehemu kubwa. Jezi hizo Simba wamekuwa wanazitumia katika mazoezi.

Simba Queens sijajua walianza lini ila wameanza rasmi kuzitumia jezi hizo za blue katika mechi zao. Inawezekana kabisa kuwa Simba kwa kuwa walionyesha blue kuwa ni rangi wanayoikubali walikuwa kwenye mipango ya kuintroduce jezi za blue kwa timu ya wanaume pia na Yanga wamefanya tu kuwapiku na inawezekana ilichangia wao kuwa na munkari ya kuzileta jezi hizi wakati bado hawajakubaliana na SportPesa. Inawezekana waliona wakichelewa tu itakula kwao.

View attachment 2503614
Nadhani pia Yanga wanaenda kuachana rasmi na rangi za kijani na njano. Hizi siyo rangi nzuri kwenye soka ndyo maana timu chache sana kubwa duniani zimewahi kuzitumia. Uwanjani, wachezaji hawaonekani vizuri maana rangi za jezi zinashindana na majani ya uwanjani.

Na hata kwenye mavazi ya kawaida au yale rasmi kama masuti au magauni na hata masuruwali rangi hizo hazivaliwi sana. Ndiyo maana si ajabu tulivyoona mashabiki wa Yanga kuzikubali zaidi jezi mpya za blue kuliko zingine.

Siyo jambo geni kwa timu kubwa za ligi moja kuvaa jezi zinazofanana rangi. Huko EPL tumeona Man U, Liverpool na Arsenal wote wamekuwa watumiaji wa rangi nyekundu na nyeupe. Je tutegemee hivi karibuni kwa Simba na Yanga wote kuwa na nyuzi za blue? Mabadiliko haya yatamaanisha nini katika soka letu?
kn kitu umeniongezea,merci
 
Back
Top Bottom