Jezi ya Yanga yatumika katika wimbo rasmi wa AFCON badala ya Jezi Rasmi ya Taifa Stars

DullyJr

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
13,979
11,816
Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania ’Taifa Stars’ imefuzu kwa AFCON 2023 ambayo itachezwa 2024 kule Ivory Coast, hii ni mara ya 3 Tanzania kufuzu baada ya 1980 na 2019.

Kuelekea fainali hizo za mwaka huu zitakzofanyika mwakani, CAF wameamua kutengeneza wimbo maalumu wa mashindano, ambapo kwenye muziki huo washiriki wametumia Jezi za Mataifa Shiriki isipokuwa Tanzania ambapo jezi ya Klabu ya Yanga imetumika na sio jezi ya Taifa Stars!

Maswali ni mengi juu ya kwanini jezi ya Yanga na sio ya Taifa Stars?

Habari za uhakika zinasema hata TFF hawajui kwanini imetumika jezi ya Yanga kwenye huo wimbo na si jezi ya Stars.

Inasemekana TFF wamewaandikia CAF wakitaka maelezo kwanini imetumika jezi ya Yanga kwenye huo wimbo na sio jezi za Stars ambazo zinatengenezwa na Sandaland.

Nimejiuliza sana na sijapata jibu CAF wamepataje jezi kutoka Tanzania kama nchi shiriki bila kuwasiliana na TFF? Utaratibu wa mawasiliano (channel of communication) imebadilika kwamba CAF huwa wanawasiliana na wanachama wao (mashirikisho) sio vilabu au watu binafsi?

Aibu iliyoje, kama TFF hawajui CAF wamepataje jezi ya Yanga badala ya Stars, manake CAF wameipata kwa mtu wa mtaani ambaye kwa makusudi ameamua kupeleka jezi ya Yanga, Aibu. Tangu lini jezi ya nchi ikawa na tangazo la mdhamini mbele kama inavyoonekana jezi ya Yanga?

Maana yake CAF wamesahau au hawajui taratibu zao wenyewe? Je, kuna syndicate hapo kati ya maafisa wa CAF na huyo aliyepeleka jezi au kuna watu wa TFF wamehusika bila wakubwa kujua?

Nini ilikuwa nia ya aliyepeleka jezi ya Yanga badala ya Stars? Aliyepeleka amefanya kwa bahati mbaya, mapenzi kwa klabu yake,ushamba na ujinga wake au maelekezo maalumu? Kama maelekezo ni kutoka kwa nani ambaye anadhani jezi ya Yanga inaweza ikaibadili ya Stars?

Timu ya Taifa ni nembo na alama ya nchi, rangi ya jezi zake zinaakisi raangi ya Bendera ya Taifa, huu ujinga wa kupeleka jezi ya klabu unaleta tafsiri mbaya kwakuwa Stars ni timu ya Watanzania wote ila Yanga ni timu ya baadhi ya Watanzania tu, itapelekea chuki kwa timu bila sababu za msingi kwa wale ambao hawaipendi Yanga.

CAF &TFF Watanzania wanahitaji majibu Haraka.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)
 
Bila kuweka picha ya jezi ya Yanga iliyotumika huu Uzi unakuwa kama umeandikwa na mlevi aliyekunywa K-vant kubwa mbili peke yake akaamkia Jamii Forums. Kwanini usiweke picha unaogopa nini!?
Tulia wewe kiazi sio unaropoka kama upo katika siku zako

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania ’Taifa Stars’ imefuzu kwa AFCON 2023 ambayo itachezwa 2024 kule Ivory Coast, hii ni mara ya 3 Tanzania kufuzu baada ya 1980 na 2019.

Kuelekea fainali hizo za mwaka huu zitakzofanyika mwakani, CAF wameamua kutengeneza wimbo maalumu wa mashindano, ambapo kwenye muziki huo washiriki wametumia Jezi za Mataifa Shiriki isipokuwa Tanzania ambapo jezi ya Klabu ya Yanga imetumika na sio jezi ya Taifa Stars!

Maswali ni mengi juu ya kwanini jezi ya Yanga na sio ya Taifa Stars?

Habari za uhakika zinasema hata TFF hawajui kwanini imetumika jezi ya Yanga kwenye huo wimbo na si jezi ya Stars.

Inasemekana TFF wamewaandikia CAF wakitaka maelezo kwanini imetumika jezi ya Yanga kwenye huo wimbo na sio jezi za Stars ambazo zinatengenezwa na Sandaland.

Nimejiuliza sana na sijapata jibu CAF wamepataje jezi kutoka Tanzania kama nchi shiriki bila kuwasiliana na TFF? Utaratibu wa mawasiliano (channel of communication) imebadilika kwamba CAF huwa wanawasiliana na wanachama wao (mashirikisho) sio vilabu au watu binafsi?

Aibu iliyoje, kama TFF hawajui CAF wamepataje jezi ya Yanga badala ya Stars, manake CAF wameipata kwa mtu wa mtaani ambaye kwa makusudi ameamua kupeleka jezi ya Yanga, Aibu. Tangu lini jezi ya nchi ikawa na tangazo la mdhamini mbele kama inavyoonekana jezi ya Yanga?

Maana yake CAF wamesahau au hawajui taratibu zao wenyewe? Je, kuna syndicate hapo kati ya maafisa wa CAF na huyo aliyepeleka jezi au kuna watu wa TFF wamehusika bila wakubwa kujua?

Nini ilikuwa nia ya aliyepeleka jezi ya Yanga badala ya Stars? Aliyepeleka amefanya kwa bahati mbaya, mapenzi kwa klabu yake,ushamba na ujinga wake au maelekezo maalumu? Kama maelekezo ni kutoka kwa nani ambaye anadhani jezi ya Yanga inaweza ikaibadili ya Stars?

Timu ya Taifa ni nembo na alama ya nchi, rangi ya jezi zake zinaakisi raangi ya Bendera ya Taifa, huu ujinga wa kupeleka jezi ya klabu unaleta tafsiri mbaya kwakuwa Stars ni timu ya Watanzania wote ila Yanga ni timu ya baadhi ya Watanzania tu, itapelekea chuki kwa timu bila sababu za msingi kwa wale ambao hawaipendi Yanga.

CAF &TFF Watanzania wanahitaji majibu Haraka.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)
Mwanaume una wivu kama mwanamke, Hahaaa. Na bado we endelea kuichukia Yanga ipo siku utakunywa sumu ufe, shauri yako.
 
CAF wanajua huku Tanzania timu ni Yanga Tu maana ndo waliiona ikicheza Fainali ndio maana wakaona sio mbaya jezi yake ikiwaakilisha Tanzania
 
Bila ushahidi wa picha au video ya wimbo husika huu uzi hauna maana yeyote, lete ushahidi tuone
 
Imepelekwa jersey ya YANGA kwasababu ndio nembo ya Taifa (currently,YANGA inamafanikio zaidi kuliko Taifa Stars).
 
CAF hawakutumia "jezi ya Yanga" tu, bali walitumia "jezi mbili za Yanga"
1701933956135.png
pamoja na "Supu Day" ya Yanga pia.

1701933854120.png
 
Waafrika tangu lini tumekuwa serious? Hapo kuna mtu alipewa rushwa apitishe huo ujinga ili kufurahisha wajinga wenzake. Mwisho wa siku hivyo vipande vitabadilishwa, sasa watakuwa wamefaidika na nini? Kazi ya pesa chafu hii.
 
Back
Top Bottom