Nani atakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa endapo Dr. Magufuli atashindwa Urais wa Tanzania?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
CCM tangu kuanzishwa kwake imekuwa na desturi ya kuongozwa na Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jambo hilo limetokea kwakuwa CCM imekuwa ikishinda kwenye uchaguzi na kutoa Rais.

Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Utamaduni na utaratibu huo ulimhusu pia Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa. Hata sasa,Rais Jakaya Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Uenyekiti wa Rais Kikwete unakoma mwaka 2017 kwakuwa alichaguliwa mwaka 2012 kwa mara ya pili ya miaka mitano. Sasa,uenyekiti wa CCM Taifa utakuwaje au nani atakuwa Mwenyekiti endapo Dr. John Magufuli atashindwa kwenye Urais hapo Oktoba 25?
 
Baada ya oktoba CCM kinakufa rasmi kama KANU.... Wengi wa wanachama wa CCM ni wanafiki watajiunga Ukawa
 
Nadhani kwa sasa mngekua mnaulizana, nini kitachoendelea baada ya kushindwa uchaguzi huu, kila mtu akiondoka na mbao zake, nini kutabakia pale ufipa??
 
CCM tangu kuanzishwa kwake imekuwa na desturi ya kuongozwa na Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jambo hilo limetokea kwakuwa CCM imekuwa ikishinda kwenye uchaguzi na kutoa Rais.

Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Utamaduni na utaratibu huo ulimhusu pia Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa. Hata sasa,Rais Jakaya Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Uenyekiti wa Rais Kikwete unakoma mwaka 2017 kwakuwa alichaguliwa mwaka 2012 kwa mara ya pili ya miaka mitano. Sasa,uenyekiti wa CCM Taifa utakuwaje au nani atakuwa Mwenyekiti endapo Dr. John Magufuli atashindwa kwenye Urais hapo Oktoba 25?

Thread zingine zinasikitisha sana. Huna kingine cha kufanya?
 
Mwisho wa upinzani nchini unatabiriwa lowasa kaja kuua upinzani sumaye oya oya tu hana ishus ajiandae kufilisiwa mali zote alizopora
 
Hatuvuki Bahari Kabla Hatujaifikia,mwenyekiti Wetu Ni Jakaya.K Akishamaliza Muda Wake Tutatafakari Nan Apokee Kijiti Lakin Kwa Sasa Jasho Na Damu,ucku Na Mchana Ni Kuhakikisha Magufuli Anaingia Ikulu Kwanza...
 
Hizi ndo nyuzi tulizozizoea JF,zinafikirisha.Kwanza ndo itakuwa mara ya kwanza cccm wanafanya uchaguzi wa mwenyekiti toka chama kianzishwe,pili itakuwa ngumu kumpata volunteer wa kujitolea kipindi hicho kwani tayari wanachama wao watakuwa waoga wa kujaribu (kumbuka sasa ni nguvu tu zinatumika),kwa ninavyoona mmoja wa watoto wa vigogo atatupiwa mfupa kwa lazima,halafu kinafia rasmi kwenye chaguzi za mitaa
 
Back
Top Bottom