DOKEZO Nani alitoa Kibali cha Ujenzi kwa anayejenga Eneo la Mkondo wa Maji katika Mtaa wa Kibugumo, Kigamboni?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Baadhi ya sisi Wakazi wa Mtaa wa Kibugumo Wilaya ya Kigamboni pembezoni na ilipo Sheli ya Puma hapa Dar es Salaam kuna mwekezaji ameziba njia ya maji hali ambayo imetufanya tunaoishi maeneo ya karibu na eneo hilo kuingiwa na hofu endapo mvua kubwa zikinyesha basi mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi kwa kuzingirwa na maji.

Kwanza kabisa katika eneo hilo kimemwaga kifusi na mchakato unaendelea, ni kama vile anayesimamia shoo hapo anazidi kuendelea na mchakato wake kama kawaida.

Awali, kabla ya Mwaka 2021 (wakati wa utawala wa Rais Magufuli), mwekezaji huyo alionesha dalili ya kuanza ujenzi kwenye eneo hilo lakini mchakato ulikwama na inadaiwa alikuwa ‘wanted’, tunashangaa amerudi kwa kasi na kuendeleza kile alichokipanga awali.

Mwekezaji alipoanza kumwaga vifusi, kuna viongozi mbalimbali walifika eneo hilo na kumtaka atambue njia ya maji, lakini hajali.
photo_2023-11-06_08-51-43 (2).jpg

photo_2023-11-06_08-51-43.jpg

photo_2023-11-06_08-51-42 (2).jpg
Kuziba njia ya maji au kuweka miundombinu ya aina yoyote bila kuzingatia njia ya maji yanapotakiwa kupita ni kuhatarisha usalama wa raia na makazi yao.

Mvua hizi zilizoanza hivi karibuni zimeanza kusababisha maji kuja kwenye makazi yetu, eneo lote likizibwa pia hali itakuwaje sasa?

Mbali na hapo, makazi ambayo yapo nyuma ya Sheli ya Puma yapo hatarini kuzingirwa na maji.

Hakuna mitaro ya maji kwenye maeneo hayo, hivyo kunaweza kuongeza ukubwa wa changamoto kwa sababu mvua zikinywesha maji yanasambaa kwenye makazi kutokana kukosa njia rasmi.

Kadhia hasa kwa watoto wa shule inakuwa kubwa kutokana na maji kujaa njiani na kwenye baadhi ya makazi.

Sisi tuna hofu uenda kuna watu wamechukua rushwa, kwanini kipindi kile tulilalamika zoezi lililokuwa likiendelea likasitishwa, sasa wamekuja kwa kasi vifusi vinamwagwa lakini tuna viongozi ambao wanajua hili suala lakini wapo kimya.
photo_2023-11-09_17-22-01.jpg

photo_2023-11-09_17-21-45.jpg
Mara tunasikia maneno kwamba atajenga njia nyingine ya maji kupita lakini haya ni maneno tu sidhani kama kuna ukweli, sisi tunachoomba mamlaka ziingilie kati tujue imekuwaje akaruhusiwa kufanya ujenzi pale maana kuna dalili kuna ujenzi utaanza hivi karibuni maana tayari wameweka vifusi.

==== ==== ====

Maelezo ya Serikali za Mtaa walipozungumza na Waandishi wa habari hivi karibuni...

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kibugumo, Yusuf Seleman Tindwa alisema wanalifahamu suala hilo kama kero na wamewahi kuchukua hatua kwa kukutana na wahusika wanaotaka kuwekeza eneo hilo.

"Tuliwafuata walitujibu kuwa wamepewa vibali vyote, wakasema kama kuna chochote twende mbele wao wakasimamia msimamo wao kuwa wamefuata utaratibu unaohitajika, na sisi tuliwaambia pamoja na kuwa na vibali vyote lakini tuangalie ubinadamu.

"Ni kweli katika eneo hili mvua ikinyesha maji yanajaa kuna sehemu tunaweka vifusi lakini bado, na sisi tunajiuliza hawajaona kama sehemu hiyo inaweza kuleta tatizo maana hatukushirikishwa."

==== ====

1. Sasa kama hadi viongozi wa Serikali za Mtaa nao wanahoji, nani ametoa vibali?
2. Inamaana aliyetoa hajaona umuhimu wa kushirikisha Serikali za Mtaa?
3. Hawaoni madhara yanayoweza kujitokeza?
4. Huyu Mwekezaji anayejenga hapo ni nani na mbona ana jeuri sana?
 
Mkuu haki inatafutwa kwenye streets battle sio humu, soma hili...kujaa kwa maji pale Jangwani hadi kigogo, kumesababishwa na royal families kujenga pale mikokoni, ujenzi ule umeathiri mkondo wa maji wa kiasili kwa mto msimbazi kuingia baharini (karibu na daraja la slander),kulalama humu hakutakusaidia wewe na wenzako, mnatakiwa kufanya push back
 
Back
Top Bottom