Tabata Dar es Salaam: Nani ametoa Kibali cha Vituo 3 vya Mafuta kujengwa ndani ya eneo la Makazi tena chini ya umbali unaotakiwa?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121

Kuna vitu nchi hii vinafanyika kihuni sana. Hivi nani anatoa kibali kujenga Vituo vya Mafuta bila kujali umbali unaotakiwa wala kuangalia athari kwa makazi ya watu? Pale Baracuda Tabata kuna Vituo vitatu vinajengwa ndani ya eneo moja tena vimekaribiana mno kiasi ambacho unajiuliza kwanini hatua hazichukuliwi kwa wahusika?

Pale kuna Ofisi ya Mtendaji, Diwani na Serikali za Mitaa wanaona kabisa kinachofanyika lakini wamekaa kimya ujenzi unaendelea. Kuna kituo cha Meru kimejengwa chini ya Miezi 3 na kimeanza kazi huku vingine vikiendelea na ujenzi usiozingatia sheria.

Ni muda sasa Waziri Jerry Slaa afike katika eno hilo na kuchukua hatua za haraka kunusuru usalama wa watu na kuangalia wanaohusika kutoa vibali wanavyofanya uhuni.
 
Mkuu fanyeni push back,mama wa vichenji alikomaa na RC mpaka kile kituo kikaondolewa, nanyi pia fanyeni push back sio kulalama humu, angalia pale Mafinga, ukitokea Sao Hill hadi Kinanyambo roughly 10km, kuna vituo 12 vya petrol ⛽️/diesel, hii ni craze
 
Kuna umbali gani kati ya kituo na kituo?
kile cha barakuda na cha tabata mangumi sidhani kama kilomota moja inazidi au hata kufika kabisa, na kile olimpic pale karibu na kwa bibi (segerea) haizidi kilomita moja. kwa kifupi kutoka kituo cha kwanza, cha pili na cha tatu kuna umbali wa kama kilomita 2 tu.
 
Kuna vitu nchi hii vinafanyika kihuni sana. Hivi nani anatoa kibali kujenga Vituo vya Mafuta bila kujali umbali unaotakiwa wala kuangalia athari kwa makazi ya watu? Pale Baracuda Tabata kuna Vituo vitatu vinajengwa ndani ya eneo moja tena vimekaribiana mno kiasi ambacho unajiuliza kwanini hatua hazichukuliwi kwa wahusika?

Pale kuna Ofisi ya Mtendaji, Diwani na Serikali za Mitaa wanaona kabisa kinachofanyika lakini wamekaa kimya ujenzi unaendelea. Kuna kituo cha Meru kimejengwa chini ya Miezi 3 na kimeanza kazi huku vingine vikiendelea na ujenzi usiozingatia sheria.

Ni muda sasa Waziri Jerry Slaa afike katika eno hilo na kuchukua hatua za haraka kunusuru usalama wa watu na kuangalia wanaohusika kutoa vibali wanavyofanya uhuni.
Hivi na pale opposite na Kitambaa Cheupe Night Club/Pub Tabata hiyo hiyo kinachojengwa pale pia ni kituo cha mafuta au ni kituko gani? Kama ni kituo cha mafuta basi nchi hii haina wasimamizi wa sheria ila wapindisha sheria.
 
Ukiona mambo yanaenda shagalabagala sheria zinavunjwa na wenye pesa popote duniani jua utawala uliopo madarakani ndio umeruhusu huo uvunjwaji wa sheria ufanywe, kibibi ndio kinasababisha yote haya, sio huko tu ndugu, kimara vimejengwa viwili ndani ya 2km katikati ya makazi ya watu.
 
kile cha barakuda na cha tabata mangumi sidhani kama kilomota moja inazidi au hata kufika kabisa, na kile olimpic pale karibu na kwa bibi (segerea) haizidi kilomita moja. kwa kifupi kutoka kituo cha kwanza, cha pili na cha tatu kuna umbali wa kama kilomita 2 tu.
Unajua sheria ni umbali gani kati ya kituo na kituo? Hii ni kwa upande mmoja wa barabara.
 
Msichangie kwa hisia. Sheria inaruhusu kituo na kituo kuwa na umbali wa mita 200 tu vikiwa upande mmoja wa barabara. Mjenzi wala havunji sheria, labda walioweka sheria ndio wamekosea{wabunge wenu}
 
Back
Top Bottom