Nani alitarajia kina Halima Mdee wangesaliti vyama vyao?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Usemi kwamba "adui yako mwombese njaa" una mantiki kubwa sana. Hakuna mbabe wa njaa.

Nani alitarajia kuwa Halima Mdee angepingana na Mwenyekiti wa Chama kilichomlea kisiasa hadi kuwa maarufu kwenye medani za siasa za Tanzania? Alikuwa ni mmoja wa wanachama ambao CHADEMA ilikuwa ikimjivunia kuwa nao.

Lakini alipoona mrija wa ulaji wake upo mikononi mwa watawala, ilimlazimu akubali kuwasikiliza wao badala ya Chama kilichomfunza Siasa.
 
Nani alidhani kuwa David Kafulila , aliyewahi kuitwa tumbili baada ya yeye kumwita Waziri mwizi kisa kashfa ya ufisadi aliyoifichua? Lakini baada ya kulala "njaa" kwa muda, aliamua kuomba wimbo wa walioshiba ili na yeye akaribishwe kwenye meza ya wenye chakula, na hatimaye ikawa hivyo. Jitihada zake zilizaa matunda na kufanikiwa kuonja teuzi za Rais.
 
Inasemekana Wakurya ni watu wenye misimamo sana, hivyo si rahisi kununulika. Wapo tayari kufa lakini si kuwa wasaliti.

Lakini hiyo lugha ilibadikika kwa Mwita Waitara. Ingawa alikuwa ni Mwanachama wa CHADEMA, alipoona kuwa Magufuli kadhamiria kuwamiliki wabunge wote, aliamua kujisalimisha zake mapemaaa!

Sasa hivi kashasahau animba wimbo wa "wembe ni ule ule..."
 
Aliyenichekesha zaidi ni Dr. Godwin Mollel. Yeye siyo kwamba aliikimbia tu CHADEMA, lakini aligeuka pia mwiba mkali ingawa haukuonekana kuwa na madhara sana CHADEMA. Yeye ni miongoni mwa wanasiasa waliodai kuwa Mbowe ndiye aliyemshambulia Lissu kwa risasi.

Huyo ni Daktari, lakini hana misimamo ya kisomi.

Au mtu akishaingia kwenye Siasa anazaliwa kwa namna nyingine kiasi cha kusahahu miiko yake ya kitaaluma?
 
Usemi kwamba "adui yako mwombese njaa" una mantiki kubwa sana. Hakuna mbabe wa njaa.

Nani alitarajia kuwa Halima Mdee angepingana na Mwenyekiti wa Chama kilichomlea kisiasa hadi kuwa maarufu kwenye medani za siasa za Tanzania? Alikuwa ni mmoja wa wanachama ambao CHADEMA ilikuwa ikimjivunia kuwa nao. Lakini alipoona mrija wa ulaji wake upo mikononi mwa watawala, ilimlazimu akubali kuwasikiliza wao badala ya Chama kilichomfunza Siasa.
Mdee alifanya la maana sana kupinga udikteta wa Mbowe.

Mdee ni shujaaa, mwanamke wa shoka

Njaa ndiyo imemfanya mbowe kuanza kupokea ruzuku inayotokana na wabunge aliowaita haramu
 
Mdee alifanya la maana sana kupinga udikteta wa Mbowe.

Mdee ni shujaaa, mwanamke wa shoka

Njaa ndiyo imemfanya mbowe kuanza kupokea ruzuku inayotokana na wabunge aliowaita haramu
Aisee!
 
Nani alidhani kuwa David Kafulila , aliyewahi kuitwa tumbili baada ya yeye kumwita Waziri mwizi kisa kashfa ya ufisadi aliyoifichua? Lakini baada ya kulala "njaa" kwa muda, aliamua kuomba wimbo wa walioshiba ili na yeye akaribishwe kwenye meza ya wenye chakula, na hatimaye ikawa hivyo. Jitihada zake zilizaa matunda na kufanikiwa kuonja teuzi za Rais.
Hamwezi kumshinda "SHETANI" kwa akili zenu wenyewe.
 
Siasa za kweli na zenye manufaa kwa jamii na nchi zahitaji watu waliokomaa na wanaojua mahitaji ya jamii na nchi badala ya maigizo ya kukariri, kutafuta maisha na umaarufu.
Hata hivyo, tulitaka hao wanawake waliomalizia pesa zao kwenye kampeni, Magufuli amebana siasa za upinzani (mbunge mmoja tu), washindwe hata kumudu mahitaji ya kawaida katikati ya misukosuko ya kisiasa? Uamuzi wao ulikuwa wa kipekee kwao (afadhali lawama kuliko fedheha). Kwao ilikuwa mapambano ya kufa na kupona kwa maisha baada ya uchaguzi.
Halima alikuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda na alijiamini.
Tatizo kubwa kwa hao wanaume waliosaliti vyama vyao.
Ni watu wa kuwekwa kwenye kundi kama walivyo na kukaa nao kwa akili.
 
Mdee alifanya la maana sana kupinga udikteta wa Mbowe.

Mdee ni shujaaa, mwanamke wa shoka

Njaa ndiyo imemfanya mbowe kuanza kupokea ruzuku inayotokana na wabunge aliowaita haramu
Shujaa hufanya mambo yake hadharani na siyo gizani.Mdee alifanya mambo yake gizani hivyo hana ushujaa wowote.
 
Mdee alifanya la maana sana kupinga udikteta wa Mbowe.

Mdee ni shujaaa, mwanamke wa shoka

Njaa ndiyo imemfanya mbowe kuanza kupokea ruzuku inayotokana na wabunge aliowaita haramu
Shujaa hufanya mambo yake hadharani na siyo gizani.Mdee alifanya mambo yake gizani hivyo hana ushujaa wowote.
 
Usemi kwamba "adui yako mwombese njaa" una mantiki kubwa sana. Hakuna mbabe wa njaa.

Nani alitarajia kuwa Halima Mdee angepingana na Mwenyekiti wa Chama kilichomlea kisiasa hadi kuwa maarufu kwenye medani za siasa za Tanzania? Alikuwa ni mmoja wa wanachama ambao CHADEMA ilikuwa ikimjivunia kuwa nao.

Lakini alipoona mrija wa ulaji wake upo mikononi mwa watawala, ilimlazimu akubali kuwasikiliza wao badala ya Chama kilichomfunza Siasa.
🔊👍🙏
 
Mdee alifanya la maana sana kupinga udikteta wa Mbowe.

Mdee ni shujaaa, mwanamke wa shoka

Njaa ndiyo imemfanya mbowe kuanza kupokea ruzuku inayotokana na wabunge aliowaita haramu
🤔⁉️
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kustaajabu usaliti wa mwanasiasa.

Mwanasiasa na kahaba tofauti yao ni ndogo tu, jinsi gani wanafanya ukahaba wao.

Kauli/ahadi/utiifu wa mwanasiasa hauna thamani yeyote maana mwisho wa siku atakwambia unachotaka kusikia na kufanya kinachomnufaisha.

Haitokuwa ajabu hata Samia akija kuhamia CHADEMA mbeleni ikiwa kuna manufaa nae. Hivyo hakuna la ajabu kwenye siasa, hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa milele.

Ulishawahi hata kuwaza kuwa Lowassa angeweza kwenda CHADEMA?
Siasa ni biashara kama ilivyo mpira. Mchezaji wa simba leo kuchezea yanga kesho ni kawaida kabisa.
 
Back
Top Bottom