Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Kumekuwa na mijadala mirefu inayoendelea nchini, Kwa wananchi kujiuliza, hivi kuruhusiwa Kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa, ni nani watakaofaidika zaidi, je ni CCM au vyama vya upinzani?
Kwanza, kabla ya kutafakari ni nani atafaidika zaidi, tujiulize kwanza, nini chimbuko la kufungiwa Kwa mikutano ya kisiasa?
Tunajua wazi kuwa utawala wa awamu ya 5, chini ya Mwendazake Hayati Magufuli, ulivunja Sheria ya vyama vya siasa pale alipopiga marufuku mikutano yote ya kisiasa mwaka 2016, wakati anaelewa fika kuwa alikuwa akivunja Sheria.
Kwa kuwa tokea mwaka 1992, wakati nchi yetu iliporejea kwenye mfumo wa vyama vingi, moja ya misingi mikubwa ya mfumo huo ni kuruhusu mikutano ya hadhara Kwa vyama vyote vya kisiasa nchini, kutangaza sera zao kupitia kwenye mikutano hiyo ya hadhara.
Vile vile tutambue wazi kuwa mikutano hiyo ya kisiasa ilizuiwa Kwa vyama vya upinzani pekee, wakati chama tawala, kilikuwa kikiendelea kama "Kawa" na mikutano yake ya kisiasa nchi nzima, Kwa kisingizio kuwa ni chama tawala, kilichounda Serikali, Kwa hiyo wao pekee ndiyo wanaopaswa kuzunguka nchi nzima, kuwaeleza wananchi, maendeleo yao!
Sasa tujiulize ni sababu zipi, zilizofanya mtawaka wa wakati huo, "akurupuke" tu na kuzuia mikutano hiyo ambayo alikuwa akijua ni kuwa ni kuvunja Sheria za nchi?
Hakuna sababu nyingine iliyomfanya mtawala huyo azuie mikutano hiyo, zaidi ya woga wake kuwa kwenye uwanja sawa wa kisiasa, chama Cha CCM, kisingeweza ushindani na vyama vya upinzani.
Kwanza, watanzania watakuwa na shauku kubwa ya kuwasikiliza vyama vya upinzani, Ili kujua ni kitu gani, watawala wetu walipata "mchecheto" Hadi CCM waliamua kuvipiga marufuku vyama hivyo kufanya mikutano ya kisiasa, ambayo ni haki yao kisheria.
Pili, wananchi watakuwa na shauku kubwa kwenda kwenye mikutano hiyo, Ili kujua, ni kwanini Jeshi la Polisi, lilikuwa linazuia mikutano hiyo, wakati wao jukumu lao, Kwa mujibu wa PGO yao, ambayo ndiyo mwongozo wa utendaji wa kazi yao, siyo kuruhusu mikutano hiyo, Bali ni kupokea taarifa tu kutoka kwenye vyama hivyo na wao wanachotakiwa kufanya ni kuilinda mikutano hiyo Ili iweze kufanyika Kwa amani na utulivu. Full Stop
Kwa hiyo Kwa maoni yangu, wananchi hawatakuwa na shauku ya kwenda kwenye mikutano ya CCM, Kwa kuwa wanajua hawatakuwa na jipya, Kwa kuwa katika kipindi chote Cha tokea mwaka 2016, walikuwa "wamependelewa" wao pekee kufanya mikutano hiyo ya hadhara ya kisiasa.