CottonEyeJoe
JF-Expert Member
- Jan 8, 2008
- 331
- 72
Angekua mwaminifu angekupa taarifa kabla ya kumpa Mama mkwe hizo hela... pole kaka...
SIdhani kama issue ni kuwa nikimpa mzazi wangu basi na yeye ampe wakwake..muhimu nadhani ni kuzingatia tulivyokubaliana!..Na yeye ndio angekuwa kaniachia mshahara angekubali kuona nafanya jambo kwa hela yake bila consultation??
Nani anamtilia mashaka mwenzie, si wewe! Umeambiwa be patient, mama wa watu akiweka mambo sawa atarudisha; na hasa kama umemgombeza mwanawe; ningekuwa mimi (mama mkwe) ningekopa kungine ili nikulipe isiwe taabu!
Sasa wewe unalalamika nini, si umeyataka mwenyewe? Kuwa mpole tu
Jamani hiyo laki 5 tu unataka kuleta shida; tena umeambiwa ana matatizo kazini. Mimi kama mwanamke, ningetegemea mchumba wangu aseme hiyo pesa muachie tu mama mkwe atatue matatizo na wala asinirudishie.
Najua yaweza kuwa ni nyingi lakini jua unachokitengeneza kina thamani zaidi ya hiyo laki 5. Mkijibana matumizi inaweza kuwa compesated rahisi tu.
Khah! Ila umenisikitisha sana.
Good one!
Wanaume wengine du!
Kama humuamini basi mpigie simu mama mkweo umuulize, halafu uone impression unayotengeneza. Unashauriwa vya maana lakini hutaki. Hata kama kipato ni kidogo bado hiyo laki 5 hainunui kiwanja, so ni pesa ndogo bado!
WanaMMU salaam mbele!
Ni hivi..Niko na mchumbaangu na huu ni mwaka wa tatu na Mwenyezi Mungu akijaalia huenda mwaka huu tukajitia kitanzi (pingu za maisha). Lakini wajameni kuna kitu kimenishangaza kidogo ndo maana nikaja hapa walau mnisaidie kwa kulitizama kwa mapana jambo lenyewe!
Kwa muda takribani miezi sita sasa nimekuwa nje ya Bongo, na kwa kuwa niko na wazazi wananitegemea na wako mbali na Dar ninakoishi niliamua kumuachia mchumbaangu ATM Card yangu ili awe ana'access' mshahara wangu kwa ajili ya kuwatumia wazee na wadogo zangu matumizi. Kwa kipindi kirefu sikuwa nimeona kama kuna walakini kwenye hesabu zangu coz mara moja moja nilikuwa naomba bank statement ili kujiridhisha kama mambo yanaenda vizuri ( ikumbukwe hizi ni pesa na zina vishawishi). Of course kuna wakt kumekuwa na vijimatumizi visivokuwa na kichwa wala miguu na kwa kuwa haikuwa figure kubwa sikuwa najali sana zaidi ya kumkumbusha tu awe makini.
Kama miezi miwili iliyopita niliomba tena bank statement bahati mbaya nikakuta kuna hela kama laki tano imetolewa nje ya matumizi niliyomwidhinishia. Niliamua kumuuliza mchumbaangu kisa cha ku'draw' mkwanja huo. Cha ajabu alishtuka na kuniomba 'sorry' kuwa mamamkwe (yaan mamaake) aliziomba ili akatatulie matatizo ofisini kwao..yaan alikuwa na loss( she is an accountant). Na pia alimuambia asiniambie coz angezirudisha soon!..Nimekuwa nikimuuliza kama zimerudishwa na mpaka naandika huu uzi naona bado ni kimya...Sasa kwa kuwa huku nilipo sipigi deal wala nini na mkwanja wa huko Bongo ndo nautegemea (kumbuka kuna harusi hapa mbeleni) nimebaki nimeduwaa!..Natamani nimuulize mamamkwe but nakosa 'guts'..Je? Nimuamini tu mchumbaangu au nijikakamue tu nimuulize my mother in law???..sasa kumuuliza ndo naanzaje???
Angekua mwaminifu angekupa taarifa kabla ya kumpa Mama mkwe hizo hela... pole kaka...
shemeji@Mbu hiyo laki tano ni tsh au usd ... maana sijaelewa......hahaha....mama mkwe alimwambia bintiye asimwambie jamaa....
Kwa mtazamo wako binti anastahiki awe muaminifu zaidi kwa mama'ke au dhamana aliyopewa?
Jibu lako pia laweza geuka kitendawili ujue?
laki tano? au umekosea? laki tano jamani....mmmhh laki si pesa...
au nimeshindwa kusomaa??laki ????? unaamwanzishia mama mkwe thread? ..upo nje sehemu gani waja kulilia laki tano humu? au somalia kaka ..loh napita tu
au ni usd?