Namuanzaje mamamkwe???

SIdhani kama issue ni kuwa nikimpa mzazi wangu basi na yeye ampe wakwake..muhimu nadhani ni kuzingatia tulivyokubaliana!..Na yeye ndio angekuwa kaniachia mshahara angekubali kuona nafanya jambo kwa hela yake bila consultation??

sasa yeye awe anatoa pesa kupeleka kwa ndugu/wazazi wako wakati na wazazi wake wanahitaji....... labda kosa alilofanya nikutokukwambia kabla ya kutoa........utakaporudi zungumza nae unaweza kupata ukweli
 
Nani anamtilia mashaka mwenzie, si wewe! Umeambiwa be patient, mama wa watu akiweka mambo sawa atarudisha; na hasa kama umemgombeza mwanawe; ningekuwa mimi (mama mkwe) ningekopa kungine ili nikulipe isiwe taabu!

Haya bana nimekusoma!..na ninaomba iwe kama hapo kwenye bold
 
Mi ningekushahuri uachana na hizo laki 5, zimesha enda
Ila lazima uongee na mchumba wako, aelewe maana ya hakiba
Hawezi kuamua kutoa pesa kiasi hicho bila kukutaafiru kwanza
Pia ni bora upate uhakika kwanza kua mama mkwe ndie aliziomba
Ukute hamna cha mama wala nini, amezichukua kwa matumizi yake
halafu amemtaja mama mkwe sababu anajua utashindwa kuuliza tu.
Talk to her and make sure it doesn't happen going forward.
 
Sasa wewe unalalamika nini, si umeyataka mwenyewe? Kuwa mpole tu

Of course sijalalamika..nilichofanya ni kuuliza kama njia ninayotaka kutumia ni sahihi!..Lakini pia kumbuka sijasema kazitafuna manake hoja iliyoko mezani ni kuwa kampa mamamkwe!..Mengine yanaweza kufahamika kama nitakitegua hiki kitendawili...
 
Jamani hiyo laki 5 tu unataka kuleta shida; tena umeambiwa ana matatizo kazini. Mimi kama mwanamke, ningetegemea mchumba wangu aseme hiyo pesa muachie tu mama mkwe atatue matatizo na wala asinirudishie.

Najua yaweza kuwa ni nyingi lakini jua unachokitengeneza kina thamani zaidi ya hiyo laki 5. Mkijibana matumizi inaweza kuwa compesated rahisi tu.

Khah! Ila umenisikitisha sana.

Good one!
Wanaume wengine du!

Kama humuamini basi mpigie simu mama mkweo umuulize, halafu uone impression unayotengeneza. Unashauriwa vya maana lakini hutaki. Hata kama kipato ni kidogo bado hiyo laki 5 hainunui kiwanja, so ni pesa ndogo bado!

Bwana SnowBall, nadhani huyu Kaunga ndo mchumba ako...ongeeni vizuri sasa...PM shud do th trick!!!
 
Last edited by a moderator:
Mimi nadhani katika hili issue ya pesa kurudi ama la ni minor. Issue kubwa ni je huyo unayemwita mchumba wako kwa matendo aliyokwishayaonesha kwako mpaka sasa bado anazo sifa za kuendelea kuwa mchumba wako (na baadae mkeo)? Mimi naona ameonesha bila ya shaka yoyote kuwa sio mwaminifu kwako na kama uki ignore hii, inaweza kuwa tatizo hapo baadae. Offcourse ni vema kujiuliza pia...je ameonesha kutambua kuwa alichofanya sio kitendo cha kiungwana? Au haoni kabisa kama amekutendea ndivyo sivyo?

Sina hakika wewe ni wa imani gani, lakini mambo haya yote pengine Mungu wako anasema na wewe na anakufunulia kweli yote juu ya mtarajiwa wako ili uweze kufanya maamuzi sahihi!
 
WanaMMU salaam mbele!
Ni hivi..Niko na mchumbaangu na huu ni mwaka wa tatu na Mwenyezi Mungu akijaalia huenda mwaka huu tukajitia kitanzi (pingu za maisha). Lakini wajameni kuna kitu kimenishangaza kidogo ndo maana nikaja hapa walau mnisaidie kwa kulitizama kwa mapana jambo lenyewe!

Kwa muda takribani miezi sita sasa nimekuwa nje ya Bongo, na kwa kuwa niko na wazazi wananitegemea na wako mbali na Dar ninakoishi niliamua kumuachia mchumbaangu ATM Card yangu ili awe ana'access' mshahara wangu kwa ajili ya kuwatumia wazee na wadogo zangu matumizi. Kwa kipindi kirefu sikuwa nimeona kama kuna walakini kwenye hesabu zangu coz mara moja moja nilikuwa naomba bank statement ili kujiridhisha kama mambo yanaenda vizuri ( ikumbukwe hizi ni pesa na zina vishawishi). Of course kuna wakt kumekuwa na vijimatumizi visivokuwa na kichwa wala miguu na kwa kuwa haikuwa figure kubwa sikuwa najali sana zaidi ya kumkumbusha tu awe makini.

Kama miezi miwili iliyopita niliomba tena bank statement bahati mbaya nikakuta kuna hela kama laki tano imetolewa nje ya matumizi niliyomwidhinishia. Niliamua kumuuliza mchumbaangu kisa cha ku'draw' mkwanja huo. Cha ajabu alishtuka na kuniomba 'sorry' kuwa mamamkwe (yaan mamaake) aliziomba ili akatatulie matatizo ofisini kwao..yaan alikuwa na loss( she is an accountant). Na pia alimuambia asiniambie coz angezirudisha soon!..Nimekuwa nikimuuliza kama zimerudishwa na mpaka naandika huu uzi naona bado ni kimya...Sasa kwa kuwa huku nilipo sipigi deal wala nini na mkwanja wa huko Bongo ndo nautegemea (kumbuka kuna harusi hapa mbeleni) nimebaki nimeduwaa!..Natamani nimuulize mamamkwe but nakosa 'guts'..Je? Nimuamini tu mchumbaangu au nijikakamue tu nimuulize my mother in law???..sasa kumuuliza ndo naanzaje???

....ahhh, .....jikubalishe hasara bana, BTW hayo ni makaratasi tu...mtakatana wenyewe mbele ya safari...

Binti wa watu umemuamini na ATM card yako na acct...ya nini una panic sasa na kutaka kuharibu mambo? Learn from it....

Mkweo to be huyo, it's too early for you to show your true colours :cool:
 
Muulize tu ili ujiridhishe sio kama vile unazidai na unaweza kumueleza kuwa asiwe na wasiwasi,atakapoona mambo yake yamekaa vizuri anaweza kuzirudisha ili kuonyesha kama vile hujali sana ingawa utakuwa na uhakika kuwa kapewa mama mkwe.Lakini hata hivyo mama mkwe ndio anaanza kuwa mamaako tena ndugu yangu,hivyo huna haja ya kupaniki ndio ma-committment yenyewe yanaanza hivyo mkubwa.
 
laki tano? au umekosea? laki tano jamani....mmmhh laki si pesa...
au nimeshindwa kusomaa??laki ????? unaamwanzishia mama mkwe thread? ..upo nje sehemu gani waja kulilia laki tano humu? au somalia kaka ..loh napita tu
au ni usd?
 
pole. bora hio pesa uipotezee tu cuz ni kosa la kwanza
siku nyengine ATM muachie dada au mama yako, hata wakichukua M1 haitokuma
 
wewe samehe lakini elewa wanawake nikama akili zao kunamtu amewashikia unaweza kuta anahonga jemba kwa hiyo hela yako. uwe makini maana lolote laweza tokea
 
......hahaha....mama mkwe alimwambia bintiye asimwambie jamaa....

Kwa mtazamo wako binti anastahiki awe muaminifu zaidi kwa mama'ke au dhamana aliyopewa?

Jibu lako pia laweza geuka kitendawili ujue?
shemeji@Mbu hiyo laki tano ni tsh au usd ... maana sijaelewa
kama ni tsh huyu jamaaa kwenye ndoa huyu mkewe atakoma maana vitunguu tu atadai receipt.... kweli wanaume wazuri wa kuoa hawapo
 
laki tano? au umekosea? laki tano jamani....mmmhh laki si pesa...
au nimeshindwa kusomaa??laki ????? unaamwanzishia mama mkwe thread? ..upo nje sehemu gani waja kulilia laki tano humu? au somalia kaka ..loh napita tu
au ni usd?

Ni Laki tano wala hujakosea kuona...na nje nilipo sio Somalia...unaweza kutizama hapo juu upande wa kulia!..Ukitazama hii thread kwa jicho moja utakuja na comment kama hii!!
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom