Namuanzaje mamamkwe???

SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
2,840
WanaMMU salaam mbele!
Ni hivi..Niko na mchumbaangu na huu ni mwaka wa tatu na Mwenyezi Mungu akijaalia huenda mwaka huu tukajitia kitanzi (pingu za maisha). Lakini wajameni kuna kitu kimenishangaza kidogo ndo maana nikaja hapa walau mnisaidie kwa kulitizama kwa mapana jambo lenyewe!

Kwa muda takribani miezi sita sasa nimekuwa nje ya Bongo, na kwa kuwa niko na wazazi wananitegemea na wako mbali na Dar ninakoishi niliamua kumuachia mchumbaangu ATM Card yangu ili awe ana'access' mshahara wangu kwa ajili ya kuwatumia wazee na wadogo zangu matumizi. Kwa kipindi kirefu sikuwa nimeona kama kuna walakini kwenye hesabu zangu coz mara moja moja nilikuwa naomba bank statement ili kujiridhisha kama mambo yanaenda vizuri ( ikumbukwe hizi ni pesa na zina vishawishi). Of course kuna wakt kumekuwa na vijimatumizi visivokuwa na kichwa wala miguu na kwa kuwa haikuwa figure kubwa sikuwa najali sana zaidi ya kumkumbusha tu awe makini.

Kama miezi miwili iliyopita niliomba tena bank statement bahati mbaya nikakuta kuna hela kama laki tano imetolewa nje ya matumizi niliyomwidhinishia. Niliamua kumuuliza mchumbaangu kisa cha ku'draw' mkwanja huo. Cha ajabu alishtuka na kuniomba 'sorry' kuwa mamamkwe (yaan mamaake) aliziomba ili akatatulie matatizo ofisini kwao..yaan alikuwa na loss( she is an accountant). Na pia alimuambia asiniambie coz angezirudisha soon!..Nimekuwa nikimuuliza kama zimerudishwa na mpaka naandika huu uzi naona bado ni kimya...Sasa kwa kuwa huku nilipo sipigi deal wala nini na mkwanja wa huko Bongo ndo nautegemea (kumbuka kuna harusi hapa mbeleni) nimebaki nimeduwaa!..Natamani nimuulize mamamkwe but nakosa 'guts'..Je? Nimuamini tu mchumbaangu au nijikakamue tu nimuulize my mother in law???..sasa kumuuliza ndo naanzaje???
 
Mkuu Snowball kwanza jina lako limenikumbusha kitabu cha animal farm lol. pili kuhusu hizo laki tano kwa kweli ni bora uachane nazo kama kweli unataka kuoa huyo mke. la sivyo zitaleta maneno ambayo hata hukutegemea, jitahidi tu ukiludi utafute zingine na nina uhakika utapata laki tano ni hela kidogo sana
 
Mkuu usikubali kabisa kusamehe huo mkwanja, kwanza kama mama mwenyewe ni accountant it means naye mambo yake si mabaya kama walivyo watanzania wengi, angekuwa ni mkulima wa jembe la mkono kule Bumbuli au Tandahimba ningekuambia msamehe.

Otherwise include huo mkwanja kwenye Mahali kama bado hujatoa mahali, but otherwise dai chako aisee, ndo kwanza hata kumuoa bado, ukiisamehe hiyo jiandae kukutana na changamoto kibao mbeleni.
 
pole mkuu namna ya kwenda kumwuliza mama mkwe mmmhhh pana ugumu.
Swali je wakati unamwambia atoe pesa kwa ajili ya wazazi/ndugu zako kuna kiasi chochote ulikuwa unampatia kwa ajili ya wazazi wake pia?
 
Jamani hiyo laki 5 tu unataka kuleta shida; tena umeambiwa ana matatizo kazini. Mimi kama mwanamke, ningetegemea mchumba wangu aseme hiyo pesa muachie tu mama mkwe atatue matatizo na wala asinirudishie.

Najua yaweza kuwa ni nyingi lakini jua unachokitengeneza kina thamani zaidi ya hiyo laki 5. Mkijibana matumizi inaweza kuwa compesated rahisi tu.

Khah! Ila umenisikitisha sana.
 
Kama wataka mke hizo laki 5 samehe tu mkuu....ni hela ndogo sana kulinganisha na thamani ya huyo ulienae....pia fanya haraka urudi na uchukue ATM yako....

Mkuu kusema ni hela kidogo au nyingi inategemea na kipato cha mtu husika. Binafsi sina kipato kikubwa kivile na pia si unajua maextended family. Nia yangu ilikuwa kujua kama ni kweli mamamkwe ndio kazikopa au bidada ananzingua..Na kusema niwahi kurudi kwa ajili ya ATM card naona bado ngumu..issue hapa ni uaminifu ndo nautafuta!
 
pole mkuu namna ya kwenda kumwuliza mama mkwe mmmhhh pana ugumu.
Swali je wakati unamwambia atoe pesa kwa ajili ya wazazi/ndugu zako kuna kiasi chochote ulikuwa unampatia kwa ajili ya wazazi wake pia?

Good one!
Wanaume wengine du!
 
Kama humuamini basi mpigie simu mama mkweo umuulize, halafu uone impression unayotengeneza. Unashauriwa vya maana lakini hutaki. Hata kama kipato ni kidogo bado hiyo laki 5 hainunui kiwanja, so ni pesa ndogo bado!
 
Mkuu Snowball kwanza jina lako limenikumbusha kitabu cha animal farm lol. pili kuhusu hizo laki tano kwa kweli ni bora uachane nazo kama kweli unataka kuoa huyo mke. la sivyo zitaleta maneno ambayo hata hukutegemea, jitahidi tu ukiludi utafute zingine na nina uhakika utapata laki tano ni hela kidogo sana

Umenifurahisha sana na hiko kitabu cha animal farm..baki to ze topiki..kiasi nakubaliana na wewe kiasi nashindwa..coz nahofu isije kuwa kazitumia kwenye mambo mengine ila kwa kujua siwezi kumuuliza mamamkwe ndio maana kaamua kuniijia kiivi!..BTW i am still thinkin!
 
kosa la kwanza kumuachia mchumba wako atm card?
wazazi wako wanaishi mahali kusiko na benki?
kwa nini usingempeleka mama yako kumsigninsha?

kwa vile ulishachemka kutoka mwanzo vumilia.....
usikute wala sio mama mkwe aliyepokea huo mshiko..... si ajabu kakwambia mama mkwe akijua hutoweza kumdai...
hapo imekula kwako mkuu potezea tu,.....
ila usishangae mwezi ujao ukakuta milioni imeyeyuka..

maana kawaida kama alikuwa anataka kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ili kusolve tatizo angekuarifu wewe mwenyewe.........
 
pole mkuu namna ya kwenda kumwuliza mama mkwe mmmhhh pana ugumu.
Swali je wakati unamwambia atoe pesa kwa ajili ya wazazi/ndugu zako kuna kiasi chochote ulikuwa unampatia kwa ajili ya wazazi wake pia?
SIdhani kama issue ni kuwa nikimpa mzazi wangu basi na yeye ampe wakwake..muhimu nadhani ni kuzingatia tulivyokubaliana!..Na yeye ndio angekuwa kaniachia mshahara angekubali kuona nafanya jambo kwa hela yake bila consultation??
 
Ukisha mwachia mtu open account, usiulize zinatumikaje. Inabidi umuamini bila ya shaka yoyote.

Unaonesha bado ni kijana mdogo sana na hujayajuwa maisha.

Huwezi kumuuliza mama mkwe kwa kuwa si yeye uliyempa access ya account yako. Usimuingize kwenye mambo yako na hawara yako.
 
Mkuu usikubali kabisa kusamehe huo mkwanja, kwanza kama mama mwenyewe ni accountant it means naye mambo yake si mabaya kama walivyo watanzania wengi, angekuwa ni mkulima wa jembe la mkono kule Bumbuli au Tandahimba ningekuambia msamehe.
Otherwise include huo mkwanja kwenye Mahali kama bado hujatoa mahali, but otherwise dai chako aisee, ndo kwanza hata kumuoa bado, ukiisamehe hiyo jiandae kukutana na changamoto kibao mbeleni.

Kuinclude kwenye mahali??..duh!..otherwise nimekusoma
 
WanaMMU salaam mbele!
Ni hivi..Niko na mchumbaangu na huu ni mwaka wa tatu na Mwenyezi Mungu akijaalia huenda mwaka huu tukajitia kitanzi (pingu za maisha). Lakini wajameni kuna kitu kimenishangaza kidogo ndo maana nikaja hapa walau mnisaidie kwa kulitizama kwa mapana jambo lenyewe!

Kwa muda takribani miezi sita sasa nimekuwa nje ya Bongo, na kwa kuwa niko na wazazi wananitegemea na wako mbali na Dar ninakoishi niliamua kumuachia mchumbaangu ATM Card yangu ili awe ana'access' mshahara wangu kwa ajili ya kuwatumia wazee na wadogo zangu matumizi. Kwa kipindi kirefu sikuwa nimeona kama kuna walakini kwenye hesabu zangu coz mara moja moja nilikuwa naomba bank statement ili kujiridhisha kama mambo yanaenda vizuri ( ikumbukwe hizi ni pesa na zina vishawishi). Of course kuna wakt kumekuwa na vijimatumizi visivokuwa na kichwa wala miguu na kwa kuwa haikuwa figure kubwa sikuwa najali sana zaidi ya kumkumbusha tu awe makini.

Kama miezi miwili iliyopita niliomba tena bank statement bahati mbaya nikakuta kuna hela kama laki tano imetolewa nje ya matumizi niliyomwidhinishia. Niliamua kumuuliza mchumbaangu kisa cha ku'draw' mkwanja huo. Cha ajabu alishtuka na kuniomba 'sorry' kuwa mamamkwe (yaan mamaake) aliziomba ili akatatulie matatizo ofisini kwao..yaan alikuwa na loss( she is an accountant). Na pia alimuambia asiniambie coz angezirudisha soon!..Nimekuwa nikimuuliza kama zimerudishwa na mpaka naandika huu uzi naona bado ni kimya...Sasa kwa kuwa huku nilipo sipigi deal wala nini na mkwanja wa huko Bongo ndo nautegemea (kumbuka kuna harusi hapa mbeleni) nimebaki nimeduwaa!..Natamani nimuulize mamamkwe but nakosa 'guts'..Je? Nimuamini tu mchumbaangu au nijikakamue tu nimuulize my mother in law???..sasa kumuuliza ndo naanzaje???

SnowBall ushauri wangu unazingatia hizo kauli kwnye red. Nahisi alishtuka kwa sababu hakutegemea kuwa utajua kabla mamake hajazirudisha hizo pesa - si umesema mwenyewe kuwa alitegemea zirudishwe soon.

Sasa kwa kuwa lengo si kuchukua bali ni kukopa, mi nakushauri endelea kuwa patient, tena usithubutu kumuuliza mama mkwe coz hatajisikia vizuri kabisa! Kaa kimya hata usimuulize mchumba wako kwa sasa. Ila ukirudi bongo kabla hazijarudishwa ndo tafuta muda muafaka wa kuuliza mchumba wako. Tena ingekuwa vizuri umuulize wakati mnaongelea masuala yenu ya harusi, na hapo ndo utachomekea kwamba zinatakiwa kwa ajili ya shughuli ya harusi. Ila ukiona kuna hakuna muelekeo wa kuzilipa, achana nazo kabisa mkuu - sometime hizo ndo gharama za mapenzi, ila tu take that as a lesson.

Kiujumla ulifanya makosa kumwachia kadi ya ATM, it's too early kufanya hivyo sasa, angekuwa mkeo tayari ingekuwa haina tatizo! Ila ktk stage ya uchumba - it's too risky mzee! Isitoshe unaanza ku-raise unnecessary expectations bure!
 
Usidai hiyo hela, uache kama utarudishiwa na kama hajakurudishia kaa kimya. Kwanza yawezekana wanakupima ukoje? huyo ni mkweo huwezi kumdai utaonekana huna nidhamu, japo kuwa ni halali yako Pili siyo vema sana kumkabidhi mchumba ATM card yako.sina ,maana mbaya, ila kwa taadhari huyo ni mchumba na sio mke uchumba huwa unabadilika wakati wowote. Ukiona ushauri unafaa fuata, ukiona haufai uache, siku njema

Mkuu usikubali kabisa kusamehe huo mkwanja, kwanza kama mama mwenyewe ni accountant it means naye mambo yake si mabaya kama walivyo watanzania wengi, angekuwa ni mkulima wa jembe la mkono kule Bumbuli au Tandahimba ningekuambia msamehe.

Otherwise include huo mkwanja kwenye Mahali kama bado hujatoa mahali, but otherwise dai chako aisee, ndo kwanza hata kumuoa bado, ukiisamehe hiyo jiandae kukutana na changamoto kibao mbeleni.
 
Kama humuamini basi mpigie simu mama mkweo umuulize, halafu uone impression unayotengeneza. Unashauriwa vya maana lakini hutaki. Hata kama kipato ni kidogo bado hiyo laki 5 hainunui kiwanja, so ni pesa ndogo bado!

Dadaangu sijakataa ushauri la sivyo nisinglileta hapa...najaribu na mimi kutoa ideas zangu ili mjadala uwe mpana..Kumbuka hatujaoana, na kama tutaanza kutiliana mashaka kuanzia hapa unadhani huko mbeleni itakuwaje??..Natambua laki tano sio kubwa lakini inapotumika pale ambapo hujapanga lazima uulize bana!
 
Nani anamtilia mashaka mwenzie, si wewe! Umeambiwa be patient, mama wa watu akiweka mambo sawa atarudisha; na hasa kama umemgombeza mwanawe; ningekuwa mimi (mama mkwe) ningekopa kungine ili nikulipe isiwe taabu!
 
hmm uyu mangi wangu kabisaa..Yesuuu na Maria...et akupe atm kiruu...atarusha tu western union au mpesa babangu....lols anyway usimulize but mtell asitoe tena ela kwani una mambo umepangilia uje uyafanye kwa ajili yenu,so asitoe hela hata iweje,ukienda bongo ndo u'l knw wat to do,
 
kosa la kwanza kumuachia mchumba wako atm card?
wazazi wako wanaishi mahali kusiko na benki?
kwa nini usingempeleka mama yako kumsigninsha?

kwa vile ulishachemka kutoka mwanzo vumilia.....
usikute wala sio mama mkwe aliyepokea huo mshiko..... si ajabu kakwambia mama mkwe akijua hutoweza kumdai...
hapo imekula kwako mkuu potezea tu,.....
ila usishangae mwezi ujao ukakuta milioni imeyeyuka..

maana kawaida kama alikuwa anataka kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ili kusolve tatizo angekuarifu wewe mwenyewe.........
[/QUOTE

Hapo ndio umeua kweli yaani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom