Leo nimejisikia vibaya sana wakuu!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Siku ya leo kwangu imekuwa siku mbaya sana kwasababu mimi huwa nina huruma sana na huwa naguswa na matatizo ya watu wengine wanayopitia!.

Leo nilikuwa nimeenda Hospitali moja pale Sinza,nilimpelekea Dada mmoja hivyo ikabidi nipaki nje kumsubiri!, Sasa wakati nikiwa pale nje kuna dada mmoja alitoka ndani ya hospitali mwanaye akiwa analia kweli!

Alipofika kwangu akawa ameniomba nimsaidie nauli ya kumfikisha kwake,ikabidi nimuulize maswali kadhaa,baada ya kujiridhisha kutokana na majibu yake kiukweli niliumia sana!.

Yeye " Kaka mambo"

Mimi " Poa,Kwema"

Yeye "Samahani kaka,naomba unisaidie!"

Mimi " Nikusaidie nini Sister?"

Yeye " Kaka pesa yote niliyokuwa nayo nimefanya vipimo vya mwanangu na nyingine nimechukulia dawa!"

Aliendelea " Naomba tu unisaidie nauli ya kunifikisha nyumbani kaka"

Mimi "Pole sana,Unaishi wapi?"

Yeye " Nakaa Banana"

Mimi "Umemtaarifu Mumeo kwamba umeishiwa nauli?"

Yeye "Wee acha tu kaka,ni kama huyu mtoto hana Baba"

Mimi "Kwanini?,Baba yake yuko wapi?:

Yeye " Baba yake alimkataa mwanaye!"

Mimi "Usione kama nakuuliza maswali dada,nisamehe kama nitakuudhi lakini nataka kujiridhisha maana matapeli huu mji ni wengi mno!"

Yeye "Mimi si tapeli kaka naomba unisaidie tu nauli"

Mimi "Hapana sister,sijasema wewe ni tapeli,nilikuwa nakuelewesha tu!:

Yeye "Basi ngoja nkutolee kadi la kriniki uone"

Kweli,alinitolea kadi la kriniki pamoja na dawa ambazo aliandikiwa akanunue kwa ajili ya mwanaye!

Sikutaka kumchimba sana maana pengine niliona isingekuwa vema kumpeleleza,mimi niliamua tu kujiongeza!

Sasa ni kwamba, kwa maelezo yake ni kuwa jamaa aliyempa mimba alimkimbia akiwa mjamzito na jamaa anafanya kazi Tanesco Mkoa wa Kitanseco wa Ilala!.

Kiukweli mwanamke ni mzuri na amezaa mtoto wa kike mzuri sana kama mama yake!. Nilijaribu kumuuliza sababu za yeye kuachana na huyo mshikaji akadai ni wivu wa kimapenzi!.

Leo nimenikuta natoa Tsh 50,000/= namsaidia yule dada, Kiukweli sijawahi kutoa kiasi hicho cha pesa kusaidia kutokana na nature ya kazi yangu (Hayo mambo niliyafanya zamani nilipokuwa Don kabla sijarudi kuanza moja).

Kiukweli baada ya kumpa hiyo hela huyo Dada nimejihisi amani sana na nimekuwa na furaha ya moyo ingawa nimehuzunika sana!

USHAURI:

Wanaume wenzangu, hata kama utakuwa umekosana na mwanamke ambaye amekubebea mimba yako kiasi gani, tafadhali usimtelekeze,kiukweli huwa wanapitia mateso makubwa mnooo!, nawaomba sana msije mkafanya hivyo!.

Hata kama huyo mwanamke awe ameekuudhi kiasi gani, tafadhali jifanye mjinga tu ili umnusuru mtoto kwasababu dogo anakuwa hana tatizo, tatizo linakuwa kwenu, hivyo mtoto mpeni haki yake ya matunzo na malezi!.

Mwanamke hata akiwa amekosea kiasi gani lakini machozi na maumivu yake ni laaana tosha!, huwezi kutoboa kamwe kama akiwa anamuangalia mwanaye anateseka na wakati Baba yake yupo kazi kulewa tu na kubadili wanawake, hakika huto toboa!.

Hebu wanaume wenzangu tubadilike ndugu zangu,kiukweli inaumiza sana kukutana na mwanamke anaomba nauli wakati Baba yake yupo!

Chanzo cha watoto wetu kuaribika tatizo huanzia pia kwa Wanaume wanaowatelekeza wanawake wao! Tusiishie kuwalaumu Marekani na Nchi zilizoendelea kwa kutuleta Ushoga bila kubadilika sisi wenyewe na kutatua matatizo yetu!.

Wewe unamuacha mwanao wa kiume analelewa na mama yake, unategemea nini?!.

Hebu naomba tubadilike! Tuache Upuuzi!
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Siku ya leo kwangu imekuwa siku mbaya sana kwasababu mimi huwa nina huruma sana na huwa naguswa na matatizo ya watu wengine wanayopitia!.

Leo nilikuwa nimeenda Hospitali moja pale Sinza,nilimpelekea Dada mmoja hivyo ikabidi nipaki nje kumsubiri!,Sasa wakati nikiwa pale nje kuna dada mmoja alitoka ndani ya hospitali mwanaye akiwa analia kweli!

Alipofika kwangu akawa ameniomba nimsaidie nauli ya kumfikisha kwake,ikabidi nimuulize maswali kadhaa,baada ya kujiridhisha kutokana na majibu yake kiukweli niliumia sana!.

Yeye " Kaka mambo"

Mimi " Poa,Kwema"

Yeye "Samahani kaka,naomba unisaidie!"

Mimi " Nikusaidie nini Sister?"

Yeye " Kaka pesa yote niliyokuwa nayo nimefanya vipimo vya mwanangu na nyingine nimechukulia dawa!"

Aliendelea " Naomba tu unisaidie nauli ya kunifikisha nyumbani kaka"

Mimi "Pole sana,Unaishi wapi?"

Yeye " Nakaa Banana"

Mimi "Umemtaarifu Mumeo kwamba umeishiwa nauli?"

Yeye "Wee acha tu kaka,ni kama huyu mtoto hana Baba"

Mimi "Kwanini?,Baba yake yuko wapi?:

Yeye " Baba yake alimkataa mwanaye!"

Mimi "Usione kama nakuuliza maswali dada,nisamehe kama nitakuudhi lakini nataka kujiridhisha maana matapeli huu mji ni wengi mno!"

Yeye "Mimi si tapeli kaka naomba unisaidie tu nauli"

Mimi "Hapana sister,sijasema wewe ni tapeli,nilikuwa nakuelewesha tu!:

Yeye "Basi ngoja nkutolee kadi la kriniki uone"

Kweli,alinitolea kadi la kriniki pamoja na dawa ambazo aliandikiwa akanunue kwa ajili ya mwanaye!

Sikutaka kumchimba sana maana pengine niliona isingekuwa vema kumpeleleza,mimi niliamua tu kujiongeza!

Sasa ni kwamba,kwa maelezo yake ni kuwa jamaa aliyempa mimba alimkimbia akiwa mjamzito na jamaa anafanya kazi Tanesco Mkoa wa Kitanseco wa Ilala!.

Kiukweli mwanamke ni mzuri na amezaa mtoto wa kike mzuri sana kama mama yake!.Nilijaribu kumuuliza sababu za yeye kuachana na huyo mshikaji akadai ni wivu wa kimapenzi!.

Leo nimenikuta natoa Tsh 50,000/= namsaidia yule dada,Kiukweli sijawahi kutoa kiasi hicho cha pesa kusaidia kutokana na nature ya kazi yangu (Hayo mambo niliyafanya zamani nilipokuwa Don kabla sijarudi kuanza moja).

Kiukweli baada ya kumpa hiyo hela huyo Dada nimejihisi amani sana na nimekuwa na furaha ya moyo ingawa nimehuzunika sana!

USHAURI:

Wanaume wenzangu,hata kama utakuwa umekosana na mwanamke ambaye amekubebea mimba yako kiasi gani, tafadhali usimtelekeze,kiukweli huwa wanapitia mateso makubwa mnooo!,nawaomba sana msije mkafanya hivyo!.

Hata kama huyo mwanamke awe ameekuudhi kiasi gani,tafadhali jifanye mjinga tu ili umnusuru mtoto kwasababu dogo anakuwa hana tatizo,tatizo linakuwa kwenu,hivyo mtoto mpeni haki yake ya matunzo na malezi!.

Mwanamke hata akiwa amekosea kiasi gani lakini machozi na maumivu yake ni laaana tosha!,huwezi kutoboa kamwe kama akiwa anamuangalia mwanaye anateseka na wakati Baba yake yupo kazi kulewa tu na kubadili wanawake,hakika huto toboa!.

Hebu wanaume wenzangu tubadilike ndugu zangu,kiukweli inaumiza sana kukutana na mwanamke anaomba nauli wakati Baba yake yupo!

Chanzo cha watoto wetu kuaribika tatizo huanzia pia kwa Wanaume wanaowatelekeza wanawake wao!,Tusiishie kuwalaumu Marekani na Nchi zilizoendelea kwa kutuleta Ushoga bila kubadilika sisi wenyewe na kutatua matatizo yetu!.

Wewe unamuacha mwanao wa kiume analelewa na mama yake,unategemea nini?!.

Hebu naomba tubadilike!,Tuache Upuuzi!
kama n kwel bas MUNGU akujalie ndugu...ila nikikumbuka maya na ww nachoka kabisaaa
 
Ukimuona mwanamke yeyote barabarani anauza kitu ukinunua usidai chenji, wewe ujui tu chenji yako inaenda kuleta faraja gani Kwa familia yake iliyobakia nyumbani.

Pana watoto wadogo, mama mzazi mzee mgonjwa anasubiria wanasubiria huyo muuza mihogo, karanga, maji nk barabarani jioni ili jiko liwashwe.

Hayupo mwanamke anaehangaika juani asiye na mtoto tegemezi nyumbani.
 
Mleta uzi unachokiandika hapa ni kweli au unatafuta attention za watu tu ? Maana Mimi ni msomaji sana wa Simulizi zako na nimegundua wewe unaweza ukamtelekeza mwanamke bila huruma. Usiniulize Kwanini we jitafakari ni mara ngapi ulishahadaika ukaingia kwenye mtego wa Mwanamke na ukataka kumsaliti Mkeo ambaye ni Mwalimu huko Morogoro? Wilaya nimesahau.
 
Ukimuona mwanamke yeyote barabarani anauza kitu ukinunua usidai chenji,we ujui tu chenji yako inaenda kuleta faraja gani Kwa familia yake iliyobakia nyumbani.
Pana watoto wadogo,mama mzazi mzee mgonjwa anasubiria wanasubiria huyo muuza mihogo,karanga,maji nk barabarani jioni ili jiko liwashwe.
Hayupo mwanamke anaehangaika juani asiye na mtoto tegemezi nyumbani.

Kweli kabisa mkuu umenena ukweli mtupu!
 
Ukimuona mwanamke yeyote barabarani anauza kitu ukinunua usidai chenji,we ujui tu chenji yako inaenda kuleta faraja gani Kwa familia yake iliyobakia nyumbani.
Pana watoto wadogo,mama mzazi mzee mgonjwa anasubiria wanasubiria huyo muuza mihogo,karanga,maji nk barabarani jioni ili jiko liwashwe.
Hayupo mwanamke anaehangaika juani asiye na mtoto tegemezi nyumbani.
Yani ninunue kitu alafu nisidai Chenji? Unayemuonea huruma anaingiza hela kuliko wew msamaria mwema ...alafu tz Lia Lia wengi sana unajikuta baba huruma mwishowe wenzako wanashusha mijengo wew unabaki kutoa macho
 
Mleta uzi unachokiandika hapa ni kweli au unatafuta attention za watu tu ? Maana Mimi ni msomaji sana wa Simulizi zako na nimegundua wewe unaweza ukamtelekeza mwanamke bila huruma. Usiniulize Kwanini we jitafakari ni mara ngapi ulishahadaika ukaingia kwenye mtego wa Mwanamke na ukataka kumsaliti Mkeo ambaye ni Mwalimu huko Morogoro? Wilaya nimesahau.

Mkuu mimi ndiye sikielewei ulichoandika,au Ulichoandika ndicho akieleweki?
 
Yani ninunue kitu alafu nisidai Chenji? Unayemuonea huruma anaingiza hela kuliko wew msamaria mwema ...alafu tz Lia Lia wengi sana unajikuta baba huruma mwishowe wenzako wanashusha mijengo wew unabaki kutoa macho

Mkuu tupe mfano wa mtu uliyemkuta anauza ndizi barabarani ukanunua ndizi bila kudai chenji halafu huyo mtu ukakuta anajenga Ghorofa!
 
Back
Top Bottom