Namna bora ya kurekebisha mtu ambaye dishi limeyumba

Ghaysh

Member
Feb 12, 2015
24
43
Baada ya wastani miaka mitatu ya vipigo na vitisho vingi vya mara kwa mara kutoka kwa baba ake ambavyo kimsingi vilikuwa vinaniumiza na kunikera, siku moja nikiwa naamini nimepevuka nilimtafuta mama wa mtoto ambaye ni jirani yetu. Kwa sababu nilikuwa nimeshamzoea nikaanza kwa kumtania kwamba kila mwaka ninapokuja likizo vitu ambavyo nakuta havibadiliki kwenye mji huu ni pamoja na kipigo anachopewa mwanao.

Anatabasamu lakini lakini siyo kwa bashasha bali tabasamu la kidonda cha moyo . Akaniambia:

"Ugomvi mkubwa wa Sele na baba ake ni tabia ambazo sijui hata zimeibukia wapi. Alikuwa na akili sana tangu shule ya msingi, lakin cha ajabu alipofika kidato cha pili akawa hataki shule, anaondoka nyumbani kama anaenda shule anakuwa kwenye Mapool table huko akafikia hatua anacheza kamali. Sijui hata kama hajaanza kuvuta bangi mwanangu".

Baada ya mazungumzo mareefu nikajiridhisha kuwa kuna namna Baba ANATAKA na Mama ANATAMANI Sele awe kwa mustakabali mzuri wa maisha yake na famili kwa ujumla. Nikamuomba Sele akija anitafute nina zawadi yake.

Jioni yake Sele alinifuata Nyumbani, nikakaa naye kirafiki sana kutaka kujua nini tatizo. Kwa hisia sana Sele alinieleza:

"Kaka kiukweli hata mimi sijielewi, kuna wakati sitamani kiwa hivi ila sijui inakuwaje nashindwa kubadilika. Baba ananipiga na Mama ananiambia maneno makali ambayo yananiumiza lakini sijui kwa nini nashindwa kubadilika, sielewi kaka". Akaanza kulia!

Vimachozi fulani hivi vilitaka kunitoka ila nikazuga nikamwambia asilie mimi nitamsaidia. Ila kiukweli nilikuwa sijui nitamsaidiaje .

Siku moja nikiwa na Bethel Radio tukifanya matangazo ya moja kwa moja ya Semina ya Neno la Mungu, Mtumishi akawa anazungumza umuhimu wa Wanawake kutumia Muda mwingi sana Kuombea Waume zao na kuombea watoto zao hasa wanapokuwa wanapita kwenye nyakati ngumu zinazowafanya waugue mioyoni. Akasema kuna wakati Mama unaugua kwa ugomvi kati na baba na mtoto, baba anatandika mtoto akae kwenye mstari lakini hakuna matokeo mpaka mtoto anakuwa sugu. Wakati somo linaendelea kichwani akawa anapita Sele.

Baada ya kufunga matangazo ya moja kwa moja nikamtafuta Mama Sele kwa simu, nikamwambia najua unamwamini Mungu sasa ni wakati wa kuongeza imani yako. Anza maombi rasmi ya Kumuombea Sele na Baba yake. Nikamtumia App ya Bethel Radio afuatilie semina siku zinazofuata.

Nway itoshe tu kusema Sele ameoa na nilipofuatilia mke wake ni church girl mzuri, niliwahi kumtania mbele ya mumewe kuwa mafanikio ya huyu jamaa yapo kwenye maombi yako, akaniambia shemeji katika eneo nafanya vizuri ni kwenye kumuombea huyu mtu. Na ni kweli kwani mara mbili nimekutana na Sele anapiga story na baba ake kama marafiki. Na nimeshuhudia akipeleka vifurushi vinavyoashiri kuwahudumia wazazi wake. Kifupi Sele ni Dereva aliaminiwa na kukabidhiwa gari apeleke hesabu kwa bosi wake.

TUWAOMBEE WENZI WETU, TUWAOMBEE WATOTO WETU, TUWAOMBEE WAZAZI WETU. TUEPUKE KUWALAUMU, KUWALALMIKIA NA PENGINE KUWATAMKIA MANENO YA LAANA. KAMA BINADAMU LAZIMA WATAPITA NYAKATI NGUMU AMBAZO SIYO KAMA MAJIRA YA MWAKA BALI HAZITAKUWA NA TIME LIMIT ILA KWA NGUVU YA MAOMBI ZITAPITA TU.

Sijui kwa nini nimemkumbuka Sele!

Credit: Timothy Levy
 
Kuna sele huyo alaf kuna huyu wa mboso.
Inasemekana kashalaaniwa..

Anyway on a serious note, these days wanawake wengi sio waombaji kama zamani, kichwa inakua na mambo mengi, sijui wigi, sijui kikoba sijui wakwe n.k kwaio ukimwambia haya yote anaona kama unapiga pambio polisi.

Mpaka kiumane ndo wanaanzA kusifu na kuabudu. Na hapo mguu nje mguu ndani, akiona hakuna majibu, chap dera ndani ya chupi mguu na njia kwa sangoma.

Pia sisi wanaume tuna jam zetu. Unakuta wife anasali uwe salama, lakn mwamba yuko bize kuloweka mashimoni. Wife anakemea pepo, memba anaenda kulivaa kwa Ashura.

Vita ni vita mura
 
eti we selemani we, sele 😂 ukiangalia utagunduwa wenye majina ya sele wengi wanakua wakorofi
 
Back
Top Bottom