GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,736
- 109,328
Hii ni namba ya Airtel inapiga simu kwa wateja kuwaambia habari za kipuuzi kabisa. Inapiga kuwapa Taarifa za Kuhusiana na Taarifa za mechi mbalimbali. sikuendelea kusikiliza maana tayari ilikuwa imeshanikwaza.
nmekuwa nikilalamika sana kuhusu suala la airtel kuwapigia wateja simu kuwapa habari za matangazo yao. mfano mimi leo nlikuwa kwenye shughuli maalum. nlipoona hiyo call kutokana na shughuli zangu ikabidi nikatishe shughuli ile nikitegemea kuwa atakuwa mtu wa maana amenipigia simu. nlipopokea ndo nikaanz akusikia habari hizo za kipuuzi nikakata simu. je kuna namna ya kublock simu kama hizi?
Ingekuwa ni namba ya Demu imekupigia bado ungekimbilia huku JF kushtaki? Mkuu punguza ' stress ' najua yawezekana ' muamala ' bado haujasoma hivyo umejawa na zigo la msongo mawazo ambalo linakufanya uone kila jambo ni baya Kwako. Walioweka hiyo namba iwe inawapigia Watu siyo ' wajinga + wapumbavu ' bali ni Watu makini kama ulivyo Mtandao wangu bora kabisa ninaoutumia wa Airtel. Mbona hulalamikii Mitandao mingine ambayo na yenyewe ndiyo inaongoza kwa kuwa na mambo ya hovyo hovyo?