Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,727
218,289
Kama kawaida kesi hii yenye kuvutia mamilioni ya watu duniani inaendelea tena leo 14/01/2022, kila siku inapotajwa yanaibuka mambo mapya yenye utata mkubwa, ya miamala umeyasikia, sasa hatujui leo kutaibuka jambo gani.

Peter Kibatala na timu yake wapo tayari.

Wakili_Msomi_John_Malya_anaandaa_nondo_zake..jpg
MAHAKAMA_IMEANZA.%0A%0AJaji_ameingia_Mahakamani_Muda_huu_Saa_4_Dakika_6%0A%0A%3A_Kesi_namba_16...jpg
Muda_huu__nje_ya_Mahakama_watu_Wapo_Tayari_kusikiliza_kesi_ya_michongo.%0A%0AMpooo!%3F.jpg

=======

Kufahamu ilipoishia, soma hapa: Yaliyojiri Mahakamani katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, Januari 13, 2022. Kesi imeahirishwa hadi Januari 14 2022

Jaji ameingia Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu.

Wakili wa Serikali Robert Kidando:

Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Esther Martin
Nassoro Katuga
Ignasi Mwinuka
Tulimanywa Majige

Wote kwa Pamoja tunawakilisha Jamhuri

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikipendeza Mahakama hii Tukufu Majina yangu naitwa Peter Kibatala, Nipo pamoja na wakili

Jeremiah Mtobesya
John Mallya
Dickson Matata
Seleman Matauka
Faraji Mangula
Michael Lugina
Gaston Garubindi
Evaresta Kisanga
Khadija Aaron

Jaji anaita washtakiwa Wote Nne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na sisi tupo tayari

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Na sisi pia Tupo Tayari

Jaji: Shahidi Unakumbuka Kuwa Wakati unaanza Kutoa Ushahidi Wako Uliapa na Bado Upo chini ya Kiapo.. Bwana Mallya unaweza Kuendelea

Mallya: Mheshimiwa Jaji Naweza Kukumbushwa nilipoishia Jana

Jaji: Ulikuwa Unamaliza Kueleza Kielelezo namba 20, pale ambapo P and P Inatumika na akajibu Kuwa Ni pale ambapo Mteja kwa Mteja na Kwa agent

Mallya: Ni sahihi Shahidi Kuwa Cash out ni Kutoa pesa Kwa Wakala?

Shahidi: Ndiyo anapotoa Pesa yake Kwa Wakala kwa namba yake

Mallya: naomba Kielelezo namba 15

Mallya: Je ni sahihi Muamala umeandikwa Cash out hapo Kwenye Kielelezo, Kwamba Mtu aliye tumiwa laki 5 akaenda Kutoa Laki 3

Shahidi: Ndiyo sawasawa

Mallya: Inaonyesha kuwa Hiyo laki 3 aliifanyia nini

Shahidi: Haionekani

Mallya: Kuna uwezekano Mtu Kujiwekea Pesa Mwenyewe Kupitia Kwa Wakala

Shahidi: kimya

Mallya: Hiyo laki 5 ambayo inaonekana iliwekwa kwa Wakala, Je Kuna uwezekano huyo Mtu alijiwekea hiyo Laki 5 Mwenyewe?

Shahidi: Naomba urudie tena

Mallya: Kwenye Hiyo laki 5 ambayo inaonekana iliwekwa kwa Wakala, Je Kuna uwezekano huyo Mtu alijiwekea hiyo Laki 5 Mwenyewe

Shahidi: haijatoka kwa Wakala

Mallya: Lakini Ame Cash out kwa Wakala?

Shahidi: Ndiyo Ame Cash out kwa Wakala

Mallya: Inawezekana Mtu Kuitumia Pesa yake Kutoka Namba Yake ya Tigo Kuja namba ya Airtel

Shahidi: Ndiyo inawezekana

Mallya: Wewe Ulitueleza hiyo namba ya Tigo ni ya Nani

Shahidi: Hapana sijaeleza

Mallya: Kuna Record Yoyote Uliyo leta hapa Mahakamani Inayoonyesha hiyo Elfu 80 Baada ya Hapo ilienda wapi

Shahidi: Hapana

Malya: Kwenye Kielelezo Namba 20, Ulizungumzia Muamala Wa TSh 199,000 wa Tarehe 22 July 2020?

Shahidi: Ndiyo nilizungumzia

Mallya: Ni Cash in au?

Shahidi: Ndiyo imeandikwa Cash In

Mallya: Line ya Airtel inauzwa TSh ngapi

Shahidi: TSh 500

Mallya: Kuna Kanuni Zinazohusu Kuhusu Ku handle Sim card, Je unazijua

Shahidi: Ndiyo nazijua

Mallya: Je Kwa Mujibu wa Hiyo Barua iliyoomba Taarifa Ulichukulia Serious.?

Shahidi: Ndiyo Nilichukulia serious

Mallya: Hiyo namba Unayosema kuwa ni ya Khalfani Bwire imeuzwa kwa GODSON MNUO

Shahidi: Mimi sifahamu

Mallya: Nyie mmeuza namba ya Khalfani Bwire Kwa TSh 500?

Shahidi: Sikujua kama wameuza

Mallya: Khalfani Bwire alicha pesa zake mule, na hatujui kuwa za ugaidi au Lah, Je anapata wapi pesa zake?

Shahidi: Pesa zake zinawekwa kwenye collection Akaunti

Mallya: Kwa hiyo Airtel mnayk Collection akaunti za kutunza oesa za ugaidi?

Shahidi: Hapana, Hapana.. Si Kweli..

Wakili wa Serikali: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Namna Wakili Mallya anavyouliza Maswali Kwa Shahidi Anaaanza yeye Kutoa Ushahidi, Hakuna Sehemu Shahidi Kasema Kuwa Kuna Collection Akaunti ya Ugaidi huko Airtel..

Sitaki Kuingilia Mahakama, Mimi nimesikia Kuwa anasema Kwenye Collection Akaunti Ya Airtel Kuna Pesa za Ugaidi, Tunaomba Wakili aelekezwe namna Nzuri...

Mallya: Mheshimiwa Jaji, naamini Mahakama imerekodi Vizuri,

Jaji: nilikuuliza mahakamani Mara Kadhaa, Je hayo Mengine unayosema unayatoa wapi, Kuna wakati Unaulizwa kwa wewe Kwa kutoa Maelezo.. Sasa unakwenda mbali wakati unazungumzia na kuyasema hayo, hayapo Kabisa Katika Proceedings, Naomba Uulize Yale Yaliyopo Mahakamani Tafadhali

Mallya: Mheshimiwa Jaji Nimesikia, ila Nina Haki ya Kuuliza Kuwa Mimi nafahamu hivi Je wewe Unafahamu Vipi?

Jaji: Kuna Maswali ambayo Umekuwa unamuuliza wewe, Ndiyo Uwe Unauliza Maswali tu.

Mallya: kwa hiyo mnasema kwamba zile pesa za Khalfani Bwire zipo kwenye collection Akaunti?

Shahidi: Nitaomba kuelezea

Mallya: Utaelezea baadae, Hapa jibu swali tu.

Mallya: Sasa Wewe Ulipokea Barua Kuwa Hawa watu wanachunguzwa, Je hiyo Siyo Exception ya Kuzuia hiyo namba?

Shahidi: Sikujua Kama Wanachunguzwa

Mallya: Soma Barua ya Uchunguzi wa Kisayansi walisema nini..

Shahidi: Wanaomba Taarifa Kwa Uchunguzi zaidi

Mallya: Kwa hiyo Nyie Mkauza Ushahidi Wa Khalfani Bwire Kwa Tsh 500

Shahidi: atazikuta zimewekwa

Mallya: Je Mteja wangu akitaka Kujitetea so itabidi ampokonye huyo GODSON MNURU?

Shahidi: Taarifa zake zipo lakini

Mallya: Ulitoa ufafanuzi huo

Shahidi: Sikuulizwa

Mallya: Jibu swali

Shahidi: Sikuulizwa

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba ajibu swali Langu

Jaji: Umeelewa swali?

Shahidi: Si Kutoa Ufafanuzi

Mallya: Kwenye Barua Yako Soma Paragraph ya Mwisho

Shahidi: Tupo tayari Kuendelea Kutoa Ushirikiano zaidi

Mallya: Kwenye Muamala ulijisumbua Kujua Wakala alikuwa nani?

Shahidi: Sikufuatilia

Mallya: Kwa hiyo unasema Namba Inakuwa Dormant Kwa Siku Ngapi, kuwa Deactivated?

Shahidi: Siku 90

Mallya: Mshtakiwa Nmab Moja Kizimbani Khalfani Bwire, alikamatwa Tarehe 9 August 2020 Je Wewe Uliombwa Lini Taarifa za Hiyo namba?

Shahidi: Tarehe 1 July 2021

Mallya: Ni Miezi Mingapi Ilikuwa Imepita

Shahidi: Kama 10 au 11

Mallya: Kwa hiyo ni zaidi ya Miezi 3 ya Kisheria Kuwa Namba Inakuwa Deactivated

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Sasa tangu yule Bwana amekamatwa Mpaka Wewe Unaombwa Taarifa Tayari Namba ilikuwa Deactivated

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Sasa Bwana GODSON MNURU anasema Kuwa alinunua hiyo line Mwezi January 2021, ni sahihi Kwamba KYC ya Hii namba ingesoma namba yake siyo Khalfani Bwire?

Shahidi: Hakuna Record Yoyote, Kwa hiyo siwezi Kutoa Jibu

Mallya: katika hali ya kawaida kwa miezi 10 namba ya Bwire ingekuwa deactivated au isingekuwa deactivated

Shahidi: Ingekuwa Deactivated

Mallya: Mheshimiwa Jaji sina swali lingine

Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji sina Swali Kwa niaba ya mshtakiwa wa tatu

Wakili Peter Kibatala: Shahidi Gazeti la The Citizens la Tarehe 12 January 2019 Serikali kupitia waziri Kabudi, Serikali Ilifanya mazungumzo na kampuni ya BHART AIRTEL ili kuongeza Hisa zake kutoka 40% Mpaka 49%

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa hiyo Serikali ya Jamhuri Wa Muungano Wa Tanzania ni Ma' boss zako?

Shahidi: Si Kweli

Kibatala: Je unafahamu Kuwa Serikali ya Jamhuri Wa Muungano Wa Tanzania Ina Nominate Wakurugenzi Kuingia katika Kusimamia Kampuni ya AIRTEL?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Je hao nWakurugenzi Maboss Wako au siyo Maboss zako?

Shahidi: Siyo Maboss zangu

Kibatala: Kwa hiyo wewe Uli report kwa Bodi ya Wakurugenzi iwe Direct au Siyo Direct?

Shahidi: Siyo Maboss zangu

Kibatala: Kwa hiyo wewe Legal Manager una report wapi

Shahidi: Kwa Managing Director

Kibatala: Ambaye yeye ana report kwa nani

Shahidi: Kwenye Bodi

Kibatala: kwa hiyo Bodi wakitoa Malekezo Managing Director akufukuze Kazi with Regard ya Labour Law, Utafukuzwa au hautofukuzwa?

Shahidi: Ushasema Labour Law

Kibatala: Nataka Kujua Wana Uwezo wa Kuagiza, au hawana?

Shahidi: Wana uwezo Wa Kuagiza

Kibatala: Kwenu ninyi Airtel Kipi ni Paramount

Shahidi: Mteja ni Mtu muhimu kwetu na tunaangalia sana taarifa zake lakini pale panapohitajika Kisheria Ku' Comply na Sheria, tunafuata Sheria..

Kibatala: Kama Mteja hataki Data zake ziwe Relesed, Wakati Inforcing Organ Wanataka Data zake, wewe kama mwanasheria Una' ishauri nini board ya Directors?

Wakili wa Serikali: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Law enforcement wanahitaji taarifa, swali lake limejengewa katika premises na wanataka kumtengenezea kesi shahidi, Yeye aseme tu Polisi wanataka taarifa...

Kibatala: Kwa Heshima Mhe Jaji, Sitamjibu Kwa Kuokoa Muda

Shahidi: Sitajua, Sababu ni Opinion

Kibatala: Je Unafahamu Kuwa Freeman Mbowe ni Kiongozi Wa Chadema au hufahamu

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kuwa Mr Mbowe amekuwa na Kesi Mbalimbali na Law enforcement Organ

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je unafahamu hapa unakuja Kutoa Ushahidi Anashtakiwa Kwa Kesi Kesi gani

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Umekuja Kutoa Ushahidi Kuhusu Kesi gani inayo Mkabili Mteja wako

Shahidi: Economic Crime

Kibatala: Unafahamu Ni Kesi ya Ugaidi?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kabla ya kuwa the Guardians ulikuwa kampuni gani ya Mawakili?

Shahidi: Hallmark

Kibatala: Nilisikia Unazungumzia Kuhusu Summons, Je Ile summons inasema Wanashtakiwa kwa Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Mpaka nitazame tena

Kibatala: Jana Ulitaja Namba 3 kwa Kumbukumbu zako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ila Kuhusu Summons Hukumbuki

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Barua Imekufikia Tarehe Ngapi Mwezi gani na Mwaka gani

Shahidi: Tarehe 02 July 2021

Kibatala: na wewe Umejibu Tarehe Ngapi

Shahidi: Tarehe 02 July 2021

Kibatala: Ni sahihi Kusema ulijibu Siku ileile

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wakati Unafanyia kazi Ulijua Unafanyia Kazi Namba ya Freeman Aikael Mbowe

Shahidi: Ndiyo Niliona kwenye KYC kwenye Picha

Kibatala: Iambie Mahakama na Mteja wako Freeman Mbowe, Je ni Juhudi gani Ulichukua Kulinda Taarifa za Mteja wako

Shahidi: Niliombwa na Chombo chaUchunguzi

Kibatala: Hilo Jibu ni zuri ila si la Swali langu, Swali Ni Kwa namna gani ulijaribu Kulinda Taarifa za Mteja wako Kama Ulijibu Siku hiyo hiyo?

Jaji: umeliewa swali?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Nimeelewa swali, ila Chombo kilichoniomba Kina Ruhusiwa Kisheria

Kibatala: kwa hiyo Unasema kuwa Ulijibu Ile Barua Kwa sababu Imetoka Police?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kwa hiyo Tutaona wapi Kama Airtel Wali balance kati ya Mteja wao na Police?

Shahidi: huwezi Kuona

Kibatala: Jana Mawakili Walitaja Sheria ya Makosa ya Mtandao wewe Ukataja Sheria ya Electronic and Post Communication Act, Je unafahamu Regulations ya Proctection of Consumers?

Shahidi: Naweza Kupata nijikumbushe?

Kibatala: Ngoja Mawakili Wako wa Serikali Wajiridhishe Kwanza

Kibatala: Sasa Tusomee Rule 6(2)(d)

Shahidi: Inasema 6(2) The Collection and Maintenance of Information on Individual's Consumer...... ANASOMA

Kibatala: Je Ni kweli Nyie kama Licensee Mnatakiwa Ku' balance Haki zingine za Mteja?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ni sahihi Hizo Haki ni pamoja na Privacy

Shahidi: hapo itabidi tuangalie Kwenye Interpretation

Kibatala: Unafikiri Utaweza Kuona, Ngoja nikuonyeshe

Shahidi: Ni kweli Haijasema

Kibatala: Nilijua haijasema, Sasa Unasemaje

Shahidi: Ni kweli Inajumuisha Haki ya Privacy

Kibatala: Katika Sheria hii Kuna sehemu Inaonyesha Mteja Haki zake zitupwe Kapuni for the Name of Compliance?

Shahidi: Hapana,

Kibatala: Je Unafahamu Kuwa kuna Judicial Review?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Iambie Mahakama Nyie Kama Airtel Mnaweza Kufungua Judicial Review Pale Mnapopewa Amri

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je Kuna Sheria Inakataza Nyie Airtel Ku Challenge Order ya Kutoa Taarifa za Mteja wenu

Shahidi: Hakuna Sheria hiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Airtel Ilienda Mahakamani Ku' Challenge Haki ya Mteja Wake

Shahidi: Hapana Haikwenda

Kibatala: Je Uliwandikia Barua Police Kuwa Wawawape Details Kutaka Kujua Nini Kinafanyika

Shahidi: Hapana hatukuwaandikia

Kibatala: Je kuna Jambo Lolote Liliwazuia Kufanya hivyo Kisheria?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Shahidi Na Kuonyesha Kielelezo P16 Cha Requisition letter, Je Mwambie Mheshimiwa Jaji ni wapi Barua hiyo iliwaharakisha Nyie Airtel Muwape hizo Taarifa

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Kwa hiyo Hakuna Kwenye Barua Mahala ambapo Pameonyesha Palikuwa na Haraka katika Kujibu Barua

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Na Jana Hukusema Kabisa Kama Ulifanya Kwa Haraka Kwa Sababu Gani

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji zaidi ya Kungalia BARUA yenyewe Kuna Hatua gani Ulichukua Ku Authenticate.

Shahidi: Hakuna Kingine Nilicho fanya zaidi Ya Kuangalia Barua

Kibatala: Huyo aliyesaini Barua Unamfahamu?

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Mpaka Leo hujawahi Kumuona

Shahidi Sijawahi Kumuona

Kibatala: Kwenye hiyo Barua Kuna Namba za Simu

Shahidi: Ndiyo Kuna namba za Simu

Kibatala: Ulizitumia hizo namba za Simu

Shahidi: Hapana

Kibatala: Badala Yake Baada ya Wiki 1 Ukaenda Kutoa Maelezo Yako Kwa Inspector Swila

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Ulichukua Hatua Kuchunguza Kama anayekuhoji alitoka Cyber

Shahidi: Sikuchunguza

Kibatala: Na Wala Hukuchunguza Mpaka Leo Kuwa Swila alikuwa anapeleleza Makosa ya Ugaidi na Siyo Cyber

Shahidi: sikuchunguza

Kibatala: Na Swila Haku kwambia Kuwa anaandika Maelezo Kuhusu Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Hakuniambia

Kibatala: Wewe Ulijua Anakuhoji Maelezo Kwa Makosa gani

Shahidi: Barua inasema Kuwa Walikuwa Wanaomba Taarifa Kwa ajili ya Kuchunguza Tuhuma Za Jinai

Kibatala: Hizo tuhuma Za Jinai Wakati Unajibu Ulikuwa Unaifahamu au Huzifahamu

Shahidi: Nilikuwa sifahamu

Kibatala: Hii Barua ya P16 Inasema Kuwa Iliandaliwa Chini ya Kifungu cha 34 cha Sheria gani

Shahidi: ilikuwa inataka Taarifa kwa kutumia Sheria Ya Makosa Ya Mtandao

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji, Hii Barua Ilikuwa addressed Kwa nani

Shahidi: Ilikuwa addressed Kwa Mwanasheria

Kibatala: Kwa hiyo wigo uliokuwa nao wa Kushughulika na hiyo Barua ni Uanasheria Wako tu?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na Hiyo Barua Haikuelekezwa Kwa HR, Wala Mfagiaji?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wewe Kama Mwanasheria Wa Miaka 8, Je ni wapi Katika Barua, Kielelezo namba 15, Ni wapi Mheshimiwa Jaji akiangalia ataona Iliandikwa na Wewe Gladys au Mwanasheria?

Shahidi: Neno Mwanasheria Halipo

Kibatala: Tukitaka tujue Kuwa amejibiwa na Mwanasheria Tunaangalia wapi?

Shahidi: Hakuna.... Lakini Gladdys ni nani?

Kibatala: Sitaki Maswali mimi hapa

Kibatala: Ombi limeletwa Kisheria, Kwa Watu waotegemewa Kutoka Jeshi la Polisi.... Na Kwa terms of reference, Je ni sahihi Kwamba na wewe Ulitakiwa Kujibu kwa Kufuata terms of reference

Shahidi: Ni Kweli

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Barua Iliomba Taarifa namba Ngapi

Shahidi: Namba 3

Kibatala: Na wewe Ukapeleka Majibu ya Taarifa za namba ngapi

Shahidi: Namba 2

Kibatala: Zina oana au zipo tofauti

Shahidi: Zipo tofauti

Kibatala: Jana Ulisema Kuwa kuwa Barua ilipokelewa Wapi

Shahidi: Reception

Kibatala: Baada ya Hapo Ikawaje

Shahidi: Waka minutes kuja Kitengo Cha sheria

Kibatala: Wewe Kama Mwanasheria Wa Airtel, Miaka 8 Unafahamu Kitu kinaitwa Chain of Custody?

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Na Ni Mwanasheria Miaka 8

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Okey Tuendelee, Ni wapi Barua hiyo Mheshimiwa Jaji akiangalia ataona Kuwa Ilipokelewa Mapokezi Airtel

Shahidi: Hapana

Kibatala: Barua hiyo inaonyesha Kuwa Ilifika Kitengo Cha Sheria

Shahidi: Hapana

Kibatala: Maelezo Yako Ulizungumzia Kuhusu Dispatch au Register

Shahidi: nilizungumzia

Kibatala: Hiyo Register Kamq Mwanasheria Mkuu wa Airtel Ungetaka Kuja nayo Ungenyimwa

Shahidi: Hapana nisingenyimwa

Kibatala: Register hiyo Ulileta Mahakamani

Shahidi: Hapana Sikuleta

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Register hiyo ilipotea au ipo Mbali

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulimwambia Jaji Kuwa Mpaka Wewe Unaleta Barua Hapa Mahakamani Ulimwambia Jaji Ulitoa wapi hiyo Barua

Shahidi: Sikueleza hayo Unayo yasema

Kibatala: Ulimwambia Jaji Kuwa Barua Kama hizo Zilizotoka POLISI zinahifadhiwa wapi Pale Airtel

Shahidi: Si kumwambia

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Barua hiyo Uliyotoa inalingana na Nakala ya Barua iliyopo Jeshi la Polisi

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa Barua ilifika Vipi Polisi

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Wewe Unafanya Kazi Masijala Ya Polisi?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Barua Uliyotoa Jana na Uliyopeleka Jeshi la Polisi Zinafanana Content

Shahidi: Hapana Sikumwambia

Kibatala: Ndiyo Maana Nilikuuliza Hapa Unajua Maana ya Chain of Custody?

Shahidi: Nili Jibu sifahamu

Kibatala: Twende eneo Lingine

Kibatala: Ni kweli Taarifa Unazo leta, zinaonyesha zipo Uncorrupted?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nianze Kielelezo namba 17, 19, na 20

Kibatala: Je Ile Taarifa Ulivyopokea Uli' print au Ulim' taarifu Boss wako?

Shahidi: Nili Print tu..

Kibatala: Mpaka Unatoa Taarifa Hii Mahakamani Airtel Wanafahamu Kuwa Ulitoa Taarifa hii?

Shahidi: Ndiyo Wanafahamu

Kibatala: Je Ulimwambia Sasa Mheshimiwa Jaji Kuwa Uliwa taarifu Ma' boss zako Kuwa Uliingia Katika Mfumo Ukatoa Taarifa?

Shahidi: Hapana Sija Mwambia

Kibatala: Ni Kitengo Gani pale Airtel kina husika na statutory Liability, Consumers Liability?

Shahidi: Sisi Pale Vitengo Vinashirikiana, Kitengo Cha Sheria ndiyo kina Mamlaka ya Kushughulika na Mambo yote ya Kisheria

Kibatala: Ni lini Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Baada ya Kutoa Taarifa, Ulimtaarifu MD au Boss Wako?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ananiuliza Utaratibu ambao sisi hatuna..

Kibatala: Je ni kweli au siyo Kweli Kwamba Kabrasha la Sheria lazima lipelekwe board of Directors??

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Twende Eneo Lingine

Kibatala: Jana Nilisikia Unasema Mojawapo Ya Mambo Uliyo yataja Ulitaja System Kama AGILE, BUSSINESS INTELLIGENCE na MOBIQUIT sasa Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa AGILE ni nini

Shahidi: Ni Mfumo wa Kungalia Taarifa za Mteja

Kibatala: na Ukiwa Chini ya Kiapo unasema AGILE ni Mfumo, na siyo Utaratibu Wa Kuangalia Mauzo, Idadi ya wateja Ili Kuongeza ufanisi wa Kampuni?

Shahidi: AGILE ni Mfumo

Kibatala: Unatengenezwa na Nani?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Na nani ana Hakimiliki ya Trademark ya AGILE?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Jana Nani hapo alisimama Kusema Kwamba alienda Training?

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Twende kwenye BUSSINESS INTELLIGENCE, yenyewe ni Software?

Shahidi: Ndiyo ni Software

Kibatala: Inatengenezwa na nani

Shahidi: Sijui

Kibatala: Ina Version Ngapi

Shahidi: Sijui

Kibatala: Nani Jana alileta Habari za Bussiness Intelligence hapa?

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Wakati Jana Unatoa Ushahidi Kuhusu Bussiness Intelligence, Ulitolea Ushahidi Ku Impress Kuwa unafahamu au Ulijua Kuwa ni authentication?

Shahidi: Nilitaja Kutoa Ushahidi

Kibatala: Mwambie Mhe Jaji Kuwa kweli BUSSINESS INTELLIGENCE ina Exists inahusiana Vipi na Vielelezo 17, 18, 19 na 20

Shahidi: Haihusiani

Kibatala: Ya 3 inaitwa nini

Shahidi: MOBIQUIT

Kibatala: Unafahamu Kweli?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Airtel Wame Install lini Hiyo MOBIQUIT

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ina Version Ngapi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ipi Version ni safety and latest of MOBIQUIT?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni lini Ulifahamu Kuwa Kuna MOBIQUIT ipo na Inafanya kazi Shahidi Nimajiriwa Airtel Nimekuta Inafanya kazi

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba MOBIQUIT Ilikuwa Upgraded lini

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Weeknes za MOBIQUIT Kama Kweli ina Exists

Shahidi: Si kumwambia

Kibatala: Ulimwambia inatofauti gani na Software zingine

Shahidi: Hapana Sikumwambia

Kibatala: Hizi Data Zinakuwa Stored kwenye servers?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: unafahamu Kuna aina Mbalimbali za Server?

Shahidi: Hapana, Sifahamu

Kibatala: Kama Hufahamu hata Aina ya Server ya Airtel Bado unataka tuamini Kuwa hizi Data hazijachezewa?

Shahidi: kimyaaaa

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Sever ya Airtel ni ya Aina fulani

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: Je Ulimwambia Kuwa Hizo Saver Zinakuwa Upgraded lini

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Twende eneo lingine

Kibatala: Hizi System zote Kuna Watu wanazi Mantain Pamoja na Kuzifanyia Auditing?

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kuna Internal auditors

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Nyie Mna External Auditors au HAMNA?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Nilisikia Unazungumzia Kuhusu Firewalls, Kama Ukuta For Protection

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Zipo aina Nyingi sana za Firewall

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na Ulitaja ili Kuonyesha Taarifa zipo salama

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuhusu aina ya Firewall wanazotumia Airtel

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulitoa Sababu yoyote kwa Jaji Kuwa huwezi Kutaja aina ya Firewall Mnazotumia kwa ajili ya Industrial Secrets?

Shahidi: Hapana Sikumwambia

Kibatala: Ni kweli Kuna aina Mbalimbali za Firewall

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na Ni kweli zinatofautiana Ubora..?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Twende eneo lingine

Kibatala: Uliwahi Kupokea Barua ya Jeshi la Polisi Kuwa Muifanyie Uangalizi Miamala Ya Freeman Mbowe?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Nyie Kama Airtel Mlifahamu Kuwa Mbowe anafanyiwa Uchunguzi wa Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Baada ya Tarehe 02 July 2020, Freeman Mbowe aliendelea Kuwa Uraiani na Kuendelea Kutumia namba zake, Je Nyie Kama Airtel mlishawahi Kuwa na Wasiwasi na Miamala ya Freeman Mbowe?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Nyie si Reporting authority?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Moja ya Majukumu yenu Kama Reporting Authority si Mngeli' taarifu Jeshi la Polisi kama Kuna Miamala Yenye Mashaka??

Shahidi: Hapana

Kibatala: Katika wakati wote Hamkuwahi Kupata Kengele ya Kiusalama Kuhusu Kiwango Cha Pesa Kama Sehemu ya Kigezo Chenu cha Kutilia Mashaka Namba ya Freeman Mbowe?

Shahidi: Namba Yake Haikuwa Kupiga Kengele ya Kutilia Mashaka

Kibatala: Miamala ya Tarehe 20 July 2020, Zinahusisha namba gani na namba gani

Shahidi: Ni 780900174 ambayo ilituma Kwenda 787555200

Kibatala: Kwa hiyo Hizo namba zinaanza na 7 na Siyo Sifuri?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Namba Ambazo zipo katika Kielelezo Cha Polisi na Hizo, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ndiyo namba hiyo hiyo?

Shahidi: Si kutolea Ufafanuzi

Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kuwa Kuna Utofauti Katika Kielelezo P20 hizo namba hazianzi na Sifuri lakini Katika Barua ya Maombi Zinaanza na Sifuri?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: ambapo Tunasema Hukumfafanulia Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nilisikia Mnasema Kuwa Kuna Collection Akaunti au Wallet sijui nini na nini..

Shahidi: Unaweza Kuita Wallet

Kibatala: Ni ya kampuni gani

Shahidi: Ni wallet ya Tigo

Kibatala: Wewe Ni Mtu sahihi Kuzungumzia Wallet ya TIGO TZ?

Shahidi: Ndiyo naweza Kuzungumzia

Kibatala: kati yako wewe na Mtu wa Tigo nani yupo Competent Kuzungumzia Originating namba ya Tigo?

Shahidi: Ni Mtu wa Tigo

Kibatala: katika Barua Yako ya Tarehe 02 July 2020 Hukutoa Maelezo Yoyote

Shahidi: Ni kweli Siku toa

Kibatala: Transactions Ya Chini yake umesema ni Namba ya Agent, Je unamfahamu

Shahidi: Hapana Simfahamu

Kibatala: Airtel Mnasajili namba za Agent na Mna File Lake, Je ni kweli?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je Hilo file lipo Hapa Mahakamani ili tujue Kama Ana Uhusiano Na Mbowe?

Shahidi: Hapana Halipo Mahakamani

Kibatala: Katika Barua Yako ya 02 July 2020 uliwaambia Polisi Juu ya huyu Wakala?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: nikitumiwa namba yangu ya Airtel siwezi kumtuma House girl, akifika kwa Wakala anitumie namba niweze Kutoa Fedha hiyo?

Shahidi: Haiwezekani

Kibatala: kwa hiyo Nikimtuma mtu aende kwa Wakala Wangu Kutoa Pesa na nikatoa Bila Mimi Kuwepo pale siwezi Kutoa Pesa? Haya Niambie Kwa Sheria gani inayokataza

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: angalia katika taarifa ya namba ya Mbowe, tarehe 20 July 2020, mnasema kuwa alituma TSh 500,000 kwa Denis Urio

Shahidi: HAKUNA MUAMALA HUMU WA HIYO TSh 500,000

Kibatala: Twende Kielelezo namba 20, nitafutie Tarehe 22 July 2020 Kuna miamala miwili ambayo namba ya Freeman Mbowe ilituma pesa kwenda Kwa Denis Urio au Khalfani Bwire either Tsh 190,000 au 199,000..

Shahidi: HAKUNA MIAMALA HIYO

Kibatala: Primary source ya Taarifa Ya mteja ambazo Zinakuwa Reflected katika KYC zipo NIDA ndiyo Maana Mna retrieve Kutoka NIDA?

Shahidi: Sawa sawa

Kibatala: Na wewe hufanyi kazi NIDA

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na wewe Hukutoa Chochote Kutoka NIDA

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nilisikia Kuwa Uliitwa Polisi Kuwa Ukaandike Maelezo Yako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kama Uliyaandika kwa nia Njema, na yalikuwa ya Kweli, kwanini hutaki Kuyatoa Mahakamani

Shahidi: Siyo Kwamba Sitaki Kuyatoa

Kibatala: Ndiyo sasa Nakuuliza Kwa Nia Njema Kama Kweli Uliyaandika Chini ya Kiapo chq Mungu, kwanini Usitoe?

Shahidi: Jana Kuna Uamuzi Ulitoka Kuwa nisitoe..

Jaji: Mr Kibatala Jana Mtobesya alisema Kuwa Mlikubaliana Kuwa Kama Jopo Mna Withdraw.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Na Taadhima Ni kweli Kwamba Wakili Mwingine alifanya Cross Examination Mimi siruhusiwi Kuhoji tena hilo Jambo???

Jaji: yeye alisema Kuwa Mlikubaliana "Sisi ni Jopo" na Kwa Bahati Mbaya Hayupo.

Kibatala: Kama Ikiwezekana naomba Utusomee Ulicho Rekodi Mheshimiwa Jaji

Jaji: Hapana sisomi, Kwani wewe Jana Hukusikia?

Kibatala: Basi Mheshimiwa Jaji sitaki Kubishana na Mahakama, na Nitaomba Kuishia Hapo Kibatala anaketi

WS Jenitreza Kitali: anasimama na Kufanya Re:Examination

Wakili wa Serikali: Jana Uliulizwa Kuhusu Taarifa ya KYC Taarifa za Msajili hazionekani Katika hiyo Taarifa, Ni kwanini labda

Shahidi: Ni kweli Haionekani Lakini Hizo Taarifa Zipo na Zikihitajika zinaweza Kuletwa Mahakamani

Wakili JOHN MALLYA: OBJECTION Taarifa kuwa zipo katika Mfumo wa Usajili Zikihitajika Zinaweza Kuletwa Mahakamani si Sawa na ni taarifa Mpya..

Wakili wa Serikali: Kwa Maoni yetu ni Explanation, na Kwa Upande wetu sisi hatuwezi Kuzuia Shahidi Kueleza jambo

Jaji: Basi eleza Katika Namna ambayo hatoleta Jambo Jipya

Wakili wa Serikali: Jana Shahidi Uliulizwa Kwamba Katika Taarifa Yako Msajili haionekani, Kwa nini ipo hivyo

Shahidi: Mfumo ndiyo Ulivyo lakini Endapo zitahitajika zitaletwa

Wakili wa Serikali: Umeulizwa Kuhusu namba ya Simu Ikiwa Dormant, haitumiki na Kwamba Airtel Wamemuuzia Mtu Mwingine anaitwa GODSON MNURU, Ukasema hwezi Kueleza Mpaka Uone Nyaraka

Shahidi: Ni kweli Nilitaka anithibitishe Jina, Kwa sababu Nisingeweza Kujibu kabla Sijathibitisha

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Wakala kuwa Hukutoa Details za Wakala aliye fanya huo Miamala Wa TSh 300 000, ni Kwanini ilijitokeza

Shahidi: Sikuwa Nimeombwa Taarifa

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kuhusiana Jukumu lako Kutoa Taarifa Kuhusiana na Kutoa Taarifa, Lakini Pia Kuna Kifungu Cha Wewe Kukataa Kutoa Taarifa Ukamtaka Mtoa Taarifa aende Mahakamani, Ukasema Ni kweli Vifungu Unavijua ila Hukutaka Kufanya hilo

Shahidi: Kuna Vitu Vingi Tunaangalia katika Kutoa Taarifa, Kuna Sheria Zinaniruhusu Kufanya Hivyo na Sheria Siyo Moja, Kwa Hiyo Sheria Inaniruhusu Kufanya hivyo pale Ninapo takiwa Kutoa Taarifa

Shahidi: Kuna Vitu Vingi Tunaangalia katika Kutoa Taarifa, Kuna Sheria Zinaniruhusu Kufanya Hivyo na Sheria Siyo Moja, Kwa Hiyo Sheria Inaniruhusu Kufanya hivyo pale Ninapo takiwa Kutoa Taarifa

Wakili wa Serikali: Pia Jana Kuna Taarifa kwenye Kielelezo namba 17 kuhusu NENO "kanda" Kimoja Kina Neno hilo Kanda Kimoja Hakina , Ieleze Mahakama Kwanini Ilijitokeza hivyo

Wakili JOHN MALLYA: Hizo ni fact Mpya

Jaji: alisema Jana kuwa Wana Extract na Kuprint, haiwezi kuzichanganua

Wakili JOHN MALLYA: Sawa Mheshimiwa Jaji

Wakili NASHON NKUNGU: Mheshimiwa Jaji nina maswali na majibu ya Mtobesya ya jana

Jaji: Umesoma wapi?

Nashon Nkungu: Wenzangu walikuwa wame rekodi

Jaji: Umetoa wapi, Naona una refer kwenye simu, wala huna karatasi

Nashon Nkungu: Basi Mheshimiwa Jaji naomba nikae.

Jaji: Inavyoonekana ni kama kuna source nyingine, Maana proceedings bado sija' certificatify, sasa huyo ana refer kwenye simu, inaonekana kuna source nyingine kwenye simu zaidi yangu....

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Technology imekuwa Kubwa Pia, maana hata sisi mawakili tuna Group la WhatsApp na tuna' share Taarifa na nyaraka mbalimbali humo ndani..

Jaji: Ndiyo Nimeona yeye kashika simu na ninachojua Mtobesya atakuwa kaondoka na simu yake, sasa yeye (Nashon Nkungu) anatoa wapi au ana source nyingine?

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naona tusifungue mambo mengine, itoshe tu kusema, hakuna wakili atavunja kanuni za Mahakama wala Kwenda Nje ya utaratibu wa mahakama au Taaluma yake, mengine ni mambo ya kibanadamu tu...

Jaji: tuendelee...

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kwamba Mara baada ya Kupokea Barua Kutoka Kamisheni ya Uchunguzi, Kwamba Waliomba Taarifa hizo Kupitia Cyber Act, Ukasema Kweli Waliomba Ila Ukasema Hukuona Maelezo Zaidi, labda kwa nini

Shahidi: Hapakuwa na Uwezekano wa Kuomba Taarifa Za Ziada, Vile ambavyo tumeomba ni Kwa Utaratibu Wa Sheria na tulifuata Sheria

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kuwa Tarehe 02 July 2021 Uliombwa Taarifa, Ukajibu Tarehe 02 July

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuwa Wakati Unaomba Taarifa hizi, za Usajili na Mihamala Kama Ulijua Zilikuwa Taarifa za Freeman Mbowe Ukasema Hufahamu, Ukasema Ulijua Baada Kuingia Kwenye Mifumo, Ni Kwanini Ulisema Hivyo

Shahidi: Baada ya Kupata Taarifa, Ndiyo Nilifahamu lakini niliwasilisha kama Nilivyo Ombwa kwenye Barua

WS: Ulirejewa hapa Kuhusu Sheria ya Electronics na REGULATION kuhusu Protection of Consumers Rights, Ukasema Kwamba hazisema Kwamba Haki za Mteja zinatupwa kampuni

Shahidi: Ukiangalia Kifungu hicho Kinatoa Exception, Pale Unapoombwa Taarifa, Paramount ni Mteja lakini Ukienda Mbele Sheria Inatoa Exception Kwenye hilo suala

Wakili wa Serikali: Sawa Labda Kwa Nini Ulijibu Siku hiyo hiyo

Shahidi: Ni kazi niliyo kuwa assigned Siku hiyo hiyo.. Ni Sababu Palikuwa na Volume Kubwa ya kazi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Tunaomba Neno Volume lisiingie

Wakili wa Serikali: Hatuoni sababu, Ni sawa na Kuzuia Shahidi Kutoa Ushahidi

Jaji: Hoja yake Neno Volume. Haku lisema Mwanzo na lisiingie..

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusu Ku' authenticate Barua hiyo, wewe ukasema Barua hiyo ilikuwa imejitosheleza

Shahidi: Sikuwa na Haja Ya Kuona Vitu Vingine Sababu Niliona Vingine vimetimia katika Ile Barua

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Barua Iliyotoka Polisi ambayo ni Kielelezo Namba 16 kuwa palikuwa na Namba za Simu Pale Na Fax Lakini hukuhakiki kama Ile Barua Ilikuwa inahitaji Mambo hayo

Shahidi: Sikutaka Kufanya Hivyo Kwa sababu Barua Ilikuwa inajitosheleza Kutoka katika Ofisi ya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali, Wakati anaandika Ile Barua Kama Ulikuwa unajua Kama Unaandika Ile Barua Tuhuma ambazo ulikuwa Unachunguza zilikuwa Zinahusiana na Ugaidi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusu Kuleta Barua Kutoka Legal office Ya Airtel Kama Kweli Ulipewa idhini ya Kujibu ile Barua

Shahidi: Sikuwa Nimeombwa Ushahidi huo

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Barua Yako ya Majibu Hakuna Neno Mwanasheria wala Majina yako, Ni Kwanini Ipo hivyo Shahidi: Sikuwa Nimeandika kwa sababu Niliandika Kwa Niaba ya Airtel, na Kuongeza sababu Kitengo Kinanitambua

Wakili Peter Kibatala: Hayo ya Kwamba Kitengo Kinamtambua Yasiingie..

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kama Ile Barua ya Airtel Kwemda Polisi uliwasilisha wewe, Ukasema Kweli, na Ukasema hukulinganisha hizo Barua ndiyo ile Uliyoleta Hapa Mahakamani

Shahidi: Nilieleza Ni Barua ambayo Niliandika

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kama Baada ya Kutoa Taarifa Ulirudi Kuwataarifu Ofisini Ukasema Huku rudi, Ni Kwanini

Shahidi: Ni Utaratibu Wa Ofisi, Unarudi pale tu Unapokwama.

Wakili PETER KIBATALA: OBJECTION Mheshimiwa Jaji suala la Utaratibu ni Fact Mpya..

Wakili wa Serikali: Labda ni Kwa Nini Hukurudisha Taarifa Ofisini

Shahidi: Sikuhitajika Kufanya hivyo

Wakili wa Serikali: Uliulizwa hapa Swali ktk Usha wako Kama Ulisema Kuhusu tofauti ya Software Ya Kuhifadhi Kumbukumbu za Miamala , Ukasema Hukusema

Shahidi: Mifumo ya Uhifadhi Wa Taarifa za Kumbu Kumbu za Miamala ni Mmoja, Kwa hiyo Nisingeweza Kutoa Utofauti wakati ni Moja

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kwanini baada ya Kujibu Maombi na baada ya Kujua Taarifa Hii ya Freeman Mbowe, Ukaulizwa kwanini hamkufanya survalance, Ukasema hamkufanya survalance baada ya pale

Shahidi: Barua Haikututaka tufanye hivyo

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Kuhusiana na Suala la Kama Unaweza Kuzungumzia collection akaunti Ukasema Hauwezi Kuzungumzia Originating Namba Iliyotuma pesa Katika Collection Akaunti, Je ni Kwanini Ulisema hivyo

Shahidi: Kwa sababu ni Namba ambayo originated na Tigo ambayo Inatengenezwa Kama Reference ya Airtel..

Wakili wa Serikali: Ulisema Hapa Kwamba Katika Kielelezo namba 20, Tarehe 20 kama namba Ya Freeman Mbowe Ilituma Miamala kwenda Kwa Denis Urio Ukasema Hapana

Wakili wa Serikali: Tufafanulie Kwanini Kielelezo hicho hakionyeshi

Shahidi: Kielelezo hiki kina namba ya Mteja 787555200 ambapo Ukirudi Kwenye KYC ni Namba ya Denis Urio, Kuna Muamala Wa Kupokea TSh 500,000 ambapo Denis alipokea Kutoka Kwenye Tigo Wallet na siyo Mbowe

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusiana na Taarifa ambazo ni Primary Source kwenye KYC ambapo Ukasema Ni NIDA Kwanini Unasema Primary Source ni NIDA?

Shahidi: Airtel tuna Mfumo wa Kusajili Kutoka NIDA ambao Unatambulika Kisheria

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kukomea Hapo

Wakili wa Serikali: Naomba Kurejesha Vielelezo

Jaji: Shahidi Asante Kwa Ushahidi Wako

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji huyo ndiye shahidi tuliyekuwa naye kwa leo.. Tunaomba hairisho mpaka Jumatatu Tarehe 17 January 2022, tulete shahidi mwingine...

Shahidi tuliye mtegemea baada ya shahidi huyu alipata udhuru wa kuuguliwa na sababu ni Askari Mstaafu na alisharejea kwao, hakuwezi kufika Tunaomba hairisho mpaka Jumatatu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Jambo jingine ambalo lilijotokeza hapa Mahakamani, Tunaomba suala la kisheria liweze kutatuliwa...

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kuna Mmoja ya watu waliokuwa ni wasikilazaji wa kesi alionyesha Kitendo Cha Kutotii Mwenendo wa Kesi hii..

Jaji: tukubaliane tunaendaje, Kwanza tunaye Mjadili hayupo humu....

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji utaratibu upo kwa mtu simu inapoita hata mapolisi humu simu zao zimekuwa zinaita mara nyingi tu... Suala la Kwamba kuna mtu alikuwa anarekodi proceedings twende chamber, Kidando apewe simu akague atuonyeshe hizo records kisha ndiyo tujadili

Jaji: Basi tunahairisha hili jambo kwa muda, mawakili tukutane chamber, lakini pia mhusika naomba aitwe. Na kwa sababu ya mazingira ya chamber tupate wawakilishi wangapi?

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa wawili wawili wanatosha..

Jaji anatoka TUTAREJEA PUNDE TU!


========

Mahakama imerejea Kesi inatajwa. Mawakili wa pande zote mbili wanajitambulisha


Jaji: niliahirisha kwa muda kwaajili ya kile tulichowaeleza awali, Na tumeongozwa na busara tukaamua kama tulivyoamua. Na Bwana Fue Fue tumem' subject kwenye maamuzi yetu yale ya awali. Hataruhusiwa kuingia tena. Na tunaahirisha shauri hili mpaka Jumatatu 17/01/2022

Jaji anatoka Mahakamani
 
Back
Top Bottom