Najuta nimezaa nje ya ndoa, ushauri wako muhimu sana

paulss, kosa umeshalifanya then face the Quonsequences . vyovyote itakavyokuwa, make sure mke wako ni wa kwanza kujua, mambo ya kwenda kutafuta ushauri pembeni alafu mke wako asikie kutoka pembeni, ni mbaya sana, yaani ataona umemdhalilisha maradufu.
pole sana mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Wadau wakati mwingine katika maisha tunafanya mambo ambayo ukikaa utulie unajiona mpumbavu na kutoamini kama kweli ni wewe umefanya au ulirukwa na akili.

Mkasa ulio nikuta ni matokeo ya uzembe wangu ambao naujutia hakuna mfano, so naomba ushauri wako badala ya kuendelea kunihukumu kwani tayari nimejifunza

Mwaka juzi tulienda kwenye shughuli fulani mkoani kwetu kwa wiki mbili, na katika katiza katiza za hapa na pale nikapata kabinti kamoja nikaanza nako uhusiano huku nikiwa na mke wangu na watoto wawili ambao niliwaacha Dar,
Kibaya zaidi mazingira tuliyokuwepo kondom zikawa hakuna na nikafanya kosa la mwaka kwa kujamiiana naye bila kinga.

Baada ya shughuli kwisha nikarudi Dar na kuendelea na maisha na nikawa sina tena mawasiliano na yule binti kwani alikuwa hana simu,hata hivyo ilikuwa ni kama hit and run

Sasa mwezi machi nikaenda likizo mkoa na familia, tukiwa katika wiki ya mwisho kama bahati nikakutana na yule binti akiwa na rafiki yake wote wamebeba watoto, basi yule binti kuniona tu alishtuka na kupiga kelele almanusura anguke na kuzirai, akaja akanikumbatia na kunishikilia kwanguvu huku akilia na kuongea maneno yaliyonichangaya kabisa.

Ikabidi tutafute sehemu tukae atulie kisha akamtoa mtoto mgongoni na yule wa rafiki yake akasema wanao hawa wako mapacha.
Kiukweli nilipo waona tu roho ilipasuka maana kitu fotokopi,huitaji hata mtaalamu kubaini kama wale watoto ni wangu kwani tumefanana nao mno.

Baada ya maongezi marefu nikajiridhisha kuwa watoto kweli ni wangu kwa mujibu wa maelezo yake na mfanano wa watoto.
Na akanieleza jinsi alivyohangaika kunitafuta kwani hakuwa hata anajua ninapokaa nikiwa mkoa na jina nilimpa la uongo hivyo na watoto kawapa jina hilo kama ubini wao.

Ilibidi nimpatie pesa ya matumizi kwanza palepale na nikachukua tax na kuwapeleka kwao kwa ahadi kuwa nikapajue kwao kisha kesho yake ntakwenda na wazee kujitambulisha kama mimi ni baba wa watoto wale,akanipa namba zake za simu alikuwa nayo nikazuga nita mbeep nkiweka vocha kisha nikaondoka bila kushuka na kusalimia kwao na nikamwambia asiseme kitu kwanza nijipange kwani anaishi na wazazi wake.

Niliporudi home nikajiuliza usiku kucha sikupata majibu,
Nampenda mke wangu na ananiamini sana kila nikifikiaria akijua akili haikubali, nahisi nitaharibu familia yangu
Baada ya tafakuri ya muda mrefu nikafanya maamuzi ambayo nayo naona yanaanza kunishinda ndio maana nipo hapa kwa ushauri wenu.

Nilichoamua ni kuhakikisha natunza siri hii peke yangu, nikaamua kesho yake nikanunua line mpya ya simu na kuisajili jina lile feki nikampigia simu kuwa nimepata dharura nimeondoka alfajiri na nikamtumia pesa laki3 kwaajili ya matumizi na kuahidi nitarudi soon.
Baada ya hapo nikamaliza wiki yangu mkoa nikiwa nashinda home tu hadi nilipoondoka na familia kurudi Dar.

Huu ni mwezi wa 6 sasa ninachofanya ni kila mwezi natuma laki moja ya matumizi kwa ile line na kama anataka kunitaarifu kitu labda watoto wanaumwa basi atatuma meseji na mimi kila siku jioni huwa naweka line ile kwa muda mchache na kuangalia kama kuna ujumbe au nataka kujua jambo then naitoa.

Nafanya haya yote kujaribu kuprotect familia yangu lakini pia kuhakikisha watoto wale wanapata huduma kama watoto wengine.

Siku za karibuni presure toka kwa wazazi wa yule binti imekuwa kubwa, wanataka kunijua na kubeba jukumu kama baba kweli na si kutuma tu pesa wakati hawamjui mzazi mwenza wa binti yao, wamejaribu sana kuni trace bila mafanikio maana kila nikiwasha ile line jioni nakutana na sms kali kali kuto kwa wazazi wake, wanaongea maneno makali hadi kufikia kunitisha.

Hakuna ndugu yangu anajua maana niliogopa angeweza kusababisha mimi kujulikana kitu ambacho sipo tayari kitokee kwani mke wangu akijua nahofu ya kupoteza furaha ya familia yangu

Lakini pia wakati mwingine nawafikiria wale watoto wanahitaji baba anayeoneka hata kama sita ishi nao .
Pia najiuliza ni kwa muda gani nitaweza kukaa na jambo hili peke yangu huku likinipa hofu na kuniondolea furaha ambayo ndio naogopa kuipoteza kwenye familia yangu

Wakuu naombeni mawazo yenu tafadhali, kama ni kosa limeisha fanyika lakini I feel like I can't hold it anymore, but when I think about my family I got stuck

Mkeo nae ni muhimu katika suala hili, lakini je umewafkiria watoto wako pia? je ungependa wakue huku wakifahamiana na wenye furaha au unataka waje wafahamiane wakiwa wakubwa. hapo kuna hatari ya kuletewa nyumbani mkwe ambaye ni mtoto wako pia. kama unataka kuepuka hayo muome msamaha mkeo na umueleze ukweli.
 
Ndugu yangu hapo kama wewe ni mwanaume halisi ni vema uwajibike tu, namaanisha inakupasa kueleza ukweli bila kuficha chochote kwa mkeo, kwa huyo binti na wazazi wake na kwa ndugu zako wote, ni bora wote waujue ukweli kupitia wewe mwenyewe kuliko wakiujua kutoka kwa wengine. Kumbuka wewe na mke wako siyo ndugu, lakini wewe na watoto wako ni ndugu. Nakushauri uwe upande wa watoto zaidi kuliko kwa mkeo ili kuhakikisha wanapata malezi bora. Ikibidi kawachukue uishi nao huko dar. Kama mkeo hatopenda basi itabidi umruhusu aende mbele. Watoto ni bora kuliko mke. Kiongozi katika familia ni mwanaume, lazima uwe na maamuzi magumu inapobidi.
 
biblia inasema tusichangie wazinzi;HAPO HAPO INASEMA ANASAMEHE SASA BASI kwa kuwa sijaona sehemu uliyomwomba MUNGU msamaha kwa kitendo cha kutoka nje ya ndoa nashindwa hata kuendelea ;labda ushauri tu kama ulivyoandika yooote naomba uandike unaomwomba mungu akusamehe si kwa kuzaa nje ya ndoa bali kwa kutembea nje ya ndoa yako
nahisi hata mawazo yanayokuja baada ya hapa yatakuwa ya hekima kuliko hayo 75 naushee niliyyaona
mungu akubariki

samahani hapo kwenye red ulimaanisha nini vile???/
 
kaka paulss nakuomba uwaombe hawa wakupe mchango wao wahawawatu maana ni wamuhimu sana gfsonwin na Mtambuzi wanauzoefu kwenye hiyo secta sijaona michango yao hapa nafikiri wataweka conclusion nzuri
 
Pole sana mpendwa nimejiweka upande wako na kujikuta nasikitika sana.
Cha msingi andaa mazingira mazuri ya kuongea na mkeo
Mwambie juu ya hili na pia umuombe msamaha kwa katika hali ya kujutia
Najua sisi wanawake huwa tunapanic kwa muda give her time..baada ya muda itamuingia akilini na atakuelewa bila shaka
Ni wewe unamjua mkeo yuko vip lina ana furaha na lini ana huzuni

Na akiwa na furaha anakuwaje ,pia akihuzunika anakuwaje
Lakini cha msingi mweleze kweli
Hata kama hataaccept fact leo au kesho baada ya muda ataelewa janga lipo .
Baada ya hapo utakuwa huru kuwatunza wanao
Ungekua wewe ndio mke wa ndugu yetu huyu ungechuka uamuzi gani?
 
Unafikiri kumwambia akaombe msamha kwa mkwe wake si ushauri? au ulitaka nisemaje hapo zaidi ya kukemea tabia za kizinzi zifanywazo na wana Ndoa?

si ajabu hata wewe mzinzi sema tu hayajakukuta, mtu ana tatizo badala ya kujaribu kutatua tatizo mambo yakiwa poa then unaweza kumkemea, sasa wewe eti wakati anafanya uzinzi alikuwa hajui...jaribu kufikiri kama yangekuwa yamekupata wewe
 
Hiyo furaha ya familia yako unayojaribu kuiprotect siyo genuine furaha. Iko kwa sababu kuna mambo mkeo hayajui.
Has it ever occur to you that you may be happy and trust your wife but there is something she isn't telling you?
Be a man and face your mess with confidence, we all have sinned and fall short of God's glory. Confess your sins and walk with true happiness...Ukishaona extent ya ulichokifanya ndo utaona madhara ya hit and run na pia utatuletea ushuhuda ili wenye tabia kama hizo waache.

1) Just remember, Utapata credit nyingi toka kwa mkeo kama wewe ndio utamwambia na si ajue vinginevyo!
2) U owe the mother of the twins to go and be acknowledged by her people-Ili warudishe japo sehemu ya heshima yake iliyoondoka kwa kuleta watoto wakati hana mawasiliano na baba yao (assume dada yako ndo huyo wewe ungejisikiaje?)

3) Hebu wafikirie na wengine kwenye maamuzi please (Mkeo, wanao na huyo mdada)
4) kama wazazi wako wamekulea na wewe ujue kwamba wanao mapacha wanastahili uwepo wako katika malezi yao!
 
si ajabu hata wewe mzinzi sema tu hayajakukuta, mtu ana tatizo badala ya kujaribu kutatua tatizo mambo yakiwa poa then unaweza kumkemea, sasa wewe eti wakati anafanya uzinzi alikuwa hajui...jaribu kufikiri kama yangekuwa yamekupata wewe
<br>
<br>Hata mimi ni mwanaume na nimeoa na mke pia lakini siwezi kutetea hili. Haya ndio yanasababisha watoto wa mitaani na hata magonjwa kwanini tusiwewaaminifu ili tusivuruge ndoa zetu? Hapo iwe isiwe mke wake lazima atajua kama si leo kesho ataficha mpaka lini? ujinga wa leo ni maafa ya kesho
 
Nimependa uchambuzi na ushauri wa snowhite sioni alichoacha!

I hope cheaters wengine watajifunza from ur mess.
 
Last edited by a moderator:
Binadamu wote tumepungukiwa na utukufu wa aliye juu!so kama ni kosa ndo hivyo lmeshafanyka hatuwez kusaidiana kwa kujilaumu,just pray sana kwa dini yako yoyote b4 hujamwambia wyf wako as lazima umwambie sababu atajua tu siku moja so ni bora alsikie hili kutoka kwako!all the best,tunasubir feedback!

Hongera kaka kwa kupata mapacha uwezi jua ndio bahati yako,Tafuta mtu wa familia mwenye kutunza siri mkae nae muonge jinsi gani yakujitambulisha kule an kuwaeleza kama una mke na watoto pia utawatunza watoto wako wote kadri ya uwezo wako,utalipishwa faini za kidizaini mambo yataisha baada ya mda utalileta home ilo jambo kwa utaratibu.
 
Back
Top Bottom