Msafiri Kasian
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 2,133
- 659
Hivi karibuni nilijikuta nimeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mmoja pasipo kumfahamu vizuri.Kwa kifupi ni kwamba alitokea kunipenda japo hakuweza kuniambia moja kwa moja,na mimi kama utani nikamchombeza akanikubalia.Aliniambia mengi kuhusu mahusiano yake ya zamani ikiwemo kwamba alishazaa mtoto na mwanaume flani bila kutarajia lakini.Na mambo mengine mengi,ila hili la mtoto lilinishtua zaidi,kwasababu nilijiuliza nitaishije na mtu mwenye mtoto hapo ndani wakati mimi sina? na huyo aliyezaa nae je ataelewa? ila nilipotezea tu huku nikiwa natafakari kitu gani nifanye.
Pia huyu mwanamke sijawahi kufanya nae(lile wanaloita tendo la ndoa) zaidi ya mawasiliano ya simu pekee.Sasa ilinilazimu nianze kuchunguza background yake na ndipo nilipogundua,huko nyuma hakuwa na mwenendo mzuri na pia katika historia fupi ya maisha yake aliyonipa,ilisheheni uwongo mwingi(niligundua huko nyuma hakuwa ametulia).Nikaamua kutaka kumwacha kitu ambacho kilimsababisha kulia muda wote,hali chakula na pia kushuka kimasomo(ni mwanachuo),rafiki zake walinisumbua sana kuhusu hali yake kuwa mbaya kwasababu yangu,hivyo nikaamua kumwambia yaishe tu ili kumtuliza kwa muda ili nitafute njia nzuri ya kumwacha.Nimekuja kwenu wana MMU mnisaidie njia nzuri ya kumwacha huyu.Natanguliza shukrani.