Nahitaji kuachana na huyu mwanamke,naomba ushauri wako tafadhali!

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,133
659
Hivi karibuni nilijikuta nimeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mmoja pasipo kumfahamu vizuri.Kwa kifupi ni kwamba alitokea kunipenda japo hakuweza kuniambia moja kwa moja,na mimi kama utani nikamchombeza akanikubalia.Aliniambia mengi kuhusu mahusiano yake ya zamani ikiwemo kwamba alishazaa mtoto na mwanaume flani bila kutarajia lakini.Na mambo mengine mengi,ila hili la mtoto lilinishtua zaidi,kwasababu nilijiuliza nitaishije na mtu mwenye mtoto hapo ndani wakati mimi sina? na huyo aliyezaa nae je ataelewa? ila nilipotezea tu huku nikiwa natafakari kitu gani nifanye.


Pia huyu mwanamke sijawahi kufanya nae(lile wanaloita tendo la ndoa) zaidi ya mawasiliano ya simu pekee.Sasa ilinilazimu nianze kuchunguza background yake na ndipo nilipogundua,huko nyuma hakuwa na mwenendo mzuri na pia katika historia fupi ya maisha yake aliyonipa,ilisheheni uwongo mwingi(niligundua huko nyuma hakuwa ametulia).Nikaamua kutaka kumwacha kitu ambacho kilimsababisha kulia muda wote,hali chakula na pia kushuka kimasomo(ni mwanachuo),rafiki zake walinisumbua sana kuhusu hali yake kuwa mbaya kwasababu yangu,hivyo nikaamua kumwambia yaishe tu ili kumtuliza kwa muda ili nitafute njia nzuri ya kumwacha.Nimekuja kwenu wana MMU mnisaidie njia nzuri ya kumwacha huyu.Natanguliza shukrani.
 
Kumbe hujado naye mkuu inakuwaje shida????? Wewe ni rahisi panga naye siku moja mtoke eneo ambalo siyo hatarishi lakini ni zuri kwa mapumziko au maongezi.

Mwambie ukweli kuwa wewe katika maisha yako kwanza jambo la kuona liko mbali kwa sasa na hata ikitokea unataka kuoa basi hutaoa mwanamke aliyezaa kwa sababu;

1.0 Hupendi usumbufu wa mawasiliano ya mke wako na mzazi mwenzake pale inapobidi kwa kuwa wewe una wivu sana,
2.0 Una mifano mingi ya watu waliooa wanawake waliozaa na baadae ndoa zao kuyumba (Hiyo ni sababu ila haina ukweli wowote, wala haijawa researched)

Mwisho unamnyooshea sasa, hivyo naomba kama utaweza tuwe marafiki tena wa kawaida sana na usiwe na wivu hata ikitokea ukaniona mimi nina mwanamke mwingine ambae anaweza kuwa mke wangu mtarajiwa kwa kipindi hicho kijacho.

Akilia isikutishe maana kuna wanawake wengine kulia ni mazoea kitu kidogo tu mchozi unaweza kujaza debe!!!!!!!!!
 
Preta kasema.. Kama una uhakika humpendi, usimpotezee wakati wala wewe kupoteza wako.
Kigezo cha mtoto,au hstory cyo tatizo..pengne ndo chance yake ya kubadilika.
But u'v to listen to ur heart kata mawasiliano.,.ila mshirikishe Mungu pia.
 
Sa na wewe vipi uingie kwenye uhusiano na mtu humjui vizuri.

Any way achana naye.
 
Ukitaka kumuua nyani usimuangalie USONI!! We muache kwa kumpa makavu kuwa umejua huko nyuma alijiachia bila simile!!!! Tena mwambie huweki kulea mtoto wa mtu!!! Kadri unavozidi kumpa moyo wa kipuuz ndo atakuganda sanaa! Tena usionje!!! Ohoooo! Ukionja tu mwenzio Mimba ndiii! Hapo hamna ugumu wowote ni wasiwasi wako tu! Kinachomliza ni majuto yake ya matendo yake ya zamani! BAAAAAAAAAASS. DONT SACRFISE YOUR OWN HAPPINESS TO MAKE SOMEONE ELSE HAPPY!!!! Not acceptable at all!!!
 
Kulia mbwembwe man, hawa viumbe wana phd ktk kuongopa! Na ukirudiana nae tu blv t o nt, utafall wewe na weakness zake me nina experience nazo so take a move man! Take it frm me
 
Haimaniishi kwamba mtu alikua na historia mbaya basi tabaki kuwa hivyo daima, wapo machangu na machangu wa kiume (malaya wa kiume na wa kike) ambao baada ya ndoa zao wametulia ajabu na pia wapo waliojiita wasafi na watakatifu ( Kama wewe) lakini walipoingia kwene ndoa mambo yamebadilika kabisaaaaaaaa, so sikiliza roho yako tu inavyokutuma pls
 
usipende kuishi kwa historia,wewe mwangaliae kuanzia hapo ulipo maana hakuna aliye mwema.yaweza kuwa Mungu amekutumia wewe kubadilisha maisha yake.
cha maana,chek afya zenu then mwangalie kama akiwa safi mpe haki yake.

hakuna kitu kinauma kama kuachana na umpendaye..
 
binadamu mnatafuta malaika chini ya jua......

Hebu mwambie huyo dada mapema kuwa humtaki, maana ulishaanza oooh ana mtoto ...oooh itakuwaje.... Mwambie huwezi kuwa nae, ataliaaaaaaaaaaa lakini atasonga mbele na si kumpotezea muda.......
 
Ukitaka kumuua nyani usimuangalie USONI!! We muache kwa kumpa makavu kuwa umejua huko nyuma alijiachia bila simile!!!! Tena mwambie huweki kulea mtoto wa mtu!!! Kadri unavozidi kumpa moyo wa kipuuz ndo atakuganda sanaa! Tena usionje!!! Ohoooo! Ukionja tu mwenzio Mimba ndiii! Hapo hamna ugumu wowote ni wasiwasi wako tu! Kinachomliza ni majuto yake ya matendo yake ya zamani! BAAAAAAAAAASS. DONT SACRFISE YOUR OWN HAPPINESS TO MAKE SOMEONE ELSE HAPPY!!!! Not acceptable at all!!!

NANI KANUNA!????????????????

nimependa ushauri wako esp. the fact that its coming from a lady...
 
sitisha mawasiliano nae,unless unampenda!mi sidhani kama ni dhambi kama kuoa mwanamke mwenye mtoto hasa kama unaamini amebadilika,jamani kwenye haya maisha ya kuanza mahusiano mapema na hiki kizazi chetu nani ana hakika kuwa hana mtoto mahala fulani,hasa kama ni mwanaume!,wanaume ni wangapi mna hakika kuwa mabinti mliokuwa na mahusiano wakati fulani hamkuawaachia watoto,?mtoa mada kama ukijitafiti nafsi yako na ukgundua humpendi nafsi yako mwambie mapema huyo dada na kwa uwazi kuliko kuendelea kumuonea huruma wakati unajua huwezi kuwa nae eti kwa kuwa amezaa!
lakini kama unahisi unampenda sidhani kama kuwa na mtoto kunafanya ushindwe kupata unachokihitaji maishani!
sa si bora huyo amezaa?je ukioa ambaye hajazaa lakini kumbe kwenye maisha yake alishatoa mimba kibao ?haya maisha jamani na mambo yake ni mengi sana!
 
Haimaniishi kwamba mtu alikua na historia mbaya basi tabaki kuwa hivyo daima, wapo machangu na machangu wa kiume (malaya wa kiume na wa kike) ambao baada ya ndoa zao wametulia ajabu na pia wapo waliojiita wasafi na watakatifu ( Kama wewe) lakini walipoingia kwene ndoa mambo yamebadilika kabisaaaaaaaa, so sikiliza roho yako tu inavyokutuma pls
:A S-coffee: ahsante!
 
Back
Top Bottom