Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,206
- 18,995
Niite jina lolote, lakini mimi ni mojawapo ya watu ambao huwezi hata kabisa kunishawishi kwamba hii nguvu na mbwembwe ambazo Makonda amekuwa akizionyesha zinatokana na kuwa kwake na cheo cha katibu mwenezi wa CCM. Tusidanganyane hapa.
Makonda sio katibu mwenezi wa kwanza CCM, na wamekuwapo wengine huko nyuma, lakini ni mara ya kwanza tunapata katibu mwenezi wa CCM ambae anaonyesha kujiamini kupita mamlaka yanayostahili ya katibu mwenezi wa CCM.
Leo hii katibu mwenezi awapigie simu mawaziri, amkebehi mwanasheria mkuu wa serikali, awaamrishe wakuu wa mikoa, ma-RPC, eti kwa sababu yeye ndie msemaji mkuu wa chama, hilo tu? Haiwezekani.
Leo hii katibu mwenyezi apewe bajeti, misafara ya magari, kuliko inavyokuwa kwa makamu mwenyekiti wa CCM au katibu mkuu wa CCM, kwa sababu gani? Kwamba katiba ya CCM imebadilishwa kisiri na hawa wote wameambiwa kuanzia sasa bosi wenu ni katibu mwenezi wa CCM? Pamoja na mawaziri? Wakuu wa mikoa? Mwanasheria Mkuu? Wenyeviti wa CCM wa mikoa?
Sote tunajua msemaji mkuu wa chama chochote anasema yale chama kilichoamua katika vikao vyake rasmi. Kuwa msemaji wa chama haina maana wewe ndio unakuwa unakisemea chama, hata siku moja. Kuwa katibu mwenyezi sio katika mpangilio wa vyeo vya chama, ni nafasi tu. Huwezi hata kusema katibu mwenezi wa CCM ni mkubwa kuliko mwenyekiti wa CCM wa mkoa. Lakini sio hivyo kwa Makonda. Yeye amejipa madaraka ambayo nadhani yanazidi hata ya kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, au katibu mkuu wa CCM. Kujiamini huko kunatoka wapi? Mamlaka haya yanatoka wapi? Kwamba siku zote hatukujua kuwa katibu mwenezi wa chama ni mtu mkubwa namna hii? Ni kweli?
Nyie watu wa CCM, nyie mawaziri, nyie wakuu wa mikoa, tuambieni ukweli. Kinachowafanya muufyate Makonda akiunguruma ni nini hasa, Ukatibu mwenezi wa CCM? Na kwa nini sasa wenye akili tukiwauliza mbona mambo yako hivi, mnaishia kutabasamu tu bila kusema lolote? Kuna kitu gani msichotuambia?
Na niwaambie wazi nyie watu wa CCM. Kama nguvu ya Makonda sio ya kikatiba ndani ya CCM, kama kuna chanzo kingine kisicho rasmi kinampa nguvu na kujiamini kiasi hiki, basi anguko la CCM liko karibu sana!