Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
Muimba taarabu mashuhuri nchini Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuph Mwinyi maarufu kama Mzee Yusuph, leo majira ya saa sita mchana amedondoka ghafla na kupoteza fahamu kisha kukimbizwa katika Hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili.
Tukio hilo la kushtukiza limetokea wakati Mzee Yusuph akiwa katika ofisi za Radio Clouds FM, jijini Dar es Salaam alikokuwa amekwenda kwa shughuli zake za kikazi. Akiwa mapokezi(Reception), ghafla hali yake ilianza kubadilika na akaanza kulalamika kuwa anasikia kizunguzungu kabla ya kudondoka chini na kupoteza fahamu.
Kwa sasa yuko Hospitalini Muhimbili na madaktari wanahangaika kuyanusuru maisha yake.
source:Global Publishers Ltd