Simulizi: Mtoto wa Mzee Martin

Apr 19, 2023
77
123
IMG_8261.jpg


Ni asubuhi na mapema. Unaamka na kijiandaa kuelekea kazini kwako.
Baada ya kumaliza kujiandaa, unavaa viatu kuelekea kazini kwako.
Mara ghafla simu inaita,
Unapokea simu ambayo imeingia kwa namba ngeni na kuulizwa “wewe ndiye Martini?” unasema “ndio”
unaambiwa unahitajika shuleni kwa mtoto wako MALANGALA SEC SCHOOL.

Unajaribu kuuliza “kuna shida gani?”Unajibiwa kuwa utafahamu hapo hapo, muhimu ufike kwanza. Na zaidi sana unaambiwa ujitahidi ufike haraka iwezekanavyo.

Uko Dar es salaam na shule hiyo iko Kilimanjaro. Kwa kufikiria gharama za kwenda huko tena haraka iwezekanavyo, inakubidi uulize shida ni ipi haswa

Unaambiwa ni muhimu sana kufika kwani ni tatizo kubwa limetokea.
Mpiga simu anakata simu
Unaanza kupata wasi wasi ni nini kimetokea huko.

Inakubidi uanze mpango wa ghafla kwa ajili ya safari hiyo. Mfukoni huna hela, account bank haina kitu. Kuna malipo umetoka kuyafanya hivi karibuni hivyo hela ya ghafla hauna.

Na inakubidi ukate tiketi mapema ya kwenda kilimanjaro ili isije kutokea namna ukakosa usafiri na umeshaambiwa kuna tatizo kubwa.
Akilini kwanza unajiuliza kuna tatizo gani huko lakini unajiuliza unapata wapi hela ya haraka hivo. Unapata wazo la kuongea na boss wako.

Kwanza, umjulishe kinachoendelea ili upate ruhusa ya haraka lakini pia kumuomba msaada wa kifedha kama rafiki, kwani ni rafiki yako pia pamoja na kuwa ni boss wako.

Boss anakuelewa anakupa ruhusa ya kwenda na anakusaidia kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya huko unakoenda.

Unafanya haraka kukata ticket ya safari unapata gari ambalo safari itaanza saa kumi na mbili asubuhi.
Unafurahi, angalau umepata suluhu ya haraka haraka, Mungu ni mwema.

Usiku unakuwa ni mrefu sana ukijiuliza ni nini kinaendelea. Una mawasiliano na mwalimu mmoja pale shuleni ambaye huwa unaongea naye maendeleo ya mtoto wako
Kila ukimpigia hapatikani na texts zote hazifiki. Ni kama hayupo hewani, hivyo huna mtu wa kumuuliza mwingine zaidi

Asubuhi na mapema unaamka unawahi shekilango kupanda hilo Basi.
Safari inaanza, kama saa moja hivi.
Simu ile ya mwanzo inaita tena, unapokea anakuuliza “umefikia wapi?”unamjibu uko njiani umeshapanda basi

Anakujibu, “ni heri, ukifika kilimanjaro njoo moja kwa moja mpaka shuleni, usianze kwenda sehemu yoyote hata kama utakuwa umefika jioni sana”
Halafu anakata simu. Anakushtua sanaa. Unajaribu kumpigia tena akuambie kuna shida gani,
unapiga hapokei tena

Safari inafika Kama nusu hivi,
Gari linapata matatizo
Mafuta yanaanza kumwagika wakati gari bado linaendelea na safari.
Ile dereva anashika break ghafla chuma fulani kinachomoka kwenye gari, tatizo jingine hilo. Unakaa muda mrefu gari likitengenezwa

Mara jitihada za kulitengeneza Gari zinagonga mwamba, wanaamua kuwaletea gari jingine lililokuwa Tanga mjini.

Gari linaletwa imeshakuwa jioni tayari.
Umeshachanganyikiwa mpaka basi
Unapanda ndani ya gari lililokuja
Baada ya dakika kama 20. unapigiwa tena Unaulizwa ulipofika Unaanza kumuelezea kilichotokea.

Anakupa pole halafu anakata simu
Unachanganyikiwa tena unafika Kilimanjaro eneo shule ilipo saa saba za usiku.

Kwa muda huo huwezi kwenda moja kwa moja shule

Asubuhi buhi na mapema unaamkia shule. Unafika shule unakuta wanafunzi wamejikusanya mahali fulani na
wengine wakilia Ni jambo la kawaida kuwaona wanafunzi wakilia shule kwani kuna viboko.

Lakini vilio hivi vinakushtua kidogo.
Unaamua kuelekea ofisini kwa mkuu wa shule, lakini ofisi zimezingilwa na wanafunzi ambao wanalia
ni kama kuna tukio limetokea.

Unashtuka zaidi pale
ambapo unainua macho yako na kuona baadhi ya walimu wakilia.
Hadi Walimu wanalia?!
Kuna nini?!

Hayo alikuwa akituelezea Mr. Martin katika kipindi chetu cha visa na mikasa.
Nini kilikuwa kimetokea pale?

walikuwa wanalia kwa sababu gani hadi walimu?

Na je, aliitwa kwa sababu gani?
Je, lilikuwa ni kosa yeye kuchelewa kufika?!

Sehemu ya pili ya story hii inajibu yote hayo. Unaweza kupata break fupi kwa ajili ya sehemu ya pili.

SEHEMU YA PILI

Baada ya kufika shuleni na kukuta wanafunzi wanalia halafu wamejikusanya vikundi vikundi, alisogea mbele Mr Martin na kushangazwa zaidi kuona hata walimu
pia walikuwa wakilia.

Ikabidi aende moja kwa moja kwenye ofisi ya mkuu wa shule
Alipofika kwa secretary aliambiwa asubiri kidogo mkuu wa shule aitwe kwani yupo katika ofisi ya walimu.
Mzee Martin hakuweza kuendelea kusubiria hivo alienda moja kwa moja kwenye ofisi ya walimu.

Alifika mlangoni ambapo wanafunzi wengi walikuwa wamejaa pale nje
Akawauliza, “kuna kitu gani kinachoendelea hapaa?!”
ndipo wakamuambia kuwa Mwanafunzi mwenzao amewatoka (amefariki) Mr Martin alishtuka sana na kwenda mbio moja kwa moja mpaka ndani ya ofisi kumbe kuna mwili wa mwanafunzi humo ndani ambaye amefariki na ndio sababu ya vilio vyote
Aliingia ndani ya ofisi kwa speed wala hakuna ambaye angeweza kumzuia pale.

Alifika na kufungua mwili haraka haraka

Alipigwa na butwaa kubwa sana pale anapofungua na kuona kumbe sio mwili wa mtoto wake. Maana akilini na moyoni mwake haraka haraka alikuwa ameshawaza kuwa ndo basi tena hayuko na mtoto wake.

Ni jambo la huzuni kwamba shule imepoteza mwanafunzi wao lakini angalau kwa mzee martin ilikuwa ni faraja kwake kwani mawazo yaliyomjia
haraka hapo mwanzo yalikuwa huyo ni mtoto wake, kwani wito wake pale shuleni ulikuwa ni wa dharura
sana na aliambiwa awahi haraka iwezekanavyo

Sasa alianza kujiuliza ni nini sababu ya wito wa haraka kiasi kile. Akifikiria zaidi aliyefariki sio mtoto wake. “Kuna kitu gani kinaendelea?”

Mkuu wa shule alitokea kwa nyuma na kumshika mkono Mr Martin na kumpa ishara ya kwamba watoke nje mara moja.

Wanafunzi walitangaziwa kurudi madarasani zoezi litakaloendelea watajulishwa. Mkuu wa shule akamwambia Mzee Martin kuwa mtoto wake yuko hospitali na yuko hali mahututi. Kuuliza nini kimetokea akaambiwa atasimuliwa Ngoja wajaribu kwanza kwenda tena kama wataruhusiwa kuingia kumuona

Walipofika hospital tena hawakuruhusiwa kuingia ICU
Martin akamuuliza mwalimu “ni kitu gani kimetokea?” Mwalimu akawa anaogopa kuongea kilichotokea, Wakati huo simu ikapigwa kutoka shuleni kuja kwa mkuu wa shule. Akaambiwa anahitajika pale shuleni haraka iwezekanavyo

Na kumbe Mbunge na mkuu wa wilaya wameshafika pale shuleni pamoja na viongozi wengine wa serikali pamoja na polisi.

Na baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vimeshafika kuchukua habari huku wakizuiwa na polisi kuchukua taarifa yoyote.

Waliamrishwa Camera zote zizimwe
Wakisema habari haiwezi ikatolewa ili hali kizima hakijaeleweka (sasa walikuwa sahihi au hawakuwa sahihi, mimi sifahamu)

mkuu wa shule alikuwa kama kachanganyikiwa baada ya kuongea na simu ile, wakati huo Martin alikuwa
hajajua kinachoendea kwa wakati huo.
Mkuu wa shule aliondoka haraka pasipo kujulikana kaelekea wapi. Martin akabaki na bumbuwazi hajui hili
wala lile. Ikabidi aendelee kuwepo pale maeneo ya hospitali. Mawazo yake yote sasa ni kwa mtoto wake, ni nini kimemtokea.

Baadaye kidogo hivi kama nusu saa alifika mkurugenzi wa halmashauri pamoja na baadhi ya viongozi
wengine wa serikali. Walifika wakiwa na wanafunzi wawili kutoka huko shuleni. Na hiyo ndiyo sababu ya Mr Martin
kuwatambua hao viongozi na kuamua kuambatana nao.

Alijaribu kuwaomba wamsaidie aweze kumuona mtoto wake. Wakati huo baadhi ya madaktari walikuwa wameshafika na kuanza kuzungumza na waheshimiwa. Kumbe walikuja kupata taarifa za huyo mtoto aliyepo hapo hospitali ambaye ni mtoto wake Martin

Sasa kibaya kinakuja kuwa, pale pale taarifa zikaja kuwa naye amefariki tayari. Mr Martin alikuwa ni kama kapigwa mshale katikati ya kifua.
Alihisi ni kama yuko ndotoni au kachanganyikiwa. Mwili ulitolewa ICU uliletwa wakauona na Mr Martin akathibitisha kuwa ni mtoto wake kweli.

Sasa kitu kilichokuja kumshangaza zaidi Mr Martin ni kuona mwili wa mtoto wake ulivyokuwa umekatwakatwa vibaya. Yaani ni alikuwa na majeraha makubwa mnoo Akakumbuka hata mwili wa yule wa shuleni ulikuwa umekatwa katwa usoni Alipiga kelele kwa uchungu mkubwa sanaaa lakini wakamshikilia Ukapelekwa chumba cha kuuhifadhi, na Martin akaambiwa huo mwili ni mali ya polisi kwa sasa mpaka uchunguzi utakapo kamilika.
Kumbe kuna kitu kilichokuwa kinaendelea na ndio sababu ya mkuu wa shule kukimbia. Na ndio Sababu
pia ya ujio wa hao wakuu wa serikali pamoja na polisi

Machozi yalimtoka Mr Martin akitusimulia hayo katika kipindi chetu cha visa na mikasa.

Ili kujua ni tukio gani lililowapata watoto hao mpaka kuifikia polisi na mkuu wa shule kukimbia basi pata break fupi tuone majibu yote.

SEHEMU YA TATU
(The Last Episode)
Wanasema ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Filauni.
Katika shule ambayo ilionekana bora miongoni mwa shule nyingi za secondary isingetarajiwa kukuta
kwamba kuna kitu cha namna ile kinafanyika.

Mr. Martin aliiamini sana shule hiyo. Na ndio sababu ya kumpeleka mtoto wake pale. Mkuu wa shule hiyo ya MALANGALA SEC SCHOOL
alikuwa anafanya kazi katika Kampuni binafsi ya kutengeneza Viberiti
Hiyo ikiwa ni sehemu yake ya part time job, kwani boss wa kampuni hiyo alikuwa ni rafiki yake hivyo akampa nafasi kubwa tu katika hiyo kampuni.
Jambo hilo likamfanya kuwa na access ya taarifa nyingi za kampuni, na kwa sababu alikuwa ni mdadisi pia aliweza kujua taarifa zote.

Sasa Kwa sababu ya tamaa ya fedha na ubaya wa moyo wake, nia mbaya iliingia ndani yake ya kutaka kupata
fedha zaidi kutoka katika kampuni hiyo.
Hivyo akaamua kutafuta vijana ambao atakuwa anawapa ramani nzima ya store ya kampuni halafu wanaiba mzigo na kutunza mahali akauze yeye
Na kutokana na kuogopa kupata reputation mbaya kwenye jamii yake kwani ni mkuu wa shule, hakutaka
kutumia vijana wa mtaani kwake au jirani, lakini pia alihisi watahitaji gharama kubwa zaidi Ikabidi atafute ambao hawako kwenye jamii yake na ambao wanamuogopa hawatadai kikubwa

Alienda akawatafuta wanafunzi wake kadhaa ambao aliwajua kwa tabia zao na muonekano wao watafaa kwa mpango huo, na miongoni mwao ni akiwepo mtoto wa mzee Martin.
Aliwaambia atakuwa anawapa ramani nzima ya kule na muda wa kwenda na taarifa zote.

Na hata kutoka nje ya shule alitumia mamlaka yake kuwatoa nje bila kuathiri chochote wala kushtukiwa.
Walifanya matukio matatu makubwa ya wizi successfully na hela zao alikuwa akiwalipa vizuri kama walivyo kubaliana. Walikuwa ni wanne jumla.
Waliitunza siri ile kwa ukamilifu kabisaa wala hakuna waliyemuambia.
Na mkuu wa shule alihakikisha
anawafanyia upendeleo katika mambo yao mengi hapo shuleni ili kuendelea kuwatunza katika himaya
yake.

Wanasemaga siku za mwizi ni Arobaini. Na sasa za kwao ziliishia nne. Walipanga tena tukio la nne, kama kawaida mkuu wa shule akawapa ramani na formula huku naye akisaidia
mambo fulani.

Baada ya kuchukua kigari walichokuwa wakikitumia (aina ya kirikuu)
Walifika mpaka eneo la tukio na kulitunza gari hilo la kubeba bidhaa sehemu ambayo wanawekaga siku
zote.

Jengo hilo lilikuwa na walinzi wa bunduki kutoka kampuni fulani ya ulinzi, na walikuwepo wamasai ambao hawatumii bunduki wao walikuwa na vile visu vya wamasai na fimbo zao
Sasa upande walio ingilia ulikuwa ni upande wa walinzi wa bunduki.
Lakini kutokana na mbinu ambazo
walizisuka vizuri, waliweza kuwapita na kuingia ndani na gari yao kwani kuna mambo mkuu wa shule alikuwa ameshayatengeneza tayari.
Waliingia ndani ambapo sasa wanalinda wamasai

Sasa katika harakati za kubeba na kuweka mzigo kwenye kirikuu ikatokea bahati mbaya kumbe kuna masai wawili walikuwa hawajapuliziwa dawa ya kuwazimisha kama walivyofanyiwa wengine. Na kazi hiyo pia
ilifanywa na yule mkuu wa shule.

Hivyo walizisikia zile purukushani, wakaamua kusogea ndani na ndipo walipo wakuta wale vijana
Vita kali ilizuka ambapo vijana walipigwa sana, wawili
wakakimbia na kirikuu, wawili waliobaki wakawa wanapigana na hao masai huku wanakimbia ambapo kwenye yale mapigano Walijeruhiwa sanaa kwani wale masai walitoa visu vyao, na walikuwa wanavirusha bila huruma.

Walifanikiwa kutoka nje salama kwani walikuja kusaidiwa na wale walinzi wa bunduki ambao tayari walikuwa wanajua kila kitu kwani wameshalipwa na mkuu wa shule

Vijana waliachiliwa wakakimbia kwa miguu. Na kwa sababu walikuwa wamejaruhiwa sanaa, na damu nyingi zilikuwa zikiwatoka. safar yao haikufika
mbali walianguka barararan na kupoteza fahamu, ambapo alitangulia mmoja, akaanza kuvurutwa na
mwenzake na huyo baada ya dk kama 10 akafuata. Kibaya zaidi ni kuwa miongoni mwa hao wawili ndo alikuwepo mtoto wa mzee Martin.
Waliokotwa na wasamalia wema na kupelekwa hospitali.

Sasa wale wawili waliofanikiwa kutoroka, wakaona hawawezi kuitunza hiyo siri kwani hakuna atakayejua
wale wengine walipo. Hivyo walichukua simu (shule za boarding wanafunzi huingia sana na simu kinyume na sheria) na kuwatafuta wazazi wao na kuwaeleza kisa chote.

Na ndipo wazazi wakapiga simu kwa mkurugenzi wa halmashauri na mzazi huyo huyo akapiga simu pia kwa mkuu wa wilaya, na habari zikasambaa

Na kwa bahati nzuri kwenye mfuko wa mtoto wa Mr Martin kulikuwa na kikaratasi cha mtihani kinachoonyesha jina la shule yao. Hivyo kule hospital walipoona waliingia kwenye website ya shule na kuchukua namba ya shule
walipiga simu mara moja kwa sekretari wa shule na kumueleza kilichotokea
Na hicho ndicho kilichotokea na kusabisha vifo vya hao wanafunzi wawili na ndio sababu mkuu wa shule
alikimbia japo baadaye alikamatwa na kuwekwa ndani Mzee martin alilia sanaa wakati akitusimulia hayo katika kipindi chetu cha visa na mikasa.

Kwa kweli inasikitisha sanaMaana ilikuwa ni kama masihara na kumbe ndo amempoteza mtoto wake hivo.

MWISHO
 
Back
Top Bottom