Mzee Kingunge N. Mwiru atangaza Rasmi kuachana na CCM

Mzee Kingunge ameitisha press conference kuzungumzia mwenendo Wa Uchaguzi. Msikilizeni
 
Kama anataka kwenda ukawa si aende tu kuliko kupoteza muda kwa kurudia mambo ambayo yameshazungumzwa na kila mtu anafahamu kitu muhimu chama hakikutaka kusimamisha fisadi

Kama ni hivyo, wewe wasiwasi wako ni upi? Mbona Dr Slaa alitoa ya Moyoni, mbona Prof Lipumba alitoa ya Moyoni, mbona Mzee Sumaye alitoa ya moyoni. Tanzania ni nchi huru. Hata wewe ukitaka unaweza kuita Waandishi na ukaamua kuhamia ACT,TLP, CUF et al. Cha muhimu ni kutovunja sheria za nchi
 
Huko alikohamia Mgombea wake jee kanuni zilifuatwa? Alipitishwa kuwa Mgombea Urais wa Ukawa kabla hata hajajiunga na Chadema jee taratibu ndivyo zisemavyo? Hata Mkutano Mkuu wa Chadema ulipoutishwa Pale Mliman city Mbowe aliamuru wanaokubali Fisadi kuwa Mgombea wapuge kelele za ndio bila ya kujua huo mkutano pia ulisheheni wageni waalikwa kibao tu
 
Mzee Kingunge muda huu live itv anaongea na vyombo vya habari


karibu kwa updates

-------
-------

Anaanza kwa kueleza nini yalikuwa malengo ya kuundwa kwa ccm

Mchakato wa kumpata mgombea urais ccm ulikuwa na mizengwe mchakato haukufuata kanuni

Anakumbushia mchakato wa kumpata mgombea urais mwaka 1995 ulivyokuwa wazi na kanuni kufuatwa kwa kuwapa nafasi wagombea kueleza kwenye kamati kuu kwanini wanagombea


Pia mwaka 2005 halikadhalika hali ilikuwa hivyohivyo kwa wagombea wote 11 walijieleza na kuulizwa kila mmoja maswali matatu na huo ndo utaratibu unaoendana na katiba na taratibu zetu

Kilichotokea mwaka huu ni tofauti kabisa na kilichotokea 1995 na 2005, safari hii mwenyekiti wetu ni Mh. Kikwete na kilichotokea nchini kwetu ni jambo kubwa.


Mimi pale ambapo naona katiba inachezea au inavunjwa au inakusudiwa kuvunjwa nakemea kwa nguvu zangu zote
 
Kingunge-1972 akiwa RC wa Singida kwenye marekebisho ya Katiba kuhusu wabunge wanaoteuliwa kuwa wakuu wa mikoa,kwenye caucus ya chama iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Kawawa alipinga marekebisho ya katiba yenye lengo la kulinda maslahi ya wachache!!!
 
lowasa keshafanya maamuzi sasa yy anasumbuka na nn? si amfuate huko aliko wakafanye siasa-kwani huko lowasa alipo kunq kikao gani kilimpitisha?
 
Hiki kizee kilimuendesha sana na kumjaza hofu Mzee Mkapa alipotaka kumkata Jk kwenye mchuano wa Urais 2005 kikafanikiwa kwa ushirikiano na wana genge wenzie jina Lowassa na Rostam wakawapania na baadae kuwasamabaratisha wazalendo wawili Mzee Sozigwa na Butiku waloandaa file jeusi la Michezo yao michafu na ya hovyo, Safari hii wakajaribu tena bila ya kujua wanaetaka kumhadaa alikuwa mwenzao na anazijua mbivu na mbichi, Sasa kingunge yupo njia panda ama Achague Ccm au Lowassa muda unayoyoma kashindwa na anashindwa kufanya uamuzi. Siasa ni dynamic game Mzee alisahau kuwa Mbinu za 2005 zikizofanikiwa sio lazima zifanikiwe 2015

ukweli mtupu mkuu japokua nasikitika kuna wengine hawatoweza kukuelewa.
 
Halafu huyu Mzee akijikiunga Chadema kesho utamsikia kwenye majukwaa anasema ccm haijafanya kitu halafu watu wamnashangilia.....
 
Matangazo yanarushwa live na ITV mzee anaongea na waandishi wa habari
========

Anasema kamati kuu haiwezi kusema watu watano au sita ni hawa bila kuwasikiliza, kilichotokea mwaka huu ni tofauti kabisa kilichotokea mwaka 1995, safari mwenyekiti ni Jakaya Kikwete, kilichotokea ni jambo kubwa katika historia yetu na mimi katika historia yangu pale ambapo naona kwamba katiba inavunjwa nimekuwa na tabia ya kusema waziwazi na kuwaambia wenzangu si sawa.

Mwaka 1972 nikiwa mkuu wa mkoa Simiyu, kulikuwa na Bunge Dar es Salaam, nikakuta kuna mswada wa kurekebisha katika kuhusiana na swala la wakuu wa mikoa.



Correction kidogo hapo...!!

1972 akiwa Mkuu wa Mkoa wa SINGIDA...!!
 
Huko alikohamia Mgombea wake jee kanuni zilifuatwa? Alipitishwa kuwa Mgombea Urais wa Ukawa kabla hata hajajiunga na Chadema jee taratibu ndivyo zisemavyo? Hata Mkutano Mkuu wa Chadema ulipoutishwa Pale Mliman city Mbowe aliamuru wanaokubali Fisadi kuwa Mgombea wapuge kelele za ndio bila ya kujua huo mkutano pia ulisheheni wageni waalikwa kibao tu

Fuatilia michakato ya kupata mgombea urais CDM mwaka 2005 na 2010 halafu ndio useme kama kuna tofauti mwaka huu
 
Bado Kingunge anazunguka mbuyu...hajaanza kunena kwa lugha..
 
Back
Top Bottom