Sishangai sana kwa wazee kama hawa kutoa kauli za namna hiyo kwa sababu wanaishi kwa ufadhili wa ccm na hawaoni tatizo ambalo linawakabili waalimu la kuishi maisha ya shida na huku wakidai haki zao miaka nendamiaka rudi. Makada hawa wanaona kili kitu kinachofanyika sasa ni nguvu toka vyama vya siasa lakini wanasahau madai ya waalimu ni ya muda mrefu na yamekuwa yakipuuzwa sasa wamefikia mwisho wa kuvumilia makada wanakimbilia sababu nyepesi. Na tatizo kubwa hawa wanasiasa watoto wao aidha wako shule za nje au wako shule za ada kubwa hivyo hata adha ya mgomo wa waalimu hawapati madhara yake kama mimi na wewe Tuwapuuze makada hawa tuwasaidie kwa kupiga kelele ili waalimu waboreshewe huduma, ili watoe elimu stahiki kwa watoto wetu.
Katika kipindi cha tuongee asubuhi,
Mzee Falijara kada wa CCM akiwa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu ameamuru jeshi la polisi kukamata na kuwatia ndani Walimu wote wanaogoma.
Ameenda mbali na kusema Walimu ni watu wadogo sana katika nchi hii na wanatumiwa ili kuyumbisha Serikali ya Awamu ya Nne.
Amemsisitiza IGP Mwema kuwapa amri makamanda wote ya kuwakamata Walimu wote wanaoendelea kugoma.
Source: Star Tv