MTK
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 8,927
- 6,850
Katika kipindi cha tuongee asubuhi,
Mzee Falijara kada wa CCM akiwa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu ameamuru jeshi la polisi kukamata na kuwatia ndani Walimu wote wanaogoma.
Ameenda mbali na kusema Walimu ni watu wadogo sana katika nchi hii na wanatumiwa ili kuyumbisha Serikali ya Awamu ya Nne.
Amemsisitiza IGP Mwema kuwapa amri makamanda wote ya kuwakamata Walimu wote wanaoendelea kugoma.
Source: Star Tv
kama una hakika ulimsikia huyo mtu verbatim sikuelewi ni kwa nini kwenye jina lake unatanguliza prefix ya Mzee?! au ni Mzee jina? maana huyu angelikuwa mzee kweli angelikuwa anajiheshimu na kuheshimu wanataaluma hawa ambao ndio chanzo cha kuwa tulivyo sisi tunaojiona leo tuna nafasi nzuri na vigogo!! he must be suffering from some unknown mental disorder. down with his superiority complex!