Jayfour_King
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 1,135
- 128
Kwa imani yangu ni kwamba mapenzi mema huanza na mtu kujipenda mwenyewe. Siamini kama unaweza kuwa wewe mwenyewe hujipendi halafu tukategemea ukapenda kwa mapenzi ya dhati watu wengine. Hivyo hivyo naamini kwa jinsi JK alivyotuudhi wafanyakazi wa nchi hii wakati huu ameonyesha chuki ya dhahiri kwetu na jamii nzima ya watanzania. Watoto wa mjini wana sema "punda afe mzigo ufike" ndivyo alivyotufanya na ndivyo anavyoamini. Pia ametufanya jogoo "yaani tuwike tusiwike kutakucha"Mnaoelewa juu ya ubovu wa kauli za yule jamaa ni wachache sana, na yeye analijua hilo, ndo maana akathubutu kusema kuwa ..."sihitaji kura zenu"...
Kwani broda hujasikia watu wanaandamana huko Tabora na Mbeya kuunga mkono hotuba yake?
Anyway, hata kama atashinda, wafanyakazi tumwondolee uvivu kwa kumpigia NO"
Hivyo kama jamii yenye nguvu na ndio wengine huwa tunafanikisha wizi wa kura kwenye chaguzi mbalimbali inabidi tubadilike sasa kwani inaonyesha wazi kwamba aina ya urafiki tulionao wafanyakazi wa tanzania na serikali iliyopo madarakani ni wa mashaka.
Hivyo kwa nia njema tu na nguvu tuliyonayo inabidi tuonyeshe kwamba pamoja tunaweza bila kikwete wala sisiem. Na kwamba sisi wafanyakazi kama jamii ambayo ni ya wafanya maamuzi ya hatma ya nchi tuonyeshe kwamba sisi ni aina ya jogoo ambaye asipowika hakukuchi na tuonyeshe hivyo october.