Mwitikio wa Wananchi juu ya Hotuba kali ya JK dhidi ya TUCTA

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Bi kizee asafiri km 50 kupinga hotuba ya JK

* Amuonya asitumie madaraka yake vibaya

WAZEE zaidi ya 1,000 waliokuwa wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete juzi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee walikuwa wakimshangilia mara kwa mara, lakini si Bi Asha Omary, 70, aliyekuwa kijijini kwake wilayani Kisarawe.

Kikongwe huyo alisikiliza hotuba hiyo, iliyobatilisha mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kuanza leo, kwenye redio akiwa Kijiji cha Bwana, Kata ya Kibuta na hasira alizopata kutokana na kauli za rais, zilimfanya aamue kusafiri takriban kilomita 35 kuanzia saa 1:00 asubuhi kuja jijini Dar es salaam kueleza jinsi alivyokerwa.

“Kama kiongozi wa taifa, rais angetumia maneno ya busara na hekima yasiyo na ukali ndani yake katika kutatua tatizo kwa sababu wafanyakazi wanadai haki yao na wanayo haki ya kufanya hivyo,” alisema Asha alipofika ofisi za gazeti la Mwananchi majira ya saa 4:30 jana.

“Rais amejisahau na anatumia vibaya mamlaka aliyopewa na Watanzania kuwakandamiza wafanyakazi, amesahau kuwa nafasi hiyo imetokana na wananchi wote wakiwapo hao wafanyakazi.”

Bi Asha alikuwa akizungumzia hotuba ya Rais Kikwete kuhusu mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kuanza leo, hotuba ambayo iliwashambulia viongozi wa Tucta kuwa ni "waongo, wanafiki, wazandiki na wafitini" kwa madai kuwa wamekuwa hawawaelezi wanachama wao kuhusu maendeleo ya mazungumzo baina ya pande hizo.

Katika hotuba hiyo ya dakika 95, ambayo pia ilirushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), TBC Taifa na redio Uhuru, Rais Kikwete, ambaye alikuwa akishangiliwa mara kwa mara na wazee hao ambao wengi walivalia mavazi ya rangi za njano na kijani, alitangaza mgomo huo kuwa ni batili kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.

Bi Asha, ambaye ni mkulima wa jembe la mkono, alisema rais hakutumia hekima na busara katika kutatua kero za wafanyakazi bali alitumia cheo chake kuwatisha wafanyakazi katika kutetea haki zao.

Alisema kwamba serikali inapaswa kuweka umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi kwa kuwa ndio wanaotoa huduma zote muhimu kwa wananchi wote hasa masikini ambao ni wakulima.

Alisema rais na familia yake wanatibiwa nje ya nchi ndiyo mana haoni umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi badala yake anatoa majibu ya dharau kuwa kama hawataki kufanya kazi waache.

“Au kwa kuwa rais na viongozi wenzake wanatibiwa Ulaya na Marekani ndio maana anatoa vitisho au anataka uwe kama mgomo wa mwaka juzi kwenye Hospitali (ya Taifa) ya Muhimbili ambako watu walipoteza maisha,” alihoji Asha.

“Kama wafanyakazi nao wakisema liwalo na liwe wakachukua hasira kama alizochukuwa rais, itakuwaje; madaktari, manesi na watumishi wengine wakigoma, je haitasababisha maafa kwa Watanzania?”

Asha ambaye alitumia muda wa dakika 70 kueleza masikitiko yake, alisema wakati rais anawatisha wafanyakazi ili wasigome, anapaswa kufunga safari kwenda maeneo ya vjijini kujionea hiyo misaada ya matrekta na ‘Power Tiller’ kama imewafikia wananchi au inatumiwa na viongozi wa vijiji kwa maslahi yao.

Rais katika hotuba yake alisema serikali haiwezi kulipa kima cha chini cha Sh315,000 kwa watumishi wa umma kwa sababu wananchi wengine watakosa huduma za afya, pembejeo za kilimo na hata vifaa vya elimu na walimu.
“Sisi wakulima hatuwezi kugoma lakini kwa muda mrefu hata hizo pembejeo na matrekta anayoyazungumzia hatuyaoni, mbona hachukui hatua na kutoa hotuba kali kwa maafisa wake ili na sisi tupate hizo pembejeo,” alihoji Asha ambaye ni mtoto pekee katika familia yao.

“Sisi vijijini hatuna huduma bora za afya, maji, barabara, shule na rais anasikia kila siku Watanzania wakilalamikia hali hiyo. Je kwa nini rais asitumie cheo chake kuchukua hatua kutatua matatizo ya wananchi kama alivyoamua kwa wafanyakazi,” alisema Asha kwa hasira.

Akizungumzia kupanda kwa gharama za maisha, Asha alisema enzi za utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, bei za vyakula zilikuwa zinafanana katika maduka yote, lakini sasa kila mfanyabiashara ana bei zake.

“Je serikali inashindwa kusimamia tatizo la kupanda kwa gharama za maisha au rais anawaogopa wafanyabiashara... na kama anawaogopa itakuwaje kwa Watanzania,” alihoji Asha.“Namuomba rais siku moja angalau afanye ziara ya kupita katika maduka na kuhoji au kuangalia bei za vyakula halafu alinganishe na vipato vyetu sisi Watanzania kama tunamudu.”

Katika harakati za kutatua tatizo la ugumu wa maisha yake, bibi huyo alisema alishaenda ikulu mara mbili na kugonga hodi ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), inayoongozwa na mke wa rais, Mama Salma Kikwete ili kuomba mkopo kwa ajili ya kufanya biashara.Asha alisimulia kuwa alifanikiwa kuonana na mmoja wa watendaji wa Wama na kumuelea shida yake, lakini alijibiwa kwamba fedha za Wama zina mlolongo mrefu na kwamba yeye hawezi kuzipata.

“Nilipohoji ni mlolongo gani, hakunifafanulia ila aliishia kuniambia tu kwamba ni mkubwa na huwezi kupata fedha hizi... rudi nyumbani. Nikamuuliza je hizo fedha mnazotangaza kwamba mnawakopesha wanawake ni wanawake wote au mna wanawake maalum ambao wanastahiki, sikupata jibu,” alisema Asha huku akionekana kuwa na hasira.

Baada ya hapo nilijua kuwa fedha za Wama ni za watu maalum na sio kila mwanamke.

Hata hivyo, Asha alimuomba Mwenyezi Mungu ampe amuweke katika afya njema Rais Kikwete ili aweze kutumia hekima na busara katika uongozi wake; amuepushe na kutumia ubabe na cheo chake katika kuwaongoza Watanzania.

“Uongozi ni dhamana aliyopewa na Mwenyezi Mungu na Mwenyezi: Mungu pia ndiye anayeweza kumnyang’anya dhamana hiyo wala si Watanzania kama anavyodhani, hivyo ajitahidi kuwa mwadilifu, mwenye hekima, busara na imani katika uongozi wake,” alisema Asha.Pia aliwaombea wafanyakazi ambao wanataka kuingia katika mgomo kutofanya hivyo kwa kuwa wakifanya hivyo watadhulumu haki za Watanzania.

“Nawaombea kwa Mungu viongozi wa Tucta wawashawishi wafanyakazi wasigome ili wasibebe dhima ya kudhulumu haki za Watanzania watakaokosa huduma mbalimbali kwa muda wote watakaogoma, Aaaammmiiin,” alisema Asha ambaye ni mkulima wa kilimo cha jembe la mkono.

Source: Mwananchi
 
Huyu bibi ni mjasiri sana i wish watanzania wangelikuwa wajasiri kama bibi huyu
 
Bi kizee asafiri km 50 kupinga hotuba ya JK

* Amuonya asitumie madaraka yake vibaya

Bi Asha Omary, 70, aliyekuwa kijijini kwake wilayani Kisarawe.
Kikongwe huyo alisikiliza hotuba hiyo, iliyobatilisha mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kuanza leo, kwenye redio akiwa Kijiji cha Bwana, Kata ya Kibuta na hasira alizopata kutokana na kauli za rais, zilimfanya aamue kusafiri takriban kilomita 35 kuanzia saa 1:00 asubuhi kuja jijini Dar es salaam kueleza jinsi alivyokerwa.

"Kama kiongozi wa taifa, rais angetumia maneno ya busara na hekima yasiyo na ukali ndani yake katika kutatua tatizo kwa sababu wafanyakazi wanadai haki yao na wanayo haki ya kufanya hivyo," alisema Asha alipofika ofisi za gazeti la Mwananchi majira ya saa 4:30 jana.

"Rais amejisahau na anatumia vibaya mamlaka aliyopewa na Watanzania kuwakandamiza wafanyakazi, amesahau kuwa nafasi hiyo imetokana na wananchi wote wakiwapo hao wafanyakazi."

Bi Asha alikuwa akizungumzia hotuba ya Rais Kikwete kuhusu mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kuanza leo, hotuba ambayo iliwashambulia viongozi wa Tucta kuwa ni "waongo, wanafiki, wazandiki na wafitini" kwa madai kuwa wamekuwa hawawaelezi wanachama wao kuhusu maendeleo ya mazungumzo baina ya pande hizo.

Katika hotuba hiyo ya dakika 95, ambayo pia ilirushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), TBC Taifa na redio Uhuru, Rais Kikwete, ambaye alikuwa akishangiliwa mara kwa mara na wazee hao ambao wengi walivalia mavazi ya rangi za njano na kijani, alitangaza mgomo huo kuwa ni batili kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.

Bi Asha, ambaye ni mkulima wa jembe la mkono, alisema rais hakutumia hekima na busara katika kutatua kero za wafanyakazi bali alitumia cheo chake kuwatisha wafanyakazi katika kutetea haki zao.

Alisema kwamba serikali inapaswa kuweka umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi kwa kuwa ndio wanaotoa huduma zote muhimu kwa wananchi wote hasa masikini ambao ni wakulima.

Alisema rais na familia yake wanatibiwa nje ya nchi ndiyo mana haoni umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi badala yake anatoa majibu ya dharau kuwa kama hawataki kufanya kazi waache.

"Au kwa kuwa rais na viongozi wenzake wanatibiwa Ulaya na Marekani ndio maana anatoa vitisho au anataka uwe kama mgomo wa mwaka juzi kwenye Hospitali (ya Taifa) ya Muhimbili ambako watu walipoteza maisha," alihoji Asha.

"Kama wafanyakazi nao wakisema liwalo na liwe wakachukua hasira kama alizochukuwa rais, itakuwaje; madaktari, manesi na watumishi wengine wakigoma, je haitasababisha maafa kwa Watanzania?"

Asha ambaye alitumia muda wa dakika 70 kueleza masikitiko yake, alisema wakati rais anawatisha wafanyakazi ili wasigome, anapaswa kufunga safari kwenda maeneo ya vjijini kujionea hiyo misaada ya matrekta na ‘Power Tiller' kama imewafikia wananchi au inatumiwa na viongozi wa vijiji kwa maslahi yao.

Rais katika hotuba yake alisema serikali haiwezi kulipa kima cha chini cha Sh315,000 kwa watumishi wa umma kwa sababu wananchi wengine watakosa huduma za afya, pembejeo za kilimo na hata vifaa vya elimu na walimu.
"Sisi wakulima hatuwezi kugoma lakini kwa muda mrefu hata hizo pembejeo na matrekta anayoyazungumzia hatuyaoni, mbona hachukui hatua na kutoa hotuba kali kwa maafisa wake ili na sisi tupate hizo pembejeo," alihoji Asha ambaye ni mtoto pekee katika familia yao.

matatizo ya wananchi kama alivyoamua kwa wafanyakazi," alisema Asha kwa hasira."Sisi vijijini hatuna huduma bora za afya, maji, barabara, shule na rais anasikia kila siku Watanzania wakilalamikia hali hiyo. Je kwa nini rais asitumie cheo chake kuchukua hatua kutatua

Akizungumzia kupanda kwa gharama za maisha, Asha alisema enzi za utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, bei za vyakula zilikuwa zinafanana katika maduka yote, lakini sasa kila mfanyabiashara ana bei zake.
"Je serikali inashindwa kusimamia tatizo la kupanda kwa gharama za maisha au rais anawaogopa wafanyabiashara... na kama anawaogopa itakuwaje kwa Watanzania," alihoji Asha."Namuomba rais siku moja angalau afanye ziara ya kupita katika maduka na kuhoji au kuangalia bei za vyakula halafu alinganishe na vipato vyetu sisi Watanzania kama tunamudu."

Katika harakati za kutatua tatizo la ugumu wa maisha yake, bibi huyo alisema alishaenda ikulu mara mbili na kugonga hodi ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), inayoongozwa na mke wa rais, Mama Salma Kikwete ili kuomba mkopo kwa ajili ya kufanya biashara.Asha alisimulia kuwa alifanikiwa kuonana na mmoja wa watendaji wa Wama na kumuelea shida yake, lakini alijibiwa kwamba fedha za Wama zina mlolongo mrefu na kwamba yeye hawezi kuzipata.

"Nilipohoji ni mlolongo gani, hakunifafanulia ila aliishia kuniambia tu kwamba ni mkubwa na huwezi kupata fedha hizi... rudi nyumbani. Nikamuuliza je hizo fedha mnazotangaza kwamba mnawakopesha wanawake ni wanawake wote au mna wanawake maalum ambao wanastahiki, sikupata jibu," alisema Asha huku akionekana kuwa na hasira.

Baada ya hapo nilijua kuwa fedha za Wama ni za watu maalum na sio kila mwanamke.
Hata hivyo, Asha alimuomba Mwenyezi Mungu ampe amuweke katika afya njema Rais Kikwete ili aweze kutumia hekima na busara katika uongozi wake; amuepushe na kutumia ubabe na cheo chake katika kuwaongoza Watanzania.

"Uongozi ni dhamana aliyopewa na Mwenyezi Mungu na Mwenyezi: Mungu pia ndiye anayeweza kumnyang'anya dhamana hiyo wala si Watanzania kama anavyodhani, hivyo ajitahidi kuwa mwadilifu, mwenye hekima, busara na imani katika uongozi wake," alisema Asha.Pia aliwaombea wafanyakazi ambao wanataka kuingia katika mgomo kutofanya hivyo kwa kuwa wakifanya hivyo watadhulumu haki za Watanzania.

"Nawaombea kwa Mungu viongozi wa Tucta wawashawishi wafanyakazi wasigome ili wasibebe dhima ya kudhulumu haki za Watanzania watakaokosa huduma mbalimbali kwa muda wote watakaogoma, Aaaammmiiin," alisema Asha ambaye ni mkulima wa kilimo cha jembe la mkono.

Source: Mwananchi

Tamwa, Tawla, Kituo cha sheria na haki za binadamu, ubalozi wa marekani na wengineo mnaotoa vyeti kwa watu kadhaa huyu mama anastahili kupewa nishani ya juu ya ushujaa, mwanaharakati wa kweli aliyesimama kusema yaliyomo moyoni hakuogopa jua, hakuogopa uexpose identity yake, hakukaa ofisini wala wapi ametoka openly kusema kitu cha kweli bila kuficha neno. Asipopewa Tuzo utakuwa unafiki wa hali ya juu kwetu sisi wote.

Inanikumbusha yule mama mweusi wamarekani aliyekataa kusimama ili kumpisha mzungu kwenye basi. mpaka leo anachukuliwa kuwa ni chimbuko la harakati za watu weusi kujikomboa. Ndio maana walisema sikimbuki vizuri yale maneno ila ni kama vile she sat so that we could walk, martin luther king walked so that we could run and obama is now running and he is the first black president.

The old lady has walked so that we do what is necessary for our beloved country. What will you do to support the lovely old lady???????
 
Baada ya kuangalia na kusikiliza hotuba ya Jk kwa wezee wa Dar es salaam. Nimeshindwa kuelewa kama wazee wa Dar es Salaam wana hekima na busara. Nionaomba mnisaidie wanajamii. Kutatizwa kwangu kunatokana na kuona wazee wakishangilia rais wao akitoa mipisho bila hata ya kumsikitikia.
 
“Rais amejisahau na anatumia vibaya mamlaka aliyopewa na Watanzania kuwakandamiza wafanyakazi, amesahau kuwa nafasi hiyo imetokana na wananchi wote wakiwapo hao wafanyakazi.”

Ni kweli Bi. Asha Amejisahau. Inawezekana amelewa madaraka. Hatufai toka mwanzo!
 
YUPI HAJATUMIA STAIL YA MBAYUWAYU?MGAYA AU JK
Kwa mfano angalia gazeti la RAIA MWEMA,la leo tarehe 05/05/2010.UKURASA WA KWANZA.
Je ile barua JK aliiona au hakuiona,pia labda Imepikwa baada ya hotuba kutolewa?Naomba tuichunguze jamani kwa makini.

SIASA ZINAHARIBU NCHI HII

Mgaya Umetumia Busara sana. Hongera
 
Nani kakwambia dar kuna wazee? nenda sehemu zote zenye watu wanaojua kutukana vizuri, iwe bandrini, shirika la reli, sokoni, kwenye vilabu vya michezo na vilabu vya pombe hao wanaodhaniwa wazee ndio mabingwa wa matusi na maneno machafu, pale walikuwa wakitathmini uwasilishaji wa yale waliomfundisha kijana wao kuwa mpashaji na mtukanaji aliyefuzu lugha za hovohovyo.
 
Baada ya kuangalia na kusikiliza hotuba ya Jk kwa wezee wa Dar es salaam. Nimeshindwa kuelewa kama wazee wa Dar es Salaam wana hekima na busara. Nionaomba mnisaidie wanajamii. Kutatizwa kwangu kunatokana na kuona wazee wakishangilia rais wao akitoa mipisho bila hata ya kumsikitikia.
Lyangalo, pole usitatizwe, Dar kuna wazee wenye hekima kama walipo wazee wengine mahali popote pale, yaani hekima ya wazee, inatokana na umri wao mkubwa na sio mahali walipo.

Ukienda Uzaramoni kwenye ngoma zao, na ukaona mambo yanayofanyika, kama wewe sii mhusika, unaweza dhania ni mambo ya aibu, lakini wazee wenyewe wa Kizaramo, watasifu na kushangilia, na bado wazee hao wana hekima zao.

Ukienda Usukumani, unawezxa kukuta Mzee wa Miaka 70, anachumbia kabinti ka miaka 15 (tayari kameshavunja..), ili kawe kamke chake cha 20!. Wewe kama sio mhusika wa kabila hilo utaona kama ni ajabu lakini wezee wenzake watampongeza na bado wote muoaji na wapongezaji wana hekima na busara.

Ukienda kwa jamii ya Wabarbaig/Wasandawe na Wataturu, hawavai nguo, wanafuni tuu sehemu sehemu na kinamama maziwa nje. Unahitaji huduma, unajiendea tuu hapo pembeni mnamaliziana tuu kichakani na kuendelea na maisha ya kuokota matunda na kuvinda wanyama, lakini hata wazee hao, pia wana hekima na busara.

Sifa kubwa ya morani wa kimasai ni uwezo wa kumwaga damu ya adui yako within a split of second, ili kuwa shujaa inabidi uue simba, kwa vile siku hizi simba ni protected animals, Morani wa Kimasai, hulazimika kuua ng'ombe in a very brutal way wewe utaona ni ukatili wa ajabu, wezee wa Kimasai watawashangilia vijana wao, na wana hekima na busara zao.

Hivyo ndivyo walivyo Wazee wa Dae es Salaam waliolikwa pale, 90% ni Wazee wa CCM, Wakwere ni Wazaramo wale wale ama ni lao moja, kushangilia mipasho ndizo busara zenyewe kama kushangilia ngoma ya Mdundiko. Hivyo Wazee wa Dar es Salaam wana hekima na busara.
 
Ukidanganywa mara moja sio tatizo, ukidanganywa mara tano mfululizo..........basi hapo tunakila sababu ya kutilia shaka up-stairs ya huyu mkulu
 
Yaan huyu bibi mmoja wa kijijini Kisarawe amebeba ubongo mzuri zaidi kuliko wazee 1000 wa Dar es Salaam waliohudhuria mkutano ule.
 
Baada ya kuangalia na kusikiliza hotuba ya Jk kwa wezee wa Dar es salaam. Nimeshindwa kuelewa kama wazee wa Dar es Salaam wana hekima na busara. Nionaomba mnisaidie wanajamii. Kutatizwa kwangu kunatokana na kuona wazee wakishangilia rais wao akitoa mipisho bila hata ya kumsikitikia.
Analysis yako inachekesha..Hivi ni kweli unaamini kuwa JK alihutubia 'wazee wa Dar es Salaam'? Kaa unaamini hili basi utaamini na mengi mengineyo..lol
 
stunning! jamani ni elimu tu, wapo Watanzania wasiowaoga, wenye kuthubutu kudai haki zao na za wenzao. Huyu bibi jamani bravooo
 
Wote inafaa kumuiga huyu bibi! Tuache uoga na kuwa wajasiri.
 
ndio ubaya huo wa kujibu mambo bila data za kutosha unaishia kutumia nafasi yako kutoa maneno ambayo hayakufikiriwa kabla. this will go to hurt him.
 
Back
Top Bottom