Mwitikio wa Wananchi juu ya Hotuba kali ya JK dhidi ya TUCTA

That's why I no longer trust Tanzanian media. Best subiri atoke madarakani utaona kama haitakuwa kama Kaka Ben, alipokuwa madarakani walipiga kelele ili katiba ibadilishwe aongezewe muda na alipotoka wote tuliona media ilivyokuwa. Kimsingi ni walewale kama walomwimbia kaka Jesus siku ya j2 ya matawi alinyokuwa akiingia Jerusalem na ni walewale walokimbia au walopiga kelele "mwondoe, mwondoshe, msulibishe" siku ya ijumaa kuu. Tuombe uzima ndo tutaconclude na kuelewa watangazaji wetu Bongo!
 
Mimi sielewi
Lakini hata Nyerere alikuwa anatukana sana wakati akiudhika ktk hotuba zake. Sema watu waseme jk hafiti kuwa Rais kwa kuwa kashindwa mwenyewe kutimiza na kulinda alichokihubiri, lakini kama kutukana karibu marais wote wamekuwa wakitukana ama kusema lugha kali kwa nyakati zao.
 
Hivi kwa nini yeye anagomba viongozi wa TUCTA "kuwaahidi wafanyakazi kisichowezekana" wakati na yeye ndicho hicho kilichomuingiza madarakani? Yaani kuahidi wananchi maisha bora na uwongo mwingine kama huo?

Ile siku niliudhika sana. Bora nimerudi toka likizo akili yangu nitaijaza mambo mengine hilo lihotuba linitoke kichwani
 
Mkama ni matusi gani ya mwl. nyerere unayakumbuka, ila nimesikiza juzi tbc radio hotuba ya mwl kwa wafanyakazi alikua mkali lakini si kwa kcc ila ni kwa mabosi walidai marupurupu zaidi, lakini huyu amejinadi kwa kusema sina shida na kura zenu na msiponipigia na nizikose japo wafanyakazi wapo wachache lakini haba na haba hujaza kibaba. Kwa umoja wetu tutashinda
 
Mkama ni matusi gani ya mwl. nyerere unayakumbuka, ila nimesikiza juzi tbc radio hotuba ya mwl kwa wafanyakazi alikua mkali lakini si kwa kcc ila ni kwa mabosi walidai marupurupu zaidi, lakini huyu amejinadi kwa kusema sina shida na kura zenu na msiponipigia na nizikose japo wafanyakazi wapo wachache lakini haba na haba hujaza kibaba. Kwa umoja wetu tutashinda

Katafute ile Hotuba inayosadikika walitaka kumpindua akina kambona. Kusema sitaki kura zenu hiyo ndo deemokrasia ama ulitaka aseme je? kwamba kura zenu mnipe ila siongezi kipato chenu? Sahizi tulipofikia hizi kauli ndo zinatakiwa kwamba sifanyi hiki na kile na nitafanya hiki na kile sasa mpira unabaki kwako kusuka ama kunyoa.
 
Sasa kama ndio kauli basi nawaambie na wasio watumishi wauma kwamba maisha bora hakuna yameshindikana na kama mtanipa kura nipeni kama hamnipi basi tutajua kweli ndizo kauli thabiti, hapa hatupo jeshini anatakiwa awe na kauli nzuri kama zile alizowabembeleza waliochukua pesa za epa warudishe na wengine mpaka leo hawajarudisha na yanaishia hivihivi pesa haijarudi na kesi kama hawatashinda sijui,lugha za delux hatuzitaki
 
Tatizo hapa ni kwamba civil sociaties yaani vyama vya wafanyakazi, siasa na asasi nyingine za raia hapa tanzania hazina nguvu kabisa, rais wa africa kusini akiongea kama kikwete kwenye national tv, cosatu wangeifunga ile nchi na zuma angejiuzulu, hapa kwetu tupo kama makondoo hata kwenye haki zetu za msingi kabisaaa, hivi vyama vya wafanyakazi vilivunjwa nguvu na ccm na kufanywa jumuia za chama na mpaka leo havina nguvu kwa kweli inabidi vijitahidi na viongezi wake wasiogope vitisho vya wana siasa, mgomo si kuandamana tu wanaweza kuhamasisha watu wakakaa nyumbani tu tuone nani atatoa huduma na hao ffu watampiga nani, watawafuata wafanyakazi majumbani wawapige? mimi nasema wakati umefika, soote tukajiandikishe kupiga kura, kama hatuwezi kwenda mtaani kudai haki zetu basi tuzidai kwa njia ya kura, hiki chama kikiondolewa madarakani hata kwa awamu moja tu kitajisafisha sana.
 
Wanaweza wakawa wamepata shinikizo/tishio kwamba wasipofanya hivyo watafutiwa sababu ya kufungiwa vyombo vyao vya habari. Hivi ikitoka directive kutoka State House kwamba vituo hivyo vinatakiwa viitoe hotuba hiyo mara kwa mara, wenye vyombo vya habari wana ubavu wa kukataa?

Kubenea alimwagiwa tindikali na hatimaye gazeti lake likafungiwa. Hakuna kisichowezekana kwa Serikali inayotaka ishinde uchaguzi kwa nguvu hata kama haina sifa za kuweza kushinda.

Star TV ni ya Anthony Diallo aliyetemwa uwaziri baada ya kashfa ya EL na Richmond. Labda anataka kudondokewa na uwaziri tena.
 
Katafute ile Hotuba inayosadikika walitaka kumpindua akina kambona. Kusema sitaki kura zenu hiyo ndo deemokrasia ama ulitaka aseme je? kwamba kura zenu mnipe ila siongezi kipato chenu? Sahizi tulipofikia hizi kauli ndo zinatakiwa kwamba sifanyi hiki na kile na nitafanya hiki na kile sasa mpira unabaki kwako kusuka ama kunyoa.
Mkuu wangu unazungumza vitu ambavyo havifanani kabisa. Hotuba ya Nyerere kuhusu Mapinduzi ya kina Kambona yalihusu Mapinduzi na umwagaji damu na Nyerere aliwalenga wale waliotaka kupindua serikali yake. Hakuna sehemu hata moja alizungumzia kutohitaji kura za Wananchi wakulima au Wafanyakazi.
Pili, mimi nilikuwa Bongo wakati Kikwete akitoa hotuba ya kwanza akiwaomba wafanyakazi kutofanya mgomo... Hii ilikuwa kabla ya mei mosi. Ilikuwa makini na wengi wetu tulimuunga mkono na kuomba majadiliano yafanyike zaidi..Pia niliona mahojiano ya viongozi wa Tucta na star TV..Viongozi hawa walisema kwamba vikao vingi vimekwisha fanyika toka 2008 na hakuna muafaka wowote uliokwisha fikiwa wala hakuna dalili ya kuwepo makubaliano.
Nakumbuka mtangazaji mmoja aliwauliza kama huo haukua wakati mzuri kutokana na uchaguzi kuwepo karibu. Wakamjibu kwamba hakuna wakatimzuri wa kuipa pressure serikali kama wakati huu kwani wamekuwa wakizungushwa pasipo serikali kuzingatia hali ngumu ya maisha ya wafanyakazi ambayo inazidisha rushwa maofisini. Hili halina Ubishi iwe kwa mtazamo wowote ule, rushwa nchini limekithiri kutokana na mishahara midogo na kwa mtaji huo hatuwezi kuendelea hata kidogo.

Katika mazungumzo yaliyofuata rais mwenyewe hakuchukua hatua yoyote kujihusisha na mazungumzo yaliyofuatia. Tatizo la Kikwete ni ufuatiliaji wa maswala magumu..Hana muda wala hajali zaidi ya kuhudhuria sherehe na mazishi - Uswahili mtupu. sasa ilipofikia mei mosi na kutangazwa kwamba viongozi wote hawataalikwa shehere hizo, mzee wa kaya aka mind, na hata aliposikia tena mgomo aka panic na kutoa hotuba ya kijeuri pasipo kufikiria..

Hotuba ya Kikwete ya majuzi na hasa ule mfano wa Mbayuwayu ina maana wananchi na hasa Wafanyakazi hawana AKILI isipokuwa za kushikiwa. Na kibaya zaidi aliwataka wafanyakazi wafikirie zaidi kukosa Ajira zao namaisha yao baada ya mgomo kuliko adha ya mishahara midogo.. Ni ujeuri mkubwa sana inapofikia rais kuwatisha wananchi akitumia ajira na kwamba hawahitaji! atawafukuza kazi kwa kudai haki yao.. kimsingi huu ni Udikteta uliopitiliza..
Binafsi sikuamini na wala sitaki kuamini kwamba Kikwete alijiandaa kuyasema haya kwa wananchi..Nadhani hofu yake ya Upinzani toka ndani CCM ni moja ya hofu kubwa iliyomsukuma kuamiini kwamba Mgaya alitumwa na kuwa madai haya yalikuwa ya kisiasa sana badala ya Ukweli uliosimama. Kikwete hakufanya homeworkyake kujua hali halisi ya wafanyakazi napengine Ikulu kumejaa wasanii watupu ambao hawafanyi kazi zao ila kupiga majungu ya kutafuta mchawi kama ilivyo ktk vikao vya CCM...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom