TUCTA Yampongeza Rais Samia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA), limempongeza Rais Dk. Samia Suluhu. Hassan kwa mabadiliko na maboresho makubwa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na umma, ikiwemo kuogeza kiwango cha mshahara kwa mwaka ambacho kilikuwa hakijaongezwa kwa miaka tisa iliyopita.

Pia, TUCTA imemshukuru Rais Dk. Samia kwa dhamira yake ya dhati ya kuendelea kushirikiana na TUCTA kwa kufungua milango ya majadiliano, kusikiliza changamoto kupitia vikao ambavyo wamekuwa wakifanya na serikali, ikiwemo mkutano wa hivi karibuni walipokutana na Rais.

Hayo yamesemwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa TUCTA, Said Wamba, alipozungumza na waandishi wa habari, juu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi, iliyofanyika mkoani Morogoro hivi karibuni.

"Katika kipindi cha awamu ya sita cha uongozi wa Rais Dk. Samia, kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kushughulikia changamoto mbalimbali za wafanyakazi, ikiwemo nyongeza ya mishahara ambayo ilisimama tangu mwaka 2013,"alisema.

Alisema, wanaipongeza serikali kwa jitihada zake za kuboresha maslahi ya wafanyakazi, kushirikiana na TUCTA kupitia majadiliano mbalimbali yanayolenga kuendelea kuboresha maslahi ya kundi hilo nchini.

Wambwa alisema, jambo la kutia moyo kwao ni kwamba serikali imekuwa na utayari na imefungua milango kwa TUCTA, hivyo watatumia vyema fursa hiyo kufanya majadiliano yenye tija kwa wafanyakazi.

"Vyama vya wafanyakazi siyo chombo cha mapambano, bali ni sehemu mojawapo inayowaunganisha watumishi katika kufanya majadiliano ya changamoto zao yatakayo zaa matunda ya kero walizonazo, wala siyo sehemu ya mapambano na serikali, alisema.

Alieleza kuwa katika kudhihirisha hilo, hivi karibuni walikutana na Rais Dk. Samia na kujadiliana naye masuala mbalimbali ya wafanyakazi, ambapo aliahidi kuendelea kufanya maboresho ya maslahi yao kwa kushirikiana pande zote mbili. Aidha, alisema Rais Dk. Samia alitoa maagizo kwa Wizara husika kukutana na TUCTA, kufanya mazungumzo ya kuendelea kuzifanyia kazi changamoto zilizopo na kutumia vyema fursa iliyopo.​
 
Kuna vyama hapa duniani ni vya kipuuzi! Ila TUCTA, na CCM; nadhani vimepitiliza.
Hata kuvipa hadhi ya vyama unakosea,hivi ni vigenge vya wahuni tu wasaka tonge . Kuna wafanyakazi hasa sekta ya afya wanadai malimbikizo ya nyongeza za mishahara zaidi ya miaka minne hadi leo na Rais anasema bado madai yao yanafanyiwa uhakiki,this is bullshit ! Halafu Tucta wanampongeza.
 
Mshahara wa Julai utakapotoka, moderators naomba mrudishe nyuzi kama hizi
 
Walijadili madhila ya kikokotoo kwa wastaafu? Na Kama walijadili, rais aliahidi kukifuta au alijibu nini? Au wastaafu siyo wanachama wao?
 
SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA), limempongeza Rais Dk. Samia Suluhu. Hassan kwa mabadiliko na maboresho makubwa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na umma, ikiwemo kuogeza kiwango cha mshahara kwa mwaka ambacho kilikuwa hakijaongezwa kwa miaka tisa iliyopita.

Pia, TUCTA imemshukuru Rais Dk. Samia kwa dhamira yake ya dhati ya kuendelea kushirikiana na TUCTA kwa kufungua milango ya majadiliano, kusikiliza changamoto kupitia vikao ambavyo wamekuwa wakifanya na serikali, ikiwemo mkutano wa hivi karibuni walipokutana na Rais.

Hayo yamesemwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa TUCTA, Said Wamba, alipozungumza na waandishi wa habari, juu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi, iliyofanyika mkoani Morogoro hivi karibuni.

"Katika kipindi cha awamu ya sita cha uongozi wa Rais Dk. Samia, kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kushughulikia changamoto mbalimbali za wafanyakazi, ikiwemo nyongeza ya mishahara ambayo ilisimama tangu mwaka 2013,"alisema.
Alisema, wanaipongeza serikali kwa jitihada zake za kuboresha maslahi ya wafanyakazi, kushirikiana na TUCTA kupitia majadiliano mbalimbali yanayolenga kuendelea kuboresha maslahi ya kundi hilo nchini.

Wambwa alisema, jambo la kutia moyo kwao ni kwamba serikali imekuwa na utayari na imefungua milango kwa TUCTA, hivyo watatumia vyema fursa hiyo kufanya majadiliano yenye tija kwa wafanyakazi.

"Vyama vya wafanyakazi siyo chombo cha mapambano, bali ni sehemu mojawapo inayowaunganisha watumishi katika kufanya majadiliano ya changamoto zao yatakayo zaa matunda ya kero walizonazo, wala siyo sehemu ya mapambano na serikali, alisema.

Alieleza kuwa katika kudhihirisha hilo, hivi karibuni walikutana na Rais Dk. Samia na kujadiliana naye masuala mbalimbali ya wafanyakazi, ambapo aliahidi kuendelea kufanya maboresho ya maslahi yao kwa kushirikiana pande zote mbili. Aidha, alisema Rais Dk. Samia alitoa maagizo kwa Wizara husika kukutana na TUCTA, kufanya mazungumzo ya kuendelea kuzifanyia kazi changamoto zilizopo na kutumia vyema fursa iliyopo.​
Nosense
 
Hata kuvipa hadhi ya vyama unakosea,hivi ni vigenge vya wahuni tu wasaka tonge . Kuna wafanyakazi hasa sekta ya afya wanadai malimbikizo ya nyongeza za mishahara zaidi ya miaka minne hadi leo na Rais anasema bado madai yao yanafanyiwa uhakiki,this is bullshit ! Halafu Tucta wanampongeza.
Pale layman wa mtaani anapojikuta anaumia Kwa mambo yasiyomhusu kuliko Mfanyakazi Mwenyew 😀😀

Mimi ni Mfanyakazi na nimeona ahueni awamu ya mama mfano,

Kufuta retention money mwezi July namalizia mkopo wa loan board,

Ongezeni la salary mwaka Jana halikuwa kubwa kwangu ila iliongezeka,

Posho ndio nilizifaidi Kwa rates Mpya japo Bajeti ilikuwa inabana but mwaka huu kasema mwenyewe kwamba wataongeza Bajeti ya posho iendane na viwango Vipya

Pia karudisha annual increment unataka tuseme nini tena,
Mwisho ukiacha mambo mengine mengi ila tunasubiria jambo letu July
 
Pale layman wa mtaani anapojikuta anaumia Kwa mambo yasiyomhusu kuliko Mfanyakazi Mwenyew

Mimi ni Mfanyakazi na nimeona ahueni awamu ya mama mfano,

Kufuta retention money mwezi July namalizia mkopo wa loan board,

Ongezeni la salary mwaka Jana halikuwa kubwa kwangu ila iliongezeka,

Posho ndio nilizifaidi Kwa rates Mpya japo Bajeti ilikuwa inabana but mwaka huu kasema mwenyewe kwamba wataongeza Bajeti ya posho iendane na viwango Vipya

Pia karudisha annual increment unataka tuseme nini tena,
Mwisho ukiacha mambo mengine mengi ila tunasubiria jambo letu July
Mpumbavu kama wewe unayezungumzia tumbo lako ilhali sisi tuzungumzia maslahi mapana ya umma wa wafanyakazi nakupuuza, nakuona kama kahaba wa pale Kimboka akipata danga la kumnunulia Safari beer kwa vile amezoea kunywa gongo anaona kama dunia yote ni yake.
 
Umma upi sasa 😀😀😀😀

Huoni wewe ndio mpumbavu? Kwani aliyoyafanya Rais ni kwangu pekee?

Yaani mpuuzi mmja ambae sio mtumishi eti anaumia sana kuliko sisi Watumishi 🤣🤣
 
Back
Top Bottom