Mwitikio wa Wananchi juu ya Hotuba kali ya JK dhidi ya TUCTA

Pole sana haujui unaloongea. Unadhani Tanzania ni mali ya Kikwete kumbe nchi ya Tanzania ni ya Watanzania. Madaraka yote katika nchi yanatoka kwa wanachi. Kikwete amepewa dhamana na wananchi na anatakiwa kuongoza kadri ya matakwa ya wananchi. Kwa kuwa ametangaza vita dhidi ya wananchi-wafanyakazi anadharau chanzo cha madaraka yake na wananchi tupo tayari kupigana vita hiyo aliyoanzisha ili kurejesha madaraka kwetu wananchi. Kikwete sasa ni rais wa wanyonyaji wafanyabiashara na wanyonyaji wanasiasa.

wewe peke yako ndo unasema hivyo, wenzio walio wengi bado watasukuma gari lake wakati wa kampeni. we utaona.
 
Kikwete kasema vile kwa sababu anajua udhaifu wa katiba yetu, hivyo kulingana na hilo anajua kabisa hata wafanyakazi msipompa kura zenu atashinda tu. Kwanza yeye ndie anateua tume ya uchaguzi na pia Wakurugenzi wa halmashauri ndo wasimamizi wa uchaguzi na hao ndo makada wa CCM. Mi nadhani ifike mahali tukubali kwamba kushiriki uchaguzi chini ya mfumo wa namna hiyo, CCM Itatawala hadi kiama. Wanachofanya ni mchezo wa KEKUNDU weka hapa. Hatuoni ya Zanzibar? Kwani nani asiyejua kuwa Karume ameshindwa na Seif chaguzi zote? Watanzania na vyama vya upinzani makini lazima kwa pamoja tupambane kwanza kurekebisha kasoro za kimfumo katika usimamizi wa uchaguzi ndio hata kura zetu zitakuwa na nguvu ya umma. Kwa mfumo uliopo ni kama maigizo kupiga kura. Mungu ibariki Tanzania.
 
Watanzania,
Hivi wakulima hao wako kundi lipi hapa maana umetaja wafanyabiasha+wanasiasa/wafanyakazi.
Ninavyojua kundi la wakulima ingawa halina watetezi maana vyama vya ushirika ambavyo vilikuwa kimbilibo na watetezi wao waliungana na wanasiasa kuwakandamiza. Na hawa ndio wanaompa kiburi Kikwete!Wakulima!
Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya wafanyakazi na wakulima. Wengi wa wafanyakazi ndio haohao wanaobeba mzingo wa kuwasaidia ndugu zao wakulima maskini. Ndio maana Mwasisi wa taifa hili alikuwa akitaja nchi hii kuwa ya wakulima na wafanyakazi. Kikwete anapombana vita na wafanyakazi anapambana na wakulima pia.
 
wewe peke yako ndo unasema hivyo, wenzio walio wengi bado watasukuma gari lake wakati wa kampeni. we utaona.
Jina lako zuri sana lakini haliendani na haya unayoyaandika. Mwana wa Mungu siku nzote yuko upande wa wanaoonewa. Unamtetea Kikwete wakati ndiye anayewaonea wafanyakazi. Ukiona wanaosukuma gari lake mwaka huu jua ni wale tetere aliowasema Mwanakijiji.
 
Kisa cha mwenye nyumba aliyempa kazi ya ulinzi mbwa ,kisha mbwa huyo akageuka na kula yamini na wezi na kumgeuka mwenye nyumba kumuuma ,kumbwekea na kusaidiana na wezi kuiba au kuhakikisha mwenye nyumba hawafikii wezi na kuwadhuru

sitaki kuongea kitu kuhusu Rais wetu mpendwa
 
Na wenye nyumba ni Wafanyakazi na wakulima...
 
Modes naomba habari hii ikae hapa kwa kuwa ina jambo la kipekee la kujadiliwa yaani vita kati ya Kikwete, wanyabiashara na wanasiasa kwa upande mmoja dhidi ya wafanyakazi.

Kauli ya Kikwete kuwa bora kukosa kura za wafanyakazi kuliko kuongeza kima cha chini na kuwa hata baada ya miaka minane (8) kima cha chini hakitafikia 315,000 ni kauli ya kutisha sana na kutangaza vita na wafanyakazi. Kitu kisichoeleweka ni kwa manufaa ya nani Kikwete anatoa kauli hiyo? Katika kutafakari nimenga'mua kuwa Kikwete anatangaza vita na wafanyakazi kulinda wafanyabiashara na wanasiasa. Hawa ndio wanaofadhili chama chake na pia ni hawa hawa wanasiasa ndio wafanyabiashara. Hataki kuinua maisha ya wafanyakazi kwa vile hataki wafanyabiashara na wanasiasa walipe kima cha chini cha juu kwa wafanyakazi wake. Kwa maana hii Kikwete anabariki unyonyaji kwa wafanyakazi ambao unafanywa na kampuni binafsi, ambazo zingine zinamilikiwa na wanasiasa. Pia anabariki unyonyaki kwa wafanyakazi waliowengi wa Serikali huku wanasiasa wachache wakiwemo wabunge, mawaziri, rais wakilipwa mafao ya juu mno na marupurupu ya kutisha .

Uamuzi wa Kikwete ni kutangaza vita rasmi na wafanyakazi. Kwa hiyo wafanyakazi hima na tuamke sasa kupambana na Kikwete na Serikali yake ya CCM inayojali maslahi ya wafanyabiashara na wanasiasa tu.

Ametangaza hivyo kwa manufaa ya mafisadi kwasababu wanasema wakiguswa nchi haitakalika,sasa ni zamu ya wafanyakazi vs mafisadi halafu tuone nani hatakaa nchini,damn it!
At least hata wakati wa chama kimoja mwalimu aliwajali wafanyakazi licha ya kwamba mgombea mpinzani alikuwa kivuli!
 
Jina lako zuri sana lakini haliendani na haya unayoyaandika. Mwana wa Mungu siku nzote yuko upande wa wanaoonewa. Unamtetea Kikwete wakati ndiye anayewaonea wafanyakazi. Ukiona wanaosukuma gari lake mwaka huu jua ni wale tetere aliowasema Mwanakijiji.

usijaji kutumia majina au mtu alivyo, mimi nimesema ukweli, mimi kama mtz mwenye uhuru wa kuongea, niaweza kukuambia kuwa sijawahi kumpigia kura kikwete, na sitakuja nimpigie hata siku moja. pili, siipendi CCM kabisa. siku zote tumekuwa tukiumiza mioyo tunapoona wafanya kazi, na wakulima wengi wanachukuliwa akili kwasababu ya maslahi ya siku chache bila kufikiria future yao....mfano, kama angesema anaongeza mshahara nakwambia sifa ambazo mngempa hapa zisingetosha pamoja na kwamba selikali ya ccm ina mapungu mengi na inatakiwa kuondolewa madarakani ili tuendelee. siku zote nyie wenyewe ndo mmekuwa mnawasapoti hawa jamaa, sasahivi walipowageuka kidogo tu ndo mnawaka kweli. imagine kama kikwete akitangaza kesho kuwa anaongeza mishahara ya wafanyakazi lakini hakuna subsidies kwaajili ya wakulima, na wanafunzi mikopo inaendelea kuwa migumu kama tunavyojua, wewe mwenyewe hapo utageuka na kuanza kumsifia kwasababu amekupatia kile ambacho wewe (minority) ulikuwa unahitaji bila kujali maslahi ya watu wengine wengi ambao sio wafanyakazi na wanahangaika kutokana na kwamba selikali haiwajali. so, usijijali wewe peke yako na hili liwe fundisho siku ingine watu tuwe tunajali maslahi ya watz wote, sio wafanya kazi tu. sio kwamba kwasababu wafanyakazi wamepigwa chini basi ndo tuchanganyikiwe akili wakati watu wenyewe hata hawaaminiki kesho tu hapa utakuwa wamevaa mashati ya kijani wanapunga bendera ya ccm....

kwa upande wangu mimi, sijali maslahi ya wafanya kazi peke yake, actually ninyi ni fungu moja tu kati ya watz wengi wanaoonewa, tunatakiwa kujali na kuhakikisha maisha yanakuwa mazuri kwa watz wote. nawapa pole lakini kwasababu ya tamko la rais juu yenu, lakini basi tuungane ili kutetea maslahi ya watz wote sio yenu tu. OK!
 
Ni kweli,lakini kubeza misimamo ya wafanyakazi kwasababu unataka haki za hata wananchi wasio na kazi na huku kazi zenyewe zilizopo hazikidhi mahitaji muhimu ya wafanyakazi wenyewe ni kufikiri backwards,hata JK mwenyewe alidanganya maisha bora kwa kila mbongo,wafanakazi wana ushawishi wa kueneza habari njema kuwa sasa basi inatosha kuganganywa,kutukunwa,kutishwa na kuonekana les of a human being wakati wanalipa kodi ambazo ndizo mishahara ya mafisadi,na walimu wahakikishe hongo wanazopewa kuiba kura kwa manufaa ya mafisadi havitawaongezea mishahara wala maisha bora,bali wanajifanya too cheap,hamnazo na hawameogopeshi Rais kama ilivyo kwa mafisadi,ukondoo na ujinga wao utawaponza,wakibadilika watakuwa chachu kwa watanzania wote!
 
Usishangae Tabora maana sisi m Tanzania yote ndivyo walivyo. Sura ya sisi m Diamond Jubilee ndio sura ya sisi m Tanzania nzima. Kila swaga la mwenyekiti wao linawavutia. bwahahahahahahahaha

Sikubali,si mitanzania yote iko hivyo,hiyo ya huko Tabora na some other places maybe,wengine wana maendeleo,nchi igawanywe wakishatia akili wataomba tujiunge tena halafu ubaguzi utaisha,haina haja ya kulisha mikoa ya watu wavivu huku wana chuki na wale wanaowalisha!Nchi ipigwe panga wakiingiza akili wataona umuhimu wa kujiunga maana they will learn it the hard way
 
usijaji kutumia majina au mtu alivyo, mimi nimesema ukweli, mimi kama mtz mwenye uhuru wa kuongea, niaweza kukuambia kuwa sijawahi kumpigia kura kikwete, na sitakuja nimpigie hata siku moja. pili, siipendi CCM kabisa. siku zote tumekuwa tukiumiza mioyo tunapoona wafanya kazi, na wakulima wengi wanachukuliwa akili kwasababu ya maslahi ya siku chache bila kufikiria future yao....mfano, kama angesema anaongeza mshahara nakwambia sifa ambazo mngempa hapa zisingetosha pamoja na kwamba selikali ya ccm ina mapungu mengi na inatakiwa kuondolewa madarakani ili tuendelee. siku zote nyie wenyewe ndo mmekuwa mnawasapoti hawa jamaa, sasahivi walipowageuka kidogo tu ndo mnawaka kweli. imagine kama kikwete akitangaza kesho kuwa anaongeza mishahara ya wafanyakazi lakini hakuna subsidies kwaajili ya wakulima, na wanafunzi mikopo inaendelea kuwa migumu kama tunavyojua, wewe mwenyewe hapo utageuka na kuanza kumsifia kwasababu amekupatia kile ambacho wewe (minority) ulikuwa unahitaji bila kujali maslahi ya watu wengine wengi ambao sio wafanyakazi na wanahangaika kutokana na kwamba selikali haiwajali. so, usijijali wewe peke yako na hili liwe fundisho siku ingine watu tuwe tunajali maslahi ya watz wote, sio wafanya kazi tu. sio kwamba kwasababu wafanyakazi wamepigwa chini basi ndo tuchanganyikiwe akili wakati watu wenyewe hata hawaaminiki kesho tu hapa utakuwa wamevaa mashati ya kijani wanapunga bendera ya ccm....

kwa upande wangu mimi, sijali maslahi ya wafanya kazi peke yake, actually ninyi ni fungu moja tu kati ya watz wengi wanaoonewa, tunatakiwa kujali na kuhakikisha maisha yanakuwa mazuri kwa watz wote. nawapa pole lakini kwasababu ya tamko la rais juu yenu, lakini basi tuungane ili kutetea maslahi ya watz wote sio yenu tu. OK!
Ni sawa wafanyakazi ni sehemu kati ya watanzania wanaoonewa. Lakini hawa wafanyakazi wanahusiana na wakulima na makundi mengine yanayoonewa. Kinachotakiwa mwana wa Mungu ni wewe kushiriki kusaidia katika kupigana vita hivi vya kuonewa na wanasiana wanaoshirikiana na wafanyabiashara. Kesho wafanyakazi wataungana na makundi mengine yanayoonewa kutetea haki zao. Tukianza kupingana sisi kwa sisi tunaoonewa itakuwa vigumu kufikia haraka malengo ya kujikwamua kutoka kwenye unyonyaji wa haya makundi ya wanasiana na wafanyabiashara.
 
Tabora ilokuwa tunu kupigania Uhuru wetu enzi za Mirambo, Isike nk
Tabora palipofanyka maamuzi muhimu ya kura tatu na kutupeleka kwenye Uhuru
Tabora ilokuwa MAkao makuu ya Jimbo la Magharibu enzi hizo- sasa ni mahame imebaki Tanganyika; imetengwa na Tanzania, hakuna barabara za kuiunganisha na Tanzania, hakuna treni miezi sita sasa, Uwanja wa ndege haufai, masika ikifika ndege hazitui.
Tabora ilong'ara kielimu enzi hizo na kutoa viongozi mashuhuri na shule zenye hadhi- St Marys, Tabora Boys/ Girls, Kazima nk; sasa imedorora na kuwa ya mwisho mwisho kwenye matokeo ya Kitaifa.

Miaka 50 ya uhuru, Tabora imerudi nyuma hatua mia badala ya kusonga mbele.

Pole zenu Sikonge na wana Tabora

Nina wasiwasi hawajui walitendalo yawezekana hata news hawapati kama miundo mbinu yote ni Kaputi na bado wanajiona wako kwenye neema TANZANIA BILA NEEMA INAWEZEKANA (POLENI TAABORA)
 
Hivi ndivyo ilivyo Tabora mjini, sasa vijijini ndiyo wala usiseme. Ndiyo maana huu mji umekuwa kiota cha Vibaka maarufu Tanzania kama Merehemu Nyau, Marehemu Surambaya, Marehemu Kessy Mchemba, na wengine wengi wadogowadogo. Mchemba Family karibu wote walikuwa vibaka. Msafiri hadi alichomwa mikono na baba yake na wakapigwa marufuku kwenda kwa mtoto pekee mwenye akili aitwaye Abbas Mchemba ambaye alikuja chezea Costal Union.

Picha ya kwanza ndiyo Sokoni hapo. Kama Dar basi ni Kariakoo.
View attachment 9985

Picha ya pili ni Mita kama 500 kutoka Sokoni na mita kama 20 kutoka kituo cha Mabasi ambacho pia kipo kama mita 480 kutoka Soko kuu la Tabora.
View attachment 9984

Mkuu umenikumbusha mbali sana, Tabora ilikuwa enzi hizo, kwa sasa mzunguuko wa pesa nasikia ni sawa na sifuri. Sijui tena kama Kilimo cha tumbaku bado kinaendelea na kulipa. Karibu 95% ya nyumba ni za udongo wanaita "biscuit" - mtu anayekufahamu akikuona unakunywa soda basi anakutangaza wewe unamatumizi mabaya ya fedha au ni tajiri. Biashara ndogondogo kama nyanya, vitunguu, vitumbua ndiyo vinawaweka watu mjini. Tabora mtu anaamka hajui atakunywa chai au atakula lunch, ikifika jioni anashukuru mungu na kuanza kufikiria tena kesho itakuwaje, yaani maisha ni afadhali ya jana.

Sioni ajabu hao walioandamana maana kama mtu kama kaahidiwa kupewa shs 1,000 kwa Tabora hiyo inatosha kumfanya asahau jana alilala na njaa na kujikuta anashawishika kufanya jambo asilolijua. Nina imani 95% ya walioandamana kuunga mkono hotuba, hawakuwa na muda wa kuisikiliza na kujua JK alisema nini.

Mungu ibariki Tanzania, huenda siku moja tukapata viongozi kutoka mainstream na wenye kukaa chini na kufikiria walikotoka na kuvaa viatu vya wale waliopo na kuwa na moyo wa dhati wa kuwakwamua.
 
Kwa kweli mimi naona bado niko kwenye mshtuko wa hotuba aliyoitoa mkuu wa Taifa letu....nimekuwa nikifuatilia maoni ya watu ktk vyombo mbali mbali na humu jamvini lakini....bado sijaondokwa na fadhaa niliyoipata

Katika maoni yooote niliyo bahatika kuyapitia mi naona Muungwana ajiuzulu tu....
 
Ni sawa wafanyakazi ni sehemu kati ya watanzania wanaoonewa. Lakini hawa wafanyakazi wanahusiana na wakulima na makundi mengine yanayoonewa. Kinachotakiwa mwana wa Mungu ni wewe kushiriki kusaidia katika kupigana vita hivi vya kuonewa na wanasiana wanaoshirikiana na wafanyabiashara. Kesho wafanyakazi wataungana na makundi mengine yanayoonewa kutetea haki zao. Tukianza kupingana sisi kwa sisi tunaoonewa itakuwa vigumu kufikia haraka malengo ya kujikwamua kutoka kwenye unyonyaji wa haya makundi ya wanasiana na wafanyabiashara.

mheshimiwa, tupo pamoja, mimi ni wa kwanza kupigania haki za wanyonge kama ulikuwa haujui na ni mmoja ya watu walioumia moyo kuona wananchi hawaelewi kinachoendelea hapa nchini ktika selikali ya ccm. Mungu atasaidia kuna siku wananchi watakuwa na uelewa wa kinachoendelea na historia hii itabaki kuwa aibu kwa viongozi walioko madarakani kwa sasa na hao waliopita. tupo pamoja mkuu ktk kutetea haki, wala sipingi.
 
Kwa kweli mimi naona bado niko kwenye mshtuko wa hotuba aliyoitoa mkuu wa Taifa letu....nimekuwa nikifuatilia maoni ya watu ktk vyombo mbali mbali na humu jamvini lakini....bado sijaondokwa na fadhaa niliyoipata

Katika maoni yooote niliyo bahatika kuyapitia mi naona Muungwana ajiuzulu tu....
.
Ajiuzulu kwa lipi?. Mbona muda wake umefika na uamuzi ni wa kwako hiyo October 31, kama umrudishe au la!.
 
Ukweli na uongo wa watanzania ni vyema ukadhihirika katika uchaguzi wa october kwani itakuwa bado inakumbukwa kadhia hii aliyoufanyia umma mzima wa watanzania. Nitafurahi kuhudhuria mikutano yake ya kampeni ili nimsikilize anaongea nini hasa pale atakapokuwa anaulizwa maswali magumu kupitia ujinga alioufanya na kushindwa kujibu.
 
JK: Tungekuwa sote tunapiga kura kutokana na maamuzi ya vichwa vyetu, na si myoyo yetu, mjamaa huyu tunaweza kumtokomeza hapo Oct.
 
Mnaoelewa juu ya ubovu wa kauli za yule jamaa ni wachache sana, na yeye analijua hilo, ndo maana akathubutu kusema kuwa ..."sihitaji kura zenu"...
Kwani broda hujasikia watu wanaandamana huko Tabora na Mbeya kuunga mkono hotuba yake?
Anyway, hata kama atashinda, wafanyakazi tumwondolee uvivu kwa kumpigia NO"
 
Back
Top Bottom