Mwitikio wa Wananchi juu ya Hotuba kali ya JK dhidi ya TUCTA

Wakuu, kwa mara nyingine tena Rais ameaibishwa tena na wasaidizi wake.
Kulingana na maelezo aliyotoa Kaimu katibu mkuu wa TUCTA Bw. Mgaya mbele ya vyombo vya habari jana na kuonyesha ushahidi wa barua ya mwaliko wa kikao toka hazina ni kuwa kikao chao cha maridhiano na ujumbe wa serikali kilikuwa kiwe saa 8 na sio kama alivyowatukana JK kuwa wao ni waongo na wanafiki kwamba waliitwa kikaoni saa 4 asubuhi na wakaja saa 8 mchana. Mgaya alifika mbali na kusema waziri Kapuya ( ambaye alimwita ALHAJI AKUDO ) kamdanganya rais na kumsababishia aseme uongo hadharini akiamini kuwa huo ni ukweli.
Naona sasa hawa wasaidizi wake hawana mashaka yeyote na mkuu hata kama ataaibika hadharani kutokana na kumpotosha. Hakuna watakachofanywa. NAANZA KUHISA KUNA MAKUSUDI FULANI KATIKA KUMPOTOSHA.
 
Sasa wale wazee ni wa wapi? kama taarifa zinbasema wazee wa dar?
Tatizo ni kwamba 'wazee wa Dar es Salaam' inaonekana kana kwamba ni special name ya kikundi fulani cha watu, which is illogical, senseless and laughable.lol
 
Sasa ukitaka kujua Tanzania hatuna vyama vya siasa vya upinzani ni hapa. Huyu bibi kajitolea, lakini amimni usiamini, CHADEMA, NCCR, CUF ( hii naiita CCM B) ambako naamini wana matawi ya vijana, ambao ndio hasa wako kwenye shida ya ajira, hawatandamana. Ilitakiwa vyama , vijibu kwa maandamano na viongozi wa vyama hivyo watoe hotuba MBADALA ili tuone utashi wao. Kufafanua hoja za raisi tu, bila action ni unafiki. Vyama vichukue nafasi hii kuandamana na kutoa hope kwa watanzania. Hata vyama vya kijamii kama TAMWA nk navyo vinabidi vimuonyeshe raisi kwamba kakosea. Majeshi watumie muda huu, si kuandamana , lakini wamweleze Mkuu wao Gen. Davis Mwamunyange, Saidi Mwema na yule wa Usalama wa Taifa, kwamba wametuonyesha in advance kuwa hakuna uchaguzi huru mwaka huu. Wameandamana na Amiri jeshi mkuu, ili kutisha umma wa Watanzania, ambao nao ni sehemu. Sasa hilo bado ni jeshi la wananchi?
Tunaomba vyama vya siasa viache unafiki, na viwasaidie wafanyakazi ambao pia ni wanachama wao. Huu ni wakati wa kutake advantage!
Tunataka kujua ukali wa kina Zitto, Dr. Slaa sasa. Tunataka akina Maalim Seif waonyeshe njia sasa. Kama haki sawa kwa wote, iweje wafanyakazi wawe so ignored na vyama vya siasa vimekaa kimya?
NO!
 
binafsi nimempenda bibi ni jasiri,watanzania tungekuwa wote hivi maendeleo chap tu wala haipiti muda, wangekuwepo wazee kama yeye mle ndani kikwete akiutubia skuile chamoto angekiona sababu hata mawe angepigwa na asingejua yametokea wapi. ni jambo la ajabu sana bibi asha kaskiliza redioni kaona mapungufu, mi nahisi wale waliokuwa pale walikuwa hawaskiliza kilichokuwa kikisemwa walikuwa wanamwangalia jamaa akicheka nao wanacheka na kupiga vigele gele, nawashauri wakae chini wasikilize tena mara nyingine, watakaa chini na kumuunga bibi asha mkono na tutapata wazee wengi kama bibi asha
 
Hii si dalili nzuri hataka kidogo ingawa mara nyingine stock pile ya risasi na mabomu huwa inatudanganya kwamba yoyote atakaye kaidi atakiona cha mtema kuni. The same story continues...we live in the world of fantansies and not in the world of realities!!!
 
Hongera Sana Mama kwa upendo wa dhati wa Nchi yako bora useme wenye sikio wasikie na wasio na sikio wadharau wazee kama wewe ndio mulitakiwa muwepo pale Diamond sio wale wengine ambao walienda kutaka waonekana kwamba wanajua kushangilia,Huyu ameona mbali na nadhani amefuatilia mambo yote yanavyoendeshwa kwenye serikali hii akaona hakuna matumaini nadhani Wana JF tuandamane kesho Kuunga Kauli ya huyu mama,kwa kweli amejitahidi kutanabaisha ukweli
 
HAKUNA UMASKINI MBAYA DUNIANI KAMA UMASKINI WA MAWAZO, kAMA AKIJA MTU AKAKUPA MAWAZO YA UPUMBAVU NA WEWE UKAYAPOKEA BASI ATAKUDHARAU SANA NA KUKUONA WEWE NI MPUMBAVU: jK Nyerere
 
Ndo maana Alhaji Akudo alikuwa nyuma ya JK akisikilizia uwongo wake kimyaaaaaa. sijaona chochote anachofanya Kapuya, HATUFAIIII
 
Hii video nimeipata huko kwenye blog ya jirushe, tafadhali msikilize huyo Mzee kwa makini


 
Last edited by a moderator:
Hihiiiii :) , homeboy Kapuya kamuingiza mjini RAIS wetu? Nilifikiri Wanyamwezi ni Vilaza kumbe na sisi tumo..... Daa, hii imekaa vizuri sana.
 
Watanzania wenzangu mnanifurashisha sana, kila siku mheshimiwa akichemsha hamchelewi kuwalaumu watendaji, washauri na wasaidizi wake, mwishoye mtakuja hata kumlaumu paka wake, kuku na ule mwembe nyumbani kwa mzee Abdallah Machinjio. Kwanini tusiangalie ni nani hasa aliyechemsha? Kwanza kama baadhi yetu tulivyoainisha hapa juu sio kila kitu unachoambiwa na wapambe wako ni lazima ukichukulie kama kilivyo la sivyo itakuwa ni hatari kubwa na mtu mzima kama yeye aliyepewa dhamana kubwa na nzito ya kuliongoza taifa hili ni lazima awe na uwezo wa kukaa chini, kufanya tafiti zake, kutafakari, kupembua n.k kabla ya kuja kulihutubia taifa.

Pili tunasahau ya kwamba hao wasaidizi, wapambe, watendaji na washauri ni yeye mwenyewe ndiye aliyewateua na hivyo kama ameteua watu wasio makini ni jukumu lake yeye mwenyewe mteuzi kuwajibika ipasavyo. Analogy nzuri ni kwenye timu za michezo, kwa wale wapenzi wa kandanda watakuwa wanajua ni kitu hutokea pindi timu inapochemsha, ni kocha ndiye huwajibishwa na sio wachezaji
 
This is the longest theater movie, with the world class actors
 
Mi nashangaa mnamlaumu Kapuya msifieni bana ana akili kwani kumuokota mkulu kama huyo basi lazima uwe na akili we Kiongozi gani udanganyike wewe tu kila mara?
 
1.RAIA MWEMA:RAIS KADANGANYWA
2.NIPASHE:TUCTA WASALIMU AMRI
3.MTANZANIA TUKTA WAMJIBU JK
4.MAJIRA:JK KAPOTOSHWA
5.CITIZEN:UNDERFIRE TUCTA CALLS OFF STRIKE
6.MWANAHALISI:KIKWETE ACHEMKA
7.MWANANCHI: BI KIZEE ASAFIRI KM 40KUPINGA HOTUBA YA JK
8.TANZANIA DAIMA:KIKWETE HATIHATI OCTOBA
9.JAMBO LEO:MGAYA AMGWAYA JK
10.DAILY News:TUCTA LEADERS SUSPEND STRIKE.
11.UHURU:TUCTA YAFYATA
Haya, hizo ndizo leadstory au niseme habari moja MUHIMU iliyobeba magazeti, lakini imeandikwa kwa mtazamo tofauti. SASA.....Mfano wewe unatabia ya kununua gazeti moja tu kila siku,na huna tabia ya kumuagiza mtu ila unaenda mwenyewe unachekiiiiiiiii vichwa vya habari halafu unanunua. Hapa leo utachukua/nunua lipi?
TAHADHARI,WAKATI UNATOA MAONI,USIJEPONDA AU KUKEJELI GAZETI LOLOTE.ILA KUSIFIA HIYO IMO,SIFIA SANA GAZETI UNALOLITAKA KULINUNUA.MASHARTI NA KANUNI ZA JF ZIZINGATIWE.

Maoni haya angalau yatatoa mwanga kuwa waandishi waandikapo story,watumie angle/mtazamo ipi/upi unaopendwa na wengi.
 
Duh!! hii nikali inamaana hata yeye hakutumia akili za Mbayumbayu..... kazi kwelikweli
 
Huyu ndiye mzalendo wa kweli. Hawa wengine wote ni wapambe na walamba miguu ya wkubwa. Napata imani kabisa kuwa wale wazee serikali iliwapa rushwa na itakuwa haizidi shs5000/= na kwa sababu ya njaa zao na upeo wao wakazipokea wakaanza kushangilia bila kujua wanachoshangilia, lakini, si walaumu sana maanake waswahili kwa mipasho nidyo wenyewe na siku hiyo waliyapata mipasho ya kutosha zaidi hata ya yale ya zamani ya Muungano na TOT.
 
Back
Top Bottom