Mwitikio wa Wananchi juu ya Hotuba kali ya JK dhidi ya TUCTA

Headline ya The Daily News imetulia kwani imekwepa ushabiki na ushankupe kama uliooneshwa na Uhuru au Jambo Leo. Sina hakika lakini inawezekana magazeti kama Raia Mwema na Mwanhalisi wameandika uchambuzi badala ya habari (reporting). Kwa maana hiyo magazeti mawili ningeyaondoa kwenye hiyo list yako. Hata hivyo ni muhuimu kujua nini zaidi wameandika kabla ya kufikia hitimisho.
 
Unajua shehe yahya hakukosea aliposema rais wa awamu ya tatu atakua mwanamke, si ndio mambo kama haya?mipasho kwa kwenda mbele na kidole kwa juu huku wada wakiitikia sema babaaaa, hapo ndio walipompandisha munkari kama mcheza kiduku. Eti wafanyakazi laki nne watamaliza bajeti ya serikali,ambayo ni trlion 5, hivi hesabu nyepesi tuu ukichukua watumishi 500,000 ukizidisha na 500,000/= mara miezi kumi na mbili utapata trilioni ngapi?kama sio tatu

rais anapojinadi alikuta mshahara wa 45,000/= na sasa 100,000/=, mbona hakusema alikuta petrol 800 na sasa ni 1,800/=. Kwa kweli hakuna maisha bora ila anazidi kuwafanya watu wa mujini kukuna bongo na kuzidisha wizi na watu wa vijijini kuendelea na umasikini sababu wamesahauliwa
 
Hongera Sana Mama kwa upendo wa dhati wa Nchi yako bora useme wenye sikio wasikie na wasio na sikio wadharau wazee kama wewe ndio mulitakiwa muwepo pale Diamond sio wale wengine ambao walienda kutaka waonekana kwamba wanajua kushangilia,Huyu ameona mbali na nadhani amefuatilia mambo yote yanavyoendeshwa kwenye serikali hii akaona hakuna matumaini nadhani Wana JF tuandamane kesho Kuunga Kauli ya huyu mama,kwa kweli amejitahidi kutanabaisha ukweli

Huyu mama sio kiashiria cha JF bali ni kiashiria cha watanzania wote, hivyo wanaotakiwa kumuunga mkono sio JF tu bali Tanzania nzima. Alikuwa anaongea kwa niaba ya watanzania wote. Ona statements zake:

"Rais amejisahau na anatumia vibaya mamlaka aliyopewa na Watanzania kuwakandamiza wafanyakazi, sahau kuwa nafasi hiyo imetokana na wananchi wote wakiwapo hao wafanyakazi."

halafu akasema:

"Kama wafanyakazi nao wakisema liwalo na liwe wakachukua hasira kama alizochukuwa rais, itakuwaje; madaktari, manesi na watumishi wengine wakigoma, je haitasababisha maafa kwa Watanzania?"

akasema:

"Sisi wakulima hatuwezi kugoma lakini kwa muda mrefu hata hizo pembejeo na matrekta anayoyazungumzia hatuyaoni, mbona hachukui hatua na kutoa hotuba kali kwa maafisa wake ili na sisi tupate hizo pembejeo," alihoji Asha ambaye ni mtoto pekee katika familia yao.

"Sisi vijijini hatuna huduma bora za afya, maji, barabara, shule na rais anasikia kila siku Watanzania wakilalamikia hali hiyo. Je kwa nini rais asitumie cheo chake kuchukua hatua kutatua matatizo ya wananchi kama alivyoamua kwa wafanyakazi," alisema Asha kwa hasira.

akaendelea:

"Je serikali inashindwa kusimamia tatizo la kupanda kwa gharama za maisha au rais anawaogopa wafanyabiashara... na kama anawaogopa itakuwaje kwa Watanzania," alihoji Asha."Namuomba rais siku moja angalau afanye ziara ya kupita katika maduka na kuhoji au kuangalia bei za vyakula halafu alinganishe na vipato vyetu sisi Watanzania kama tunamudu."

akamalizia:

"Nawaombea kwa Mungu viongozi wa Tucta wawashawishi wafanyakazi wasigome ili wasibebe dhima ya kudhulumu haki za Watanzania watakaokosa huduma mbalimbali kwa muda wote watakaogoma, Aaaammmiiin," alisema Asha ambaye ni mkulima wa kilimo cha jembe la mkono.

She is a hero no doubt.
 
Nahisi kama kuna ajenda ya kumtetea mtu, kwa nini kama Mkulu kachemka tuseme kadanganywa? Kama ni issue ya kundaliwa speech nadhani bosi kubwa ndiye anayeagiza maudhui ya speech husika na baada ya kuandaliwa anatakiwa kupitia ili kujiridhirisha kwamba kilichoandikwa ndicho anachokusudia kupresent mbele ya hadhira inayolengwa. Kwa hiyo hapo bosi kubwa hakudanganywa, alikuwa anajua anachokisema na hakika alikusudia kufanya hivyo........."akili ya kuambiwa changanya na ya kwako".
 
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi kidogo kuhusu raisi wangu mh.jk kuhusu hotuba yake kupitia kwa wazee wa dsm.

1. Je ilikuwa ni sehemu muafaka kutuma ujumbe kupitia kwa wazee?
2. Je lugha ya vitisho na kebehi aliyotumia mbele ya wazee wake ilikuwa sahii?

Lengo la hotuba yake ilikuwa kuongelea ugeni tunaotaajia juu ya mkutano wa wef na majibu ka wafanyakazi na viongozi wa tucta, je wazee wanahusika vipi na hili?

Je haikuwa busara na bora zaidi kama angewaita waandishi na kuongea nao na kuwaomba wafikishe ujumbe wake?
Kwanini raisi hapendi kukutana na waandishi wa habari live?
Je ni mara ngapi katika kipindi chake ame-interact na waandishi wa habari?

Mi naona kama raisi angekuwa anakutanana waandishi mara kwa mara ange-clarify mambo mengi sana na huenda tungemjua zaidi tumfikiliavyo ndivyo alivyo.

Namshauri mh.raisi asiwaogope waandishi, na ikiwezekana awaite baada ya huu mkutano lada atoe ufafanuzi na kuomba radhi wale wazee kwani ninavyoona hakuwatendea haki lakini pia hata wafanyakazi nao hakuwatendea haki....

"muungwana ni vitendo"
 
SIJAONA EVIDENCE ZA KUITWA KIKAONI SAA 4 HAPA BADALA YA SAA 8. Lakini kama ndivyo,mheshimiwa Kapuya kakosea.
 
Mimi kawaida yangu huwa nanunua/nasoma gazeti la Mwananchi, lakini siku kama ya leo nanunua/nasoma (ninayoyaita MAGAZETI YA JUMATANO), MwanaHalisi na Raia Mwema; Kwa hiyo kama kawida yangu, leo niyo hayo magazeti mawili!!!
 
Wakuu, kwa mara nyingine tena Rais ameaibishwa tena na wasaidizi wake.
Kulingana na maelezo aliyotoa Kaimu katibu mkuu wa TUCTA Bw. Mgaya mbele ya vyombo vya habari jana na kuonyesha ushahidi wa barua ya mwaliko wa kikao toka hazina ni kuwa kikao chao cha maridhiano na ujumbe wa serikali kilikuwa kiwe saa 8 na sio kama alivyowatukana JK kuwa wao ni waongo na wanafiki kwamba waliitwa kikaoni saa 4 asubuhi na wakaja saa 8 mchana. Mgaya alifika mbali na kusema waziri Kapuya ( ambaye alimwita ALHAJI AKUDO ) kamdanganya rais na kumsababishia aseme uongo hadharini akiamini kuwa huo ni ukweli.
Naona sasa hawa wasaidizi wake hawana mashaka yeyote na mkuu hata kama ataaibika hadharani kutokana na kumpotosha. Hakuna watakachofanywa. NAANZA KUHISA KUNA MAKUSUDI FULANI KATIKA KUMPOTOSHA.
Hakuna aliyemdanganya labda nawe kama una ajenda ya siri na Kapuya au unamtetea JK. Anapoongea alikuwa na evidence na ndiyo maana alitamka aliyoyatamka!!! Sasa kusema kadanganywa huo si ukweli na kama ni kweli haikuwa saa nne basi ni yeye mwenyewe kasema uongo kwa wa TZ!
 
Headline ya The Daily News imetulia kwani imekwepa ushabiki na ushankupe kama uliooneshwa na Uhuru au Jambo Leo. Sina hakika lakini inawezekana magazeti kama Raia Mwema na Mwanhalisi wameandika uchambuzi badala ya habari (reporting). Kwa maana hiyo magazeti mawili ningeyaondoa kwenye hiyo list yako. Hata hivyo ni muhuimu kujua nini zaidi wameandika kabla ya kufikia hitimisho.

Hata mimi leo ni gazeti mbili tu kama hapo juu.
 
Headline ya The Daily News imetulia kwani imekwepa ushabiki na ushankupe kama uliooneshwa na Uhuru au Jambo Leo. Sina hakika lakini inawezekana magazeti kama Raia Mwema na Mwanhalisi wameandika uchambuzi badala ya habari (reporting). Kwa maana hiyo magazeti mawili ningeyaondoa kwenye hiyo list yako. Hata hivyo ni muhuimu kujua nini zaidi wameandika kabla ya kufikia hitimisho.
Mkuu umecheza faulo japo mawazo yako mazuri na nayaheshimu sana, nilisema, SIFIA tu usiliponde gazeti. Hapa neno unshankupe halikustahili liwepo.
 
Wale walichukuliwa watu wenye njaa zao na mawazo finyu akapewa posho na kazi moja tu ya kushangilia bila kujali wanashangilia nini.
 
Hivi ndivyo inatakiwa iwe, we must dare not onl to talk but also to take actions and necessary actions,
watu wakipata tukio hukimbilia kujaza threads tu hapa kwenye jf na kuleta wakati wingine hata majungu na umbea lakini hamna hatasiku moja mtu akatoa wazo la kuchukua hatua, tujifunze kwa mama huyu...inabidi tumpe hata zawadi na sio kungoja azawadiwe na watu wengine...
 
Tall mbona una limit watu wasieleze bana? sasa siungeweka vote tu hakuna kuandika ukisema kuandika tena siyo uchaguzi kaka. Sasa mimi nacheza faulo hapa.
Kwanza ningeyaona tu ningesema kuna jambo hapa mpaka hawa wanasema hivi kwa sababu kila mtanzania alisikia hivyo gazeti ni playback sasa playback ikija vibaya inakuwaje? Potelea mbali magazeti yangu mimi huwa 1)Mwananchi 2)Tanzania Daima 3)Jumatano (2): Haya magazeti manne hata yakiandika heading mbaya lazima niyanunue. Sasa tall unakosea ukisema watu wachague gazeti watakalonunua kwa heading ya leo tu hapo unakuwa unataka nini katika uchambuzi wako hasa? Unataka kupandisha chati gazeti ambalo silo.
 
kwani wapuuzi na wajinga hawawi wazee? wanakufaga? ile mijitu mijinga inayokuaga ya mwisho darasani enzi za utoto kwani wanakufaga kabla ya kufika uzeeni?
 
Serikali sio kwamba haiwezi kulipa wafanyakazi 315,000 lakini inashindwa kutokana na matumizi mabaya na ya juu kwa maofisa wake,kuanzia Raisi mwenyewe misafara ya nje ikiwa na ujumbe mkubwa,hata ya mikoani inakuwa ni mikubwa sana,huwa najiuliza hivi watanzania tunaakili timamu kweli tunaendelea kuangalia mambo haya,utasikia Raisi anakwenda kuzindua zahanati ya Milion 18 lakini garama ya msafara wake milion 50 inaingia akilini hii?Baadhi ya tenda za serikali watu wana inflate rate ili wapate cha juu.Baadhi ya ofisi za PCCB ambazo zinajengwa kwenye baadhi ya wilaya zinajengwa kwa garama ya juu sana bila sababu na kutokanana na idadi ya watumishi wa kitengo hicho katika wilaya hakuna sababu yoyote ya kujenga majengo makubwa ya gorofa kwa garama kubwa sana ilihali idadi ya wafanyakazi ni ndogo_Ofisi ya PCCB wilaya haina wafanyakazi zaidi ya kumi jengo kubwa la nini?hili hapa ni jengo la gorofa moja ambalo litakapomalizika litatumika kama ofisi za PCCB wilayani kwa muheshimiwa sana linajengwa kwa thamani ya milion 800 za kitanzania sijakosea ni (million mia nane),majengo ya aina hii hii yanajengwa Maswa,Manyara,kiomboi,na kwingineko Tanzania, Why huge office like this for not more than ten staffs?while no medicine in hospitals,no enough beds even in municipal hospitals?are we MAD?
 
raia mwema is the most credible as always, certainly i will never buy uhuru or nipashe as the headline itself shows ni magazeti ya kinafiki na ya kinazi ya ccm.
 
Wakuu, kwa mara nyingine tena Rais ameaibishwa tena na wasaidizi wake.
Kulingana na maelezo aliyotoa Kaimu katibu mkuu wa TUCTA Bw. Mgaya mbele ya vyombo vya habari jana na kuonyesha ushahidi wa barua ya mwaliko wa kikao toka hazina ni kuwa kikao chao cha maridhiano na ujumbe wa serikali kilikuwa kiwe saa 8 na sio kama alivyowatukana JK kuwa wao ni waongo na wanafiki kwamba waliitwa kikaoni saa 4 asubuhi na wakaja saa 8 mchana. Mgaya alifika mbali na kusema waziri Kapuya ( ambaye alimwita ALHAJI AKUDO ) kamdanganya rais na kumsababishia aseme uongo hadharini akiamini kuwa huo ni ukweli.
Naona sasa hawa wasaidizi wake hawana mashaka yeyote na mkuu hata kama ataaibika hadharani kutokana na kumpotosha. Hakuna watakachofanywa. NAANZA KUHISA KUNA MAKUSUDI FULANI KATIKA KUMPOTOSHA.

mkuu kama unaweza kutupatia nakala ya barua ya mwaliko nitashukuru sana
 
wuuui .Naanza kupata nafuuuu

Mbayu wayu versus AKUDO AMPACTO mavijana wajanja , mavijana ya masauti - presida KAPUYA mutu ya watu..................Ngwasuma ..............
 
Hivi ndivyo inatakiwa iwe, we must dare not onl to talk but also to take actions and necessary actions,
watu wakipata tukio hukimbilia kujaza threads tu hapa kwenye jf na kuleta wakati wingine hata majungu na umbea lakini hamna hatasiku moja mtu akatoa wazo la kuchukua hatua, tujifunze kwa mama huyu...inabidi tumpe hata zawadi na sio kungoja azawadiwe na watu wengine...

Naomba upendekeze zawadi, nimeangalia picha gazetini hata ndala zake zinaonyesha ni jinsi gani yuko down to earth very poor but couregous lady.
 
Back
Top Bottom