Mwijaku afunguka: Pesa ya kujenga ghorofa nimeitoa kwa Diamond Platnumz

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,525
7,377
Ukweli unatuweka huru.

Mwijaku aamua kuwa mkweli na kusema kilicho ndani ya moyo wake.
Ghorofa lake alilojenga na kutrend mitandaoni pesa imetoka kwa Diamond Platnumz.

Hongera mwijaku kwa kuwa muungwana.

Pia sifa ziende kwa diamond kwa kuendelea kubadilisha maisha ya watu.
Mungu ataendelea kukupa baraka.

===

Siwezi kupinga ukweli ..! Safari yangu ya kwanza Qatar (WorldCup) na malipo yake ndio yalio nifanya ninunue eneo na kuanza safari yangu ya kujenga KASRI langu (Ndoto yangu).

Ukweli usemwe, Ulinipa rizki kupitia kampuni yako, nami nikaitumia vizuri, sitakiii kua mchoyo ya kushukuru, Nakumbuka tulipo kua Qatar ulinambia kua "Pambana wakati wako huu DC" nami nikaichukua hiyo kauli.

Tarehe 5/01/2024 Nimekamilisha ndoto yangu. Kupitia Kampuni yako ilinipa mkataba zaidi ya miaka miwili na malipo ya kila mwezi na nikatumia kama sehemu ya uwekezaji kwangu.

Nasema Asante MWAMBINO. Diamond Platnumz sitaki kuja kusubiria ukifa au nikifa ndio yasemwe haya. Ulinifaa wakati wa shida na wakati wa mahitaji Muhimu.

Asante kwa Don Fumbwe Nakumbuka mzigo ulio nipa magomeni usiku wa saa mbili baada ya kupokea simu toka kwa mwambino ndio ulizaa uwekezaji huuuu. Asante kwako kwa kua hukunizunguusha kunikabidhi haki yangu.

Nimshukuru pia mama mzazi wa MWAMBINO mama Dangote, ulinipa ushirikiano mkubwa pale QATAR na kunambia fanya kazi uisaidie familia yako na niache CHUKI binafsi. Nikakwambia simchukii MWAMBINO but ni kuchangamsha mitandao yetu. Asante kwa kunielewa mama yangu.

Haya Mengine ya mtandaoni ni sehemu zetu za kunogesha game na kuhakikisha tunapambana kukuza burudani.

Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa fikra za kuwasaidia wengine kwa kuwapa kazi na kuwapa usia wa kutumia vizuri vipato wanavyo vipata. Asante kwa hili MWAMBINOOO.

Mungu akubariki wewe na kizazi chako. Sema na mimi nakushaurii OA mkubwa wakati wako huu Muoe ZUCHU ana UPEPOO WAKO 🙏🏾.
 
Harmonize amewahi kumwinua hata kijana mmoja mjini awe hata na kitu cha kumbukumbu?
Alikiba naye vipi?
Nimeuliza kwa nia njema kuwa kati ya hawa wasanii wanaoitwa wanyonyaji nani angalau anatoa ajira angalau mtu awe na chochote?

Diamond
Ali kiba
Harmonize
Diamond Platinumz,kaajiri sana,kakitangaza sana kiswahili lakini pia ndie aliyefanya mapinduzi makubwa ya muziki kuwa biashara kuliko msanii yeyote wa Tanzania.
 
Harmonize amewahi kumwinua hata kijana mmoja mjini awe hata na kitu cha kumbukumbu?
Alikiba naye vipi?
Nimeuliza kwa nia njema kuwa kati ya hawa wasanii wanaoitwa wanyonyaji nani angalau anatoa ajira angalau mtu awe na chochote?

Diamond
Ali kiba
Harmonize
Kwenye upande wa kugawa rizki Diamond ni special one.
Hii kitu huwezi ifanyia maigizo inaanzia kwenye roho.
 
Back
Top Bottom