Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Lipumba akamatwa na wafuasi wake, kisha waachiwa kwa dhamana!

Jamani msikubali kudanganywa mtu yeyote aliye angalia Hot mix (EATV) na ITV habari atakubaliana nami kuwa lipumba hakubebwa na mtu kwenda kwenye gari bali alikwenda mwenyewe na kama polisi walipanga kumbeba basi hawakufanikiwa maana video zilionesha vyema hili tukio japo ilitoke purukushani kubwa lakini Lipumba hakupigwa virungu wala kubebwa mzobemzombe!

Jamani hebu punguzeni uongo kila mtu ana macho.

Kubebwa mzobemzobe haimaanishi kuwekwa mgongoni. Hiyo ni lugha pana zaidi. Hata kusukumwa na kusukwasukwa hovyo huo ni mzobemzobe ambao kwa heshima ya Lipumba aliyo nayo katika nchi hii na nje hakustahili kufanyiwa na wale wahuni waliovaa beji za dola.
 
Mkuu wameshatiwa mbaroni na sasa wako wanapata kibano STK-UKONGA pale chini ya mwembe alfajiri ili wataje mtandao wao! Wanaendelea kutiwa mbaroni mmoja baada ya mwingine, aisee usiombe hao jamaa wakakutia mikononi utajuta kuzaliwa!

Sina imani na Jeshi letu.. hapo kuna uwezekano mkubwa wamekamata wasiohusika.... Tumekuwa tukiona taarifa zao zinakuwa zinapishana... Hao kazi yao kubwa ni kuzuia maandamano ya vyama vya upinzani.
 
Mimi kama mwanachama wa act-tanzania
nalaani kitendo cha mwenyekiti wa cuf
ndugu ibrahim lipumba kupigwa na
kudhalilishwa yeye na wafuasi wake,kama
chama cha act-tanzania katika msingi wetu
wa "utu wa mtu utu" wana act hapa
tunasema lazima utu wa mtu uthaminiwe
tena kiongozi huyu ni kiongozi mkubwa sana
katika chama kikubwa cha kisiasa
wamemdhalilisha sana na ninaishauri polisi
iache kutumia nguvu kwa kila jambo mengine
yanahitaji busara.natoa pole kwa prof.
Lipumba na wafuasi wote wa cuf na kwa
pamoja tulaani kitendo hichi cha kuirudisha
demokrasia nyuma
kamwe hatutarudia nyuma katika kuikuza
demokrasia
 
You're of no effect.
 
Siku panya road walivyokuwa mtaani polisi walikuwa wapi? Raia wasiyo na silaha wakiandanana tu......polisi watamwagwa kila kona.
 
Kwanini hao intelijensia intelijensia wasitumie hizo nguvu na gharama kuwasaka hao magaidi popote walipo kupitia watu waliowaambia nia ya magaidi kuwalipua CUF na kuwapa ulinzi CUF? Kwa akili ya kawaida ukisikia mwanao anazengewa na adui, unapaswa kumlinda mwanao na kumsaka adui, kumuangamiza na siyo kumuangamiza mwanao kwa kuwa ameelekea matembezini bila uangalizi wako mzazi huku ukiwa huna mpango wowote wa kumtafuta adui, mbona hatuwaoni polisi wakiwapiga albino mabomu kwa kutembea mtaani wakati wakijua kuna watu wanawatafuta ili wawaue na kutoweka na viungo vyao?!
Very wise wisdom
 
Siku panya road walivyokuwa mtaani polisi walikuwa wapi? Raia wasiyo na silaha wakiandanana tu......polisi watamwagwa kila kona.
Polisi wanatimiza wajibu wao. CUF walikuwa wanataka kufanya siasa za kijinga
 
Mimi kama mwanachama wa act-tanzania
nalaani kitendo cha mwenyekiti wa cuf
ndugu ibrahim lipumba kupigwa na
kudhalilishwa yeye na wafuasi wake,kama
chama cha act-tanzania katika msingi wetu
wa "utu wa mtu utu" wana act hapa
tunasema lazima utu wa mtu uthaminiwe
tena kiongozi huyu ni kiongozi mkubwa sana
katika chama kikubwa cha kisiasa
wamemdhalilisha sana na ninaishauri polisi
iache kutumia nguvu kwa kila jambo mengine
yanahitaji busara.natoa pole kwa prof.
Lipumba na wafuasi wote wa cuf na kwa
pamoja tulaani kitendo hichi cha kuirudisha
demokrasia nyuma
kamwe hatutarudia nyuma katika kuikuza
demokrasia
hili haliwahusu nyie..
 
Kubebwa mzobemzobe haimaanishi kuwekwa mgongoni. Hiyo ni lugha pana zaidi. Hata kusukumwa na kusukwasukwa hovyo huo ni mzobemzobe ambao kwa heshima ya Lipumba aliyo nayo katika nchi hii na nje hakustahili kufanyiwa na wale wahuni waliovaa beji za dola.

ImageUploadedByJamiiForums1422431757.957329.jpg
 
Back
Top Bottom