Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Lipumba akamatwa na wafuasi wake, kisha waachiwa kwa dhamana!

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
10897978_678282712282706_5939579278398548602_n.jpg

10383082_10202504774020957_1649851934240776124_n.jpg

Wana JF,

Niko Dar huku Kijichi. Nasikia milipuko. Watu wametoka nje ya nyumba zao wakitaka kujua.

Mwenye taarifa atujunze.

Maandamano ya CUF... polisi wachafuwa hewa.....
Kuna taarifa mbaya kwamba wafuasi wa CUF wametawanywa kwa mabomu huko temeke na mmoja wa walioumizwa ni mwenyekiti wa Taifa prof Ibrahim Lipumba.

Kuna taarifa mbaya kwamba wafuasi wa CUF wametawanywa kwa mabomu huko temeke na mmoja wa walioumizwa ni mwenyekiti wa Taifa prof Ibrahim Lipumba.

Maandamano yalikuwa ni maadhimisho ya kumbukumbu za mauaji ya wafuasi wa cuf yaliyotokea zanzibar miaka kadhaa iliyopita.

Source: ITV


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

PROFESA LIPUMBA AKAMATWA NA POLISI KWA NGUVU! TAARIFA KAMILI.

Ndugu zangu, hivi punde nimeongea na Maharagande Mbarala na Bonifasia Mapunda na wamenijulisha kuwa, Profesa Lipumba na Manaibu Wakurugenzi wawili wa Chama Cha Wananchi CUF (Shaweji Mketo na Abdul Kambaya), pamoja na walinzi wa Profesa Lipumba, wamekamatwa na polisi. Pia, nimeongea na mhe. Joram Bashange, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF, tayari yuko Central Police lakini hajaruhusiwa kuwaona viongozi. Mawakili wa CUF wanaelekea polisi pia.

KUMBUKIZI YA MWAKA 2001

Ukamataji huo uliotumia nguvu kubwa umetokea leo majira ya Mchana wilayani Temeke. Leo ni Januari 27 na ni siku yenye kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Wananchi CUF baada ya matukio ya mauaji yaliyofanyika tarehe na mwezi kama huu huko Zanzibar ambako wafuasi wa CUF zaidi ya 100 waliuawa kwa risasi na vyombo vya dola. Mauaji hayo yalifuatiwa na maandamano mbalimbali yakiwemo ya Dar Es Salaam yaliyoongozwa na Prof. Lipumba ambaye alivunjwa mkono, kuporwa saa yake ya thamani na polisi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

MAANDAMANO YA CUF KILA MWAKA:

Baada ya tukio hilo CUF imekuwa na utaratibu wa kuandamana kila mwaka (maandamano ya amani) ili kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya Januari 2001 na kuwaenzi waliopata ulemavu wa kudumu kutokana na kipigo cha vyombo vya dola. Mwaka jana 2014 mwezi kama huu Bendera za Chama cha Wananchi CUF zilipepea nusu mlingoti na pia maandamano yalifanywa maeneo kadhaa ya nchi na vyombo vya dola viliyalinda.

Mwaka huu nimeambiwa kuwa CUF ililijulisha jeshi la polisi juu ya maandamano ya leo kupitia barua ya Alhamisi, Tarehe 22 Januari 2014. Baada ya CUF kuandika barua hiyo, maandalizi ya maandamano na mkutano wa hadhara yaliendelea, ikiwemo kufanya matangazo kwenye wilaya za DSM, kukodi vifaa mbalimbali na hata kulipia matangazo LIVE kwenye redio kadhaa ili hotuba za viongozi ziweze kurushwa. Jeshi la polisi lilipokea barua hiyo tokea tarehe 22 Januari na likakaa kimya muda wote huo.

ZUIO LA POLISI:

Leo tarehe 27 Januari, maandamano yalipangwa kuanza saa 8 mchana kuanzia Temeke Mwisho kwenda hadi viwanja vya MBAGALA ZAKIEM ambako mkutano wa hadhara ungefanyika kuanzia saa 10.00 - 12.00 jioni. Cha ajabu ni kuwa, asubuhi ya leo ndipo Jeshi la Polisi limepeleka barua kwenye Ofisi Kuu za CUF Buguruni KUZUIA MAANDAMANO na MKUTANO WA HADHARA.

Barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar Es Salaam na Pwani inaeleza sababu kadhaa za zuio hilo:
1. Kwamba, maandamano ya CUF ya Mwezi Januari 2001 yaliyofanya vyombo vya dola vitumie nguvu na kuua raia hayakuwa halali na hivyo kuadhimisha siku hiyo mwaka huu ni haramu na kunaweza kuhatarisha amani ya nchi.
2. Kwamba, Taarifa za kiintelijensia zinaonesha ati kuna watu wamepanga kufanya vurugu katika maandamano na mkutano huo.
3. Kwamba, kuna vitisho vya UGAIDI katika nchi yetu na hivyo maandamano hayo na mkutano huo vinaweza kuleta madhara ya magaidi kupenya na kutekeleza azma zao mbaya.
4. Sababu nyingine za kipuuzi, dhaifu na zisizo na maana.
Baada ya kupokea barua hiyo na kwa sababu wananchi na wapenzi wa CUF walikwishajikusanya kwa maelfu kwa ajili ya maandamano, ilimpasa Profesa Lipumba na viongozi waandamizi wa chama waweze kwenda hadi Temeke Mwisho ili kuahirisha maandamano hayo.

TEMEKE MWISHO:

Majira ya mchana leo, Profesa Lipumba aliongea na wanachama na wapenzi wa CUF waliojazana Temeke Mwisho karibu na Ofisi za CUF Wilaya na akaahirisha maandamano na mkutano (Usalama wa Taifa walikuwepo, Polisi walikuwepo kwa mamia na vyombo vya habari vilikuwepo). Baada ya kufanikiwa kuwatawanya wafuasi waliokuwa Temeke Mwisho, Profesa akajulishwa kuwa kule uwanjani Zakiem tayari kuna maelfu ya wafuasi, ikampasa yeye na viongozi waandamizi waingie katika magari na kuanza safari kwenda Zakiem kwa lengo la kuwatawanya wafuasi kwa amani kama alivyofanya kwa wale waliokusanyika Temeke Mwisho. Hapakuwa na wafuasi wa chama waliomfuata.

KUELEKEA MBAGALA ZAKIEM:

Wakiwa katika Magari yao na katika safari ya kwenda Mbagala Zakiem, wakazuiwa na magari zaidi ya 10 ya polisi walio tayari kwa mapambano. Profesa na viongozi wakawajulisha Polisi azma yao ya kwenda kutawanya wafuasi walioko Zakiem, baada ya mvutano mfupi Polisi hao waliwaruhusu waende Zakiem. Safari ya magari machache ikaendelea, bila wafuasi wanaotembea kwa miguu.

Walipofika mbele (Mtoni Mtongani - Round about) wakakuta BLOCK ya pili ya mamia ya Polisi wenye magari na silaha. Hawa nao wakawazuia wasiende ZAKIEM, wakati bado Profesa anawaelewesha, mabomu yakaanza kupigwa na viongozi kusambaratishwa kwa nguvu mno kama vile kulikuwa na jambo kubwa. Profesa amebebwa mzobemzobe akipigwa virungu na kutupwa kwenye DIFENDA ya polisi yeye, wakurugenzi wake na walinzi wake. Hivi sasa tuongeavyo wako CENTRAL POLICE na mie nilitoka tu kidogo Darasani ili kupiga simu na kusimuliwa tukio zima.

CHA KUSHANGAZA:

Wakati polisi wanazuia maandamano ya CUF kwa nguvu kubwa kiasi hiki, wanawapiga na kuwajeruhi viongozi wasio na hatia na ambao wamejishusha na kuahirisha maandamano na mkutano wao, Polisi haohao kila siku tunaona wanasimamia maandamano na mikutano ya Mwigulu Nchemba, Abdulrahman Kinana, Nape Nauye na viongozi chungu mbovu wa CCM.

Hata katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yanayotarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma, nimejulishwa kuwa kuna maandamano yamepangwa yakihusisha wana CCM mbalimbali katika wilaya za jirani ili kusheherekea sikukuu yao na kwamba Polisi watayalinda maandamano hayo ya CCM.

MASWALI YA KUJIULIZA:

Je, hizi taarifa za Kiintelijensia zinafanya kazi kwa mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu? Je, hao Magaidi wao wanavamia na kulipua mikutano ya vyama vya upinzani tu? Magaidi gani hawa ambao hawaendi kuvamia wezi wa fedha za umma ati wanakwenda kuvamia viongozi waadilifu wanaopigania haki sawa kwa wote na mabadiliko makubwa katika nchi yetu? Tunadhani matendo haya ya serikali na vyombo vyake dhidi ya vyama vya upinzani yanajenga mustakabali wa taifa? Yanajenga amani na upendo miongoni mwetu? Au yanazidisha chuki na uhasama na mgawanyiko/mpasuko katika taifa?

Kwa nini mamia ya askari wanaokwenda kupiga na kujeruhi viongozi wenye nia njema yasitumike kwenda kusaka majambazi walioua askari wetu pale Ikwiriri Rufiji? Kwa nini mamia ya askari hao yasiwasake majambazi walioteka mabasi ya abiria mkoani Arusha majuzi? Kwa nini mamia ya Askari hao yasijielekeze kuwasaka wauaji wa Albino na wazee wenye macho mekundu Shinyanga?

Kwa nini mamia ya askari hao wasipelekwe kuwasaka magaidi ambao tumegundua watakuja kutuvamia? Na mbona maguvu hayo ya polisi yasielekezwe kuwasaka wala rushwa wakubwa, wafadhili na wamiliki wa mitandao ya kuuza madawa ya kulevya, wezi wa fedha za umma na waharibifu wakuu wa Taifa hili?
Mbona taifa hili linaendeshwa kipuuzi namna hii? Mbona nchi yetu inapelekwa mbele kama vile kuwa Chama Cha Upinzani ni dhambi dhidi ya watawala wezi na mafisadi? Kwa nini basi CCM hao hao wakapigia debe kuanzishwe vyama vingi mwaka 1992? Sasa wanaogopa na kuweweseka kwa lipi?

(UKIONA SERIKALI INAOGOPA MAANDAMANO YA AMANI NA MKUTANO WA CHAMA KIMOJA TU HADI KUPIGA NA KUKAMATA VIONGOZI, JUA KWAMBA SERIKALI HIYO HAINA SIKU NYINGI MADARAKANI).

"Time will determine and judge each of us".


Julius Mtatiro,
27 Januari 2015,
Masomoni.
attachment.php



------------------------------------------
Mawakili wa CHADEMA waenda polisi kumtoa Lipumba

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeshtushwa na kupigwa vibaya na kukamatwa Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA Prof Ibrahim Lipumba

Tayari Uongozi wa juu wa CHADEMA pamoja na mawakili wa chama wameelekea Police Central Station kwa ajili ya tukio la kijahili walilofanyiwa viongozi wa CUF, Profesa Lipumba na wengine.

Lengo la mawakili wa Chadema ni kuhakikisha wanamtoa kwa gharama yoyote Prof Lipumba na wanachama wote wa CUF waliokamatwa.

Tutaendelea kuwapa taarifa za tukio hili kwa kila hatua..


Updates 2....

Tunawaletea maelezo zaidi ya msemaji wa Chadema Tumaini Makene hapa chini:

Tuko Police Central Police hapa muda mrefu uliopita. Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Bara JJ Mnyika, wamefika hapa.

Chama kilimuagiza Wakili Freddy Kiwilo kufika hapa kuja kutoa msaada wa kisheria kwa wapiganaji wenzetu wa UKAWA waliokamatwa kwenye maandamano ya Chama cha Wananchi (CUF).

Kwa hiyo Wakili Freddy tayari anasaidiana na Wakili mwenzake Kilerio Job kuhakikisha Prof. Lipumba na wengine akina Mketo, Kambaya na wengine wanapata msaada wa kisheria wakati wa kuandikisha maelezo.

So far baada ya kuandikisha maelezo watapata dhamana na kutoka. Will keep you posted.

Updates...3

Mawakili wa Chadema wamefanikisha kumtoa Professor Lipumba na viongozi wengine wa CUF na wanachama wote walioshikiliwa saa 5 usiku.Wanasheria wa Chadema walikataa katakata Lipumba kulala polisi mpaka asubuhi.ilikuwa ni nguvu ya UMMA kweli kweli.

--------------------------------

Prof Lipumba mara baada ya kuachiwa



10801748_10202505965210736_5427215448914249936_n.jpg


MWONEKANO WA PROF. LIPUMBA,DAKIKA CHACHE TU BAADA YA KUACHIWA USIKU HUU.

Hapa anakumbatiana na Katibu Mkuu wa NCCR.

Muda huu viongozi na wanachama wote waliokuwa wameshikiliwa hapa CENTRAL POLICE wameachiwa kwa dhamana.

Kinachoendelea sasa hivi ni kukabidhiwa vifaa vyao walivyosalimisha awali. Kuripoti tena ni kesho saa 4.00 asubuhi. Shukrani za dhati ziwaendee mawakili wa CUF akiwemo wakili msomiHashim Bakari Mziray na wakili mzoefu Job Krario. Pia shukrani kubwa ziwaendee mawakili wengine wawili walioletwa na CHADEMA na mmoja wa NCCR (alichelewa kidogo).

Tukio la leo limeonesha kuwa UKAWA inafanya kazi kama siafu. Mawakili wengine watatu walikuwa njiani kuja hapa CENTRAL tumewarudisha, jumla wangekuwa saba. Kwa uwezo wa mungu HAKI itapatikana siku moja Tanzania. Mabadiliko ni mimi, wewe na yule na yanaanza sasa na yanaanzia kwako na kwangu na kwa yule.

Mimi na wewe ndiyo tunawakilisha Tanzania tuitakayo, tuanze sasa na tuendelee kuiunga mkono UKAWA na juhudi zake.
Kwa dhati pia niwapongeze Katibu Mkuu wa NCCR, Mosena Nyambabe, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF Joram Bashange, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu CUF Mhe. Kuruthum Mchuchuli (MP), Mjumbe wa Baraza Kuu CUF Bonifasia Mapundana Mjumbe wa Baraza Kuu mstaafu Maharagande Mbarala kwa kuwepo CENTRAL POLICE hadi sasa.

Niwapongeze viongozi na wanachama wote waliosimama kidete hadi usiku huu, malipo yenu ni kupatikana kwa Tanzania tuitakayo.

Mungu awabariki na usiku mwema.

J. Mtatiro,
27 Januari 2015,

 

Attachments

  • cuf.jpg
    cuf.jpg
    24.9 KB · Views: 30,361
Kuna taarifa mbaya kwamba wafuasi wa CUF wametawanywa kwa mabomu huko temeke na mmoja wa walioumizwa ni mwenyekiti wa Taifa prof Ibrahim Lipumba.

Maandamano yalikuwa ni maadhimisho ya kumbukumbu za mauaji ya wafuasi wa cuf yaliyotokea zanzibar miaka kadhaa iliyopita.

Source: ITV


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Wana JF,

Niko Dar huku Kijichi. Nasikia milipuko. Watu wametoka nje ya nyumba zao wakitaka kujua.

Mwenye taarifa atujunze.
Maandamano ya CUF... polisi wachafuwa hewa.....
Kuna taarifa mbaya kwamba wafuasi wa CUF wametawanywa kwa mabomu huko temeke na mmoja wa walioumizwa ni mwenyekiti wa Taifa prof Ibrahim Lipumba.
 
Isije kuwa ile kauli ya Muhongo inatimia na sasa nchi inatingishika
 
Kufuatana na Redio one ni kwamba mabomu ya machozi yamerushwa huko mtoni kwa aziz ali na Prof Lipumba, wafuasi na wanahabari wamejeruhiwa
 
Maandamano ya CUF... polisi wachafuwa hewa.....
Kuna taarifa mbaya kwamba wafuasi wa CUF wametawanywa kwa mabomu huko temeke na mmoja wa walioumizwa ni mwenyekiti wa Taifa prof Ibrahim Lipumba.

Hawa polisi ccm kazi yao ni kupiga tu wananchi,shame on them.
 
Wanajesholi pingine wako kwenye mazoezi ya kawaida. Nipo maeneo ya buza napata soda yangu lakini hali uko shwari kabisa!
 
Ni maandamano ya CUF hayo yameanzia Temeke hospital Ila sasa yamezimwa na FFU walilipua mabomu ya machozi. Lipumba wamemkamata
 
huo ndiyo weledi wa viongozi wa ccm ulipoishia. kuna tofauti gani na kumbukumbu ya kifo cha nyerere au sokoine?
 
Back
Top Bottom