Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Nachingwea ajiunga na CCM

Niliwahi kuwaambia humu JF baada ya Bunge tutaona vigogo wa Magwanda wakiondoka, wakanishutumu, wakanikejeli, sasa naona hawataki hata kuikumbusha ile nyuzi, maana mimi nilifikiri watakuwa wawili watatu, lakini sasa naona ni makundi kwa makundi. Maaaweeee!

SS (aka FF), huyo naye ni 'kigogo'? Hii wanayotumia magamba ni mbinu ya kizamani sana, wacha waendelee kuwahonga hao mnaowaita 'vugogo', lakini hamtaweza kamwe kuwahonga wananchi wenye hasira na mafisadi na serikali ya wasanii wa ccm.

Ni vigumu kumshawishi mtanzania kwa hoja kuwa ccm inastahili kuwa madarakani, jiandaeni kukaa pembeni.
 
Huyu mzee amepitwa na wakati na kwa bahati mbaya ameshindwa kwenda na wakti. mimi siungi mkono utaratibu wa kurudisha kadi za chama kimoja kwenda kwa kingine. Kadi si ya cdm warudishie mbona unapeleka huko! Inamaana mtu ukihama dini utapeleka na vitabu vyao vitakatifu dini mpya? ukiacha kazi mahali unapeleka barua ya kuacha kazi kwa mwajiri mpya! Siasa za njaa hizo
 
Sipendi siasa. Yaani siasa haina tofauti na dini, kila mmoja huvutia kwake huku akiaminisha wafuasi wake ya kuwa yeye ni bora. Kwa hiyo jamaa naye kavutiwa na mazuri aliyoyaona kule alikohamia, mwacheni afuate kile akili yake inamwelekeza kufanya.
 
Kuliko kuwa na mwanachama anayetaka kuondoka ni bora kuwa na mwanachama aliyeondoka.
 
Amekabidhiwa kadi ya ccm na makam wa rais Mohamed Ghalib Bilal.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha kadi ya CHADEMA baada ya kukabidhiwa na Hassan Mkope (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Nachingwea, aliyeamua kujiengua na kujiunga na CCM. Makamu ameanza ziara yake katika Mkoa wa Lindi jana januari 20.

source:mjengwa na michuzi blogs

Du kumbe cdm wako hadi Lindi
 
Makamu wa Rais amekwenda huko kwenye shughuli za kiserikali halafu analeta mambo ya kichama. Hawa ndio wanachafua jina la CCM yetu. Akitaka kukusanya kadi basi afanye hivyo kwa wakati wake sio wakati yuko kazini.
 
Mi sielewi hapa huyu mzee yupo ziara ya kichama au serikali.Na kama ni ziara ya kiserikali kwa nini afanye kazi za chama hichi kitu lazima tukiangalie kwa upana zaidi
 
Mzee huyo namfahamu vizuri alkuwa CCM akaja Nachigwea Lipumba akajiunga na CUF, alipokuja Dr Slaa akajiunga na CHADEMA na amekuja Dr Bilal karudi CCM, Subilini aende Mrema mtamsikia TLP na akizuka huko Mbatia mtamsikia NCCR hali ya maisha Nachingwea ni magumu hasa ukiwa na wakee 4 kama mzee wangu huyu. Mliokuwa karibu na tukio Dr Bilal aliweka mkono mfukoni lakini?.

Hii nayo imekaa sawa
 
wanaotoka cdm kurudi ccm ni wanafiki/mamluki lakini wanaotoka ccm kwenda cdm ni mashujaa,kazi kweli kweli.

Hata mtoto analijua hilo yaani uwache mahela ya kifisadi uende CDM ukatetee tu haki ya wanyonge. Hiyo alifanya Yesu tu na sasa wachache wanajitahidi kujitoa muhanga
 
CCM ya sasa inatia huruma kama :A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed:
 
kuhama ni kitu kizuri zaidi kuliko angekuwa mwanamgamba wakati amevaa GWANDA
 
Amekabidhiwa kadi ya ccm na makam wa rais Mohamed Ghalib Bilal.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha kadi ya CHADEMA baada ya kukabidhiwa na Hassan Mkope (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Nachingwea, aliyeamua kujiengua na kujiunga na CCM. Makamu ameanza ziara yake katika Mkoa wa Lindi jana januari 20.

source:mjengwa na michuzi blogs
huwa mnapenda mazuri CDM,mabaya wala hamtaki kuyasikia

muelewe kuwa panapo fuka moshi moto utawaka mda si mrefu

kaziyenu ni kuponda tuuu,bila hata kutaka kujuwa kwanini huyu bwana kaondoka na ikiwezekana mrekebishe mambo

msipende kila siku kula wali na nyama,mjifunze pia kula wali na chunga
 
hata Nepi alikuwa CCJ lakini akavaa tena GAMBA si unaona anabwekabweka kwenye vyombo vya habari?
 
huwa mnapenda mazuri CDM,mabaya wala hamtaki kuyasikia

muelewe kuwa panapo fuka moshi moto utawaka mda si mrefu

kaeni kuponda tuuu,bila hata kuataka juwa kwanini huyu bwana kaondoka na ikiwezekana mrekebishe mambo

msipende kila siku kula wali na nyama,mjifunze pia kula wali na chunga
cdm tunaakili kuliko unavyofiki unaona Shibuda alivyokuja kwetu na kushinda jimbo anacheo gani cdm kitaifa zaidi ya ubunge wake
 
Makamu wa Rais amekwenda huko kwenye shughuli za kiserikali halafu analeta mambo ya kichama. Hawa ndio wanachafua jina la CCM yetu. Akitaka kukusanya kadi basi afanye hivyo kwa wakati wake sio wakati yuko kazini.

sikweli mkuu

hata Rais anapokwenda mkoa furani kwa kazi za kiserikali upo uwezekano mkubwa sana akapangiwa kufanya kazi za chama na wilaya husika ama mkoa husika

kinachotokea ni kwamba atafanya kazi za kiserikali,akishamalisha anafanya kazi za chama,hiyo ni kawaida kabisa si kwa ccm hata CDM

Kwa mfano Mh zitto anaweza kwenda sehemu kwa kazi za kiserikali kama mbunge wa CDM,lakini mahali alipo kwenda hafungwi na sheria yeyote ile juu ya yeye kutembelea ofisi za CDM mahali husika na hata kufanya kazi za kuimarisha chama sehemu husika

sasa wana JF tuliowengi hatuelewi mambo ya siasa yalivyo,tumekuwa na fikra hasi mda wote
 
cdm tunaakili kuliko unavyofiki unaona Shibuda alivyokuja kwetu na kushinda jimbo anacheo gani cdm kitaifa zaidi ya ubunge wake

alikuwa na cheo labda umeshau na baada ya hapo alivuliwa vyeo hivyo pale alipo kisaliti chama,

lakini ninacho kiongelea mimi ni kwamba,mnatakiwa kujipima,sio kila siku kwenu ni pasafi,na pindi mnapopata matatizo ndio wakati wa kukaa chini na kuweka mambo sawa,lakini wanaCDM waliopo humu JF kazi yenu ni kutaka kusikia mazuri tu,mtu akienda kinyume na matakwa yenu basi ni shida

kwanza mmekuwa vigeugeu sana,mala kwa mala hapa JF Mmekuwa na tabia ya kubwatuka juu ta zitto na kumwona ni msaliti haya yote yanatokea kwa kuwa huwa mpendi kuambiwa ukweli hususani wana CDM walio humu JF,sina matatizo na viongozi wakuu kwani wao ni waelewa na wanaijuwa siasa na wanakubari kukoselewa,tatizo lipo kwa nyie ambao hamna effect yeyote na CDM,si wapiga kura na wala hakuna wenye kadi ni watu wa kupiga kelekele mitandaoni tu

Tubadilike na tuwe watu wa kukubari hata mapungufu yetu binafsi
 
huwa mnapenda mazuri CDM,mabaya wala hamtaki kuyasikia

muelewe kuwa panapo fuka moshi moto utawaka mda si mrefu

kaziyenu ni kuponda tuuu,bila hata kutaka kujuwa kwanini huyu bwana kaondoka na ikiwezekana mrekebishe mambo

msipende kila siku kula wali na nyama,mjifunze pia kula wali na chunga
Sisi watu wa Nachingwea tunamfahamu mzee huyo, yeye huhama chama kila kiongozi wa chama chochote kitaifa anapotembelea Nachingwea, sasa hapo tuta lekebisha kitu gani? sana sana akija kamanda Mbowe tuta mtonya tabia ya ovyo ya mzee huyu!
 
Huyu "kikofia" bora aende maana anaonekana ana njaa sana, aende akajenge afya asije fia CDM!
 
Back
Top Bottom