Mnasema hawana wananchi si mngeruhusu kongamano ili muwazodoe jinsi watakavyokosa watu??



Embu kaongee huu ujinga mbele ya hiyo nyomi kma utarudi hpa na mikono ya kucomment
Hiyo nyomi ambayo haina hata uwezo wa kumpambania kiongozi mkuu wa Chama ni nyomi ya kipumbavu
 
Huyo Mbowe anataka kukamatwa, na akamatwe tu kwani yeye ni anajifanya ni nani?
Mwambieni mkuu wa mkoa Kama kuna covid 19 Mwanza Nyamagana maelfu ya watu wanaangalia mpira Kati ya Pamba na Coastal union play off..mwambieni kwanza wajihi wake anaonekana Mtutsi tutaleta xenophobia Mambo ya kisiasa yakishindikana
 
Mwambieni mkuu wa mkoa Kama kuna covid 19 Mwanza Nyamagana maelfu ya watu wanaangalia mpira Kati ya Pamba na Coastal union play off..mwambieni kwanza wajihi wake anaonekana Mtutsi tutaleta xenophobia Mambo ya kisiasa yakishindikana
Mwambie wewe, mimi hainihusu.
 
Mkuu wa mkoa kaweka zuio la mikusanyiko. Makamanda wa Chadema wanasema watakusanyika kwa nguvu kufanya kongamano.

Usiku wa manane wanadakwa. Maana mkuu wa mkoa anazo taarifa za kiusalama.

Je, hapa nani amefanya kosa?

Tusilaumu bila ya kuwa na argument za msingi.
Uonevu , uovu , ufisadi na mambo yote ya kishamba barani Afrika ndicho kinachoendelea.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefunga barabara ya Bwiru maarufu kona ya Bwiru jirani na ukumbi uliopangwa kufanyia kongamano la Chadema la kudai Katiba, hakuna kinachoendelea kwa sasa polisi wametanda barabara nzima wakiwa na magari na silaha za moto
Haisaidii kitu. Ni kuchelewesha tu..., mampambano yamekwishaanza na hayatamalizika mpaka ukoloni wa CCM uondoke/ujirekebishe.

The die is cast!
 
Mkuu wa mkoa kaweka zuio la mikusanyiko. Makamanda wa Chadema wanasema watakusanyika kwa nguvu kufanya kongamano.

Usiku wa manane wanadakwa. Maana mkuu wa mkoa anazo taarifa za kiusalama.

Je, hapa nani amefanya kosa?

Tusilaumu bila ya kuwa na argument za msingi.
Viongozi wa ccm,uwt,uvccm wanazunguka mikoa yote hawana zuio lolote,mama ni kilaza...anachoweza ni kula urojo,istoshe urais wake ni kipindi hiki tu alichopata kwa bahati ya shetani kupigwa na covid
 
Kuna problem sehemu, Kwa nini Rais muislam akiwa madarakan, kwa maaskofu ni kila cku matamko na hata hawa CDM kutwa n maandamano?
Nahtaji jibu
 
Mkuu wa mkoa kaweka zuio la mikusanyiko. Makamanda wa Chadema wanasema watakusanyika kwa nguvu kufanya kongamano.

Usiku wa manane wanadakwa. Maana mkuu wa mkoa anazo taarifa za kiusalama.

Je, hapa nani amefanya kosa?

Tusilaumu bila ya kuwa na argument za msingi.
Usiulize majibu wewe, si hao wakoloni weusi wasiojitambua. Afadhali kuwa na mkoloni kweli kweli kwa sababu anaweza kutumia Akili mara chache. Huoni Mandela kakaa jela miaka 27 na katoka mzima hadi Urais. Ingekuwa hapa kwetu kwa wakoloni weusi angefia huko huko. Uraiani kwenyewe sawa na jela huku kwetu, kila ukikohoa polisi yuko nawe, huku majambazi na madawa ya kulevya kama kawa.
 
Huyu mama yameishamshinda! Mwanzoni alijishaua akaonekana wa maana, sasa hivi keshakunjua makucha yake; shetani nambari wani!
 
Hyo agenda ya katiba ingekuwa na support ya wananchi wangeandamana, Sasa wananchi tu tumevurugwa na makodi mengi mara tozo mara ajira then utuambie katiba unafikiria tutakuelewa. In short CDM waje na agenda zinazogusa wananchi ka tozo, afya na ajira uone ka watakosa support hyo katiba ni janja Yao ya kutaka madaraka

Mkuu hayo matatizo yanayogusa wananchi: tozo, afya, ajira, n.k. haitatokea yashughulikiwe kikamilifu kwa vile si katiba iliyopo wala bunge lililopo vinaweza kuibana serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi. Katiba iliyopo inamuweka Rais juu ya kila mhimili, taasisi na sheria. Kazi za kisiasa zimejazwa (overloaded) serikalini na maslahi mazito. Gharama ya kuendesha serikali (overheads) ni kubwa haiwiani na hali ya uchumi. Utashi na maslahi ya viongozi ndio kipaumbele. Hazina ya taifa inaweza kuchotwa na kutumika kwa kadiri Rais anavyojisikia na kuruhusu. Hata akiamua kujenga mji wake mpya hakuna wa kuhoji.

Watanzania hawawezi kuandamana hata wakinyanyaswa namna gani. Msg toka State iko clear: andamana uwe kilema au uache wategemezi/watoto wako yatima. Aidha, kila mtu anawaza jinsi atakavyotoboa kivyake. Hakuna mshikamano wala maslahi ya pamoja. Ukipata masahibu utajijua mwenyewe.

Kwa katiba hii hii, wakati wowote, mtu wa hatari anaweza si tu kushika madaraka kama ilivyotokea kwa SSH, bali hata kusuka mpango wa kukaa madarakani for good kama mwelekeo wa JPM ulivyokuwa. Kwa kifupi, kwa katiba hii, Watanzania wote hata makada, wanachama na mashabiki wa CCM, wanaishi kwa kutegemea fadhila na huruma ya Rais.

Ni Rais wa awamu ya kwanza pekee, JKN, ndio hakuwa na tamaa; alihakikisha maslahi ya wananchi yanawekwa mbele. Alikuwa dikteta kweli; alibana uhuru wa kisiasa, mawazo mbadala na habari lakini kwenye maendeleo ya watu na vita dhidi ya ufisadi, alikuwa genuine. A benevolent dictator. Alisacrifice. Kosa lake kuu (legacy) alituachia hii katiba ya hatari sana.

Sasa kama tunaamini katika kuishi kama Taifa kwa imani kwa serikali hii na kuliona suala la katiba ni kwa “maslahi ya CHADEMA” tu, so well and good. Hatutaki kujiuliza kwa nini CCM na Serikali ya SSH wameamua kulikimbia suala hilo kwa kisingizio cha kutaka “kurekebisha mambo” ambayo majuzi tu JPM alidai “ananyosha nchi”?

Katika hali ya kawaida kabisa, baada ya kashkash za JPM zilizofanya wengi wadai kwamba “nchi sasa inapumua; mama anaupiga mwingi“, ilikuwa dhahiri sana kwamba pamoja na hatua za dharura kurekebisha mambo, Mh. SSH angeamua kwa dhati kuwa analipa suala la katiba mpya priority.

Naamini wengi tunakubali kuwa majuzi tu tumetoka kuepuka hatari kubwa sana iliyotukabili kama taifa kwa kutegemea kuishi kwa huruma ya Rais anayekuwa madarakani. Hivyo ni budi sasa kuchukua hatua za dhati kuepuka kurudia hatari ile. Kama alivyofanya kwa Covid-19, Rais angeunda kamati ya kuandaa utaratibu na ratiba ya kushughulikia suala hilo badala ya kuwaachia “hotheads” wa CHADEMA.

Ni juu yetu kuuona na kukubali au kuupuuza ukweli huu. Wenye hekima wanasema: Those who cannot learn from history are doomed to repeat it. Na, Choices have consequences.
 
Najua wapinzani hawawezi kuelewa hili lakini ndio ukweli.

Kuwaacha Chadema wafanye kongamano kisha wangefanya maandamano na ingeibuka hali ambayo kila mtu angekuja kujutia.

Kwaio polisi kufanya vile mi naona ni sawa, Tz kwa sasa serikali hii bado ni mpya, bado inahitaji muda kuweka mambo sawa na imeanza vizuri, mambo kama kuongezeka kwa tozo ni matokeo au muendelezo wa utawala ulopita kwenye mambo ya mapato.

Wapinzani wakati mwingine inabidi wawe watulivu na wawe wanajaribu kuelewa hali halisi sio kila kitu wanashikilia
 
Iko wazi chini ya kifungu cha 390(1)(b) cha CPA, harbeas corpus inapatikanaHivyo tumieni busara na hekima ili waletwe mahakamani kwa amri ya mahakama kuliko kuhamasisha wananchi waandamane.

Mimi kama mpenda amani nawashauri msitumie nguvu tumieni akili. Msiwaingize mkenge wananchi.
Hakuna mwananchi ataingia barabarani .. tuache upuuzi huo..
 
Iko wazi chini ya kifungu cha 390(1)(b) cha CPA, harbeas corpus inapatikanaHivyo tumieni busara na hekima ili waletwe mahakamani kwa amri ya mahakama kuliko kuhamasisha wananchi waandamane.

Mimi kama mpenda amani nawashauri msitumie nguvu tumieni akili. Msiwaingize mkenge wananchi.
Sema wewe kama mkandamiza amani,
 
Back
Top Bottom