Mwanza - Meya na Naibu wake wachaguliwa toka CHADEMA

Asante sana, ila kama utaweza tafadhali rekebisha title kidogo, hapo maana inayopatikana ni kwamba walikua wako CDM na sasa wametoka huko!!! aaahh au ulikua unataka ku-draw attention? katika uandishi inaruhusiwa pia! asante kwa taarifa ndo mwanzo wa shubiri kwa CCM
 
Mkuu hii habari ipo hapa tangu saa tano.....watu wanajipongeza saa hizi
 
Halmashauri ya jiji la Mwanza imepata Meya Josephat Manyeere na Naibu wake Charles Chibela..ambao wote wanatoka CHADEMA.

Hiyo ni mbinu ya kijeshi, miji mikuu (Arusha, Mbeya, Mwanza and in somewhat DSM) na mipaka (kigoma, Mbeya,lindi, Arusha, Bukoba, musoma) inatekwa kwanza. Hapo sasa!

Watawala hamjastuka bado?
 
Ushindi uko wazi ila ccm inataka lazima iue watz ndipo ipate meya............watz wa miaka ya 40 hawapo sasa!
 
Kama sijakosea Chadema ina madiwani 15+wabunge 2 na ccm ina madiwani 13 na cuf 2.
Cuf na ccm walikubaliana kusupportina kwenye umeya cuf waunge mkono ccm na ccm waunge mkono cuf kwny naibu. Kwenye kura za umeya hesabu ni 17 kwa 15. Kwenye unaibu chadema wamepata support ya diwani wa cuf au ccm maana kura ni 18 kwa 14

Chadema inao Madiwani 15 + wabunge 2 na CCM inao madiwani 12 + mbunge 1 kiti maalum (Maria Hewa) na CUF madiwani ni 2 hii inajumuisha na diwani maalum lakini hawana Mbunge jumla idadi ni 32 ndivyo kura zilivyokuwa na hakuna kura mabyo imeharibika hivyo Chadema wameshinda kwa kura 17 dhidi ya 15. Hii 18 siyo sahihi
 
Inawezekana tukikomaa hata kura za urais tungekomaa zisingechakachuliwa slaa amwage radhi hadharani tumwagike.
 
Mshindi Meya wa Mwanza ni Julius Manyerere (Chadema) amepata kura 17 Wakati wa CCM amepata Kura 15 Naibu Meya wa Mwanza Mshindi Ni Charles Chibela ( Chadema) Amepata kura 18 wakati wa CCM amepata Kura 14

Ina maana mwana ccm mmoja kawasaliti kwenye unaibu meya
 
Hivi kafu (cuf) bado wanajiita ni an opposition party ?? Yaani wanawasaidia ccm ktk upigaji kura! Shame on them!!
Njaa zinawasumbua
 
Usahihi wa majina ya wagombea na kura zao kwa Kiti cha Umeya Jiji la Mwanza ni: Chadema-Josephat Kanyonyi Manyerere amepata kura 17 na mgombea wa CCM Stanisilaus Mabula kura 15. Kwa upande wa Unaibu Meya wagombea walikuwa ni Daud Suleiman Mkama wa CUF aliyepata kura 15 na mshindi wa Chadema aliyeshinda kuwa naibu ni Charles Marwa Chinchibera aliyepata kura 17 na siyo 18 kama alivyoandika Ogwalu Mapesa.

Thanks kwa sahihisho.

Hapa ina maana kuwa CUF iliungana na CCM kuwa dhidi ya Chadema, kwani CCM ina madiwani 13 na CUF 2. Kura zao jumla ndiyo hiyo 15 alizopata mgombea wa Umeya kutoka CCM na mgombea Unaibu-Meya kutoka CUF.
CCM na CUF sasa ni ndoa kamili.

Chadema ina wajumbe 17 (madiwani 15 na wabunge 2), na wagombea wake walipata kura hizo 17.

Hongera wana-Mwanza. Na Arusha ni mpaka kieleweke.

Na kuhusu katiba mpya tunataka Mkutano wa kitaifa wa Katiba, siyo tume ya Kikwete, Kombani na Werema.
 
Hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, arusha lazima kieleweke tuuuuuu
 
MCC wamekalia jiti na dole gumba kwa pamoja, sasa si tamu tena ni uchungu tuuuu. MAFISADI ZIIIIIIIIIIIIIIII:hat:

Farasi kapoteza mwelekeo sasa anakurupuka na kupita vichakani.

Mwiba mkali na kwa MCC au MAFISADI CHAMA CHETU.

kweli unaendana na jina lako
 
Habari wanajamii
Poleni na shughuli za kila siku

Jamani naomba kupata uhakika, nimepata za hapa na pale kuwa Chadema wamezoa Kiti cha umeya mkoa wa mwanza , Ni kweli????
 
Chadema inao Madiwani 15 + wabunge 2 na CCM inao madiwani 12 + mbunge 1 kiti maalum (Maria Hewa) na CUF madiwani ni 2 hii inajumuisha na diwani maalum lakini hawana Mbunge jumla idadi ni 32 ndivyo kura zilivyokuwa na hakuna kura mabyo imeharibika hivyo Chadema wameshinda kwa kura 17 dhidi ya 15. Hii 18 siyo sahihi
unafafanua kitu ambacho hujakielewa wewe mwenyewe! hapo ina maana mgombea unaibu meya wa chadema alipata kura zote17 za wajumbe wa chadema plus 1 from upinzani(ccm/cuf) .

ukombozi ni hatua!tulipofikia siyo pa kubeza hata kidogo!!!!thanks God. lakini naumia sana roho na maini yangu kwa damu iliyomwagika ARUSHA. nwayz tutaonyesha dunia kuwa damu ya binadamu ina thamani sana ...subirini
 
Back
Top Bottom