Mwanza: Harufu ya rushwa kuelekea ugawaji wa fremu stendi mpya ya mabasi Nyamhongolo (mkoani Mwanza)

ALT

Member
Oct 6, 2021
78
90
Wanajamvi,

Habari zenu.

Moja kwa moja kwenye mada. Ni kama wiki imepita tangu mkuu wa mkoa( mhandisi Gabriel) alipo fika stendi mpya ya mabasi iliyoko nyamhongolo kwa ajili ya makabidhiano kati ya mkoa na mkandarasi.

Wakati wa makabidhiano mkuu wa mkoa aligusia mchakato wa wilaya husika ya ilemela kupitia halmashauri yake kuanzia ijumaa hadi jumapili ya wiki iliyopita mchakato wa kuingia mikataba ya fremu za maduka izo uanze.

Katika ufuatiliaji wa fursa iyo, mwongozo ulitolewa katika siku izo tatu wenye nia waanze kuitembelea stendi na kupiga picha fremu husika alafu apeleke picha halmashauri atapewa fomu za kujaza chini ya muongozo wa mkurugenzi wa halmashauri husika then utajuzwa taratibu zitakazo fuata.

MREJESHO HADI SASA

Siku ya kwanza

Tangu ijumaa ya wiki jana, ukienda halmashauri kuulizia utaambiwa, tangazo bado, subiri tangazo.

Siku ya pili

Jumatatu ya jana, tangazo bado, subiri tangazo.

Siku ya tatu

Leo jumanne, tangazo bado, subiri tangazo. Ukiwahoji mbona kuna taarifa katika gazeti( nipashe nadhani), tangazo limerushwa jana? Wanakwambia mpaka gari letu la matangazo lipite litangaze kote ndipo mlete maombi yenu.( Na kwa msisitizo, unaambiwa, sio kwamba kutuma maombi ndio utakua umepata, la hasha, kukosa kupo.)

ZA CHINI YA KAPETI
Kwanza jumla ya fremu ni sabini na ushee. Inasemekana wenye vyeo vizito wizarani wanapiga simu moja kwa moja na kushika fremu, pia kila diwani wilaya nzima ya ilemela ameshika fremu na wadau wengine wazito. Hoja ya kusubiri tangazo ni geresha tuu.

MAONI KWA MKOA NA IKULU KIUJUMLA

Hakikisheni ushindani unakua wa uwazi na ukweli. Haiwezekani watu wanafata taratibu mlizozitoa lakini tayari ninyi wenyewe mnauharibu utaratibu.

Usalama wa taifa, mkuu wa mkoa, takukuru kwa uwezo wenu wote, ingilieni kati.

HITIMISHO
Msipofanya sehemu yenu, subirini aibu mtakayoipata mbele ya rais mwezi ujao atakapokuja kuizindua hiyo stendi. Hapo ndipo mtaijua nguvu ya umma.
 
Back
Top Bottom