Mwanaume ni yupi hapa??

i love the way you defined me hapo juu lol
if only it was the honest truth lol ukiacha hiyo part ya kuoa 'malaya....

now tukija kwenye answer....what if nikishindwa 'kumdhibiti' ??????

Stop your bragging... Hapo nimechukua sifa zoote za Sweetie na ku apply mfano kwako...lol...

Believe me you kwa mwanaume yeyote mwenye sifa nimetaja hapo juu.... Hakuna "What if akishindwa kumdhibi??"

WHY?? Mara nyiingi mwanaume wa namna hio akipenda... daima hu apply the brain to his heart no matter his juniour inasemaje!! Kama anakupenda he will treat you well mpaka uchanganyikiwe... Lakini mwanamke asijidanganye hata siku moja kua just because anapendwa anaweza leta upuzi wowote to this type of man.... Na mara nyingi jamaa wa namna hii akiachia ngazi... There is NO turning back... wala no LOVING another woman the same way again...
 
hilo tatizo tumeshapata suluhisho la kihandisi. unatumia tube tofauti kwa kila kalio. maty ukipata supplier uniambie na mie manake fidel80 kanifumbua ukope,kumbe pasi ndo inaniponza!

You naughty King'asti.....ngoja nikusemee kwa Sweetie apa...
 
Wa kwanza...

Huyo mwanaume akumbuke kua haishi in isolation. Kuoa mwanamke ambae ni the so called malaya ni mara nyingi hutokea katika Jammii. But kumbuka kua maisha ya ndoa yanahusisha nyie wanandoa kuishi kwa amani na hadi wale wanaowazunguka muishi nao kwa amani. Boss kwa Mantik hio kama kweli unajua mkeo alikua ni the so called Malaya kubali kua inabidi muhame na mkae makazi ya mbali kabisa... For siamini kabisa kua kuna mwanaume ambae atapenda aonane kila siku zaidi ya wanaume labda wa 4 walowahi lala na Mkeo... Sidhani kwa kweli....

Wa Pili....

Mapenzi ni mchezo wa ajabu saana. Boss mtu kuwa na vigezo vyoote haina maana ndio utampenda... sijui hii nyama ya moyo imeumbwa vipi na roho nayo sijui hutumia vigezo gani kutuongoza katika suala zima la kupenda. Maana ingekua hivo hawa kaka/dada zetu ambao mara nyingi hutoka basi wasingekua wanatoka; maana from observation unaona mtu ana mwenza ana vigezo vyoote but bado hatoka....

Uwanaume;

Nakubaliana kua mara nyingi kuonekana kua a Man is indeed a Man tokana na maamuzi yake... matendo yake.... na attitude yake hasa katika life na yalomzunguka... The above woote waweza onekana wanaume wa kweli; i.e Wa kwanza awe mtu mwenye heshima zake... kaweza mdhibiti the wife kiasi kwamba jammii yoote inaona kabisa the Change in the woman na kotovumilia upuzi wowote ambao Mkewe atafanya in relation na kunukia kwa a new species... hasa tokana na reputation... such a wife atakiwi a-entertain opposite sex kua nae karibu for jamii lazima imzushie... AU akaonekana sio mwanaume kwa kushindwa Mdhibiti.... Wa pili waweza oa Mwanamke mwenye vigezo vyoote but still ushindwe onesha uanaume wako... tena Boss in this case si ndo cheating kwa saana?? na nyie wanaume si ndo mnapenda define kwamba huo ndo uanaume (sijui nani alikuja na hii reasoning but thankfully ina change)

Sio kwamba nataka kukupinga, lakini kwa mtazamo wangu, swali la The Boss, limekaa kimtego na bila kujua nimeona wengi wameingia mkenge........... Mie nimejiuliza, kwa nini Malaya awe ni mwanamke tu, Je mwanaume hastahili na yeye kuhukumiwa kwa vigezo hivyo vya Umalaya?
Hapa kuna tataizo moja, tena kubwa, wanaume wengi hawaoi kama wao wanaoa kulingana na jamii inavyotaka, jamii imechukua nafasi kubwa sana katika maamuzi yetu........ naweza kusema karibu asilimia 75 ya vigezo vyote tunavyoangalia ili kufanya uchaguzi wa wenza wetu vimebebwa na jamii, sisi tunabakiwa na asilimia 25 tu basi.
Utakuta mwanaume anamtambulisha mpenzi wake kwa marafiki zake au ndugu zake halafu anauliza, "Eti mnamuonaje mtarajiwa wangu" amini wakimwambia hafai au wakimkosoa hata kidogo, jambo hilo litamsumbua sana na huenda likasababisha akabadili mawazo, hivyo ndivyo tunavyoishi...........
Swala la kuhama baada ya kuoana, AshaDii kama mtu unaishi kama wewe na sio kama jamii inavyotaka, huwezi kuhama. kwani kuhama ndio hicho kibandiko cha umalaya alichopewa huyo mwanamke kitaondoka!? utakuwa ni ujinga tu, kama umeamua kumuoa pamoja na kusemwa kwamba alikuwa malaya, ni wewe uliyeamua na hukushurutishwa na mtu, sasa kwa nini jamii iliyokuzunguka ikunyime usingizi. wewe endelea na maisha yako, na huenda wakajifunza kupitia kwako....................
 
HAKUNA 'UANAMKE 'WA MWANAUME...

ILA KUNA MEN NA LESSER MEN...

AU ile wanaita men na men's men...

ni swala la mwanaume kamili.au mwanaume dhaifu...but wote ni wanaume still

lol the Boss....hujasikia kuwa 'mbona unafanya mabo ya kike" au huyu jamaa 'kama mwanamke tu mambo yake' kumaanisha kuwa short of being a man, you become a 'woman' (no pun intended)
 
kweli mapenzi sio siasa
but huwezi amini...wanaume tulio wengi tunajali zaidi
'heshima' kuliko kufuata mioyo ndo maana kuna vimada weengi mno...
mke ni heshima,kipenda roho kinakuwa kiko pembeni....lol

Mkuu ukizungumzia uanaume ni kuoa 'mke wako' na sio 'mke wa jamii'........
Maamuzi magumu ni yale unayoona yana maana kubwa kwa maisha yako...ila yanaweza kuzusha tofauti au kutoelewana na baadhi ya watu.......

Pia kumbuka jamii huwa haina 'opinion' moja siku zote....
 
lol the Boss....hujasikia kuwa 'mbona unafanya mabo ya kike" au huyu jamaa 'kama mwanamke tu mambo yake' kumaanisha kuwa short of being a man, you become a 'woman' (no pun intended)

hizo ni 'matusi' tu
ni sawa na wengine mtu akiwa dhaifu ataitwa' gay'

while kuna ma 'gay' jeshi la marekani waliiomuua 'kidume' osama...lol

so mtu akiwa labda 'mdhaifu kwa hoja'anaweza kuitwa hivyo while si kweli kuwa mwanamke ndo kuwa dhaifu...

ni aina ya matusi...tu ..mtu anasema to someone he doesn't respect..
 
Sio kwamba nataka kukupinga, lakini kwa mtazamo wangu, swali la The Boss, limekaa kimtego na bila kujua nimeona wengi wameingia mkenge........... Mie nimejiuliza, kwa nini Malaya awe ni mwanamke tu, Je mwanaume hastahili na yeye kuhukumiwa kwa vigezo hivyo vya Umalaya?
Hapa kuna tataizo moja, tena kubwa, wanaume wengi hawaoi kama wao wanaoa kulingana na jamii inavyotaka, jamii imechukua nafasi kubwa sana katika maamuzi yetu........ naweza kusema karibu asilimia 75 ya vigezo vyote tunavyoangalia ili kufanya uchaguzi wa wenza wetu vimebebwa na jamii, sisi tunabakiwa na asilimia 25 tu basi.
Utakuta mwanaume anamtambulisha mpenzi wake kwa marafiki zake au ndugu zake halafu anauliza, "Eti mnamuonaje mtarajiwa wangu" amini wakimwambia hafai au wakimkosoa hata kidogo, jambo hilo litamsumbua sana na huenda likasababisha akabadili mawazo, hivyo ndivyo tunavyoishi...........
Swala la kuhama baada ya kuoana, AshaDii kama mtu unaishi kama wewe na sio kama jamii inavyotaka, huwezi kuhama. kwani kuhama ndio hicho kibandiko cha umalaya alichopewa huyo mwanamke kitaondoka!? utakuwa ni ujinga tu, kama umeamua kumuoa pamoja na kusemwa kwamba alikuwa malaya, ni wewe uliyeamua na hukushurutishwa na mtu, sasa kwa nini jamii iliyokuzunguka ikunyime usingizi. wewe endelea na maisha yako, na huenda wakajifunza kupitia kwako....................

umeona aisee???mimi nasema sio 75 ni zaidi ya 80.....huo ndo ukweli..
halafu umeshawahi kwenda kwenye sherehe za harusi uone majigambo ya upande wa bi harusi kuhusu binti yao???
utasema ni malaika lol
 
hizo ni 'matusi' tu
ni sawa na wengine mtu akiwa dhaifu ataitwa' gay'

while kuna ma 'gay' jeshi la marekani waliiomuua 'kidume' osama...lol

so mtu akiwa labda 'mdhaifu kwa hoja'anaweza kuitwa hivyo while si kweli kuwa mwanamke ndo kuwa dhaifu...

ni aina ya matusi...tu ..mtu anasema to someone he doesn't respect..

Mkuu The Boss

Ni matusi hayo hayo tunayatumia kusema kwamba anayeoa mwanamke 'malaya' sio 'mwanaume kamili'

Matusi tunayajenga na kuyatumia sisi.....na katika muktadha wa kufanya mambo 'kike', nisingeilinganisha na kuwa 'shoga' manake kikwetu kidogo hiyo ni extreme case...lol
 
umeona aisee???mimi nasema sio 75 ni zaidi ya 80.....huo ndo ukweli..
halafu umeshawahi kwenda kwenye sherehe za harusi uone majigambo ya upande wa bi harusi kuhusu binti yao???
utasema ni malaika lol

mkuu mimi I did just the exact opposite kwa hiyo nitakuwa hapo kwenye 80% lol

Ila ndo ivo za ki ivyo, hata wiki haipiti mwanamke/mwanaume ana kidumu/ nyumba ndogo a.k.a the real lover
 
Khaaa!!! Kaizer hauchelewi lol......AshaDii huyu bro kaweka surveillance cameras wapi??

Genuinely huwa hata mie hua namshanga... Really...lol.. I hope sasa you understand for that is just one of the reasons I LOVE him....
 
Mkuu The Boss

Ni matusi hayo hayo tunayatumia kusema kwamba anayeoa mwanamke 'malaya' sio 'mwanaume kamili'

Matusi tunayajenga na kuyatumia sisi.....na katika muktadha wa kufanya mambo 'kike', nisingeilinganisha na kuwa 'shoga' manake kikwetu kidogo hiyo ni extreme case...lol

mkuu
thread imeenda ikibadilika kwa watu kuchangia na kuanzisha vitopi ndani yake..
but ukiona mwanzo nilikuwa carefull na ndio maana nilisema 'uamuzi wa kiume'
kwa maana ya ujasiri na sio kwamba sio wanaume kamili..
 
Sio kwamba nataka kukupinga, lakini kwa mtazamo wangu, swali la The Boss, limekaa kimtego na bila kujua nimeona wengi wameingia mkenge........... Mie nimejiuliza, kwa nini Malaya awe ni mwanamke tu, Je mwanaume hastahili na yeye kuhukumiwa kwa vigezo hivyo vya Umalaya?
Hapa kuna tataizo moja, tena kubwa, wanaume wengi hawaoi kama wao wanaoa kulingana na jamii inavyotaka, jamii imechukua nafasi kubwa sana katika maamuzi yetu........ naweza kusema karibu asilimia 75 ya vigezo vyote tunavyoangalia ili kufanya uchaguzi wa wenza wetu vimebebwa na jamii, sisi tunabakiwa na asilimia 25 tu basi.
Utakuta mwanaume anamtambulisha mpenzi wake kwa marafiki zake au ndugu zake halafu anauliza, "Eti mnamuonaje mtarajiwa wangu" amini wakimwambia hafai au wakimkosoa hata kidogo, jambo hilo litamsumbua sana na huenda likasababisha akabadili mawazo, hivyo ndivyo tunavyoishi........... .

Mtambuzi the above paragraph umeongea kana kwamba we have hio luxury ya kua judged sawa... Yaani Men Vs Women.... Sio kweli.. Tunaishi in a partriachal society ambayo sasa inajaribu kuweka hizo balances ziwe sawa kwa jinsia zooote; Thus gender ... its issues and related activities... Hivo basi bado saaana kua mwanamke malaya awe sawa na mwanaume wa hivo...Mfano mdogo tu; Naweza kua na mwanaume malaya balaa na jamii yote ikatambua hilo... Siku nikiamua nitoke ili nilipishe... bado jamii hiyo hiyo - wake kwa waume wata ni judge mimi lakini sio mume wangu.

Swala la kuhama baada ya kuoana, AshaDii kama mtu unaishi kama wewe na sio kama jamii inavyotaka, huwezi kuhama. kwani kuhama ndio hicho kibandiko cha umalaya alichopewa huyo mwanamke kitaondoka!? utakuwa ni ujinga tu, kama umeamua kumuoa pamoja na kusemwa kwamba alikuwa malaya, ni wewe uliyeamua na hukushurutishwa na mtu, sasa kwa nini jamii iliyokuzunguka ikunyime usingizi. wewe endelea na maisha yako, na huenda wakajifunza kupitia kwako....................

Kuhusu kuhama.... Mtambuzi amini usiamini whether you like it or not mara nyingi day to day activities wewe hufanyaga hua influenced na jamii ilokuzunguka... La sivo basi watu tungekua na nguo pair mbili to... mana si ilimradi ujisitili?? Kama kweli umependa huyo mwanamke kweli kuhama muhimu... la sivo ita affect the whole family... maneno husimuliwa na kukua from people to people na generation to generation hasa hizi za kashfa za kifamilia.... Unataka watoto wawe pre-judged kabla hawajapewa a chance to live their own life?? Unataka mkeo kila siku akumbushiwe kua alikua malaya makosa daima kutofutwa??

Ni vigumu... lakini like i said we don't live in isolation.
 
mkuu
thread imeenda ikibadilika kwa watu kuchangia na kuanzisha vitopi ndani yake..
but ukiona mwanzo nilikuwa carefull na ndio maana nilisema 'uamuzi wa kiume'
kwa maana ya ujasiri na sio kwamba sio wanaume kamili..

Rite rite...tukizungumzia ujasiri....nini maana hasa ya ujasiri....ni kufanya jambo ambalo WENGI wageshindwa kulifanya katika hali ya kawaida, ni uwezo, katika huu muktadha, wa kufanya maamuzi ambayo wewe unaamini kama ni sahihi hata kama yataenda kinyume na matarajio ya wengi

kwa hiyo basi, huyo anayeonekana kwamba 'ameoa malaya' ni jasiri zaidi kwa sababu ame-defy expectations za jamii inayomzunguka AKIAMINI kuwa muoaji ni yeye, atakayeishi naye ni yeye

Itakuwa hatari kama tukisema what would happen next (mfano kama huyo 'malaya' atabadilika nk) kwa sababu hata ujasiri nao unaweza kubadilika with time. kwa faidi ya mjada huu nadhani ingekuwa vema kuishia kwenye kitendo cha kuoa/kuolewa
 
Kwa kusema kweli, hilo swala la "Kipenda roho" tuliache kwenye urafiki, inapofikia swala la mke, mama wa familia, mama wa watoto wako, lazima kuna vitu vinatakiwa kuzingatiwa. Sidhani kama kuna mume ambaye atavumilia mkewe akiwa malaya, hata kama anampenda vipi
 
Back
Top Bottom