Mwanaume anapotongozwa na mwanamke

Hata zamani ilikuwepo sema siku hizi wako aggresive zaidi.
Kanuni ni zile zile kama anazotumia mwanamke kupima mtu kabla ya kumkubali. Ukitia tamaa mbele utaingia mkenge.
Kama ni malaya wa kiume tumia kanuni za malaya wa kike, kama unajiheshimu angalia mwanamke anayejiheshimu anafanyaje akitongozwa.
Mi nilishatongozwa kwenye pombe nikatoroka, kesho yake nikaombwa msamaha (ile U know i didnt mean it, blah blah). Yakaisha
 
Watu tunatofautiana,wapo wengine ambao humuona msichana kama vile ni kiruka njia na hajiheshimu,wapo wengine ambao watatangaza kila kona na mengineyo mengi.Lakini kwangu mimi binafsi huwa ninamuheshimu sana msichana aliyeweza kunikabili na kunieleza ukweli wake hata kama sitakubaliana na ujumbe wake,na huwa ninamchukulia kama mtu anayejiamini na ambaye atakuwa mke bora kwa mumewe kwa kuwa ana uwezo wa kueleza hisia zake na hata kama mambo hayaendi vizuri katika familia basi atazungumza bila kuficha hisia zake.

Kwa upande mwingine kuna wale ambao hawawezi kumkabili mwanaume na kumueleza ukweli ila wanaonesha kwa vitendo,hao mimi ndio wala huwa sina muda nao hata aje kwangu hajavaa nitamuangalia tu kwakuwa ilinitokea kuiwa karibu na mkurugenzi wangu ambaye alipenda muda mwingi kuwa na mimi hasa wakati wa kunywa kahawa na mida ya lunch,tatizo alikuwa anapenda sana kuvaa vimini ambavyo viko juu yua magoti basi muda wote tunaokuwa pamoja mimi nakuwa na kazi ya kuchungulia nguo zake za ndani na alikuwa hajui hasa kukaa,na nikimtazama tukikutanisha macho basi napewa tabasamu na kurembuliwa juumambo yalikuwa mengi tu ya mitego basi mtoto wa kisukuma nikajua amenipenda nikazungumza.Alivyokuwa mstaarabu wala hakunijibu vibaya aliniambia tu nitakujibu jumatatu ofisini.Jumatatu nafika ofisini nakutana na barua ya kufukuzwa kazi kwa sababu ya utovu wa nidhamu.toka siku hiyo nikakoma kumtongoza msichana kutokana na ishara anazonionesha mpaka anitamkie wazi.

Searching...100%
Loading...100%
Network Connected !

Umetisha
 
nisaidieni jamani...napata majibu yanayonichanganya... kina kaka na hata kina dada hebu niambieni..mwanaume anapotongozwa na mwanamke anajisikiaje??? ni nini mawazo yake??? Je, unamchukuliaje mwanamke liyekutongoza

Mimi sijawahi kutongozwa na mwanamke kwa hiyo sijui inakuwaje. Ila ukweli ni kuwa wakati natafuta mke nilipenda sana wanawake kama watano hivi wanitongoze ili nichague mmoja kati yao ninayeridhika naye. Niliamini na bado ninaamini kuwa mwanamke anayekutongoza anakuwa amekupenda kweli kweli kwa sababu siku zote kutongoza ni changamoto kubwa hata kwa wanaume. Baada ya kusubiri kwa muda nikagundua approach hiyo ingenichelewesha sana kupata mke.
 
Binafsi najisikia kawaida kabisaaa, na naona ameshindwa kuzuia hisia zake kama ambavyo mimi huwa nashindwa na kuanza kumtongoza mwanamke
 
nisaidieni jamani...napata majibu yanayonichanganya... kina kaka na hata kina dada hebu niambieni..mwanaume anapotongozwa na mwanamke anajisikiaje??? ni nini mawazo yake??? Je, unamchukuliaje mwanamke liyekutongoza
Vp unataka kutongoza nn, njoo unitongoze mimiaf ntakwambia nilivyojiskia na jijsi nilivyo kuchuklia wewe
 
Naonaga ni rahisi kumtambua vizuri mtu huyo aliekudondokea, Inatia moyo kwamba huenda ukapewa penzi la dhati zaidi kuliko wale ambao tunawaanzaga sisi
 
Action is louder than words! huwa wanatafuna ili uweze kumeza kama domo zege ndo wanakutamkia kabisa kwangu si jambo la ajabu coz chelewa utakuta mwana si wako ingawa wanaumia sana kama akivunja ukimya hivyo kisha ukamtosa.
 
Daa,me nimewahi tongozwa na mdada nilimsumbua sn.Lakini alifanikiwa na nilikuja kumpenda balaa,alijitoa sn kwangu.Namiss upendo wake kwakweli.
 
kama kuna mwanaume anajifanyaga sharobaro mtaani mdada jikaze umtokee yaan atageuka domo zege na mwoga.Nilishajaribu hii pindi napokuwa nataka kukwepa usumbufu wa hawa jamaa kona flani flani.
NB:hakikisha unamchania kihiphop yaan mwenyewe atazima hata kama kuna jua.
kula like 1000 we noma aisee
 
Linda gari kwa GPS Tracker na kwa kupitia simu yako au computer itakupa ripoti:
- Eneo gari lako lilipo kupitia google map- Route za gari siku zilizopita hii hasa wenye tax,gari za kukodi na mizigo- Itakupa kilomita ilizotembea- Itakupa mwendokasi wa gari husika
Bei ni poa na hakuna malipo ya mwezi kwa maelezo tu PM au email:ngamatechn@gmail.com

Gud....
 
Demu akinitongoza clembi coz ataniona nyoka wa kibisa,nafanya mambo yangu af uyo najikataa kmya kmya kwa kuwa km aliweza kuntongoza mm ashindwi kumtongoza mwingine,nshafagia mademu 15 wenye style izo.

kwa hiyo ukitongoza mwenyewe ndio hatongozwi na mwingine? nae pia ana hisia kama wewe.
 
Siyo vibaya. Ila mwanamke akikutongoza mwenyewe unakuwa huna mzuka nae kabisa. Utamsikiliza alafu utampotozea, akiendelea utajitahidi ujue kama ni mtego au kweli. Ukiona safi unaenda nae hivyo hivyo lakini siyo kiviiile.
 
Hii kitu huwa siifagilii kweli aisee, huwa inanipotezea kujiamini mbele ya huyo binti, matokeo yake naanza kumkwepa. Tena wanaonikera zaidi ni wale wanaoshirikisha rafiki zangu, manake huwa wananiandama sana.. Kati ya mabinti wote wanaonitongoza hakuna aliyebahatika kunipata, manake huwa wananifanya niwe na aibu na kuwakwepa kuepuka ku-blush mbele yao... Napendelea kutongoza kuliko kutongozwa.
We mvulana tu
 
Back
Top Bottom