haya mambo nilishayafafanua hapa kwa kirefu.
Glory to God
weka wazi, binafsi sikusoma hayouliyofafanua
haya mambo nilishayafafanua hapa kwa kirefu.
Glory to God
Ha ha ha wanaume kutongozwa siku hizi kawaida sana. Tunatofautiana wanaume wanasema (nakutaka, nakupenda, nakuthitaji nk) lakini wanawake wanatenda kuonyesha kuwa (nakupenda, nakutaka, nimekuzimia, nakuhitaji nk)
Watu tunatofautiana,wapo wengine ambao humuona msichana kama vile ni kiruka njia na hajiheshimu,wapo wengine ambao watatangaza kila kona na mengineyo mengi.Lakini kwangu mimi binafsi huwa ninamuheshimu sana msichana aliyeweza kunikabili na kunieleza ukweli wake hata kama sitakubaliana na ujumbe wake,na huwa ninamchukulia kama mtu anayejiamini na ambaye atakuwa mke bora kwa mumewe kwa kuwa ana uwezo wa kueleza hisia zake na hata kama mambo hayaendi vizuri katika familia basi atazungumza bila kuficha hisia zake.
Kwa upande mwingine kuna wale ambao hawawezi kumkabili mwanaume na kumueleza ukweli ila wanaonesha kwa vitendo,hao mimi ndio wala huwa sina muda nao hata aje kwangu hajavaa nitamuangalia tu kwakuwa ilinitokea kuiwa karibu na mkurugenzi wangu ambaye alipenda muda mwingi kuwa na mimi hasa wakati wa kunywa kahawa na mida ya lunch,tatizo alikuwa anapenda sana kuvaa vimini ambavyo viko juu yua magoti basi muda wote tunaokuwa pamoja mimi nakuwa na kazi ya kuchungulia nguo zake za ndani na alikuwa hajui hasa kukaa,na nikimtazama tukikutanisha macho basi napewa tabasamu na kurembuliwa juumambo yalikuwa mengi tu ya mitego basi mtoto wa kisukuma nikajua amenipenda nikazungumza.Alivyokuwa mstaarabu wala hakunijibu vibaya aliniambia tu nitakujibu jumatatu ofisini.Jumatatu nafika ofisini nakutana na barua ya kufukuzwa kazi kwa sababu ya utovu wa nidhamu.toka siku hiyo nikakoma kumtongoza msichana kutokana na ishara anazonionesha mpaka anitamkie wazi.
Pole kwa kufukuzwa kazi jamaangu.
Vipi yule anayejua kuwa wewe ni mume wa mtu na anakujia kuwa anakutaka! naye tumwite jasiri ama ni nini mkuu?
Majuzi hapa nimetongozwa na kibinti na ninaomba nikili hapa kwamba hakuna kipindi kigumu kama hicho katika maisha
Hii kitu huwa siifagilii kweli aisee, huwa inanipotezea kujiamini mbele ya huyo binti, matokeo yake naanza kumkwepa. Tena wanaonikera zaidi ni wale wanaoshirikisha rafiki zangu, manake huwa wananiandama sana.. Kati ya mabinti wote wanaonitongoza hakuna aliyebahatika kunipata, manake huwa wananifanya niwe na aibu na kuwakwepa kuepuka ku-blush mbele yao... Napendelea kutongoza kuliko kutongozwa.
whuhhwhuuu!
These days, its normal. Thats y nakuwa na uwezo wa kukacha/kukubali.
Namheshimu pia coz ametumia uhuru wake kueleza kilicho moyoni mwake.