MwanaHalisi yamshambulia Sitta

Kubenea asema, Sitta mwongo


Na Fred Okoth

MKURUGENZI mtendaji wa gazeti la MwanaHALISI, Saed Kubenea, amekana tuhuma kwamba gazeti lake "limenunuliwa na watuhumiwa wa ufisadi nchini."


Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel John Sitta, amedai kuwa Kubenea na gazeti lake wamenunuliwa na watuhumiwa wa ufisadi kutokana na kumshambulia yeye na "wapiganaji wenzake" katika vita dhidi ya ufisadi.

"Mafisadi wanatumia magazeti yao na magazeti mengine kunishambulia. Huko nyuma walikuwa wanatumia magazeti ya Tanzania Daima na Tazama Tanzania. Lakini sasa, wamemnunua hata huyu kijana wetu, Kubenea na gazeti lake la MwanaHALISI…" alisema Sitta.

Tuhuma hizo nzito ziliibuliwa juzi Jumatatu wakati Sitta akihojiwa katika kipindi cha "Dakika 45" kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Spika huyo wa zamani wa Bunge alidai gazeti hilo lilianza vizuri, lakini sasa limeanza kuyumba baada ya kutumiwa kupambana na wanaopinga ufisadi.

Hatua ya Sitta kuituhumu MwanaHALISI imekuja miezi sita baada ya gazeti kuripoti ushiriki wa kiongozi huyo kwenye uanzishwaji wa Chama cha Jamii (CCJ).

Katika toleo lake la 18 Mei 2011, gazeti liliripoti juu ya Sitta kuwa nyuma ya ujio wa CCJ. Lilinukuu Fred Mpendazoe, mbunge wa zamani wa Kishapu (CCM), ambaye ni miongoni mwa waanzishili wa chama hicho na aliyekuwa swahiba mkubwa wa Sitta.

Wengine ambao Mpendazoe aliwataja kuwa ama washiriki au waanzilishi wa CCJ, ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, katibu msaidizi wa CCM wilayani Moshi Mjini, Daniel ole Porokwa na kada wa chama hicho, Paul Makonda.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake, Kubenea amesema tuhuma za Sitta "zinastahili kjibiwa kwa uzito unaostahili kwa vile ni uongo na upuuzi mtupu ambao umelega kuharibu sifa za gazeti, wamiliki na waandishi wake."

"Kuna watu wanaotuchukia na kila siku tunaongeza maadui wapya kutokana na kazi tunaoifanya. Miongoni mwa maadui wetu wa sasa, tunaona yumo Samwel John Sitta aliyechukizwa na hatua ya gazeti letu kufichua ushiriki wake kwenye CCJ. Ndiyo maana ameamua kukaa chini, kutunga tuhuma na kuziporomosha," ameeleza Kubenea.

Amesema, "Natambua mchango wa Sitta katika mapambano dhidi ya ufisadi, hasa alipokuwa Spika wa Bunge la Muungano. Lakini tatizo kubwa linalomkabili mwanasiasa huyo, ni kule kutaka kuandikwa anavyotaka na siyo alivyo…"

Kubenea amesema, "Hatujawahi, hata mara moja, kuandika habari, makala au kitu chochote chenye mwelekeo wa kushambulia Sitta binafsi. Kazi tuliyoifanya ni kuripoti kilichopo. Labda kama hilo ndilo kosa letu."

"Tulitarajia angetupongeza kwa kutimiza wajibu wetu kwa kuwaambia Watanzania ukweli, badala ya kutushambulia na kutulaani. Tulidhani angetumia makala na habari tulizochapisha kujikosoa, kwa kuwa yeye ni binadamu kama wengine. Hatukutarajia kutumia fursa aliyopewa kutushambulia," ameeleza Kubenea.

Akiongea katika kipindi hicho, Sitta alikiri kufuatwa na watu mbalimbali kujiunga na vyama vyao. Bali aligoma kuzungumzia bayana ushiriki wake kwenye CCJ. Alisema CCM kinahitaji mageuzi makubwa kabla hakijakutwa na kiama.

Inadaiwa Sitta alikuwa miongoni mwa waanzishili wa CCJ. Mkakati ulikuwa ni kuondoka ndani ya CCM kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Baadaye yeye na kundi lake walipanga kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili kuongeza nguvu ya kuiondoa CCM.

Kuna taarifa kwamba Sitta ndiye alikuwa akilipia pango la ofisi. Ndiye alikuwa anatoa fenicha za ofisi na ndiye alikuwa analipa mishahara ya katibu mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi na mwenyekiti wake, Richard Kiyabo.

Hii si mara ya kwanza Sitta kutoa kauli ambazo baadaye zimeonekana kumponza na wakati mwingine kumvunjia heshima.

Kwa mfano, Januari 2008, alibeza madai na vielelezo vilivyotolewa bungeni na Dk. Slaa kuhusu tuhuma za ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT), ikiwamo wizi uliofanywa na kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd., iliyokwapua zaidi ya Sh. 60 bilioni.

Dk. Slaa ambaye wakati huo alikuwa mbunge wa Karatu, aliwasilisha vielelezo hivyo kujenga hoja ya kutaka Bunge liunde kamati ya kukagua hesabu za BoT.

Akipinga hoja ya Dk. Slaa, Sitta alisema, "Vielelezo vya Dk. Slaa ni vipeperushi vya mitandao." Alidai hakuna wizi uliofanyika ndani ya BoT na kwamba Dk. Slaa alikuwa anatafuta umaarufu wa kisiasa.

Mfano mwingine ni pale Sitta alipoamuru kufungwa kwa mjadala wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond bungeni kwa kuwa "serikali imetekeleza maazimo 21 kati ya 23 yaliyotolewa na bunge."

Lakini baadaye alinukuliwa akisema, uamuzi wake wa kufunga mjadala huo, ulitokana na "tishio la kuvuliwa uanachama wa CCM."
 
sita mnafiki kanunua asprin milion 5 alafu anajiita mzalendo ?! intelijinsia ya nchi inaonesha kwamba sita ni al shaabab
 
Sitta ashukuru utawala wa kulindana wa JK -- angekuwa ameshatimuliwa kwa usaliti wake. CCM ni chama cha ajabu sana duniani -- kuna mafisadi, wezi, manafiki, wasaliti, macowboy (wanaotembea na silaha viunoni, wazinzi -- lakini bado iko tu madarakani!

In this country we have sheep for human beings!

Hata Kikwete ni msaliti, ahadi chungu nzima matokeo mpaka sasa hivi sifuri hakuna ahadi hata moja aliyoitekeleza. Kama si ukondoo tuliokuwa nao Watanzania si ajabu angeshakuwa history miaka mingi iliyopita. Hivi ndani ya Magamba kuanzia waliowahi kushika nafasi za juu (Mkapa, Mwinyi, Kikwete) na hadi za chini kuna yeyote ambaye si msaliti kwa Watanzania!? Kama yupo basi jina lake liwekwe hapa jamvini.
 
Mwanahalisi wamefichua "unafiki" wa Sitta. Nani atafichua unafiki wao?

Mbona Kubenea hasemi ni kwanini serikali inamlipia safari za karibu kila mwezi kwenda India huku akilipwa na posho kwa safari hizo iwapo waliompopoa kwa tindikali si serikali?

Nani alitegemea Mwanahalisi wampende Sitta wakati anatishia maslahi yao ya nyuma ya pazia? Nani hajui kuwa Mwanahalisi ni gazeti linaloendelea kuelekea udaku zaidi ya ithibati ya awali?

Kwanini tahariri haielezi ni kwanini Mwanahalisi limeacha hoja na ajenda yake kuu yaani Edward Lowassa? Ukiishi kwenye nyumba ya vioo usiwachokoze wehu.

Hata Kubenea arobaini yake haiko mbali naye wapo watakaofichua unafiki wake na umaarufu wake wa tindikali. Aweke CV yake uone kama ni mali kitu au jafafa.
 
Mwanahalisi wamefichua "unafiki" wa Sitta. Nani atafichua unafiki wao?

Mbona Kubenea hasemi ni kwanini serikali inamlipia safari za karibu kila mwezi kwenda India huku akilipwa na posho kwa safari hizo iwapo waliompopoa kwa tindikali si serikali?

Nani alitegemea Mwanahalisi wampende Sitta wakati anatishia maslahi yao ya nyuma ya pazia? Nani hajui kuwa Mwanahalisi ni gazeti linaloendelea kuelekea udaku zaidi ya ithibati ya awali?

Kwanini tahariri haielezi ni kwanini Mwanahalisi limeacha hoja na ajenda yake kuu yaani Edward Lowassa? Ukiishi kwenye nyumba ya vioo usiwachokoze wehu.

Hata Kubenea arobaini yake haiko mbali naye wapo watakaofichua unafiki wake na umaarufu wake wa tindikali. Aweke CV yake uone kama ni mali kitu au jafafa.

Saeed Kubenea ni garasa tu, Watanzania wengi ni watu wa kukurupuka na kufuata mkumbo wala hawaangalii mambo kwa undani. Wahariri wa Tanzania wanamjua Kubenea ni mbabaishaji na wala hawamuheshimu, ni wavivu tu wa kufikiria ndio wanamuona mtu huyu ni shujaa wao. Kwanza ile kesi ya kumwagiwa tindikali ilikuwa ni kutokana na ufuska, alitembea na mke wa mtu mwenye mali akaamua amfanyie kweli.

Kubenea kanunuliwa na mafisadi siku nyingi ndio maana miezi mingi sasa ameacha kuwaandika kina Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge, na badala yake anapambana na Jakaya Kikwete, Samuel Sitta, Bernard Membe, John Magufuli, Harisson Mwakyembe na watu wengine wanaonekana kuwa ni mwiba kwa mafisadi.

Buriani MwanaHALISI
!
 
Kubenea ni kweli ana roho nyepesi kama kuku, kapewa milioni 30 na nyumba na mafisadi sasa amekuwa mtumwa wao. Kweli njaa mbaya.

Sitta msema kweli amempasha Kubenea sawasawa, kama kweli Sitta angekuwa mnafiki basi angelalamika chinichini kwa chini lakini ameendelea kuonesha dhahiri kuwa yeye ni msema kweli akampasha huyu kibaraka wa mafisadi Kubenea live.

Safi sana!!!!
 
Reginald Mengi, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP amekuwa akimlea Saeed Kubenea kama mtoto wake kwa miaka mingi. Alivutiwa na Kubenea baada ya kuhisi kuwa huyu ni kijana shupavu anayepambana na ufisadi bila woga. Kutokana na hilo, Mengi alijishusha akawa kama baba na rafiki wa karibu wa Kubenea, akawa anakutana naye na kuongea naye kila siku. Mengi alimpa Kubenea msaada wa kila aina, ikiwemo wa ushauri na fedha pale alipokwama.

Mengi naye akagundua kuwa Kubenea kanunuliwa na mafisadi. Akabaini kuwa Kubenea amenyea kambi ya wapambana mafisadi na sasa amehamia kambi ya mashetani. Akamtenga Kubenea, sasa hivi Mengi hana ule urafiki wa karibu wa zamani na Kubenea.

Sitashangaa kuona Kubenea sasa anaanza kumshambulia Mengi kwa maagizo ya mafisadi. Huyu jamaa kweli anatia aibu kwa tamaa zake za kijinga. Hawa mafisadi wakimaliza kumtumia watamtupa kama lile gamba chafu ambalo watu hilivaa kwenye kiungo kimoja cha mwili na kulitupa jalalani baada ya shughuli zao.

Kubenea ataishia pabaya sana. Gazeti lake litaporomoka baada ya umma wa Tanzania kugundua kanunuliwa na mafisadi. Heshima ndogo aliyonayo kwa jamii itatoweka, mafisadi watamtosa baada ya kumtumia, atafilisika, atachanganyikiwa, atapotea. Huu ni utabiri wangu!
 
Nina choamini mimi Sitta ni mnafiki na wala simuamini hata kidogo na wala sipendi awe kiongozi wangu hata siku

Hayo ni maoni yako ambayo siyo lazima yawe sahihi. Nchi hii hamtaki kuambiwa ukweli. Mzee huyu ameamua kuwa bold and candid na sasa mnamjia juu. Kwanza haikuwa sahihi kwa mtu aliyeshutumiwa kutumia chombo chake cha habari kuwamaliza wenzake ambao hawana chombo cha habari. Angetumia forum tofauti kujibu mapigo. In any case hiyo ndiyo ilikuwa assessment ya Sitta baada ya kuona kuna departure kubwa sana ya kiuandishi na minong'ono iliyokuwa imezagaa kwamba mwenzetu ameshatekwa nyara na wenzake.
 
Hayo ni maoni yako ambayo siyo lazima yawe sahihi. Nchi hii hamtaki kuambiwa ukweli. Mzee huyu ameamua kuwa bold and candid na sasa mnamjia juu. Kwanza haikuwa sahihi kwa mtu aliyeshutumiwa kutumia chombo chake cha habari kuwamaliza wenzake ambao hawana chombo cha habari. Angetumia forum tofauti kujibu mapigo. In any case hiyo ndiyo ilikuwa assessment ya Sitta baada ya kuona kuna departure kubwa sana ya kiuandishi na minong'ono iliyokuwa imezagaa kwamba mwenzetu ameshatekwa nyara na wenzake.

Sitta pamoja na matatizo yake chungu nzima, lakini pale anaposimama kutetea maslahi ya nchi kwa mfano kupinga malipo fisadi ya sh 113 billioni kwa Dowans basi Watanzania wote tunabidi tumuunge mkono pamoja na kujua kwamba Sitta si safi. Kumbukeni umoja ni nguvu ni utengano ni udhaifu. Sijamsikia hata siku moja Kikwete, Pinda, Pinda au Lowassa wakisimama hadharani na kumuita Sitta ni mnafiki maana hawana ubavu wa kufanya hivyo ila wameamua kuwatumia vibaraka vyao kumshambulia Sitta ambaye ameamua kusimama kidete katika kuipinga Dowans.
 
SAID Nyie ndio mnamjua leo?????yule ni bonge la mnafiki japo ni rafiki yangu sana,lakini huwa sikubaliana nae na huwa namueleza wazi kuhusiana na unafiki wake na gazeti lake la mwanahalisi,said mwanzo alikua ni mtu wa karibu sana na jk na hata kwenye kuanzisha hilo gazeti lake jk alikua na mkono wake,na katika siasa za kinafiki za jk,said ndio alitumika kwa kiasi kikubwa sana kumchafua Lowassa kwa maelekezo ya jk baada ya jk kuona Lowassa amezidisha kasi ya kutaka kumrithi kabla hajafa,uhusiano wa said na jk ulishamiri haswa kutokana na uhusiano wa kindugu kati ya said kubenea na Ramadhani Dau ambae pia ni mtu wa karibu sana na jk kwa sababu za kidini zaidi,kama mtakumbuka hata said alipomwagiwa tindikalai aliyokua akidai kamwagiwa na mafisadi kina rostam na lowassa,alikua ni jk aliekwenda kumuona hospitali na kumsaidia matibabu ya mwanzo kule india kitendo ambacho kilimkera lowassa na genge lake..Kilicho mpeleka saidi mikononi mwa Rostam na Lowassa ni kitu ambacho yeye mwenyewe saidi kubenea hukiita WAR CHEST iliyoandaliwa na Genge la LOWASSA NA ROSTAM kwa ajili ya watu wa dizaini ya kubenea kuhakikisha LOWASSA anakua rais,mnaomjua kubenea mtajieni neno WAR CHEST muone atakavyostuka mmejuaje..yule awadanganye nyie msiomjua sio sisi tunaomjua toka akiwa ripota wa bukoba,kwanza ni mtu wa standard seven hata secondary hajasoma
 
sita mnafiki kanunua asprin milion 5 alafu anajiita mzalendo ?! intelijinsia ya nchi inaonesha kwamba sita ni al shaabab

We nawewe mbona unaongea vitu cheap sana?kuwa open minded kidogo what is millioni 5 kwa issue kama ya richmond dowans???it's peanuts brother watu wanaongelea issues!!mbona mnakubali kutumiwa kifala namna hiyo!!
 
Kubenea ni kweli kashanunuliwa na mafisadi siku nyingi sana. Hilo jambo linaeleweka, na MwanaHalisi limekuwa likiyumba sana. Watu wengi hatulisomi tena, ni aibu kwa Kubenea kuwa mtumwa wa kina Rostam Aziz na Edward Lowassa kwa ajili ya vipesa vidogo to. Atabaki kuwa masikini wa akili na mali milele huyu Kubenea
Mtu mzima hovyooo! huoni aibu kusema uongo we malaya?Mwanahalisi ni gazeti pekee la kuaminika, sema wewe unapiga kampeni za kisenge hapa na hao waliokutuma wambie hatudanganyiki makenge nyie.
 
Reginald Mengi, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP amekuwa akimlelea Saeed Kubenea kama mtoto wake kwa miaka mingi. Alivutiwa na Kubenea baada ya kuhisi kuwa huyu ni kijana shupavu anayepambana na ufisadi bila woga. Kutokana na hilo, Mengi alijishusha akawa kama baba na rafiki wa karibu wa Kubenea, akawa anakutana naye na kuongea naye kila siku. Mengi alimpa Kubenea msaada wa kila aina, ikiwemo wa ushauri na fedha pale alipokwama.

Mengi naye akagundua kuwa Kubenea kanunuliwa na mafisadi. Akabaini kuwa Kubenea amenyea kambi ya wapambana mafisadi na sasa amehamia kambi ya mashetani. Akamtenga Kubenea, sasa hivi Mengi hana ule urafiki wa karibu wa zamani na Kubenea.

Sitashangaa kuona Kubenea sasa anaanza kumshambulia Mengi kwa maagizo ya mafisadi. Huyu jamaa kweli anatia aibu kwa tamaa zake za kijinga. Hawa mafisadi wakimaliza kumtumia watamtupa kama lile gamba chafu ambalo watu hilivaa kwenye kiungo kimoja cha mwili na kulitupa jalalani baada ya shughuli zao.

Kubenea ataishia pabaya sana. Gazeti lake litaporomoka baada ya umma wa Tanzania kugundua kanunuliwa na mafisadi. Heshima ndogo aliyonayo kwa jamii itatoweka, mafisadi watamtosa baada ya kumtumia, atafilisika, atachanganyikiwa, atapotea. Huu ni utabiri wangu!
Kwani wewe unalipwa nanani kuleta majungu yako hapa? Nenda kawafahamishe makuadi wanaokutumia kwamba mwanahalisi ni chuma cha pua na haliyumbi.
 
Nimewasoma wote watatu - anayejiita Mtanzania Huru, Mojo na Ngao One. Nawafahamu. Ninachosikitika ni kwamba hamumfahamu Kubenea. Huyu jamaa ni chuma cha pua. Si kweli kwamba Kubenea analipiwa safari zake za India na serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Hili naweza kulithibitisha . Muache kucahfaua watu kwa hisia.

Kuhusu Kubenea kufadhiriwa na Mengi na sasa urafiki wa Mengi na Kubenea umekufa, na kwamba wakati wowote anaweza kumuandika Mengi, nadhani ninyi hamumfahamu vizuri huyu kamanda. Kubenea hana rafiki na yeyote ambaye anatia ulimi puani. Nani asiyejua kwamba Mengi anamtetea Kikwete, kwamba hahusiki na ufisadi wakati huohuo anasema nchi imejaa mafisadi?

Inawezekana kweli kwamba Kubenea haheshimiki na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini. Lakini kwangui mimi kutoheshimika kwake kunatokana na husda waliyonayo baadhi ya watu kwa kumuona Kubenea amepiga hatua kubwa ya kumiliki gazeti lake yeye mwenyewe.

Kuhusu hili la kumwagiwa tindikari kwa kuwa alikuwa na mke wa mtu, hizo ni poropaganda za wale waliotumwa kumdhuru. Tunawajua hata kwa majina.
 
Alichokifanya kamanda Kubenea ni kuonyesha sura halisi ya Sitta na wenzake. Mnaomshambulia humu ni magamba ya Nape...
 
Kubenea wajanja tulishamstukia siku nyingi, mmebaki misukule yake mnayefuata mtu bila critical thinking... safari njema Kubenea
na misukule yake kwenye kuwapamba mafisadi.
 
Back
Top Bottom