MwanaHalisi: Njama za Mauaji zafichuka, za kuwauwa Kubenea, Dr. Slaa, Mnyika na Olimboka

Status
Not open for further replies.
Ninyi mliopewa fedha na usalama wa taifa ili muwatetee ondoeni ujinga wenu humu.

Hawa watu ni wauaji na kutetea wauji ni kushiriki uuwaji. Acheni kutetea wauaji. Kama maofisa wa TISS walihusika na wizi wa fedha za umma kwenye BoT, watashindwa vipi kupanga njama za kuuwa wanaokosa serikali.

Stori ya leo ya Mwanahalisi imesheheni taarifa. Tatizo lako umesoma hii iliyopo hapa JF na ukatoa hukumu. Hii ni sehemu tu ya stori. Stori kamili imechukua kurasa mbili. Imesheheni taarifa. Imejaa uchunguzi. Imefuata maadili. Achana na Mwanahalisi.

Kama Kikwete na Zoka wanakana kuhusu hili linalosemwa, basi njia ni rahisi. Waunde tume huru kuchunguza waliomvamia Ulimboka. Kukana pekee yake hakutoshi.

Rostam Aziz alikana kumiliki Dowans. Kikwete alikana kuifahamu Dowans. Lowassa alikana kuingilia mchakato za zabuni na kuipendelea Richmond.

Lakini mwisho wa siku Lowassa akajiuzulu, mahakama ikathibitisha kuwa Rostam ndiye mmiliki halali wa Dowans na Lowassa akasema Kikwete alikuwa anafahamu kila kilichokuwa kinatendeka – kwa maana ya kwamba alikuwa anafahamu Dowans ni mali ya Rostam Aziz.

Mkuu spanner; mazoba/wachumia tumbo walikuwepo kote kuanzia utawala wa Hitler, hadi Rwanda. Ni waganga njaa!! tu wala usijali mambo yakiwa mambo utayaona yanachafua nguo za ndani tu!
 
copy and paste ya mkusanyiko wa habari za kuokoteza mitandaoni nao unaita habari za uchunguzi??????????

Wajinga huamini kila neno. Hapa ukianzisha uzi kuwa siku alipotekwa dr Uli Jk alikuwa dereva wa ile gari utaona wanavyokushangilia.
 
Usalama wa taifa wako katika idara zote za serikali. Polisi wengi walio katika idara ya detective wengi wao wapo pia kwenye usalama wa Taifa. Tusishangae kuona kama polisi waliohusika katika tukio la Ulimboka wakiwa polisi ni muda wa kazi ya ziada ya usalama wa Taifa ndio maana pengine hata katika ofisi ya polisi hakuna kumbukumbu ya watu hao kutumwa kwa kuwa wana kofia mbili.
 
Usalama wa taifa - "The killers wa wapenda maendeleo na watetezi wa haki". Sijawahi kuona popote isopokuwa TZ tu. This is too wicked which won't go without punishment from above. People are now crying to GOD hence you will soon pay for your uovu.

The killers, usalama wa ccm, the end has finally come
 
Am not support any kind of humiliation which done by human being to other human being. I think is better 4 all human to understand that world is the perishable place both 4 rich and poorer. Where are they great killers as hitler osama musolin pilato sadam. Is better to respect god than any leaders regardless popularity they have in this world.
 
Huu ni ukweli kabisa,utawala huu umeshindwa kupambana na ukweli na sasa umeamua kuwazimisha watetezi.
Makada kadhaa wa magamba Walishaonya juu ya utawala wa kimauaji wa JK akiwemo Sumaye,Mwakyembe na Sita.
 
Andishi hilo linasema, “Katika ajali, timu hiyo imeelekezwa kuangalia mbinu kama waliyowahi kuijaribu kwa Mwakyembe (Dk. Harrison Mwakyembe mbunge wa Kyela CCM). Hapa kuna vijana wamefundishwa kikamilifu njia hii. Mafunzo yao yaliandaliwa (jina la nchi tunalo) mwishoni mwa mwaka jana
Polonium (Russia)
 
Wadau;

Baada ya kurudi kwa jembe letu, saed kubenea kutoka masomoni nchini Holland, Mwanahalisi leo limemaliza kazi kabisa. Soma sehemu hii ya stori yake ya leo:


___________________________________




‘Njama za mauaji’ zafichuka
· Kigogo wa Usalama wa taifa atajwa
· Ulimboka: Walioniteka ni wa ikulu

Na Jabir Idrissa

NAIBU Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS), Jack Zoka ametajwa kuwa miongoni mwa wanaopanga mkakati wa kuangamiza wanaodaiwa kuikosoa serikali, MwanaHALISI limeelezwa.

Aidha, ametajwa kuwa mmoja wa waliounda mpango wa kutekwa na kuteswa kwa Dk. Steven Ulimboka ambaye hivi sasa anaendelea na matibabu Afrika Kusini.

Taarifa zilizofikia gazeti hili kutoka vyanzo mbalimbali zinasema, Zoka ni mtuhumiwa Na. 1 katika utekelezaji wa mpango wa siri wa mauaji, utekaji na utesaji ambao umeandaliwa mahususi na kwa watu maalum.

Miongoni mwa wanaotajwa kutaka kuangamizwa, ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibord Slaa, mbunge wa Ubungo kupitia chama hicho, John Mnyika na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), wachapishaji wa MwanaHALISI, Saed Kubenea.

Bali Zoka hakupatikana juzi Jumatatu kutoa kauli yake juu ya tuhuma hizi.

Mwandishi alimwita Zoka tangu saa nane mchana hadi saa 12.55; lakini simu yake iliita bila kupokelewa na wakati mwingine ilijibu kuwa mwenye namba hiyo hapatikani.

Hatimaye mwandishi alipeleka ujumbe kwa Zoka uliosema: “Natumai umzima wa afya. Mimi mhariri wa MwanaHALISI nataka uzungumzie tuhuma za viongozi wakuu wa Chadema, kuwa TISS na wewe binafsi, mmepanga kuua baadhi yao. Unasemaje?”

Zoka aliombwa pia kutoa kauli juu ya taarifa katika mitandao, zinazomtaja yeye binafsi kuwa nyuma ya mpango uliofanikisha kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka.

Dk. Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini 30 Juni, kwa michango ya madaktari wenzake, watu mbalimbali na kile kilichoelezwa kuwa “msaada mkubwa wa mfanyabiashara mashuhuri nchini, Dk. Reginald Mengi.”

Kwa mujibu wa mawasiliano ya imeili yaliyotumwa na mmoja wa watoa taarifa wa ndani wa Dk. Slaa na Mnyika, mpango wa kuwateketeza watu hao umeandaliwa mahususi ili “kuwatisha katika harakati za kutetea wananchi wanyonge.”

Mtoa taarifa huyo kutoka ndani ya idara ya usalama ameeleza, katika mawasiliano yake ya 27 Juni 2012, kuwa kuna mpango wa kuteketeza maisha ya Dk. Slaa na Mnyika; na kwamba mpango huo unaratibiwa moja kwa moja na Zoka.

“…the information I'm giving you is authentic (taarifa ninazokupa ni sahihi na makini). Tayari kuna timu imetumwa kwenda Dodoma kufuatilia mienendo ya Mnyika kwa maana ya mahali alipofikia, mahali anapopendelea kutembea na kula chakula na marafiki anaokuwa nao mara kwa mara, hasa wanawake kama wapo,” anaeleza mtoa taarifa.


Anasema, “Hii timu inafanya kazi moja kwa moja kwa maelekezo ya Zoka na wamepewa kazi ya kutathmini njia bora ya kumdhuru Mnyika bila kuacha trace (unyayo) yoyote. Katika options (njia za kutumia), kuna kuweka sumu kwenye maji, chakula au (kumpiga) sindano. Kuna matumizi ya ajali au ujambazi.”

Andishi hilo linasema, “Katika ajali, timu hiyo imeelekezwa kuangalia mbinu kama waliyowahi kuijaribu kwa Mwakyembe (Dk. Harrison Mwakyembe mbunge wa Kyela CCM). Hapa kuna vijana wamefundishwa kikamilifu njia hii. Mafunzo yao yaliandaliwa (jina la nchi tunalo) mwishoni mwa mwaka jana.”..............


Habari kamili katika MwanaHalisi la leo.

Chadema mnaweweseka sana aisee.
 
UWT ipo kwa ajili ya usalama wa nani? CCM au wananchi na mali zao? Au ni usalama wa genge la mafisadi wa CCM? Na hao wanaoitwa maafisa usalama wa taifa wanapatikanaje? Je, si makada wa CCM?

Kwa kuwa imefahamika hwa jamaa hawapo kwa ajili ya maslahi ya wananchi, kwa nini wananchi wasiiwajibishe genge hilo la mafisadi na UWT? Tufikirie hatua sahihi za kuchukua maana tumeshasema sana. Kwa mfano tupeleke mashtaka The Hugue kwa OCAMPO au mrithi wake. Au tupeleke mashtaka UN au nguvu ya umma ifanye kazi yake? Tusiipe ushirikiano genge hili dhalimu ndani ya serikali
 
mapambano ndo yanakaribia kuanza rasmi... Atakaethubutu kuua kati ya hao watajwa, ajue pia na uhai wake u rehani pia... Si Dhaifu, si wazir wa mambo ya ndan, si zoka.. Yoyote anayejihis yu katika mipango ya maangamizi basi ajue pia anafahamika na ajue kabisa hatoishi na atakuuawa kwa style ile ile... NOTE: POLISI HA2ENDI NG'O. 2TASHUGHULIKIANA WENYEWE KWA WENYEWE MPAKA DISCIPLINE ITAKUJA.
 
Kubenea ni mnafiki tu huu ni uongo mkubwa.wanasiasa wanatafuta umaarufu kupitia jina la usalama wa taifa
 
budget ya hawa jamaa wanaotoa ***** imepanda nini? Wapo wengi sasa na wanajituma kwelikweli.
 
copy and paste ya mkusanyiko wa habari za kuokoteza mitandaoni nao unaita habari za uchunguzi??????????

Uchunguzi unaweza kuanzia hata kwenye mitandao. Mwandishi atakachofanya nikuthibitisha kwa kuenda mahali pengine.
 
CCM mbele hakuendeki na nyuma pia hakuendeki! imenasa kwenye matope na sasa wanapanga kutoa roho za watu, wanadhani wakitoa roho za hawa watu watajinasua kwenye tope hili? Mbomoa nchi ni mwananchi mwenyewe na hapo sasa mvuruga amani ambayo wao ccm walikuwa wakiihubiri miaka yote ni ccm wenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom